Bunge lasema halijapokea barua ya Nyalandu kujiuzulu, lamvua ubunge kutokana na CCM kumfukuza uanachama

Bunge lasema halijapokea barua ya Nyalandu kujiuzulu, lamvua ubunge kutokana na CCM kumfukuza uanachama

Hawa wameshanganyikiwa kabisa bora wangekaa kimya waulizeni hiyo barua kutoka kwa katibu mkuu ikimueleza spika kumvua Ubunge na kwa kikao kipi PolePole asiropoke wakati wa press yake juzi?
Akili ya kawaida nilitegemea kuona barua kutoka ofisi ya katibu mkuu CCM ikieleza kufukuzwa kwa Nyalandu ndipo ifuate ya Spika wamechemka
Picha Lazaro Nyalandu leo akiwa na Tundu Lissu hospital Nairobi leo.View attachment 621953
Huyu jamaa sio kumuamini sana kuwa karibu na Lissu. Lolote anaweza kufanya.
 
kanunua simu kampa demu, walipoachana kampokonyaaaaaaa
 
Ofisi ya Spika wa Bunge ingependa kuwaarifu Watanzania wote kwamba mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini (CCM) Ndugu Lazaro Nyalandu ambayo amekuwa akiarifu kwamba amemwandikia Mheshimiwa Spika kumtaarifu kujiuzulu kwake.
View attachment 621958
Hata hivyo, Mhedhimiwa Spika amepokea barua toka kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ya tarehe 30 Oktoba, 2017 akimuarifu kwamba kwa muda sasa Chama hicho kilishaanza kumchukulia hatua za kiudhibiti na kinidhamu dhidi ya vitendo na kauli zake zisizoridhisha kinyume na misingi, falsafa na itikadi ya Chama cha Mapinduzi.

Hivyo, Chama cha Mapinduzi kuanzia tarehe ya barua yao kimemjulisha Mheeshimiwa Spika kuwa Ndugu Lazaro Nyalandu amepoteza sifa za Uanachama wa Chama cha Mapinduzi, na hivyo kupoteza nafasi zote za uongozi wa ndani wa Chama hicho na Ubunge kwa mujibu wa Ibara ya 13 ya Chama hicho.

Mheshimiwa Spika, angependa kuwaarifu Watanzania kwamba kwa barua hiyo toka mamlaka halali ndani ya Chama cha Mapinduzi ambacho Ndugu Lazaro Nyalandu alipata Ubunge kupitia Chama hicho na kwa mujibu wa Ibara ya 71 (1)(f) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotamka kwamba:

“Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake cha Ubunge iwapo litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo: (f) Iwapo Mbunge ataacha kuwa Mwanachama cha chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge.”

Hivyo, Ndugu Lazaro Nyalandu si Mbunge tena na hatua stahiki za kuiarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi zinaendelea kuchukuliwa.

Imetolewa na: Ofisi ya Spika S.L.P. 941

DODOMA

Ofisiya Bunge S.L.P 941 DODOMA

Comments
Yaan huyu anajidharirisha kw kweli,,, yeye sasa kawa msemaji wa magamba,,, kweli ukiugua muda mrefu CD4 za akil nazo hupungua,,,
 
View attachment 621961

Moja ya habari kubwa za sasa hivi nchini Tanzania ni Lazaro Nyalandu ambae juzi ametangaza kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na Ubunge wa Singida Kaskazini.

Baadae Spika Ndugai alihojiwa na vyombo vya habari na kusema kwamba pamoja na kusikia taarifa za kujiuzulu kwa Nyalandu kwenye vyombo vya habari, yeye bado hajapokea barua ya kujiuzulu kwa Mbunge huyo.

Sasa leo imetoka taarifa kutoka Ofisi ya Bunge Dodoma ikiwa imeandikwa kama inavyosomeka hapo juu..
Nchi sasa imekuwa ya wa huni yaani:
Kiingereza: holiganism
Kwa kichina: Liu Mang
 
hahahahahaha yaani hawa CCM aisee wanajitahid kuleta danganya toto ikiwa watanzania sasa wamekuwa na akili nyingi....zama zimebadilika sana hata wao wabadilike
 
Azam TV usiku huu wameripoti kwamba juhudi za kumpata Polepole kufafanua huu nkanganyiko zimegonga mwamba baada ya PPolepole kuwakimbia Azam TV na hata alipopigiwa simu haikujibiwa! Wameinama, ... Wameinuka . . wanaona haya haoo!!!!!
 
CCM wanafanya mambo ya kitoto sana., sasa hii maana yake nini mtu amejitangazia mwenyewe tarehe tokea tarehe 30 na wao wakaanza kumtukana na kumdhalilisha. Mbona spika aliulizwa na mwandishi kama Nyalandu amejiuzulu kasema yeye hajui si angesema basi anayo barua ya Katibu Mkuu wa CCM kufukuzwa
 
CCM ilikua zamani wazee wenye hekima na busara walikijenga chama kuanzia ngazi ya shina,kijiji,kata,wilaya,mkoa hadi taifa kwa hoja na sera zilizowavutia wananchi wakajiunga na chama,sasa hivi wazee wamekaa pembeni wanaogopa kuambiwa wanawashwa washwa chama wameachiwa Wahuni kutwa kuropoka na kutumia mabavu chama hakina mvuto tena kimebaki jina...hakuna cha Nambari wani tena kimebaki kuwateka raia wasio na hatia na kuwapiga risasi wale wote wanaowakosoa kila siku maiti zinaokotwa pembezoni mwa bahari hakuna anayelizungumzia hili wote kimya,huenda ni maagizo kutoka juu ila amini na waambieni hakuna aliyejuu na mwenye mamlaka kuhusu uhai na kifo cha kiumbe kingine isipokua ALLAH! ipo siku ichi kilio kitaisha na Nchi yetu itapata Uhuru wa kweli toka mikononi mwa wakoloni weusi CCM..
 
Kwa hiyo ndunyala badala ya kupeleka barua ya kujiuzulu kwa spika faster yeye kakimbilia mitandaoni,akili kubwa ikamuwahi faster kumtemesha !!siasa tamu sana ukiijua

Ona sasa unavyoandika jina kwa kugeuza kisa una ona aibu ya viongozi wako

Ha! ha! Just ha! ha!
 
Barua ya kuwafuta uanachama wabunge Wa cuf ilipokelewa haraka akiwa Nigeria Je iweje ya NYALANDU iwe haijafika mpka Leo tena yeye akiwa Dodoma na si Nigeria?
Aisee yawezekana barua ya kuwavua ubunge wabunge wa CUF labda alipokea maelekezo toka juu.
 
Barua ya kuwafuta uanachama wabunge Wa cuf ilipokelewa haraka akiwa Nigeria Je iweje ya NYALANDU iwe haijafika mpka Leo tena yeye akiwa Dodoma na si Nigeria?
Aisee yawezekana barua ya kuwavua ubunge wabunge wa CUF labda alipokea maelekezo toka juu.

Watakaokuelewa vyema watanisaidia kunielewesha na Mimi.
 
Back
Top Bottom