Nichukue fursa hii kumpongeza Mhe.Waziri Mkuu Kijana Mwigulu Nchemba kwa kuanza kuanika japo kwa uchache kilichopo nyuma ya pazia.
Ni muda mrefu humu tumesema juu ya mwenendo usio na afya kwa Taifa unaooneshwa na mabeberu au waite mabwana waliowatumikisha wabara na hata kuwauza utumwani .
Mabeberu haya hayachoki...yaani baada ya Waasisi wetu kuwapigia kelele waliona aibu na kutupatia Uhiru lakini kutokana na ukwasi waliojimilikisha na mikataba ya kihuni waliowasainisha kina chifu Mangungo wameendelea kuzengea rasilimali zetu.
Nyakati zile waliwasumbua machief wetu sana na hatimaye kina chief Mangungo waliona kwa usalama wa watu basi isiwe tabu japo wawape mikataba ili uhuru na utu utamalaki kwenye jamii yetu..najua tunamcheka sana Chief Mangungo wa Msovero lakini sina shaka alikuwa na mizania chanya kwa wakati wake ...watakuwa walimsumbua na kumtisha na kumhujumu vya kutosha hadi ikambidi afikie muafaka wa kile alichokifikia wakati huo.
Leo hii hawa mabeberu bado wapo na sisi tu...wanataka rasilimali zetu kiulaini tu ,kila kiongozi anayeingia anatishwa,anahujumiwa na anadhihakiwa ili tu waendeleze lengo lao ovu la kuzipata rasilimali kwa faida yao huku wakituona hatuna akili.
Ifikie mahali tuseme "funaku" na tuseme haikubaliki ..
Kama unataka rasilimali zetu njoo mezani na tukubaliane kupata pamoja.
Kamwe kwa sasa tusikubali kuwa wanyonge japo vitisho,dhihaka,mikwara na hujuma inawakuta viongozi wetu.
Hili haliwezi kusimamiwa na mmoja tu bali sisi sote kama umma wa watanzania.
Umma ukielewa na kusimama na viongozi tutashinda.
Uranium tunayo ya kutosha na inahitajika ...shida ni nini kwa mabeberu haya kuja mezani na mikataba itakayowanufaisha lakini na kuinua hali ya kiuchumi na kijamii??Uingozi wetu na hata mimi ningependa kuona Uongezaji thamani wa rasilimali zetu unawanufaisha watanzania na kuwatoa katika hali mbaya ya umasikini japo kwa kiasi tu.
Hakika umefika wakati wa mtetea kupambana na mwewe kwa njia yoyote ile vifaranga vipone.
Ni dhahiri mtetea hana mabavu ya kumzuia Mwewe lakini akishirikiana na Mbweha au yoyote yule ambaye ni mbabe kwa Mwewe atashinda tu.
Kwenu ninyi vibaraka waroho wa mali na madaraka mlichopewa kinatosha sasa acheni kwani mlinda nchi na mzalendo keshachomoa jambia tayari kwa awamu nyingine ya mapambano...anataraji kushinda na anataraji kuacha alama ya mapamnano dhidi adui wa kudumu.
Adui huyu kamwe hatoacha kuwa adui hivyo lazima irithishwe kwa vizazi vyote vitakavyokuja kuwa yupo adui wa kudumu Mwewe na siku zote atakuwa adui na inatakiwa tupambane naye hadi aache tabia kula vifaranga ...ni jaribio gumu kweli lakini linawezekana...kwani ukifuatilia visa vya Mwewe kula kuku kwa sasa vimepungua sana...sasa hivi kuku wanafugwa kwenye shelters na vifaranga vinaweza kusafuri salama ndani ya Tenga,au vikakuzwa salama kwenye incubators na hii inawafanya Mwewe wapungue kwa kukosa chakula chao...huku familia ya kuku ikiongezeka sana duniani.
TUPO NJIA SAHIHI katika kupambana na MWEWE na hata DUBU pia ...tuendelee kutumia akili zetu vizuri tu kwani hata huko kwa Mwewe na Dubu kulikuwa na matatizo haya yakaisha.
Pongezi sana kwa watumishi wa maalumu wa Umma kwa kupambana na makatili hawa...na muendelee bila woga wala huruma wala haya !
Kuna nyakati Mwewe anataka kuchukua kifaranga na Dubu anataka kumchukua mtetea ...kabla ya hapo lazima DUBU aparurane na Mwewe...na ndio maana halisi ya Mwalimu Nyerere kusema sisi Tanzania tunawataka Wote MWEWE NA DUBU wawe marafiki zetu yaani wasichukue vifaranga bali tunaweza kula mayai kwa utatu kamilifu...siku zote tusimame hivyo na watuelewe tumesimama hivyo kwa gharama yoyote.
BUNGE letu ambacho ni kisemeo cha wananchi halina budi kuja na kauli kali dhidi ya mabeberu na vibaraka wao.
Bunge liainishe kuwa tumewatambua kwa sura zao rasmi na zisizo rasmi na liweke azimio kali dhidi ya kauli za kuingilia uhuru wa Tanzania yaani sio kikaragosi cha bunge la ulaya kinasimama na kuropoka tu eti kulikuwa na "disputed election" wakati vyama 17 vimeshiriki uchaguzi na vikaridhia mchakato na matokeo.Ikibidi bunge letu liseme uovu wa mchakato wa kuwachagua hao wabunge wa bunge la ulaya na uovu wao wa kutumika na wasaliti au wafanyabiashara ili kufikia malengo yao.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lina haki kamili na mamlaka kamili kuazimia na kusema kama lilivyo bunge lolote duniani...BUNGE liseme na liazimie vilivyo dhidi ya wahuni hawa wa ulaya na vibaraka wao hapa Tanzania.
PONGEZI KWAKO MHE.MWIGULU
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!