Ukumuuliza mtu mwenye akili timamu achague kati ya maisha 'huru' au kuzungukwa na mitutu kumlinda mpaka chooni atachagua maisha 'huru'. Lakini kwa sababu maisha 'huru' yanakuwa kwenye majaribu basi mtu analamizika kuzungukwa na watu wa miraba minne tena waliobeba salaha.
Kanumba hakuuwawa na majambazi, hakuvamiwa na watu asiowajua. Bodyguard anahitajika kama mtu anaona kuwa usalama wake unaweza kuwa hatirini. Huyu Martha Mlata anataka kutuambia kuwa Kanumba amekufa kwa sababu hakuwa na bodyguard? Au kwa sababu wanaona wenzao wa Hollywood na Nollywood wamezungukwa na mabaunsa basi Mlata anaona naye aige. Asilolitambua ni kwamba huko kwa hao ma-star mambo ni tofauti kabisa - kiusalama.
Kwa vyoyote vile, Kanumba amekufa katika mazingira ya scandal. Bahati ni kwamba msiba umevamiwa na wanasiasa kwa sababu zao wenyewe hivyo kipengele cha scandal kinafifia. Ni marehemu Kanumba na huyo binti wa miaka 17 (or 18) ndio wanajua nini kimemuua na pengine hali ingekuwa hivyo hivyo hata kama alikuwa anaishi Oysterbay.