Bunge laulizwa alipo Job Ndugai, lasema halina taarifa alipo, inawezekana yupo jimboni kwake

Bunge laulizwa alipo Job Ndugai, lasema halina taarifa alipo, inawezekana yupo jimboni kwake

Vikao vitatu bado saaana ndiyo kwanza hichi ni kikao cha kwanza.

Yule mgogo alivyo mpuuzi siku atakayokuja bungeni atawachamba wanaomuulizia na kumsifia chui jike.
 
Hawezi kufukuzwa hata asipohudhuria vikao vyote.

CCM wanalindana
 
Vikao vitatu bado saaana ndiyo kwanza hichi ni kikao cha kwanza.

Yule mgogo alivyo mpuuzi siku atakayokuja bungeni atawachamba wanaomuulizia na kumsifia chui jike.
Kiboko ya Goliath ,
Mwezi wa nne hadi wa sita au wa saba kuna bunge la bajeti, unahesabika kama mkutano mmoja.

Mkutano huo mmoja unaundwa na vikao vingi. Hivyo mkutano mmoja ni mkubwa kuliko kikao kimoja.

Ile sheria ya kufukuzwa ni kwa kudoji mikutano mitatu.
 
"Attention:
👉Ndugai yupo kizuizini
👉Alichofanyiwa Aboud Jumbe ndicho alichofanyiwa Ndugai.
👉Ameondolewa hadhi ya uspika mstaafu, haruhusiwi kutoka nje ya makazi yake isipokuwa kwa kibali maalum
👉Familia yake imezuia kuongea chochote kuhusiana na kinachoendelea
👉Ni mhaini"

Huo ujumbe nimeutoa Twitter umeandikwa na mtu anayejulikana kama MCHAMBUZI.

Kama ni kweli basi Ndugai amewekwa kwenye kizuizi cha kifo..afe taratibu kwa stress.
 
Yaonekana kama vile kavunja miiko ya kichawi. Kwa hiyo anadhurika kisirisiri.
 
Kijifungia ndani hakutakusaidia mzee wangu. Unaweza jiletea magonjwa mengi kutokana na msongo wa mawazo. Tunajua fika hukutafajia hili lililotokea lakini binadamu wote hatujui kesho yetu.
Yaliyokutokea yamekua funzo kwetu kwamba vyeo na dhamana tulizopewa si za milele. Zinaweza kukoma muda wowote tena pale tusipotarajia. Jipige moyo konde utoke hadhari maisha yaendelee.
Uliyotukosea watanzania ukiwa spika wa bunge ni makubwa kuliko kosa lililokuondoa kwenye kiti. Utafanya vizuri kama utatoka hadharani pia utuombe radhi. Ukifanya hivyo nakuhakikishia mzee wangu utaishi kwa amani zaidi kuliko hata ulipokua na cheo. Toka hadharani acha kujificha. Tumejiandaa kukupokea kwa upendo tulojaliwa.

Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe. Gal 6:1​

Uongozi wa Bunge umetaja aliko aliyekuwa Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa Mkoani Dodoma, Job Ndugai.

Ndugai hajaonekana katika shughuli rasmi za chombo hicho tangu taarifa za kujiuzulu kwake wadhifa huo zilipotangazwa Januari 6, 2022 kwamba aliandika barua kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na nakala kuwasilishwa kwa Katibu wa Bunge kutoa taarifa juu ya uamuzi wa kuachia ngazi.

Alipotafutwa na Nipashe jana Aprili 7, 2022 kwa simu kuzungumzia kutoonekana huko bungeni kwa Mbunge wa Kongwa, kushiriki vikao vya Mkutano wa Bunge la Bajeti vilivyoanza Jumanne ya wiki hii, vikitanguliwa na shughuli za kamati za kudumu za Bunge, Katibu wa Bunge, Nene wa Mwihambi alisema Ndugai yuko jimboni kwake.

"Hayupo bungeni maana yake (Ndugai) yuko jimboni. Sina barua kuhusu suala hilo. Mbunge asipokuwapo bungeni, maana yake yuko jimboni kwa mujibu wa kanuni na taratibu za Bunge."

"Ni mapema mno, ndiyo kwanza kumefanyi ka vikao viwili vya Mkutano wa Bunge la Bajeti, tulianza Jumanne.. (Ndugai) ana muda wa kutosha, atakuja kuungana na wabunge wenzake kushiriki vikao vya Bunge.

Kanuni za Kudumu za Bunge zinaelekeza miongoni mwa sababu za kukoma kwa hadhi ya ubunge ni kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo ya Bunge pasina kutoa taarifa kwa Spika, kifo, kufutwa uanachama wa chama cha siasa, kujiuzulu ubunge na kutiwa hatiani kwa makosa ya jinai yanayosababisha kifungo cha zaidi ya miezi sita gerezani.

Nipashe ilipomtafuta Ndugai kwa simu jana Aprili 7, 2022 saa 6:48 mchana, simu yake ya kiganjani iliita kwa sekunde chache, ikakatwa kisha ukatumwa ujumbe mfupi wa maandishi kutoka kwe nye simu hiyo ukiwa na neno moja linalohoji nani?

Mwandishi alijitambulisha kwa sms lakini hakujibiwa na simu haikupokelewa.

Source: Nipashe
Huo ni utoro, Job Ndugai ni mtoro. Afukuzwe, afutiwe/anyang'anywe ubunge na afutiwe stahiki zake zote.
Kutingisha kiberiti kumemtokea puani na Sukuma gang waliomtanguliza kama chambo wamekaa pembeni kama wao siyo part and parcel wa kimbembe kilichomkuta, ka Jobu kananichekesha sana kwani kila kanapokuwa ni mada nakumbuka kalivyomtandika mtu bakora kwa jinsi kalivyo na uroho wa madaraka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugai alikuwa akifukuza wabunge wa CHADEMA sasa hivi yeye hata kuingia bungeni anaogopa.

Bunge limfukuze Ndugai na limnyime mafao yake kwa utoro bungeni
Yaani kuna mambo mengine hayaingi akilini, kutoka uspika alafu unakuwa mb, unakaa unagonga meza, unaomba sijui barabara, kisima cha maji jimboni mwako
Ahh kama mimi ndiye job nauachia huo ubunge najipumzikia

Ova
 
Kijifungia ndani hakutakusaidia mzee wangu. Unaweza jiletea magonjwa mengi kutokana na msongo wa mawazo. Tunajua fika hukutafajia hili lililotokea lakini binadamu wote hatujui kesho yetu.
Yaliyokutokea yamekua funzo kwetu kwamba vyeo na dhamana tulizopewa si za milele. Zinaweza kukoma muda wowote tena pale tusipotarajia. Jipige moyo konde utoke hadhari maisha yaendelee.
Uliyotukosea watanzania ukiwa spika wa bunge ni makubwa kuliko kosa lililokuondoa kwenye kiti. Utafanya vizuri kama utatoka hadharani pia utuombe radhi. Ukifanya hivyo nakuhakikishia mzee wangu utaishi kwa amani zaidi kuliko hata ulipokua na cheo. Toka hadharani acha kujificha. Tumejiandaa kukupokea kwa upendo tulojaliwa.

Kama kizuizini pia atoke bila amri
Hatuwezi kujua alipo
Hata wakati wa JKN wengi waliwekwa huko na wengi nje ya nchi
 
Issue ya Spika Ndungai si ndogo. Either itabidi gharama ya uchaguzi jimboni kwake au akabembelezwe! Hili kurudi bungeni ni gumu mno na itakuwa mara ya kwanza kihistoria kwa spika mstaafu!

I think issue yake ilipelekwa kihasira mno na kuli manage thereafter ni mtihani mgumu. Pamoja na wengi hatupendi mwenendo wa Ndugai lakini mwisho wake ktk hili utamjenga yeye zaidi.

Unaweza kulazimisha ajiuzuru ila huwezi kumbeba au kumsukuma aingie bungeni! Mtego mgumu!
Hakuna mtego mgumu wowote. Ndugai ana madhambi mengi mno hasa ya matumizi ya fedha na akileta za kuleta anaweza kujikuta anakwenda kulalia kila kirago alichokuwa analalia Mbowe wakati wa kesi ya ''ugaidi'' rumande ila tofauti na Mbowe, yeye atakuwa kule kihalali kabisa. Makosa yake ni mengi na aliyafanya kwani alikuwa anajua u-kibaraka wake kwa Magufuli ulikuwa kinga. BTW sijawahi kuona nchi zenye Media za habari mbovu kama Tanzania. Hii ingekuwa imetoka nchi nyingine waandishi wangeshafuatilia na kujua alipo!
 
Yaani kuna mambo mengine hayaingi akilini, kutoka uspika alafu unakuwa mb, unakaa unagonga meza, unaomba sijui barabara, kisima cha maji jimboni mwako
Ahh kama mimi ndiye job nauachia huo ubunge najipumzikia

Ova
Mkuu hawa watu hawana hiyo jeuri. Ukiwaondoa kwenye hayo maisha ya kisiasa ya kula vya bure mtaani nakupia hawakuwezi. Yule jamaa asipokuwa na wadhifa mtaani ku-survive ni ngumu mno. Ila kweli maisha hubadilika kwa kasi sana na wakati si milele. Ni juzi juzi tu alikuwa mmoja ya watu wenye nguvu kabisa katika huu utawala.
 
Ukimya wa Job wenye dalili za kususia shughuli za bunge, kulipuka kwa Mpina huku akimshikia bango January, naona ni kama vina uhusiano fulani.

Ukiziangalia kwa jicho la tatu hoja za Mpina, utaona zimeshiba nondo, na kwa vyovyote nyuma yake wapo watu wenye kubeba siri nzito za nchi.
Ndugai nje ya mfumo wa CCM ni kama panya. Hawezi chochote. Mimi nadhani atakuwa aliugua kwa sababu ya kunyang'anywa cheo na sasa yuko India anakotibiwa mara kwa mara.
 
Mkuu hawa watu hawana hiyo jeuri. Ukiwaondoa kwenye hayo maisha ya kisiasa ya kula vya bure mtaani nakupia hawakuwezi. Yule jamaa asipokuwa na wadhifa mtaani ku-survive ni ngumu mno. Ila kweli maisha hubadilika kwa kasi sana na wakati si milele. Ni juzi juzi tu alikuwa mmoja ya watu wenye nguvu kabisa katika huu utawala.
Lazima viongozi wetu wajifunze kuishi
Baada ya uongozi
Lazima wakubali matokeo

Ova
 
Vikao vitatu bado saana mjomba. Ndiyo kwanza kikao cha kwanza.

Pitieni kanuni za bunge zipo google huko
Tofautisha kati ya kikao cha Bunge na mkutano wa Bunge Ndugu. Joshua Nassari unakumbuka alivyofukuzwa!?
 
Ndugai hawezi kwenda Bungeni tena kwa sababu mshahara na marupurupu bado analipwa na hakuna wa kuhoji hata akifutwa Ubunge vyote atapata maana mitego yao haipo wazi kwetu...karma imefanya kazi kwa kauli zake alizokua anatoa na kunyanyasa Watumishi wenzie mwacheni augulie maumivu ya kudumu..
 
Job Ndugai yuko nyumbani ila kila kikao cha bunge analipwa posho na mshahara unaingia bank kila mwezi.

Tanzania nchi hii ni ngumu sana.
Nchi haina Ugumu wowote bali Tatizo ni VIONGOZI tuliwachagua tukiwa VIPOFU sasa tunamtafuta tukiwa Vichaa
 
Back
Top Bottom