Bunge: Wabunge wanakatwa kodi zote stahiki ikiwemo 'PAYE''

Hawa watu wana dharau sana.......
Zama zimebadilika sana watu wana taarifa zote....
Kila mtu ashinde mechi zake....
 
Wahujumu uchumi hawa.
 
Kwahiyo Jerry Silaa alivyoongea juzi ni chizi? mbunge ana posho ya miliono 9 ambayo haikatwi kodi
 
Halafu wanatuambia hawana vyanzo vya mapato wakati ‘benefits in kind’ zote hizo nchi wenzetu unalipa income tax.

Nyumba kama unakaa bure utalipa 10% ya market value kwa mwaka kutoka kwenye mshahara wako.

Thamani ya gari unalotumia utalipa 3-5% kwa mwaka kutoka kwenye mishahara wako.

Mafuta kwa mwaka utalipa percent kadhaa kwa kutoka kwenye mshahara wako.

Posho zote zitajumlishwa na mapato yako mengine utalipa income tax kwa mwaka.

Mwigulu unavyanzo vingi vya mapato acha kukamua maskini na boresha makusanyo kama ilivyokuwa awamu iliyopita.

Kuna waajiriwa wengi awalipi kodi stahiki nchi kulingana na nchi nyingine duniani.
 
Mimi ninadhani kuwapigia kelele hawa jamaa kuhusu ulipaji kodi yaweza isiwe dawa. Kodi huuma pale ambapo una mshahara kiduchu au kazi yako haina namna yoyote ya kuongeza kipato zaidi ya mshahara.

Sasa hawa jamaa wanaweza kulipishwa kodi, je, posho na marupurupu watakazojipa tutazijua? Wanaweza kupaisha huko kwenye maslahi mengine ikawa balaa zaidi.

Kinachotakiwa ni uungwana tu. Kulipwa kulingana na kipato cha nchi ili kupunguza imbalances
 
Kama wabunge wenyewe wanakili hawalipi Kodi tena wabunge wasomi wa sheria kama Jerry silaa alafu Leo mnataka kutuaminisha kua mnalipa Kodi. Lipeni Kodi kwa hizo 9m ambazo ni posho kama wazalendo
 
Hawa wanatumia ujanja wa kujificha kwenye mujibu wa sheria

Hela zote wanazopata kwa mwezi ni karibu 12milion.

Hapo iliyoandikwa mshahara ni milion 3 tu

Zingine zote wanaziita posho ili zikwepe kodi.

Milion 9 yote posho tu
Hata posho kwa mujibu wa sheria zinapaswa zikatwe kodi.
 
Nani amini matamko ya hii serikali haramu
 
Kwani hiki kikaratasi walichoprint ndio kinatosha kuwa ushahidi wanakatwa Kodi?

Waache maigizo!
 
Mbona ni PAYE tu muheshimiwa jobo? Vipi mifuko ya Jamii!! Bima ya afya na pspf mnakatwa au ni PAYE tu?? Nyoosha maelezo vizuri mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wabunge wanaficha kipato chao na kutuonesha mshahara tu, pengine hawaelewi maana ya neno kipato?

Kama ni hivyo basi wasome hapa TRA wanazungumzia nini kuhusu mapato yatokanayo na ajira:

Ni Mapato gani yanayohusishwa katika kukokotoa kodi itokanayo na Ajira?


Faida zinazohusishwa katika kukokotoa mapato kutoka katika ajira
Mapato ya ajira yanahusisha;
a) malipo ya ujira, mshahara, malipo ya likizo, ada, kamisheni, bonasi, kiinua mgongo au posho yoyote ya safari, burudani au malipo mengine yoyote yanayohusiana na ajira au huduma inayotolewa.
b) Malipo yanayoonesha msamaha au marejesho ya matumizi ya mtu binafsi au mtu mwingine anayehusiana na mtu huyo.
c) malipo kwa mkataba wa mtu binafsi katika masharti yoyote ya ajira
d) michango na malipo ya kustaafu
e) malipo ya kupunguzwa, kupoteza au kufukuzwa kazi
f) malipo mengine yanayolipwa yanayohusiana na ajira ikiwa ni pamoja malipo yasiyokuwa ya fedha yanayopatikana kwa mujibu wa sheria
g) Malipo mengine kama itakavyoonekana yanahitaji kuhusishwa

h) malipo ya mwaka anayolipwa mkurugenzi tofauti na malipo yake ya kawaida kama mkurugenzi
Source :
 
Yani izo milioni 12 zote zikatwe kodi mkuu! Mimi nimeona salary slip ya mtu wangu wa karibu yani basic inajumlishwa na posho nyingine ndo inakatwa kodi mkuu... Imagine na uyu ni mtumishi wa kawaida kabisa kwann wao basic tu ndo inakatwa kodi hii si sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Weka pay slip
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…