Bungeni Leo: Sera ya "elimu bure" kufutwa? CCM kama kawaida yao wanatanguliza mbunge Kasheku Msukuma kupima upepo. Wewe unasemaje?

Je wewe unaweza kutupa iyo idadi ya wanafunzi waliokuwa na maarifa ya dunia kipindi cha ada tofauti na sasa usomi chawa ni janga kwa nchi sasa
 

CCM kama kawaida yao wanatanguliza mbunge Kasheku Msukuma kupima upepo. Wewe unasemaje???? hIKI ULICHOANDIKA SIYO NDOTO??? NANI ALIKUAMBIA KUWA WAMEMUTANGULIZA??? EBU CHUKUA JEMBE KALIME USILAL E MCHANA NA KUTUPA NDOTO HIZI​

Hata hivyo elimu bwelele haitekelezeki
 
Hii sera ifutwe, ni sera ya kipumbavu inayolea taifa la wavivu na kudumaza ubora wa elimu yetu
Serikali kazi yake ni kujenga miundombinu ya elimu na kuajiri walimu, kusomesha ibaki jukumu la mzazi

Kama kuna masikini wasioweza kulipa basi uchambuzi ufanywe wakipiwe. Lakini nina uhakika zaidi ya 80% ya watanzania wanaweza kulipa ada ya laki moja kwa mwaka
 
Sera ya elimu bure ni mojawapo ya maeneo nilipotofautiana na Magufuli.
Nilliona elimu bure kama kufuga na kukaribisha umaskini endelevu tu. Katika dunia hii na zama hizi vitu vyote bora ni aghali,
na kwa hali ilivyo elimu ya msingi inayotolewa bure kwa ni duni sana kwa sababu ya ubure bure.
 
Kama wewe hautaki mwanao asome bure si umpeleke katika shule za kulipia
 
Msukuma hajatoa maelezo ya kutosha zaidi ya kuonyesha uwepo wa upungufu wa walimu, ambao ufumbuzi wake ni kuajiri walimu wa kutosha. Walimu wapo mitaani hawana kazi.

Labda nikuulize, kwanini wewe umekubaliana na huyo Musukuma?? Tuanzie hapo
Serikali haiwezi kuajiri walimu, kujenga madarasa na kulipia wanafunzi ada, lazima itachemsha tu, ndio maaana hakuna walimu na madarasa tunajenga kwa mikopo ya Covid

Serikali ijitue huu mzigo usiokuwa wa lazima wa kulipia watu ada..ni ujinga
 
Hiyo michango holela ndio serikali ilitakiwa kudhibiti, serikali ilitakiwa kuweka kiwango kuwa mwanafunzi anatakiwa kuchangia kiasi fulani cha fedha na hakuna mwalimu wa kuanzisha michango mipya
Mambo ya maabara, maktaba, walinzi n.k yatalipiwa kutoka kwenye hiyo ada na kama kuna upungufu serikali itatoa ruzuku
Ila hii elimu bure ni upumbavu mtupu, ni siasa za kilaghai walizokuwa wakihubiri akina Lowassa na CCM walikuwa desperate wakaingia mkenge
 
Unakuta baraza la Elimu limesema Malipo ya mtihani wa Moko, au wilaya au mkoa gharama ni 10000 likini wao wanataja 60000 na ukute Kuna vichwa 300_400 unategemea nini hapo kama siyo upigaji

Yaani mkuu upigaji upo Kila Kona wananchi wamepigwa Sana ktk hayo mashule ya kata sijui Serikali.
 
Hata sasa unafikiri hakutakuwa na upigaji wa hizo hela zinazotumwa? Upigaji always upo, dawa ni kutafuta njia ya kupambana nao tu
 
Hawa Watanzania maskini muwabane kila kona halafu bado serikali hata elimu iwalipishe? Huku bidhaa zimepanda Bei, huku mafuta, tena mnataka kuwatwika mzigo huu wa ada! Siyo haki kabisa ukizingatia hii ni katika ahadi na ilani ya uchaguzi ya CCM. Mkibadilisha hii, hapo mmevuka mipaka! Basi waambieni walipie na hayo madarasa mnayojenga. Kujibu hoja ya Msukuma, ingekuwa vyema hiyo hela ya Uviko ikaelekezwa kwanza kwenye vifaa vya kufundishia na kuzalisha walimu wengi bora badala ya kujenga madarasa.
 
Mtu anavunja sheria ya Kodi iliyopitishwa na Bunge anaachwa hivi hivi. Sijawahi kuona hii
 
Elimu bure iendelezwe,kwani kutokomeza ujinga ni vita takatifu, kwa kila mwananchi.Nimeona kuna watu maskini huko vijijini, hata kununua uniform ni shida.
Huwezi kukatisha elimu kwa wanafunzi ambao watakaoshindwa kulipa karo,ni unyama.
Hayo majigambo ya uchumi wakati ni fix,sisi na Bangladesh hatuchekani.
Baada ya miaka 10 serikali ipime ni njia ipi twende nao.
Jambo muhimu ni kuboresha elimu yenyewe.
Mwisho turudi kwenye sera ya Baba wa Taifa ya Uzazi wa Mpango.
 
Wafute tuu ni hasara Kwa Taifa.
 
Ukiniuliza mimi, nitajibu kwa herufi kubwa kabisa, kuwa YES huu ulikuwa uamuzi wa kimakosa. Wazazi na walezi ni Sharti wachangie gharama za kusomesha watoto wao ktk ngazi zote za elimu..!
Magufuli aliingizwa cha kike na wapinzani. Aliposikia wananadi elimu bure yeye hakushughulisha akili yake kujua hiyo elimu bure ingetolewa kwa mfumo gani na yeye kuingia kichwa kichwa kutekeleza sera zisizokuwa za chama chake.
 
Hiyo sera waliivamia toka CHADEMA. Hawakuwa wamejiandaa nayo.
 
Mbumbumbu wanatamnufaisha nani? Kumbuka msemo wa wahenga "usimwamshe aliyelala..."
 
Watu baadhi wamekimbilia Heading tu hawajasikiliza wanakimbilia kureply
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…