Wanabodi,
Kama kawa kila nipatapo fursa, huja na makala zangu hizi za kwa maslahi ya taifa ambazo ziko kwa mfumo wa maswali, halafu majibu utayatoa mwenyewe wewe msomaji.
Maswali ya leo ni Bunge Letu ni Bunge la Hovyo? Bunge Letu Linafanya Uhuni? Wabunge Wetu ni Wahuni? Tumshauri Spika Aanze Kuita Watu Kwenye Kamati, au Waachwe Tuu?.
Maswali haya ni kufuatia mkutano wa jana na waandishi wa habari
Bandari na DP World: Dkt. Slaa asema ni uuzaji wa Nchi. Adai Serikali iliyopo ina uhalali wa wasiwasi
Baada ya kuzisoma hizo hoja, kabla sijaandika, nikatafuta kwanza clips ili kujiridhisha ni kweli maneno haya ameyamtaka kweli?, maana fani ya uandishi wa habari siku hizi imevamiwa, kuna waandishi wa habari wa kila aina kuanzia comedians, wasanii, na waandishi wengine wa hovyo sana, usipokuwa makini, sometimes waandishi hawa wa habari wa hovyo hovyo, hawachelewi kukulisha maneno!, hivyo nikamsikiliza mwanzo mwisho
na kujirishisha kuwa ni kweli maneno hayo ameyasema, na sio tuu ameyasema, bali pia ameyaandika kwanza kisha akaja kutusomea sisi waandishi wa habari.
Kabla sijaendelea, naomba kuwakuwakumbusha wasomaji wangu, tujifunze kutofautisha definite statements na maswali. Hakuna statement kwenye bandiko hili, ni bandiko la swali!. Natoa angalizo hili kwasababu mimi mwenzenu nimeisha wahi kuitwa all the way from Dar to Dodoma, kufika kule nikaulizwa kwanini umetoa hii statement?, Nikajibu hiyo sio statement ni swali!. Hivyo hapa nasisitiza hili ni bandiko la swali sio bandiko la statement!.
Dr. Slaa ameliita Bunge Letu ni Bunge la Hovyo, na kilichofanyika kuridhia IGA ni uhuni?, ndio maana nauliza waungwana humu, hiki alichokisema Dr. Slaa kinaukweli kuhusu Bunge letu ni Bunge la hovyo?. Kilichofanywa na Bunge letu kuridhia IGA ya DPW ni uhuni?. Wanaofanya uhuni ni wahuni, jee Wabunge wetu ni Wahuni?.
Bunge letu Tukufu haliwezi kudhalilishwa hivi tukanyama!, jee tumshauri Madam Spika aanze ule utaratibu kama wa mtangulizi wake kuita watu kwenye Kamati, watu wowote watakao toa kauli za kulidhalilisha Bunge, au waachwe tuu kwasababu wanatoa maoni yao kwa mujibu wa ibara ya 18 ya katiba kuhusu uhuru wa kutoa maoni?.
Nashauri Daktari aitwe mbele ya Kamati!. Mimi nilipouliza tuu , hili swali
Je, Bunge letu tukufu linajipendekeza kwa Serikali? niliitwa Bungeni kuhojiwa na kamati!, sasa leo Bunge linaitwa la hovyo!, na kilichofanyika ni uhuni!, mtu huyu hawezi kuachwa hivi hivi tuu au aitwe mbele ya kamati kuthibitisha kauli yake?.
Na ikitokea asipoitwa, jee hii haitaaminisha alichosema ni kweli?, ndio maana nawauliza waungwana humu, jee ni kweli Bunge letu ni Bunge la hovyo?. Jee ni kweli kilichofanyika kwa Bunge kuridhia hii IGA ya serikali yetu na Mwarabu wa Dubai ni uhuni?. Mtu anayefanya uhuni ni muhuni, jee waheshimiwa wabunge wetu ni wahuni?.
Paskali