Bungeni: Musukuma amvaa Luhaga Mpina kwa kueneza uzushi wa Bwawa la Umeme la Nyerere

Bungeni: Musukuma amvaa Luhaga Mpina kwa kueneza uzushi wa Bwawa la Umeme la Nyerere

Alisema Makamba ameisababishia serikali hasara ya bilioni 30 kwa uamuzi wake wa kuondoa shilingi 100 kwenye tozo za mafuta zilizopitishwa na bunge.

Hivyo Makamba ni muhujumu uchumi.
Rais ameshachukua hatua ya kuirudisha,sasa nashangaa kuna watu bado wanasema eti serikali haijajibu hoja.
 
Mpina anwapiga pini hadi mnalialia tu , report ya CAG inasema kuwa bwawa liko 41% na lilipaswa kuwa 86% mwaka jana. Wewe unaletamavi yako hapa


USSR
Kwani Kuna tatizo report kusema hivo... Hio inamaanisha huu mradi tulikua tudanganywa na wataalam tangu uko nyuma... Hii awamu ndo kwanza Ina mwaka mmoja, kwa makadirio huu mradi ulitakiwa uwe ulishafikia asilimia 80 tangu mwaka Jana July....hivo waziri wa sas ilijumba bovu sio lake, ni waziri aliepita ndio aeleze kwann alikua anadanganya
 
ile hoja ya Mpina kwamba Makamba ni muhujumu uchumi ameisababishia serikali hasara ya bil 30 mpaka leo sijaona ikijibiwa, naona chawa wa mama mnatupigia kelele tu hapa.

Hoja ya Mpina kuwa January alikuwa ameisababishia nchi hasara kwa uamuzi wake bila kufuata taratibu ilikuwa na maana ya kuitahadhalisaha serikari na hasa Rais Samia asirudie makosa yaliyokuwa yanafanywa na Marehemu Magufuli ya kujiamulia mambo kiholela bila kufuata sheria za nchi!!
Rais Samia nae ameanza kupora mamlaka ya Bunge ya kufuta tozo kwenye mafuta bila kupata kibali cha bunge!!! Hali kama hiyo ndio ilimfanya Magufuli kujichukulia madaraka ya kuchukua fedha kwenye sandarusi na kwenda kununua ndege bila kupitia bungeni kitu ambacho kimeitia nchi hasara kubwa kiuchumi kwani ndege hazitumiki ipasavyo!! Hapa Samia anatakiwa ajifunze kuwa serikali lazima ifuate sheria za nchi katika kutoa maamuzi yake na sio kukurupuka na maamuzi ambayo yanavunja sheria na yanaweza kuwa vichochoro vya mafisadi kufanikisha mambo yao!!
 
Ivi uyu msukuma ni mdogo wake Gwaji boy mbona wanafanana
 
Tutamtumia msukuma kupambana na msukuma mwenzake.

Kete imesukumwa tayari hapo.
 
Mara nyingi Msukuma amekuwa akijinasibu kuvunja sheria katika mambo mbalimbali..mfano uuzaji mchanga wa dhahabu waliokuwa wakiiba migodini, kama gari yake ilipakia samaki waliovuliwa kinyume na sheria sheria zilizopitishwa na bunge zipo wazi na adhabu zinajulikana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpina anwapiga pini hadi mnalialia tu , report ya CAG inasema kuwa bwawa liko 41% na lilipaswa kuwa 86% mwaka jana. Wewe unaletamavi yako hapa


USSR
Sasa kama wakati wa uhai wa Mwendazake lilifika zaidi ya 50% halafu mwaka baadaye ujenzi unfikia 41% hupati picha ya kilichokuwa kinaendelea? Lilibomolewa au?
 
Mpina anwapiga pini hadi mnalialia tu , report ya CAG inasema kuwa bwawa liko 41% na lilipaswa kuwa 86% mwaka jana. Wewe unaletamavi yako hapa

USSR
Huyo kashekua ameshakula keki so anajichokonoa kwenye jino bovu kutoa uchafu wa keki uliobaki.
 
Wameanza kuumbuana.

Mbunge wa Geita Mjini Musukuma amemjia juu Luhaga Mpina kwa kumhusisha na kueneza uzushi Kuhusu Bwawa la umeme la Nyerere kwenye Clip aliyodai ilikuwa ikienea mitandaoni. Musukuma ameonya kutohisishwa kwenye uzushi usio na maslahi ya Nchi Kwa kuangushiwa jumba bovu 😆😆.

Musukuma amesifu Kazi nzuri iliyofanywa na Waziri Makamba chini ya uongozi mahiri wa Rais Samia.

My take,

Mtaendelea kuumbuana na mwisho mtawataja tuu waliowatuma.

======


Dodoma. Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Kasheku ‘Msukuma’ leo Ijumaa Aprili 8, 2022 ameeleza kuwa basi lake lililokamatwa kwa kosa la kuwa na samaki watatu linaozea kituoni lakini anashangaa aliyehusika na yeye analalamika.

Wakati Mpina akiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, basi linalomilikiwa na Msukuma lilikamatwa likiwa na samaki na kutaifishwa. Wakati huo Serikali ilizuia uvuvi na usafirishaji wa samaki wadogo Ziwa Victoria.

Msukuma ametoa kauli hiyo wakati akichangia katika hotuba ya makadilio ya mapato na matumizi kwa Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara zilizochini yake ambapo amesema kuna watu huwa wanajisahaulisha wakisha kuwa nafasi za juu.

Hata hivyo Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson amekea kauli hiyo akisema siyo sehemu ya mjadala ulio mbele ya bunge na kumtaka mbunge kujielekeza kwenye hoja mahususi huku akimsihi kufuta kauli yake aliyosema message delivery (ujumbe umefika).

Msukuma amemtaja moja kwa moja mbunge wa Kisesa, Luhwaga Mpina kwamba amekuwa mtu wa kulalamika huku akimhusisha yeye (Msukuma).

“Mimi sitaki kuangushiwa jumba bovu, nimeona katika moja ya mitandao nahusishwa na kauli yangu kuhusu ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, nililisema kweli na nikafuata taratibu zote, lakini tuliomba kibali cha kutembelea ambapo nakiri ujenzi wake umekwenda mara tatu ya alivyoacha Magufuli (Rais John Magufuli wa awamu ya tano),” amesema Msukuma.

Katika hatua nyingine ametaja hoja ya kupanda kwa bei ya mafuta Tanzania akitaka Serikali ichukue hatua za dharura kama ilivyofanya katika mazao ya wakulima, lakini ameonya bila kufanya hivyo wakati wowote mafuta yatapanda tena.
Ki Msukuma kinafiki sana,ni ka bendera fuata upepo huwa kinaangalia zilipo dili,kinalalia huko ili kulinda maslahi binafsi.
 
Hakuna mtu muongo duniani na a ayetumia mdomo wake vibaya kama kuyo anayejiita king. Kama humjui akikuletea habari unaweza kutoa maamuzi magumu dhidi ya aliyemtuhumu
 
Mpina anwapiga pini hadi mnalialia tu , report ya CAG inasema kuwa bwawa liko 41% na lilipaswa kuwa 86% mwaka jana. Wewe unaletamavi yako hapa


USSR
Asilimia 41 ? Labda 41% ya 10% mkuu
 
Back
Top Bottom