Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Bunge la Tanzania leo Jumatano, Januari 28, 2026 limewathibitisha wabunge, Deo Mwanyika, Cecilia Pareso na Najma Murtaza Giga kuwa wenyeviti wa Bunge.
Watatu hao wamethibitishwa baada ya Spika wa Bunge, Mussa Zungu kuwahoji wabunge kama wanaafiki kuwa wenyeviti. Wabunge hao waliteuliwa na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) hivi karibuni kuwa wagombea wa nafasi hizo.
Mwanyika ambaye ni Mbunge wa Njombe Mjini pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo. Giga ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama huku Pareso akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo.
Giga anashika nafasi hiyo kwa kipindi cha tatu mfululizo. Mwanyika cha pili huku Pareso akiwa ni kipindi cha kwanza, ambapo katika Bunge la 12 alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).