Bunge linaloanza leo litakuwa kama Bunge la Katiba baada ya UKAWA kususa, tutegemee kuibuka akina Othman!

Bunge linaloanza leo litakuwa kama Bunge la Katiba baada ya UKAWA kususa, tutegemee kuibuka akina Othman!

Nalifananisha bunge la Ndugai linaloanza leo sawa na lile bunge la katiba baada ya UKAWA kususia wakiongozwa na Prof Lipumba.

Tutegemee mambo mengi mazuri na mengi ya kushangaza lakini zaidi ni kuibuka watu aina ya aliyekuwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar mh Othman kadhalika aliyekuwa mbunge wa Chadema mh Arfi.

Upinzani watakuwa na wabunge 26 endapo wabunge wa viti maalumu 19 kutoka Chadema wataapishwa.

Lakini wabunge wa darasa la 7 wanaweza kufichwa kabisa kwa sababu bunge hili halitakuwa na zomeazomea, mipasho wala vijembe kwa sababu limesheheni full kijani.

Maendeleo hayana vyama!

Pamba upambavyo ila Ukweli unabaki kuwa ni Ukweli tu ,na Ukweli mara nyingi huwa ni Kanuni na Kanuni hupitia hatua ili kutoa Majibu sahihi.CCM mmesahau hatuwezi kufanana kimawazo kimtizamo na hata namna yetu ya kutatua Changamoto zetu ,Bunge la Chama kimoja linalo amriwa mambo yake kutoka Ikulu haliwezi kuwa na Matokeo chanya.

Alie wahi kuwa mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Pf Assad amewahi kulisema hili mkamuahidi Pingu ,sasa nyie jipambeni mtakavyo weza Wananchi wenu wanahitaji Matokeo ya Maendeleo ya kasi mliyo yaahidi kwa sababu kwa sasa hakutokuwa na wa kuwpainga.
 
CHADEMA wameshawapa go ahead mahawara wao waende Bungeni sema watajifanya kama vile Kamati kuu haijaridhika ili kuwazubaisha CHADEMA lia lia, si unaona sasa hivi hawaongelei tena Urais wa Tundu washahamia kwny issue ya viti maalum
Chadema wamegoma kuunga mkono uharamia wa dikteta, dikteta ateue wabunge 10 kutoka NCCR Mageuzi wakaunde KUB
 
Binafsi nafkiri hili suala la uwiano wa wabunge katika bunge linalojiita la mchanganyiko wa vyama vingi, ilipaswa uwiano wake uwe na kanuni ya kuweka idadi kuanzia kwenye majimbo! Asilimia ya majimbo kwa chama tawala isizidi 50%, na percentage inayosalia iwe kwa ajili ya upinzani tu!
Pia viti maalum viwe kawa ajili ya vyama vilivyokosa majimbo au vilivyopata majimbo machache!
lakini kwa hali ilivyo sasa bunge letu halileti maana katika uwiano sahihi wa bunge la vyama vingi!
 
Kikwete hakumteua Mbatia 2012 au ulikuwa bado mchanga?
Naona uko out na ninavyofikiria mimi.

Mimi nilikuwa nazungumzia viti maalumu vya Wanawake. Sio vya Rais ndio msingi ulikuwa hapo.

Soma tena hapo. Penye screen shot
Screenshot_20201110_075753~2.jpg
 

Attachments

  • Screenshot_20201110_075753.jpg
    Screenshot_20201110_075753.jpg
    24.3 KB · Views: 9
Hatimaye bunge limepata tena salamu ya pamoja.....
 
Back
Top Bottom