Kwa jinsi Musukuma alivyoiweka hoja yake bila maelezo mengi, ufumbuzi wa tatizo la upungufu wa walimu mashuleni ni kuajiri walimu wa kutosha. Walimu kwa maelfu wapo mitaani hawana kazi! Hela ya kuajiri hao walimu itatoka wapi, hilo ni suala lingine, lakini ufumbuzi wake si kutaka wazazi wachangie wakati tayari wanamsururu wa kodi.
Kimsingi hoja ya Musukuma ni nyepesi mno na wewe umeiunga mkono kirejareja…
Labda pia tuangalie faida za elimu bure, ili kuutendea haki mjadala huu. Miye nitaanza na moja tu, elimu bure imechangia pa kubwa kupunguza idadi ya watoto wa mitaani.
Unachanganya mambo mawili kiasi cha kukufanya ushindwe kuipata point ya mbunge huyu;
1. KULIPA KODI.
✓ Ni wajibu wa kisheria kwa kila mmoja kulipa kodi bila kujali ziko ngapi (kama ulivyosema wewe "...msururu wa kodi..")
✓ Ulipaji kodi hauangalii mtu either amezaa or hajazaa watoto. Watoto ni wako wewe, umewazaa wewe..
✓ Kodi alipayo kila mtu inawezesha serikali kutoa huduma mbalimbali kwa watu ikiwemo elimu, afya nk; kugharamia miradi ya maendeleo nk nk...
2. KUZAA WATOTO NA KUWATUNZA:
✓ Kila mtu ni ruksa kuzaa kadiri apangavyo na awezavyo yeye kulingana na uwezo wake wa kutunza watoto wake..
✓ It's a natural law kila mtu aliyezaa watoto kuwalea katika maadili mema na kuwatunza watoto wake kwa kuwahudumia kwa yote ikiwemo kugharamia elimu yao, mavazi, chakula..
IS MUSUKUMA (MB) RIGHT..?
✓ Absolutely, very right. Na yaonyesha umeamua kutoielewa hoja ya Mbunge huyu kwa kuwa una uelewa usioweza kuwa twisted either way kwa sababu yoyote ile. Haijalishi, huo ni uamuzi wako.
And may be presentation yake huyu mbunge ndiyo makes you not 🚭 to get his point...
✓ Msukuma ana maana hili, kwamba, acha kila mzazi achangie kiasi cha pesa kwa ajili ya elimu ya watoto wake mwenyewe ili zile bilioni kadhaa zitolewazo kila mwaka kwa kiitwacho " riziki ya elimu bure" zirudi huko huko mashuleni kwa jina jingine ili ziajiri walimu wapya kuziba gap linalosemwa na mbunge kisha zinunue vitabu, zijenge nyumba za walimu nk nk..
Hiyo ndiyo hoja ya Kasheku MUSUKUMA..
Umeelewa sasa? Je, una maoni gani mpaka hapo? Bado hujashawishika tu?
Asante.