Unajua ukweli mchungu ni kwamba, Mwalimu ndie ""aliiuza Tanganyika kwa ZNZ...
Mwalimu alikubali ku-sacrifice mambo mengi sana ya Tanganyika for the sake of Muungano...
Tena nikisema "alikubali ku-sucrifice" itakuwa ni kama nakosea kwa sababu, I'm certain ni yeye mwenyewe na timu yake ndie waliweka mezani ita-sacrifice ni na nini, na ZNZ atapata nini ili aweze kumshawishi Karume!!!
Moja ya sacrifice ndo kama hizi za huku haruhusiwi kumiliki ardhi kule lakini wa kule anaruhusiwa kumiliki ardhi huku...
Hata kwenye mgawanyo wa ajira mambo ndo yapo hivyo hivyo..
So, my friend, usishangae siku ukija kuambiwa kwamba hata huo mgawanyo umezingatia Sheria ya Mgawanyo wa Pesa za Mkopo!!!
Unajua hili tunaloona ni balaa la SSH kuipendelea ZNZ chimbuko lake ni Serikali ya JK ambayo ilimteua SSH kama Waziri anayeshughulikia Kero za Muungano!!
Sasa SSH akiwa waziri alifanikiwa kuyaona "madudu yetu yoooooote" ya kujipendekeza ili tuwe na muungano! Kule ndiko akajua ZNZ anapata nini na nini ambayo wala haikuzingatia population proportionality!!
Itoshe tu kusema kwamba WE SACRFICED A LOT FOR THE UNION!!
Sasa kama mwalimu ndiye alie scrifice tanganyika kwa Zanzibar, mbona wazanzibari walipotaka kuvunja muungano Lukuvi alisema hatuwezi kuicha Zanzibar lazima tutaishikilia?
Lakini pia fahamu kwamba Zanzibar ni visiwa sio kama huko ubarani eneo lake la ardhi hata hawo wazanzibari wenyewe haliwatoshi kumiliki ardhi lakini utashangaa bado kuna wanyamwezi kibao kutoka bara kule wako wamepewa mashamba wanalima viazi vitamu, wanafanya biashara mbali mbali., Nyerere kama aliyoona Zanzibar ni ndogo kwanini alilazimisha kuungana hivyo hivyo?
Zanzibar ndio nchi pekee duniani ambayo wananchi wake wanalipa kodi mara mbili - wanalipa kupitia ZRB kwa maslahi ya Zanzibar wenyewe lakini TRA kwa maslahi ya tanganyika tu, kodi ndizo zinazowapa mdomo tanganyika na kulipana mishahara yao na maposho yao wanayolipana na chakula chao.
BOT asili yake Zanzibar ndio walitoa fedha nyingi zaidi za kigeni kuanzishwa kwake lakini leo BOT inaonekana ni zao la Tanganyika pekee,
Mabalozi walioko nje huko ambao wanaiwakilisha tanzania karibu wote ni wanyamwezi kutoka bara, hakuna mzanzibari hata mmoja na Zanzibar mpaka leo ikijaribu kutaka mashirikiano na nchi nyengine kibali lazima kitoke tanganyika hivi ndivyo namna huyo nyerere wako alivyotaka kuimeza zanzibar mpaka leo., Tanganyika inafaidika kupitia mgongo wa Zanzibar ndio mana hamtaki kuachia.,
Sasaivi Mama amekuwa rais kwa mujibu katiba kwa kile kilichotokea basi kina Ndugai kelele kibao na ni miezi 9 tu sasa., wakati nyinyi mumekuwa mnaongoza serikali ya muungano peke yenu mwaka wa 60 sasa njaa tupu.,