Bunge litunge Sheria ili mali ambazo hazikuandikiwa wosia zimilikiwe na Serikali inapotokea mmiliki amefariki

Bunge litunge Sheria ili mali ambazo hazikuandikiwa wosia zimilikiwe na Serikali inapotokea mmiliki amefariki

... labda kama marehemu hakuacha mtoto, mke/mume, au mzazi hapo sawa. Ila kama hao wapo hata kama hakuandika wosia how comes serikali itaifishe mali za marehemu wakati ndugu zake wa karibu wapo? It is not fair; ni wizi wa mchana kweupe!

Ambacho ninge-suggest, ni endapo marehemu hakuacha wosia na ameacha watoto na wameshindwana kufuata taratibu za kimila au kidini katika kugawana mali basi mali hiyo igawanywe sawa sawa kwa watoto wote na mke/wake regardless of gender.

Kama hajaacha watoto ila mke/mzazi/wazazi wapo (whoever exists) basi mali igawanywe sawa baina yao. Kama hajaacha yeyote katika hao na hakuna wosia, basi mali hiyo ichukuliwe na kabidhi wasii mkuu.
Lengo la hili pendekezo ni kuwafanya wananchi wachukue hatua ya kuandika wosia na kuufanyia updates kila mara ili ikitokea mwenye mali amefariki basi taratibu za urithi zisiwe na utata.
 
Ni upuuzi
Itageuka motive for murder

Mtu ajijue atamiliki nini ukifa kwanini asikuue?.

Btw,unajua abt govt control on unclaimmed assets? Hawajalala kihivyo
Anajua vipi? Unafahamu maana ya electronic database ya kutunza wosia? Mtu anafungua akaunti online yenye muongozo wa kuandika na kuutunza wosia huko. Hakuna mtu atakayefahamu labda umfahamishe wewe mwenyewe.

Serikali inapotoa cheti cha kifo wanafanya reference na database kujua mwongozo wa mali zake.
 
Kwa uoande wa Waislam hili tatizo halipo kwa sababu kila kitu kipo wazi
nani anarithi
nani harithi
anarithi kiasi/rate gani

Na ndio maana kule Uswazi, utasikia Mwanamke kama kafiwa na Mume wake anasema "Nasubiri Kisumni changu"
Sumni => 1/8 ya mali aliyoacha mumewe
Muislam atawajibika kutamka/kuandika Wasia pindi tu atakapotaka kiasi fulani cha mali aliyoacha iende nje ya familia yake (warithi halali kulingana na Qur'an na Sunnah) kama kupeleka Wakfu kwa ajili ya Watoto Yatima au Msikiti. Ambayo vilevile (hiyo thamani ya Wakfu) haitakiwi izidi 1/3 ya mali yote aliyoacha marehemu
Baada ya kuitoa hiyo mali ambayo marehemu ame dedicate kwa ajili ya Wakfu mali yote iliyobaki ratio ziko very clear, nani apate kiasi gani
Kuna migogoro mingi sana naifahamu iliyopo kwa watu ambao ni waislamu.

Nadhani nao waandike wosia kwa mujibu wa muongozo wa quran na wautunze ili iwe clear inapotokea wamefariki.
 
Halafu serikali uchukue pia jukumu la kuwatunza hao mayatima!
Hapana, sheria itakuwa inataka aliyefariki awe ameacha wosia. Kama hakuacha na lake halipo.

Lengo ni kuwafanya wananchi waandike wosia. Na kimsingi itakuwa very rare kukuta mtu hajaandika wosia kama sheria itakuwepo.
 
Mkuu Mimi mbona sijaelewa hapa, yaani Nina Nyumba yangu mke na watoto , baadaye nife ghafra halafu serikali itaifishe Mali yangu kisa sikuandika wosia!!! vipi kuhusu mke na watoto wangu?
Leo mkuu ukijua kwamba kuna hiyo sheria utaacha kuandika wosia? Hii sheria itafanya kila mtu aandike wosia.
 
Ipo sheria ya kabidhi wasii mkuu (The Administrator General Act) ambayo kwa Sasa sheria hiyo inasimamiwa na RITA, everything has been covered, Kila kitu kimeshafanyiwa kazi. Nenda google utaikuta sheria hiyo.

Haya mambo yameanza Karne nyingi zilizopita, yameanzia uingereza, yakapelekwa India, baadae katika makoloni yetu.

Japo kama hakuna wosia si lazima ziende kwa kabidhi wasii mkuu.

Wanaukoo wanaweza kuzigawa wa wanaostahili baada ya kufuata taratibu zote za mirathi,ikiwemo kikao Cha ukoo na kuthibitishwa na mahakama

Serikali na jamii Ina maslahi na Mali za wanajamii, sheria inaweka utaratibu mzuri wa kuzifanya ziwe salama kwa maendeleo ya taifa
Sheria pendekezwa itahakikisha kila mtu anaandika wosia na hapatakuwa na aina yoyote ya mkanganyiko kuhusu umiliki wa mali za marehemu.
 
Kwani sheria za Tanzania zinasemaje marehemu anapofariki pasipo kuacha wosia(Dying intested).
 
Anajua vipi? Unafahamu maana ya electronic database ya kutunza wosia? Mtu anafungua akaunti online yenye muongozo wa kuandika na kuutunza wosia huko. Hakuna mtu atakayefahamu labda umfahamishe wewe mwenyewe.

Serikali inapotoa cheti cha kifo wanafanya reference na database kujua mwongozo wa mali zake.
Serikali ihodhi mali wakati survivors wapo?
Kisa wosia tu?
 
Haya yangesemwa na mtu ambaye hajawahi kufiwa labda ingeeleweka. Yangesemwa na mtu asiyejua wizara yetu ya ardhi ifanyavo kz, angeeleweka. Nje ya hapo huenda aliyeandika ni mwajiriwa wa hiyo wizara au hajafanya utafiti wa kutosha.

Haijui hii nchi ipasavyo.
Hajui uelewa wa haya mambo kw wanaoishi vjjn ukoje, hajui ubaya/uzuri wa sheria za kimila zikoje wala hajui sheria zilizopo zimekwamia wp au kama hazitumiki, ni kw sbb gani.

Kuna migogoro kibao ya watu kunyang'anywa ardhi na kuuziwa wengine hata kbla hawajafa na hata wngn kuzuiwa kuitumia ardhi zao watakavyo. Zipo hata nyngn zlizouzwa bila taarifa.
Labda kipengele ch kuongeza mapato-iwe Kw afsa ardhi binafsi au Kw serkali, wala hili halina mahusiano yyt mazr/mabaya ktk jamii. Badala yake ni kuongeza kero tu kwa wananchi, ni kuongeza urasimu uxio wa lazma Kw waTz ambayo pia ni mojawapo wa mambo yanayotukera Kw sana. Hakuna msaada wwt watakaopata wafiwa toka serikalini. fuatilia Kw watu waliofiwa uje na mifano toshelezi, hususan vjjn halafu andka upya.
Mwisho toa mifano ya jinsi serikali itakavoongeza mahusiano mazuri kutokana na uporaji huo wa ardhi za wafiwa, bila hivo, wngn hatutakuelewa
Mkuu sijakuelewa unachojaribu kusema.

Wosia uandikwe kwa kufuata taratibu za aidha kidini au kimila. Hilo halina shida

Hoja hapa ni kutaka kila mtu aandike wosia kwa ajili ya mali atakazoacha ikiwa amekufa.

Then utaratibu utafuatwa ili aliyeachiwa kwa mujibu wa wosia apate.
 
Serikali inazidi kubuni vyanzo vya mapato.
 
Serikali ihodhi mali wakati survivors wapo?
Kisa wosia tu?
Lengo hapa ni kulazimisha kila mtu aandike wosia.

Kwamfano leo sheria ikiwepo wewe utaacha kuandika wosia?

Kama utauandika basi hakutakuwa na mgogoro ukifariki.
 
Tabu ipo pia wanaoachiwa wosia wanaficha ili waited wao au na ndugu.
 
Rita zinachakachuliwa pia, hongo zinatembea.

Serikali isichukue labda kama wapewe wenye ndoa kwa aliyebaki na watoto wa ndoa. Wao waamue iweje hata watu wa mila wakae pembeni kisheria.
 
Dini ya kiislam inaelekeza kuwa mtu anapokufa hata bila kuacha maandishi yeyote.

Basi mali zake automatically zinarithiwa na watoto..

Na kama hana mtoto,
Mali huruthiwa na ,

- wazazi wake,
--au ndugu zake wa damu.
-Mke hupewa fungu lake 1/8 ya Mali .

Kupendekeza serikali kuleta Sheria hiyo ni dhuluma..
 
Hii itasaidia kila mtu mwenye mali sehemu awe anatunza wosia na kuufanyia marekebisho mpaka siku anapofariki.

Wosia uandaliwe kwa kufuata matakwa ya kisheria na ikiwezekana kuwe na centralized electronic database ya kutunza wosia. Mahakama ndio itoe idhini ya kufungua akaunti ya marehemu kujua wosia unasemaje.

Itasaidia sana kuondoa migogoro inayofuatia baada ya mtu kuaga dunia. Itaboresha mahusiano baina ya ndugu.

Serikali itakuwa imeongeza chanzo cha mapato ikiwa watu hawataandika wosia. Kimsingi faida kubwa zaidi kwa serikali ni uwepo wa mahusiano mazuri katika jamii baada ya misiba.
Hizo sheria kule kijijini zinajulikana na kuna wanasheria wakuwaandikia wosia wa kisheria?
 
Back
Top Bottom