Bunge linalotegemewa kupitisha Sheria za Nchi lasema limebaini dosari kwenye upitishaji wa sheria ya kumiliki laini zaidi ya 1

Bunge linalotegemewa kupitisha Sheria za Nchi lasema limebaini dosari kwenye upitishaji wa sheria ya kumiliki laini zaidi ya 1

Mitandao yenyewe ya simu wanaota huuduma kama wanavyotaka wao, bei elekezi ya matumizi ya mitandao ya simu haijawahi elezwa ni ipi halafu wanataka kutumia line moja.

Wakimaliza hapo warudi na kwenye blog nako watazame madhara ya hiyo sheria,wengi wameinyamazia kwa sababu tu ilishapitishwa na walojaribu kwenda mahakamani walishindwa kesi,ila kisiasa ina madhara makubwa kwa sababu wale ambao angalau walikuwa wanapata hata hela ya kula mchana sasa hawapati tena kwa sababu vitangazo vyao havipostiwi tena katika blog.

Pia kuna haja kabla ya sheria hizi kupitishwa rasmi,wawe wanazifanyia majaribio na kuona madhara yake katika jamii,kwa sababu sheria kama ya matumizi ya laini za simu kuwa ngapi bado haina madhara makubwa kwa jamii,mfano mtu ana line moja lakini bado atakwambia ile hela tuma kwa namba hii,huyo ndo mtu wa kudeal nae mara moja hasa katika ulimwengu wa teknolojia huendeshwa kiteknolojia zaidi kuliko sheria za kubanana banana.
 
Wakati mwingine unashangaa, sheria kama hii ya laini zaidi ya moja kwa mtandao inaletwa kutatua shida gani? What mischief is it trying to stop?
 
BUNGE limebaini dosari katika utungaji wa sheria ndogo nchini, ikiwamo sheria inayoweka zuio kwa Mwananchi kuwa na laini ya simu zaidi ya moja

bungee.jpg

Akiwasilisha bungeni jijini hapa jana, taarifa ya Kamati ya Sheria Ndogo kuhusu uchambuzi wa sheria ndogo zilizowasilishwa katika mikutano ya 18 na 19 ya Bunge, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, William Ngeleja, alisema miongoni mwa dosari hizo ni sheria ndogo kwenda kinyume cha sheria mama na sheria nyingine za nchi.

Alizitaja baadhi ya sheria hizo kuwa ni pamoja na The Water Supply, Regulations 2019 ambayo inakwenda kinyume cha Sheria ya The Water Supply and Sanitation, 2019 na Sheria Ndogo (Ada na Ushuru) za Halmashauri za Mkinga 2019 inayokwenda kinyume cha Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa Sura 290.

Ngeleja alisema dosari ya pili ni sheria ndogo kutozingatia misingi ya uandishi wa sheria, akiwakumbusha waandishi wa sheria kuzingatia kifungu cha 25(2) cha Sheria ya Tafsiri ya Sheria kinachowataka kuzingatia majedwali kuwa sehemu ya sheria.

Mbunge huyo wa Sengerema (CCM) aliitaja dosari ya tatu kuwa ni sheria ndogo kuwa na makosa katika majedwali kwa kurejea kanuni ambazo si sahihi au kurejea kanuni ambazo hazipo.

Alisema dosari ya nne ni sheria ndogo kutoendana na uhalisia wa mambo ukiwamo urahisi katika utekelezwji wake, hali ya uchumi wa walengwa na viwango vya adhabu na faini.

Alisema Sheria ya The Electronic and Postal Communication, Regulations 2020, imeweka masharti yasiyo na uhalisia yenye zuio la mtu kumiliki zaidi ya laini moja ya simu kutoka kampuni moja ya simu.

Vilevile, alisema wamebaini sheria ndogo kukiuka haki za binadamu, akiitolea mfano Sheria ya The Transport Licensing Act (Sura 317) ambayo mtu anaweza kufutiwa leseni bila hata kupewa nafasi ya kusikilizwa.

Alisema kuwa katika mikutano hiyo miwili, kamati yao ilipitia na kuchambua sheria ndogo 2,601.
Walidhani itawabana Chadema wakiipitisha, sasa inawabana wenyewe.
 
Tunasubiri tamko hizi line zetu tuzitupeee au tuzirudishe kwao
 
Back
Top Bottom