Tetesi: Bunge Live: Wanataka kujikosha ili Nape pekee aonekane ndiye aliyewasaliti wananchi

Wana CCM ni washirika na Nape alikuwa sehemu ya ushirika huo. Huwezi kuwauza watu waliokuamini kwa vipande vya fedha na cheo halafu baadae ujitetee eti yalikuwa maagizo. Huyo Nape tunayetaka kumpamba kwa sifa wakati alijiloweka mwenyewe kwenye chemba ya choo (CCM) hatumtendei haki. HUYU BADO NI MSALITI WA WATANZANIA.

Maswali ya kujiuliza ni kwanini yeye? Kwanini bunge lizimwe akiwa yeye ndiye waziri lakini siyo Mwakyembe? Tuamini kuwa ukipewa dhamana ya uongozi huwajibiki kwa utakayoyatenda na kuyapitisha kwa nafasi uliyopewa?

Nape bado sana hajafikia mahali pa kuaminika eti anapambana na uchafu unaoendelea nchini. Huyu anaona wivu wavutabangi na walevi walionunuliwa kama bidhaa kutoka upinzani upinzani kama Waitara kupewa vyeo huku yeye akiwekwa benchi. (Nadhani anajiuliza bidhaa uliyoinunua itakuwaje bosi wako?).

Kwa msiomfahamu, Nape ni aina ya watu ambao ukiwapa nafasi ya kula atafanya uchafu wowote atakaoagizwa ila akiwekwa pembeni atajifanya ni mpenda haki sana.

Hana tofauti na Polepole na Bashiru. Hawa walipokuwa hawana hili wala lile walikuwa wapiga kelele, wamepewa fedha, maisha mazuri, marupurupu, safari za kila siku, na magari ya kuwapeleka wanapotaka wamegeuka wamekuwa kabisa. Wamekuwa waovu mara mia kuliko wale tuliokuwa tunawaandama (akina Kinana).

Tusiwasikilize mbwa hawa na tusijisumbue kupambana na mbwa. Mbwa kazi yake kubweka bila kujali bwana wake ni yupi. Hawa ni sawa na polisi. Siku bwana wao akibadilika nao hubadilika na hata kufikia kumrarua bila kujali kuwa jana alikuwa bwana wao.

Vita hii tukiielekeza kwa mbwa tutapoteza uelekeo. Tupambane na wafuga mbwa
 
"Tupo negative sana ndio manager tutaendelea kubaki nyuma,let's go tuwe positive changamoto tutazitatua mbele"
 
Huo mkakati mpaka akaujue huyu NYUMBU jike mleta mada mfu utakuwa na maana ganu sasa. Yaani uwepo mkakati kabambe kama huo halafu siri azipate huyu???? Mhhh

Hamna siri ya watu wawili. Huoni waliompiga risasi Lissu wanafahamika ila madaraka yao tu ndio yanawalinda.
 
Bunge kuzimwa ni wazo la serekali za CCM, lilianza kipindi cha JK na kutekelezwa awamu hii nape akiwa waziri mwenye dhamana. Sababu ziliwekwa kubwa zikiwa ni gharama na kuwapa nafasi raia wafanye kazi, japo kwa jicho la tatu lengo lilikuwa ni kuwadhibiti wapinzani wasijijenge kupitia bunge live! huku ikisahaulika kuwa "ujenzi" (kama ulikuwepo) ulikuwa unajenga kote kote.
 
Hao hao washirika wa Nape ndio wanataka mwenzao wamuache jangwani afe peke yake.
 
Ya
Mkuu jibu analijua ila hawezi kukujibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…