Bunge lataka Watumiaji wa Daraja Tanzanite (Selander) Walipie

Bunge lataka Watumiaji wa Daraja Tanzanite (Selander) Walipie

Kamati ya Bunge ya Bajeti limeitaka serikali iwatoze tozo watumiaji wa daraja jipya la Tanzanite (New Salender).

========


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imependekeza kwamba magari yatakayopita kwenye daraja la Tanzanite (Daraja jipya la Salenda) jiji Dar es Salaam yatozwe ushuru.

Kamati hiyo imesema ushuru uwepo katika daraja hilo kama ilivyo kwa daraja la Nyerere (Kigamboni) kwani daraja la Tanzanite nalo limejengwa kwa fedha za mkopo.

“Kamati inaitaka Serikali pindi daraja hili litakapokamilika, kwa sababu limejengwa kwa mkopo kama lilivyo Daraja la Kigamboni, liwe ni daraja la kulipia yaani” amesema Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Sillo Baran.

Ujenzi wa daraja hilo ulizinduliwa Julai 23, 2018 na aliyekuwa Rais wakati huo, Hayati John Pombe Magufuli ikiwa ni mpango wa kupunguza msongamano wa magari katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi na Barabara ya Barack Obama.

Jana Rais Samia Suluhu alisema daraja hilo lenye urefu wa kilomita 1.03 na upata wa mita 20.5 linatarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2021 na kuzinduliwa katika sherehe za miaka 60 ya Uhuru.


Chanzo: Nipashe

Zaidi...

Daraja Jipya la Selander kuwa Toll Bridge

Mheshimiwa Spika, Kamati ya Bajeti ilipata fursa ya kutembelea na kukagua ujenzi wa Daraja jipya la Tanzanite na kutaarifiwa kwamba Hatua iliyofikiwa ni:

kuendelea na ujenzi wa daraja jipya (km 1.03) na barabara unganishi zenye urefu wa km 5.2 ambapo ujenzi umefikia asilimia 87.3. Katika kipindi cha mwaka 2020/21, Shilingi Bilioni 58.8 zimetumika”.

Kamati inaitaka Serikali pindi Daraja hili litakapokamilika na kwa sababu limejengwa kwa mkopo kama lilivyo Daraja la Kigamboni liwe ni daraja la kulipia yaani “Toll bridge” Kamati inaona kwa kuwa kuna njia mbadala ambayo endapo mtu hataki kulipia daraja anaweza kupita ni vyema ushauri huo ukazingatiwa.
Kuna sababu zozote za msingi ambazo kamati imezingatia?
 
Upuuzi gani huu. Daraja la kigamboni ni mradi wa mamlaka ya pensheni tozo ni ili kurudisha fedha yao. Na daraja la tanzanite ni hela ya hazina.
Yote ni madaraja ya watanzania. Acha mawazo yenye viashiria vya kushindwa kufikiri vizuri. Tofauti huko Salender wanapita matajiri wenye pesa zao, huku Kigamboni mnapita wajinga. Na mnatetea upuuzi huo.

Kama serikali imeomba pesa NSSF inapaswa izilipe kama inavyolipa mikopo mingine yote, na siyo kufungafunga uchafu barabarani.

Barabara ikifunguliwa itachochea wakazi kuhamia na automatically kodi zitaongezeka huko.
 
Nyie wabunge wa Magufuli hatuwezi lipia daraja kwani nini kazi ya kodi zetu
 
Kwa taarifa yako hili daraja limekuwa proposed kipindi cha JK na kusaini hiyo grant kutoka South Korea. Acheni kudanganyika kuwa kila kizuri kilifanywa na Magufuli kama alivyokuwa ANAWAONGOPEA

The Advantages of a Grant​

Grants offer a number of benefits that any person in need of funding should consider.

  • No repayment necessary: Grants are non-repayable. Once you’re awarded the grant money, it’s yours without any strings attached. There’s no need to worry about monthly payments or piling on more debt. Repayment is the fundamental difference between a grant and a loan, and also what makes grants more valuable than loans.
  • No risk: Grants are a no-risk way to obtain the financing you need. If a loan is not repaid, you put your credit rating and assets in jeopardy. Grants do not require repayment and will only benefit you or your business.
 
Back
Top Bottom