Bunge laulizwa alipo Job Ndugai, lasema halina taarifa alipo, inawezekana yupo jimboni kwake

Bunge laulizwa alipo Job Ndugai, lasema halina taarifa alipo, inawezekana yupo jimboni kwake

Japo siamini unachosema..ila wanasema what goes around comes around..mwisho wa kunukuu
 
Hizi ni chini chini ila ni za kweli huwezi amini ndugu zangu Job Ndungah aliyemfuta ubunge Tundu Anti pass Lisu anakarbia kufutwa ubunge kwa sababu, haonekani bungeni aise

Wandugu tuishi vyema Hali s Hali ndgu zangu, Yani nikweli alimchomtendea mwenzake ndo hicho anatendewa.
Vikao vitatu bado saana mjomba. Ndiyo kwanza kikao cha kwanza.

Pitieni kanuni za bunge zipo google huko
 
Kipimo kile kile unachowapimia wenzako ndicho utakachopimiwa - hakika ruben. ( Comedian)

Huwez taka biriani la sinza halafu mfukoni una Buku jero... Utakuwa haupo serious.
 
Ndugai Ametumwa India

Duh Maisha haya nakumbuka

Kinana Alitumwa India Kutibiwa
 
Uongozi wa Bunge umetaja aliko aliyekuwa Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa Mkoani Dodoma, Job Ndugai.

Ndugai hajaonekana katika shughuli rasmi za chombo hicho tangu taarifa za kujiuzulu kwake wadhifa huo zilipotangazwa Januari 6, 2022 kwamba aliandika barua kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na nakala kuwasilishwa kwa Katibu wa Bunge kutoa taarifa juu ya uamuzi wa kuachia ngazi...
Sasa tuache makelele,

Huko aliko mpelekeeni na Wabunge wake. Nadhani anawahitaji nao wanamhitaji

1649404867726.png
 
Ndugai alikuwa akifukuza wabunge wa CHADEMA sasa hivi yeye hata kuingia bungeni anaogopa.

Bunge limfukuze Ndugai na limnyime mafao yake kwa utoro bungeni
 
Uongozi wa Bunge umetaja aliko aliyekuwa Spika wa Bunge wa Tanzania na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai.

Ndugai hajaonekana katika shughuli rasmi za chombo hicho tangu taarifa za kujiuzulu kwake wadhifa huo zilipotangazwa Januari 6, mwaka huu kwamba aliandika barua kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na nakala kuwasilishwa kwa Katibu wa Bunge kutoa taarifa juu ya uamuzi wa kuachia ngazi.

Mara ya mwisho Ndugai kuvaa joho la Spika na kuongoza kikao cha Bunge ilikuwa Novemba 12, mwaka jana, siku ambayo pia ulikuwa ukomo wa Mkutano wa Tano wa Bunge la 12.

Hii ina maana kwamba Ndugai hakuhudhuria vikao vyote vya Mkutano wa Sita wa Bunge la 12 vilivyofanyika kwa wiki tatu Februari mwaka huu na sasa bado hajaanza kushiriki vikao vya Mkutano wa Bunge la Bajeti vilivyoanza Jumanne ya wiki hii, vikitanguliwa na shughuli za kamati za kudumu za Bunge.

Alipotafutwa jana kwa simu kuzungumzia kutoonekana huko bungeni kwa Mbunge wa Kongwa, Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi, alisema Ndugai yuko jimboni kwake.

“Ninachokijua mimi (Ndugai) yuko kwa wananchi jimboni kwake. Hayupo bungeni maana yake yuko jimboni," kiongozi huyo wa Bunge alisema.

Pia tulipotaka kupata ufafanuzi kama Ofisi ya Katibu wa Bunge ina barua ya kutoka kwa Ndugai ya kuupa taarifa uongozi wa chombo hicho kuhusu kutohudhuria kwake bungeni, Katibu wa Bunge alisema:

"Sina barua kuhusu suala hilo. Mbunge asipokuwapo bungeni, maana yake yuko jimboni kwa mujibu wa kanuni na taratibu za Bunge."

Hata hivyo tulipohitaji ufafanuzi wa uongozi wa Bunge kuhusu wananchi wa Jimbo la Kongwa kukosa uwakilishi bungeni na mustakabali wake, Katibu wa Bunge alisema:

"Ni mapema mno, ndiyo kwanza kumefanyika vikao viwili vya Mkutano wa Bunge la Bajeti, tulianza Jumanne... (Ndugai) ana muda wa kutosha, atakuja kuungana na wabunge wenzake kushiriki vikao vya Bunge."


Source:IPP
 
Back
Top Bottom