Bunge letu lina wataalam wa uchumi wangapi? NI kweli kwamba yupo mmoja pekee?

Bunge letu lina wataalam wa uchumi wangapi? NI kweli kwamba yupo mmoja pekee?

Kwanini tunaaminishwa kwamba mtaalamu na msomi wa uchumi NI mmoja tu Bungeni? Kama waziri wa Fedha ndiye mchumi pekee kwenye Bunge zima hoja za kiuchumi zitajadiliwa vipi?

Kwanini nchi ikubali kuwa na mchumi mmoja Tu na anayeamini yeye ndiye mtaalam wa uchumi na kwamba mtu mwingine yeyote atakayetaka kujadili uchumi lazima ajadili Kwa staha asimkwaze mchumi mbobevu?

Je, Kwa kiburi hiki na mwendo tunakwenda nao endapo mchumi mbobevu akikose haiwezekani wote tukawa tumekosea?
Tunae Dr. Kimei aliyewahi kuwa CEO wa CRDB BANK ni mbunge wa Vunjo. Mwigulu hamgusi Kimei katika nyanja yoyote kwenye masuala ya fedha na uchumi
Je, Kwa kiburi hiki na mwendo tunakwenda nao endapo mchumi mbobevu akikose haiwezekani wote tukawa tumekosea?
Moja ya tatizo linaloikabili nchi yetu ni kwamba wenye maarifa na uwezo ni waoga na hawana uthubutu lakini vilaza ndio wana confidence sana ndio maana tunaishia kuwa na viongozi wa type ya bashite na babu tale
Mwisho, kusoma uchumi ndiyo kujua uchumi? Kama ndivyo kwanini wasomi WA uchumi wanaishi Kwa kutegemea kuajiriwa kuliko kuibadili uchumi uwe fursa waweze kuajiri? Mbona wachumi hakuna sehemu wanaonekana kuwa wawekezaji wakubwa?
Uchumi kama ilivyo taaluma zingine uwezi kufanya mageuzi kama haupo kwenye nafasi ya kufanya maamuzi hizi unategemea mhitimu wa chuo wa mwajiriwa wa kawaida tu benki ndio haibadili hali ya uchumi wa nchi? Kuhusu wachumi kuwa wawekezaji wakubwa wapo wengi tu fatilia vizuri taarifa zako
Kwanini tuamini MTU anayetegemea salary anaweza kufikiri sawasawa juu ya kundi kubwa la watu wanaowaza kujiajiri?
Mamlaka ya uteuzi inamteua yoyote ambae inaona anafaa
 
Tuliwaambia tuweke kanuni ama sheria kwamba Mbunge awe na walau shahada moja hata kama ni ya sanaa mkagoma.
Chawa wa mama ukiwaambia katiba mpya akili yao yote inajua ni kupunguza nguvu ya chama tawala kitu ambacho kitaongeza uwezekano mkubwa wa upinzani kuchukua madaraka.. mambo kama waziri sio lazima awe mbunge, mbunge awe na angalao degree moja(kwa sasa sifa ni kujua kusoma na kuandika tu) hayo wao hawayajui
 
waziri anaposimama kujibu hoja ujue nyuma yake kuna mijitu mibobevu imedadavua na kumpa taarifa... lakini mbunge anaweza hata akapewa taarifa za uongo kwa sababu haja ya wabunge wengi hasa wa ccm ni cheap popularity ili waonekane wateuliwe tu.
Tusisahau pia mamlaka za serikali za Afrika ni mabingwa wa kupika data
 
Waziri wa fedha asiwe na uwezo wa kupata taarifa za uchumi ambazo Kimsingi zinatayarishwa na idara na taasisi zilizo chini ya wizara yake?

Alipojibu hivyo hakuonesha jazba yoyote ila alionesha kushangazwa na vijiutafiti uchwara visivyotoa hali halisi ya uchumi na wanaotoa vijiutafiti hivyo wanajua wanapotosha. Kinachomuuna yeye Taaluma anayoipenda na kuiheshimu kuona inajadiliwa kimzaha mzaha
Jamaa ana kiburi, sisi sio wachumi hila sote tunajua kwamba gharama za maisha zimepanda, alitakiwa akae ndani na wataalamu wengine kujua hizo gharama ziashuka vipi.

Ni dharura kama kupunguza kodi kubana matumizi n.k. lakini kila siku jamaa akibanwa anadai yeye ndio professional wa uchumi, wakati watu wana surfer, kwanini asitumie professional vizuri kuleta unafuu mtaani.
 
Kwanini tunaaminishwa kwamba mtaalamu na msomi wa uchumi NI mmoja tu Bungeni? Kama waziri wa Fedha ndiye mchumi pekee kwenye Bunge zima hoja za kiuchumi zitajadiliwa vipi?

Kwanini nchi ikubali kuwa na mchumi mmoja Tu na anayeamini yeye ndiye mtaalam wa uchumi na kwamba mtu mwingine yeyote atakayetaka kujadili uchumi lazima ajadili Kwa staha asimkwaze mchumi mbobevu?

Je, Kwa kiburi hiki na mwendo tunakwenda nao endapo mchumi mbobevu akikose haiwezekani wote tukawa tumekosea?

Mwisho, kusoma uchumi ndiyo kujua uchumi? Kama ndivyo kwanini wasomi WA uchumi wanaishi Kwa kutegemea kuajiriwa kuliko kuibadili uchumi uwe fursa waweze kuajiri? Mbona wachumi hakuna sehemu wanaonekana kuwa wawekezaji wakubwa?

Kwanini tuamini MTU anayetegemea salary anaweza kufikiri sawasawa juu ya kundi kubwa la watu wanaowaza kujiajiri?

Yeye mwenyewe akubali kujiajiri atakubali kuwa na watu wanaotaka kujiajiri? Au kwake Tozo na makodi makubwa huku akipitosha ununuzi wa magari ya anasa?

Tujadili wachumi wetu na kama tuna upungufu basi Bora tuchukue wachumi nje ambao awatatufokea Kwa kuangalia vyeti walivyopewa chuo wakidhani uchumi ni performance ya darasani.
Mimi mpaka kesho natamani Kimei awe Waziri wa fedha kwa CV inambeba na experience anayo.
 
Tusisahau pia mamlaka za serikali za Afrika ni mabingwa wa kupika data
ndiyo wasomi wabobevu tulionao hao. research zao vyuoni ni za kudesa, unategemea wanaweza wakaresearch wakatoa data halisi?
 
ndiyo wasomi wabobevu tulionao hao. research zao vyuoni ni za kudesa, unategemea wanaweza wakaresearch wakatoa data halisi?
Wabobevu waliopo nyuma ya pazia wanaweza kuwasilisha taarifa sahihi tatizo zikishafikishwa kwa wanasiasa mfano ripoti ya CAG iliyogundua trilioni 1.5 matumizi yake hayajulikani tunaona kilichotokea baada ya ile ripoti kufika kwenye mikono ya wanasiasa
 
hii nchi ni ya ajabu sana
 
Back
Top Bottom