Bunge limepitisha tozo kwa wote badala ya bima kwa wote

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Bima kwa watu wote sio mchezo mchezo kama huu. Watu wetu wanaugua sana kutokana na mbu wengi, funza wengi, ajali nyingi, takataka nyingi mitaani na majumbani, ukosefu wa chakula, ukosefu wa maji safi, matuzi ya Kuni, nyumba duni na bidhaa zisizo na ubora.

Huwezi kuwekea mtu bima ambae unajua ataugua TU. Hata bima za magari zisingekuwapo kama wangekuwa na uhakika kuwa magari mengi yatapata ajali.

Kila mtu akiwa na bima utashuhudia misululu mirefu sana ya wagonjwa kwenye vituo vya afya hadi washangae. Hiduma zitakuwa duni sana kutokana na uhaba wa wafanyakazi, dawa, vifaa tiba na majengo.

Wanataka pesa zao sio bima zao.

Boresha mazingira yao kwanza kabla ya bima zao.
 
Huo ndio ukweli! Hakuna mtu mwenye uchungu na afya ya mtu mwingine, wanachopigia hesabu hapo ni makusanyo tu na wakiona wagonjwa ni wengi kushinda fedha za bima walizokusanya utasikia mambo kama;

Bima yako haivuki zahanati ya Mtaa/Kijiji au ili utibiwe lazima upate barua ya Mwenyekiti wa Mtaa /Kijiji😂😂🤣🤣
 
Bima kwa watu wote sio mchezo mchezo kama huu. Watu wetu wanaugua sana kutokana na mbu wengi, funza wengi, ajali nyingi, takataka nyingi mitaani na majumbani, ukosefu wa chakula, ukosefu wa maji safi, matuzi ya Kuni, nyumba duni na bidhaa zisizo na ubora...
Tanzania sio ya kwanza kuwa na bima Kwa wote hapa Afrika na kote huko hakuna misururu ya watu.

Mimi Nina bima ila Kwa mwaka huu nimeenda hospital haizidi mara 3 au 2 tuu Sasa sijui unadhani kwenda hospital ni sifa au ikoje.
 
Unapotosha, wewe unakula vizuri, unanawa mikono baada ya haja kubwa na kabla ya kula, unalala kwenye chandarua, uko mjini hakuna nyoka Wala mbung'o, watoto wako hawaogelei kwenye madimbwi ya maji machafu. 80% ya watanzania wanaishi vikijini kusikokuwa na maji, vyandarua, viatu, vyoo, na hata watumishi wa afya hawapendi kwenda huko.
 
Hata Marekani hakuna bima kwa wote kaka, Obama care inasuasua.
 
Bima kwa watu wote sio mchezo mchezo kama huu. Watu wetu wanaugua sana kutokana na mbu wengi, funza wengi, ajali nyingi, takataka nyingi mitaani na majumbani, ukosefu wa chakula, ukosefu wa maji safi, matuzi ya Kuni, nyumba duni na bidhaa zisizo na ubora.

Huwezi kuwekea mtu bima ambae unajua ataugua TU. Hata bima za magari zisingekuwapo kama wangekuwa na uhakika kuwa magari mengi yatapata ajali.

Kila mtu akiwa na bima utashuhudia misululu mirefu sana ya wagonjwa kwenye vituo vya afya hadi washangae. Hiduma zitakuwa duni sana kutokana na uhaba wa wafanyakazi, dawa, vifaa tiba na majengo.

Wanataka pesa zao sio bima zao.

Boresha mazingira yao kwanza kabla ya bima zao.
That true ,kila mtu anaumwa ila kwa hawana access na matibabu wengi wao huamua kuvumilia sasa ngoja tuone hii hata mtu akipata mikwaruzo ya tu ataenda hospital
 
Unapotosha, wewe unakula vizuri, unanawa mikono baada ya haja kubwa na kabla ya kula, unalala kwenye chandarua, uko mjini hakuna nyoka Wala mbung'o, watoto wako hawaogelei kwenye madimbwi ya maji machafu. 80% ya watanzania wanaishi vikijini kusikokuwa na maji, vyandarua, viatu, vyoo, na hata watumishi wa afya hawapendi kwenda huko.
Huyu aliyetoa mada amekuzidi sana ,hoja zake zinaeleweka tu kwa wenye uelewa
 
Bima kwa watu wote sio mchezo mchezo kama huu. Watu wetu wanaugua sana kutokana na mbu wengi, funza wengi, ajali nyingi, takataka nyingi mitaani na majumbani, ukosefu wa chakula, ukosefu wa maji safi, matuzi ya Kuni, nyumba duni na bidhaa zisizo na ubora.

Huwezi kuwekea mtu bima ambae unajua ataugua TU. Hata bima za magari zisingekuwapo kama wangekuwa na uhakika kuwa magari mengi yatapata ajali.

Kila mtu akiwa na bima utashuhudia misululu mirefu sana ya wagonjwa kwenye vituo vya afya hadi washangae. Hiduma zitakuwa duni sana kutokana na uhaba wa wafanyakazi, dawa, vifaa tiba na majengo.

Wanataka pesa zao sio bima zao.

Boresha mazingira yao kwanza kabla ya bima zao.
Hiki ndicho kinaenda kutokea.
Wewe fikiria elimu ya msingi bure tu ambayo si kila mtanzania ana access nayo imewashinda hadi kuna watoto wanasoma chini ya mti, unadhani wataweza bima kwa kila mtanzania. Hapa ni ukusanyaji wa maokoto
 
Waboreshe kwanza huduma za afya katika hospitali zao, kabla ya kukimbilia huko kwenye bima ya afya kwa wote.
 
018100094042.JPG
 
Unapotosha, wewe unakula vizuri, unanawa mikono baada ya haja kubwa na kabla ya kula, unalala kwenye chandarua, uko mjini hakuna nyoka Wala mbung'o, watoto wako hawaogelei kwenye madimbwi ya maji machafu. 80% ya watanzania wanaishi vikijini kusikokuwa na maji, vyandarua, viatu, vyoo, na hata watumishi wa afya hawapendi kwenda huko.
Unapotosha, wewe unakula vizuri, unanawa mikono baada ya haja kubwa na kabla ya kula, unalala kwenye chandarua, uko mjini hakuna nyoka Wala mbung'o, watoto wako hawaogelei kwenye madimbwi ya maji machafu. 80% ya watanzania wanaishi vikijini kusikokuwa na maji, vyandarua, viatu, vyoo, na hata watumishi wa afya hawapendi kwenda huko.
Waoingaji wa Kila kitu Huwa hamkosekani.

Kati ya wanaokula vizuri na ambao hawali vizuri Kwa maelezo Yako wapi walipukutishwa na uviko 19? Tanzania sio ya kuzungumzia misosi.

Mwisho idadi ya maskini wasio na uwezo watatambuliwa na wengine lazima kuchangia.

Hao Maskini watalipiwa na Serikali Kupitia mfuko maalumu.
 
That true ,kila mtu anaumwa ila kwa hawana access na matibabu wengi wao huamua kuvumilia sasa ngoja tuone hii hata mtu akipata mikwaruzo ya tu ataenda hospital
Anataka akaitumie ela yake isipotee bure. Atakwenda hospital akapate dawa za akiba. Tunashindwa kusafisha miji yetu iwe misafi sembuse bima kwa wote? Tunashindwa kuhakikisha bodaboda wanavaa helmets sembuse bima kwa wote? Watu wetu wanachangia maji na fisi sembuse bima kwa wote, nyumba hazina madirisha, over clouding, nk kampuni gani ya bima itakubali kuwawekea bima watu wanaokunywa gongo Na kula madawa ya kulevya?

Tunashindwa kuendesha mabasi ya mwendokasi dar es salaam sembuse bima kwa watu wote?
 
Waoingaji wa Kila kitu Huwa hamkosekani.

Kati ya wanaokula vizuri na ambao hawali vizuri Kwa maelezo Yako wapi walipukutishwa na uviko 19? Tanzania sio ya kuzungumzia misosi.

Mwisho idadi ya maskini wasio na uwezo watatambuliwa na wengine lazima kuchangia.

Hao Maskini watalipiwa na Serikali Kupitia mfuko maalumu.
Watanzania wanaotegemea kilimo Cha mvua wako wangapi? Wafugaji wanaotafuta malisho ya kuhamahama wako wangapi? Je, mvua za kilimo na kuotesha malisho zipo? Watapata hela y kuchangia bima wakati ya kununua chakula na chumvi hawana?
 
Tanzania sio ya kwanza kuwa na bima Kwa wote hapa Afrika na kote huko hakuna misururu ya watu.

Mimi Nina bima ila Kwa mwaka huu nimeenda hospital haizidi mara 3 au 2 tuu Sasa sijui unadhani kwenda hospital ni sifa au ikoje.
Wewe ndo unampotosha Rais Samia kwenye hili. Nguvu kubwa lazima ielekezwe kwenye kuwakinga watu wasiugue kuliko kwenye tiba. Mkwezi wa minazi anaekwea minazi akiwa amelewa na bila kuvaa helmet unampa bima gani? Serikali tumieni Kodi za watanzania kutokomeza malaria, kipindupindu, funza, minyoo ya tumboni, typhoid, TB, HIV, utapiamlo, trachoma, mabusha na matende, madawa ya kulevya, uvutaji sigara, surua ili watu wasiugue wengi mara kwa mara kwanza ndio mje na bima ya afya kwa wote.
 
Bima kwa watu wote sio mchezo mchezo kama huu. Watu wetu wanaugua sana kutokana na mbu wengi, funza wengi, ajali nyingi, takataka nyingi mitaani na majumbani, ukosefu wa chakula, ukosefu wa maji safi, matuzi ya Kuni, nyumba duni na bidhaa zisizo na ubora.

Huwezi kuwekea mtu bima ambae unajua ataugua TU. Hata bima za magari zisingekuwapo kama wangekuwa na uhakika kuwa magari mengi yatapata ajali.

Kila mtu akiwa na bima utashuhudia misululu mirefu sana ya wagonjwa kwenye vituo vya afya hadi washangae. Hiduma zitakuwa duni sana kutokana na uhaba wa wafanyakazi, dawa, vifaa tiba na majengo.

Wanataka pesa zao sio bima zao.

Boresha mazingira yao kwanza kabla ya bima zao.
Sawasawa 👍 👍
 
Huo ndio ukweli! Hakuna mtu mwenye uchungu na afya ya mtu mwingine ,wanachopigia hesabu hapo ni makusanyo tu na wakiona wagonjwa ni wengi kushinda fedha za bima walizokusanya utasikia mambo kama;

Bima yako haivuki zahanati ya Mtaa/Kijiji au ili utibiwe lazima upate barua ya Mwenyekiti wa Mtaa /Kijiji😂😂🤣🤣
Sio mtu mwingine, sema Mnyonge. Wao mafua wanayapeleka India, South Africa-wanatmia mabilioni ya kodi zetu. Hayo makusanyo hayaendi Afya, ni kwny hayo mambo ya mafao ya wenza na mengne yenye kuwafraisha. Fikria jinsi wasio na uwezo wanavoteseka na hakna anayejali! Ngja uone hiyo Bima yao italeta nn, ufisadi mtupu, aibu
 
Hiki ndicho kinaenda kutokea.
Wewe fikiria elimu ya msingi bure tu ambayo si kila mtanzania ana access nayo imewashinda hadi kuna watoto wanasoma chini ya mti, unadhani wataweza bima kwa kila mtanzania. Hapa ni ukusanyaji wa maokoto
Kila shule ya msingi upewa tsh 150,000 kila mwezi, eti hiyo ndio elimu bure.
 
Wewe ndo unampotosha Rais Samia kwenye hili. Nguvu kubwa lazima ielekezwe kwenye kuwakinga watu wasiugue kuliko kwenye tiba. Mkwezi wa minazi anaekwea minazi akiwa amelewa na bila kuvaa helmet unampa bima gani? Serikali tumieni Kodi za watanzania kutokomeza malaria, kipindupindu, funza, minyoo ya tumboni, typhoid, TB, HIV, utapiamlo, trachoma, mabusha na matende, madawa ya kulevya, uvutaji sigara, surua ili watu wasiugue wengi mara kwa mara kwanza ndio mje na bima ya afya kwa wote.
Kwani bima itajielekeza kwenye tiba kuliko Kinga?

Serikali inafanya hivyo daily na mfano makazini Kuna sera ya mazoezi lakini pia unaona wanatoa vyandarua Bure,wanatafuta chanjo ya malaria,wanapeleka maji kwenye maeneo yote ya jamii Ili usafi uzingatiwe nk

Na ndio maana vifo vya Watoto wadogo na uzazi vimepungua , Changamoto ya Sasa ni Magonjwa yasiyoambukiza yanaletwa na mtindo wa Maisha Nako huko kampeni zimeanza.
 
Back
Top Bottom