bunge wa Jimbo la Ulyankulu Mhe. Rehema Migila Amshikia Shilingi Aweso Mpaka Ajibu Hoja ya Maji

bunge wa Jimbo la Ulyankulu Mhe. Rehema Migila Amshikia Shilingi Aweso Mpaka Ajibu Hoja ya Maji

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MBUNGE REHEMA MIGILA AMSHIKIA SHILINGI AWESO MPAKA AJIBU HOJA ZA MAJI KWA KALIUA, ULAMBO NA IGUNGA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora, Mhe. Rehema Juma Migila akichangia hoja kwenye Bajeti ya Makadirio ya mapatao na matumizi ya mwaka wa fedha 2023/2024 ya Wizara ya Maji

"Halmashauri ya Kaliua yenye Kata 28, Vijiji 99 na idadi ya watu 700,000 mpaka leo upatikanaji wa Maji ni asilimia 45 tu, ni aibu sana! Miaka 62 ya Uhuru sasa karne ya 21 bado tuna 45% ya miradi ya Maji, hii haikubaliki" - Mhe. Rehema Juma Migila

"Kuhusu mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria wa Miji 28 itakayonufaika. Hayati John Magufuli tukiwa Tabora, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi wakati anazindua mradi wa Maji wa Tabora, Igunga na Nzega alisema kuna fedha ilibaki bilioni 25 ili isambaze M…
MBUNGE REHEMA MIGILA AMSHIKIA SHILINGI AWESO MPAKA AJIBU HOJA ZA MAJI KWA KALIUA, ULAMBO NA IGUNGA

Mbunge wa Jimbo la Ulyankulu Mkoa wa Tabora, Mhe. Rehema Juma Migila akichangia hoja kwenye Bajeti ya Makadirio ya mapatao na matumizi ya mwaka wa fedha 2023/2024 ya Wizara ya Maji

"Halmashauri ya Kaliua yenye Kata 28, Vijiji 99 na idadi ya watu 700,000 mpaka leo upatikanaji wa Maji ni asilimia 45 tu, ni aibu sana! Miaka 62 ya Uhuru sasa karne ya 21 bado tuna 45% ya miradi ya Maji, hii haikubaliki" - Mhe. Rehema Juma Migila

"Kuhusu mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria wa Miji 28 itakayonufaika. Hayati John Magufuli tukiwa Tabora, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi wakati anazindua mradi wa Maji wa Tabora, Igunga na Nzega alisema kuna fedha ilibaki bilioni 25 ili isambaze Maji Kaliua, Ulambo na Sikonge" - Mhe. Rehema Juma Migila

"Mradi wa Maji Kaliua, Ulambo na Sikonge mpaka leo hatujui yale maji na zile pesa zimeyeyukia wapi, bilioni 25 zimeenda wapi? Mradi wa Maji umeyeyuka, hatuoni mradi ukianza, watu bado wanachangia Maji na Wanyama, hii ni aibu, ndoa bado zina zinavunjika kwa sababu ya umbali wa kufuata Maji" - Mhe. Rehema Juma Migila

"Bwawa la Ichemba nimeona limepangiwa Milioni 750 kwa ajili ya kuanza utekelezaji. Tunataka kuona Wakandarasi wanaanza kazi. Maji yetu ni ya RUWASA, Kaliua na Ulambo vyanzo vya Maji haviko karibu na Maji yaliyo karibu ni kutoka mto Ugala na Malagalasi. Kwanini hatuoni mpango wa kuleta Ulambo na kaliua kutoka Ziwa Tanganyika, Ugala na Malagarasi ambapo ni karibu?" - Mhe. Rehema Juma Migila

"Kuna utafiti gani mmefanya unaoonyesha kuwa Maji ya Ziwa Victoria ndiyo yanafaa na siyo Maji ya Ugala na Malagarasi? Hali hii kwa sababu mnatoa Maji mbali ndiyo maana gaharama ya kuunganishwa ni kubwa na bado hakuna bei elekezi. Turekebishieni bei ya Maji ili wananchi waweze kuunganisha Maji ya bomba majumbani mwao" - Mhe. Rehema Juma Migila

"Bado kuna migogoro katika miradi ya Maji maana wananchi hawashirikishwi na hali hii inasababisha miradi ikwame au isifanyike kwa wakati. Matokeo yake wananchi wanazua migogoro na fidia hawalipwi. Ninaomba wananchi washirikishwe na fidia zao walipwe kwa wakati" - Mhe. Rehema Juma Migila
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-05-13 at 13.49.54(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-13 at 13.49.54(1).jpeg
    34 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-05-13 at 13.49.54(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-13 at 13.49.54(2).jpeg
    33.8 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-05-13 at 13.49.55.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-13 at 13.49.55.jpeg
    41.8 KB · Views: 5
  • Fv3Hl8YWcAAyCqe.jpg
    Fv3Hl8YWcAAyCqe.jpg
    38.8 KB · Views: 6
Back
Top Bottom