Bungeni dakika 3 nzima inatumika kusifia na kutoa shukrani watu kufanya majukumu yao!

Bungeni dakika 3 nzima inatumika kusifia na kutoa shukrani watu kufanya majukumu yao!

Hatuna bunge
Wakuu,

Hivi mambo hayawezi kuanza kwa kumshukuru Mungu pekee na kwenda moja moja kufanya kilichokupeleka? Au kushukuru viongozi wengine waliojitoa kwa ujumla wao bila kutaja mtu mmoja mmoja na tuona watu wanasifiwa kwa kukamilisha tu majukumu yao utafikiri kodi zetu hazitumiki kwa wao kufanya majukumu yao?

Haya ndio madhara ya cheo cha kiongozi kuwa mikononi mwa mtu mmoja, ni mwendo wa kusifia na kushukuru tu ili kujiwekea mazingira mazuri ya cheo chako. Hapo mpaka ametoa sifa kwa kina Majiliwa bila hata kusema kwa nini kasifia😂😂 sifa za by the way ili waonekane kwenye ufalme wao.

Badala ya kusifiwa viongozi, shukrani na sifa ilibidi ziende kwa wananchi wanaolipa kodi ambazo nyingine hazina kichwa wala miguu kufanikisha miradi mbalimbali na kulpa madeni ya serikali.

Kiongzoi afanye kitu cha ziada zaidi ya job description hapo hapo itakuwa sawa kusifia, ila mtu anafanya majukumu yake na bado anaripua sifa ni za nini sasa?

Tuna wabunge wasiotimiza wajibu wao vyema. Kila kitu kusifia hata visivyofaa kusifiwa
 
Hiyo speech imeandaliwa yeye anasoma shida ipo wapi? Rais wa nchi ni lazima apewe heshima yake huu ni mfumo wa kidunia wala sio Tanzania. Hata wewe ukija kuwa Rais pia tutakusifia na kukupa pongezi.
Huu ndio ujinga wenyewe.
 
Kuna mbunge kasimama kuchangia kasema anamshukuru Rais kwa kupunguza vifo mahospitalini akamalizia anaunga mkono hoja, kakunja mkwanja wake wa kuhudhuria kikao najua sa hvi anapata mtori canteen za Bunge pale 😀
 
Kwa hiyo mleta mada unataka mama Samia asisifiwe kwa juhudi ambazo hakuna Rais mwengine wa kabla yake amewahi kuifanya?

Bungeni mawaziri walikuwa kila wakiulizwa swali wanasema "bajeti hatoshi", hilo umelisikia kipindi cha mama Samia?
Kusifia sana ni sawa na kumtukuza huyo Samia na ndipo inafika hatua mnasahau kuwa nae ni binaadamu hana ukamilifu ndipo akikosolewa mnaona kama dhambi vile kumkosoa.
 
"Mheshimiwa Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, mheshimiwa........"
"Mheshimiwa makamu wa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, mheshimiwa...."

Yani hadi mtu amalize ni dk tano, then aende kumshukuru Mungu, familia yake, na baada ya hapo asifie aliyemuweka madarakani...
 
Kusifia sana ni sawa na kumtukuza huyo Samia na ndipo inafika hatua mnasahau kuwa nae ni binaadamu hana ukamilifu ndipo akikosolewa mnaona kama dhambi vile kumkosoa.
Ulitaka asisifiwe kwa kazi njema anayoifanya?

Mcheza kwao hutunzwa.

Ingekuwa anasifiwa kwa asiyoyafanya hata mimi ningeponda sana. Lakini naona tena hawamsifii ipasavyo.

Yule msewmaji mpya wa serikali sijuwi anafanya kazi gani mpaka sasa?

Bado anajipanga gtu? Au na yeye ndiyo walewale? Tumeruka mkojo tumekanyaga mavi?

Tunataka atuletee takwimu za tokea mama Samia kaingia madarakani na kabla yake, tulinganishe.
 
Hoja ina msingi, nadhani ingekuwa bora kwa spika kuwajulisha wabunge waende moja kwa moja kwenye hoja ili kuokoa muda wa majadiliano na pesa za watanzania sababu wabunge wanalipwa vinono sana.
 
Ulitaka asisifiwe kwa kazi njema anayoifanya?

Mcheza kwao hutunzwa.

Ingekuwa anasifiwa kwa asiyoyafanya hata mimi ningeponda sana. Lakini naona tena hawamsifii ipasavyo.

Yule msewmaji mpya wa serikali sijuwi anafanya kazi gani mpaka sasa?

Bado anajipanga gtu? Au na yeye ndiyo walewale? Tumeruka mkojo tumekanyaga mavi?

Tunataka atuletee takwimu za tokea mama Samia kaingia madarakani na kabla yake, tulinganishe.
Kusifia sana zaidi ya hapo ni kwa nyinyi kumuabudu tu hapo ndio itakuwa mumemsifia kwa ukamilifu ambao wewe utaona umekamilika.
 
Kusifia sana zaidi ya hapo ni kwa nyinyi kumuabudu tu hapo ndio itakuwa mumemsifia kwa ukamilifu ambao wewe utaona umekamilika.
Sasa wewe inakuuma nini, si na wewe abudu upendacho?

Pilipili iko shamba inakuwashiani?
 
Ata kama watasifia hadi wagaregare kama uwezo wao ni mdogo ni mdogo tu.ndo maana nchi bado inaangaika na mambo ambayo yalipaswa yawe yamesahaulika miaka mingi iliyopita.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa wewe inakuuma nini, si na wewe abudu upendacho?

Pilipili iko shamba inakuwashiani?
Anayetakiwa kuabudiwa ni Mungu tu peke yake, halafu wewe unaniuliza mimi kinaniuma nini kwa nyinyi kumuabudu Samia?

Kama mnapenda sana kumuabudu Samia basi mjenge na majengo maalum ya nyinyi kukusanyana ili mtekeleze hiyo ibada ya kumuabudu Samia na huko ndio utawafundisha jinsi vile utakavyo Samia aabudiwe kikamilifu.
 
Hilo halina ubishi, lakini inayoongelewa hapa siyo ibada. Yanayoongelewa hapa ni mahaba. Wanaoabudu mtu Tanzania hii wanajulikan, wanaitwa Wakristo, wao ndiyo wanaemuabudu Yesu, ambae ni mtu kama mimi au wewe.
 
Ndio nimekwambia kama hizi sifa na mahaba kwa Samia unaona bado hazitoshi basi kumuabudu huyo Samia ndio kitu pekee ambacho kilichobaki ambacho ndio utaridhika.
 
Back
Top Bottom