Bunge litunge Sheria ili mali ambazo hazikuandikiwa wosia zimilikiwe na Serikali inapotokea mmiliki amefariki

Lengo hapa ni kulazimisha kila mtu aandike wosia.

Kwamfano leo sheria ikiwepo wewe utaacha kuandika wosia?

Kama utauandika basi hakutakuwa na mgogoro ukifariki.
Sijui kwanini huelewi
Unahisi ni kwanini hadi sasa hakuna sheria kama hio??

Watu watauana sana,.ina madhara kuliko faida
 
Serikali ihodhi mali itazi'manage vipi?

Shauri survivors waliobaki warithi mali za ndugu yao..huo utaratibu tayari upo ss sijui lipi jipya
 
Hii itasaidia kila mtu mwenye mali sehemu awe anatunza wosia na kuufanyia marekebisho mpaka siku anapofariki.

Wosia uandaliwe kwa kufuata matakwa ya kisheria na ikiwezekana kuwe na centralized electronic database ya kutunza wosia. Mahakama ndio itoe idhini ya kufungua akaunti ya marehemu kujua wosia unasemaje.

Itasaidia sana kuondoa migogoro inayofuatia baada ya mtu kuaga dunia. Itaboresha mahusiano baina ya ndugu.

Serikali itakuwa imeongeza chanzo cha mapato ikiwa watu hawataandika wosia. Kimsingi faida kubwa zaidi kwa serikali ni uwepo wa mahusiano mazuri katika jamii baada ya misiba.
Kila mtu ana haki ya kutoa mawazo yake hata kama ni mawazo mufilisi kama haya! Yaani baba amefariki na kuacha mjane na yatima. Halafu serikali inachukua nyumba na mashamba ya marehemu kwa kuwa tu hakuacha ameandika mirathi! Hiyo Serikali itakuwa na laana mpaka siku ya kiama!!
 
Mawazo mufilisi.🤣

Halafu umemalizia kwa mawazo ya laana. Sijui yapi hapo ndio mufilisi.
 
Ina manage unclaimmed assets za marehemu long time

Ila hii ndugu wa marehemu wapo afu inahodhi mali hata we unaona ni sawa?. Au we dhulumat
Kama umenisoma vizuri dhamira hapa wala sio serikali ichukue mali bali serikali itengeneze mazingira ya kulazimisha kila mtu aandike wosia. Hilo likifanyika migogoro itapungua kwenye jamii ikiwa mtu amefariki.
 
Mbona suala hilo kugeuka motive for murder huliongelei?
Unadhani ni kwanini hadi sasa hio sio sheria?!
 
Hii itasaidia kila mtu mwenye mali sehemu awe anatunza wosia na kuufanyia marekebisho mpaka siku anapofariki.

Wosia uandaliwe kwa kufuata matakwa ya kisheria na ikiwezekana kuwe na centralized electronic database ya kutunza wosia. Mahakama ndio itoe idhini ya kufungua akaunti ya marehemu kujua wosia unasemaje.

Itasaidia sana kuondoa migogoro inayofuatia baada ya mtu kuaga dunia. Itaboresha mahusiano baina ya ndugu.

Serikali itakuwa imeongeza chanzo cha mapato ikiwa watu hawataandika wosia. Kimsingi faida kubwa zaidi kwa serikali ni uwepo wa mahusiano mazuri katika jamii baada ya misiba.
Uislamu umeelekeza vizuri sana kuhusu Mirathi usilete hoja ambazo hazina mashiko
 
Nimeliongelea sehemu post za nyuma. Mfumo ninaopendekeza ni kuwe na centralized electronic database ambapo kila mtu anafungua online account na anaandika wosia katika template ambayo imeandaliwa kwa mujibu wa sheria.

Hakuna mtu atafahamu kuhusu kilichoandikwa isipokuwa muandikaji. Labda yeye ndio awaambie watu. Ikitokea amefariki basi taratibu za kimahakama zinafuata ili kufungua na kusoma wosia huo na kuelekeza utekelezaji.
 
Ingekuwa hilo ni kweli wala kusingekuwa na haya mapambano yanayoendelea katikati ya waislamu baada ya wazee kufariki.

Halafu utaratibu wa kiislamu ni hiari na sio sheria ya nchi. Hapa tunazungumzia utaratibu ambao ni binding kisheria.

Hata hivyo uandishi wa wosia unatakiwa kuzingatia aidha dini au mila katika muongozo wa sheria utakavyokuwa.
 
Hatuko nyuma kiasi hicho. Waafrika wengi wanataratibu za kimila- labda kama wewe unazipiga vita mila za kabila yako.
Mleta mada atauwa hakufanya tafiti ya kutosha na usahau hili

Mila za mwafrica zinatanabaisha nini cha kufanya kwa wakati gani
 
Haujui tu yanayoendelea mtu akifa ghafla , hoja ya mtoa mada ipo Sawa kabisa , taratibu za kimila Kwa sasa hazina nguvu, Mkono wa serikali ndo utakaotiisha , watu Wanauana Sana .... Wosia unatakiwa uwe updated kila mwaka
Tafuta
Government notice declaration order 1964 imesha toa maelekezo yote mkuuu
Haswa kimila
 
Nimeliongelea sehemu post za nyuma. Mfumo ninaopendekeza ni kuwe na centralized electronic database ambapo kila mtu anafungua online account na anaandika wosia katika template ambayo imeandaliwa kwa mujibu wa sheria.

Hakuna mtu atafahamu kuhusu kilichoandikwa isipokuwa muandikaji. Labda yeye ndio awaambie watu. Ikitokea amefariki basi taratibu za kimahakama zinafuata ili kufungua na kusoma wosia huo na kuelekeza utekelezaji.
Electronic for who
Wabongo watahonga kujua na mtauwawa sana

Doc confidential za Serikali ziko mitandaoni sembuse wosia?!
Hata nchi zilizoendelea hakuna hicho kitu
 
Hii itasaidia kila mtu mwenye mali sehemu awe anatunza wosia na kuufanyia marekebisho mpaka siku anapofariki.

Wosia uandaliwe kwa kufuata matakwa ya kisheria na ikiwezekana kuwe na centralized electronic database ya kutunza wosia. Mahakama ndio itoe idhini ya kufungua akaunti ya marehemu kujua wosia unasemaje.

Itasaidia sana kuondoa migogoro inayofuatia baada ya mtu kuaga dunia. Itaboresha mahusiano baina ya ndugu.

Serikali itakuwa imeongeza chanzo cha mapato ikiwa watu hawataandika wosia. Kimsingi faida kubwa zaidi kwa serikali ni uwepo wa mahusiano mazuri katika jamii baada ya misiba.
Acha uzwazwa
 
Back
Top Bottom