Bunge litunge Sheria ili mali ambazo hazikuandikiwa wosia zimilikiwe na Serikali inapotokea mmiliki amefariki

Lengo la hili pendekezo ni kuwafanya wananchi wachukue hatua ya kuandika wosia na kuufanyia updates kila mara ili ikitokea mwenye mali amefariki basi taratibu za urithi zisiwe na utata.
 
Ni upuuzi
Itageuka motive for murder

Mtu ajijue atamiliki nini ukifa kwanini asikuue?.

Btw,unajua abt govt control on unclaimmed assets? Hawajalala kihivyo
Anajua vipi? Unafahamu maana ya electronic database ya kutunza wosia? Mtu anafungua akaunti online yenye muongozo wa kuandika na kuutunza wosia huko. Hakuna mtu atakayefahamu labda umfahamishe wewe mwenyewe.

Serikali inapotoa cheti cha kifo wanafanya reference na database kujua mwongozo wa mali zake.
 
Kuna migogoro mingi sana naifahamu iliyopo kwa watu ambao ni waislamu.

Nadhani nao waandike wosia kwa mujibu wa muongozo wa quran na wautunze ili iwe clear inapotokea wamefariki.
 
Halafu serikali uchukue pia jukumu la kuwatunza hao mayatima!
Hapana, sheria itakuwa inataka aliyefariki awe ameacha wosia. Kama hakuacha na lake halipo.

Lengo ni kuwafanya wananchi waandike wosia. Na kimsingi itakuwa very rare kukuta mtu hajaandika wosia kama sheria itakuwepo.
 
Mkuu Mimi mbona sijaelewa hapa, yaani Nina Nyumba yangu mke na watoto , baadaye nife ghafra halafu serikali itaifishe Mali yangu kisa sikuandika wosia!!! vipi kuhusu mke na watoto wangu?
Leo mkuu ukijua kwamba kuna hiyo sheria utaacha kuandika wosia? Hii sheria itafanya kila mtu aandike wosia.
 
Sheria pendekezwa itahakikisha kila mtu anaandika wosia na hapatakuwa na aina yoyote ya mkanganyiko kuhusu umiliki wa mali za marehemu.
 
Kwani sheria za Tanzania zinasemaje marehemu anapofariki pasipo kuacha wosia(Dying intested).
 
Serikali ihodhi mali wakati survivors wapo?
Kisa wosia tu?
 
Mkuu sijakuelewa unachojaribu kusema.

Wosia uandikwe kwa kufuata taratibu za aidha kidini au kimila. Hilo halina shida

Hoja hapa ni kutaka kila mtu aandike wosia kwa ajili ya mali atakazoacha ikiwa amekufa.

Then utaratibu utafuatwa ili aliyeachiwa kwa mujibu wa wosia apate.
 
Serikali inazidi kubuni vyanzo vya mapato.
 
Serikali ihodhi mali wakati survivors wapo?
Kisa wosia tu?
Lengo hapa ni kulazimisha kila mtu aandike wosia.

Kwamfano leo sheria ikiwepo wewe utaacha kuandika wosia?

Kama utauandika basi hakutakuwa na mgogoro ukifariki.
 
Tabu ipo pia wanaoachiwa wosia wanaficha ili waited wao au na ndugu.
 
Rita zinachakachuliwa pia, hongo zinatembea.

Serikali isichukue labda kama wapewe wenye ndoa kwa aliyebaki na watoto wa ndoa. Wao waamue iweje hata watu wa mila wakae pembeni kisheria.
 
Dini ya kiislam inaelekeza kuwa mtu anapokufa hata bila kuacha maandishi yeyote.

Basi mali zake automatically zinarithiwa na watoto..

Na kama hana mtoto,
Mali huruthiwa na ,

- wazazi wake,
--au ndugu zake wa damu.
-Mke hupewa fungu lake 1/8 ya Mali .

Kupendekeza serikali kuleta Sheria hiyo ni dhuluma..
 
Hizo sheria kule kijijini zinajulikana na kuna wanasheria wakuwaandikia wosia wa kisheria?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…