Wakuu Nina miaka sisikilizi bunge na Jana nikabahatika kusikiliza Sina uhakika kama lilikuwa live au ni marudio ya miaka ya nyuma huko.
Takribani dk 7 nikiwa mahali nasubiria kupata huduma zilitosha kabisa kujua kumbe tangu niache kusikiliza bunge Hadi Leo Bado vitu vilevile vinajadiliwa bungeni?
Kinachojadiliwa ni maji, barabara nk. Zaidi ya yote wabunge walio wengi umri umeenda sana ni Wakati Sasa wakuwaachia vijana waingie bungeni nao tuone mawazo Yao.
Itoshe Kwa kusema hakuna maoni au plan za miaka 5-100 ijayo kuwa Taifa hili litakuwa na uchumi au litakuwa limepiga hatua zipi ni hakuna.
View attachment 3299706