Bunge lisitishe kusafirisha abiria usiku, hali sio shwari

Bunge lisitishe kusafirisha abiria usiku, hali sio shwari

Usiku haina shida shida ni dereva mwenyewe,tena serikali iltakiwa isisitize mabasi yaaanze safari za mikoani kuanzia saa mbili usiku ili kuongeza wigo wa ajira mfano mahotel na sector zingine zinazodeal na usafafirishaji wa abiria zitafanya kazi 24 hrs .
 
Njia za udhibiti vyombo vya moto ziongezwe, trafiki wawe wengi sana ,vifaa vya kisasa vifungwe, abiria waelimishwe wajibu wao, namba za simu ziwekwe wazi ili abiria akiona vitendo visivyafaa vya madereva iwe rahisi kupiga simu, kuwepo na vituo vingi vya ukaguzi , abiria wakitoa malalamiko kwa madereva safari isiendelee mpaka dereva abadilishwe mara nyingine dereva anaposhtakiwa anakuwa katika msongo wa mawazo na makosa ya dereva mmiliki pia awajibike moja kwa moja hii itawafanya wamiliki kutafuta madereva bora
Mkuu madereva wengi haswa malori ya mchanga ni mateja hivyo hata uweke polisi elfu kumi njiani bado ajali zitatokea tu
 
Nimesema tu, wenye mabasi waendelee kuchangia
Vinginevyo abiria wanao safari usiku wawe na Bima kubwa
Nchi zinazotuzunguka mabasi yao yanasafili usiku,ulishawahi kusikia wana ajali kama sisi,Istoshe mabasi yalisitishwa kusafiri usiku sababu ya usalama yaani ujambazi sio ajali
 
Malori yasafiri usiku na mabasi yasafiri Mchana
Nchi zingine mabasi yana safiri mchana tu mwisho saa 12 jioni usiku ni marufuku kabisa, na malori yana ruhusiwa kutembea usiku kucha, matrekta na mashine za ujenzi ni marufuku kutembea bara barani lazima vipakiwe kwenye ma trailer
 
Shida siyo muda..miundombinu ndo mibovu..barabara nyembamba sana..kujua kwa uchumi kunahitaji watu wafanye Kazi 24hrs mambo ya kuzuia watu kufanya kazi usiku ni mambo ya kiamani.mawazo yako hayapaswi kukubaliwa ata kwa chembe
 
Nchi zingine mabasi yana safiri mchana tu mwisho saa 12 jioni usiku ni marufuku kabisa, na malori yana ruhusiwa kutembea usiku kucha, matrekta na mashine za ujenzi ni marufuku kutembea bara barani lazima vipakiwe kwenye ma trailer
Nchi gani
 
Ajali hazitaisha huko na sababu zipo nyingi ila nitatoa mifano michache
Kwanza hakuna elimu kubwa wakati wa kutoa license kwa madereva

Unaweza kuletewa hata nyumbani ukitaka na hawajali
Tunataka license zipatikane kwa heshima yake na mtu awe amenolewa haswa kuwa dereva

Inatakiwa mishahara ya madereva wa malori na Mabasi yawe juu zaidi ila na license kuipata iwe tabu sana

Kuwe na theory and practical katika mtihani na wanaofundisha wawe private na kuingia mtihani unalipia sio chini ya laki 5

License ziwe kama nchi zingine yaani inakuwa na points hata 10 na kila kosa unakatwa points na hiyo itakuathiri kwenye insurance pia

Matapeli na wala rushwa wanaweza kudhibitiwa kwa kuweka private sekta wakisaidiana na police kwa kusimamisha magari mda wowote na kuyakagua

Hebu mnipe hiyo kazi miaka 3 tu kama hamjaona mabadiliko na hao watu wanaouwa hovyo hamtawaona tena na ajali ntazipunguza kwa 75% kwa miaka 2 ya kwanza

Kila kitu kinawezekana
Hawa wakuu wa vituo hawako serious na maisha ya watu
Aidha hawajali au wanakula na madereva

Hawajali hata wakifa kila siku
Mbona Magu alikomesha watekaji wa mabasi
Sasa nyie kwanini mshindwe kudhibiti ajali?

Unakamata gari halina break unapewa 30,000 unaliruhusu likaue
Matairi yana kipara unasema jichunge haya nenda kisa umepewa elfu 5

Ajali hazitaisha kwa mtindo huo
Poleni sana
 
Nyie kimbizeni magari

Endesheeni mjuavyooo

Likitokea jambo sisi ni kuzika tu na kula ubwabwa

Ova
 
Back
Top Bottom