JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Uongozi wa Bunge umetaja aliko aliyekuwa Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa Mkoani Dodoma, Job Ndugai.
Ndugai hajaonekana katika shughuli rasmi za chombo hicho tangu taarifa za kujiuzulu kwake wadhifa huo zilipotangazwa Januari 6, 2022 kwamba aliandika barua kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na nakala kuwasilishwa kwa Katibu wa Bunge kutoa taarifa juu ya uamuzi wa kuachia ngazi.
Alipotafutwa na Nipashe jana Aprili 7, 2022 kwa simu kuzungumzia kutoonekana huko bungeni kwa Mbunge wa Kongwa, kushiriki vikao vya Mkutano wa Bunge la Bajeti vilivyoanza Jumanne ya wiki hii, vikitanguliwa na shughuli za kamati za kudumu za Bunge, Katibu wa Bunge, Nene wa Mwihambi alisema Ndugai yuko jimboni kwake.
"Hayupo bungeni maana yake (Ndugai) yuko jimboni. Sina barua kuhusu suala hilo. Mbunge asipokuwapo bungeni, maana yake yuko jimboni kwa mujibu wa kanuni na taratibu za Bunge."
"Ni mapema mno, ndiyo kwanza kumefanyi ka vikao viwili vya Mkutano wa Bunge la Bajeti, tulianza Jumanne.. (Ndugai) ana muda wa kutosha, atakuja kuungana na wabunge wenzake kushiriki vikao vya Bunge.
Kanuni za Kudumu za Bunge zinaelekeza miongoni mwa sababu za kukoma kwa hadhi ya ubunge ni kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo ya Bunge pasina kutoa taarifa kwa Spika, kifo, kufutwa uanachama wa chama cha siasa, kujiuzulu ubunge na kutiwa hatiani kwa makosa ya jinai yanayosababisha kifungo cha zaidi ya miezi sita gerezani.
Nipashe ilipomtafuta Ndugai kwa simu jana Aprili 7, 2022 saa 6:48 mchana, simu yake ya kiganjani iliita kwa sekunde chache, ikakatwa kisha ukatumwa ujumbe mfupi wa maandishi kutoka kwe nye simu hiyo ukiwa na neno moja linalohoji nani?
Mwandishi alijitambulisha kwa sms lakini hakujibiwa na simu haikupokelewa.
Source: Nipashe