Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Hizi lawama zimekuwa zikisikika kabla hata Mama Makinda hajawa spika, na zinatoka upande mmoja kila siku.Hoja ya msingi ni kuwa Spika analiaibisha bunge, jee wewe unaonaje?
Ndio maana busara sahihi ni kuhakikisha upinzani unapata wabunge wengi zaidi ili uwe na uwezo wa kuchagua spika kwa kutegemea wingi wao.
Kulalamika ni hulka mbovu ya kitanzania, ambayo kwa bahati mbaya wala hatujui itakwisha lini, labda kizazi kijacho cha watanzania hakitataka kuirithi tabia hii ambayo siku zote ni kielelezo cha jamii inayoishi kivivu.