Ccm kwa maksudi kabisa ukiiangalia kwa jinsi wanavyoigawana keki ya taifa kwa manufaa yao, na kwa jinsi wasivyo na uchungu kwa wananchi kwa utawala huu,
Na kwa jinsi Rais asivyoshaurika kuhusu mawaziri mizigo na hataki kabisa kuwaondoa, licha ya kwamba wanamchafua sana, na yeye kukubaliana na hali ya kuchafuliwa na anaona ni sawa tuu
Mambo mengi magumu nchi inapitia na hakuna hatua za maksudi ya kuitoa nchi kwenye mkwamo huo, ukijumlisha na hili la kuondoa elimu bule, ni dhahiri kabisa kuna mpango mahususi kutoka humohumo CCM kwamba, 2025 watakipa ushindi chama B" kipya kinachohangaika kupata usajiri wa kudumu
Kwa sababu ninachokijua, CCM piga ua garagaza, hswawezi kukipa ushindi Chadema ni bora hata itokee vita Ila si chadema kupewa nchi, basi watakipa chama chochote Ila sio Chadema
Kwa maana hiyo nawahakikishieni kuwa, 2025 hata kwa fimbo, hakuna mtu atakaye mpa kura mama Samoa Rais aliyepo
Kwa sababu moja tu, wananchi watakuwa wamechoka vibaya na maisha magumu, watakuwa wamechoka vibaya na huduma mbovu kwenye nchi inayowakamua kila uchwao
Niamini mimi