Bungeni: Musukuma amvaa Luhaga Mpina kwa kueneza uzushi wa Bwawa la Umeme la Nyerere

Bungeni: Musukuma amvaa Luhaga Mpina kwa kueneza uzushi wa Bwawa la Umeme la Nyerere

msukuma aliwahi kuwa mfanyabiashara & mtumiaji mkubwa wa marijuana kwa hiyo confidence ni lazima kwa sababu ule mmea huwa una katabia ka kuwapatia watumiaji wake misimamo


"labda kwenye ganja kidogo nilikuwemo ndio maana mpaka leo bado inanipa misimamo" Sugu
That's from the mouth of the horse
 
Maisha bana sasa wamebaki wenyewe wanakulana , na ukitaka kujua malipo ni hapa hapa duniani angalia leo Kimbunga Jobo cha kule mpwapwa kinauliziwa wala hakijulikani kilipo baada ya kuandikishwa barua ya kujiudhulu kwa lazima. Wanaita what goes orround comes arround , tutaelewana tu ,ipo siku.
Mgambo wanaruka na kukanyagana.
That's when things fall apart.
 
msukuma ni chawa anaangalia upepo. msukuma ndie alimshitaki mkurugenzi kwa jpm eti kanunua gari la kifahari kwa hela ya serikali
 
Wameanza kuumbuana.

Mbunge wa Geita Mjini Musukuma amemjia juu Luhaga Mpina kwa kumhusisha na kueneza uzushi Kuhusu Bwawa la umeme la Nyerere kwenye Clip aliyodai ilikuwa ikienea mitandaoni. Musukuma ameonya kutohisishwa kwenye uzushi usio na maslahi ya Nchi Kwa kuangushiwa jumba bovu 😆😆.

Musukuma amesifu Kazi nzuri iliyofanywa na Waziri Makamba chini ya uongozi mahiri wa Rais Samia.

My take,

Mtaendelea kuumbuana na mwisho mtawataja tuu waliowatuma.

======


Dodoma. Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Kasheku ‘Msukuma’ leo Ijumaa Aprili 8, 2022 ameeleza kuwa basi lake lililokamatwa kwa kosa la kuwa na samaki watatu linaozea kituoni lakini anashangaa aliyehusika na yeye analalamika.

Wakati Mpina akiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, basi linalomilikiwa na Msukuma lilikamatwa likiwa na samaki na kutaifishwa. Wakati huo Serikali ilizuia uvuvi na usafirishaji wa samaki wadogo Ziwa Victoria.

Msukuma ametoa kauli hiyo wakati akichangia katika hotuba ya makadilio ya mapato na matumizi kwa Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara zilizochini yake ambapo amesema kuna watu huwa wanajisahaulisha wakisha kuwa nafasi za juu.

Hata hivyo Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson amekea kauli hiyo akisema siyo sehemu ya mjadala ulio mbele ya bunge na kumtaka mbunge kujielekeza kwenye hoja mahususi huku akimsihi kufuta kauli yake aliyosema message delivery (ujumbe umefika).

Msukuma amemtaja moja kwa moja mbunge wa Kisesa, Luhwaga Mpina kwamba amekuwa mtu wa kulalamika huku akimhusisha yeye (Msukuma).

“Mimi sitaki kuangushiwa jumba bovu, nimeona katika moja ya mitandao nahusishwa na kauli yangu kuhusu ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, nililisema kweli na nikafuata taratibu zote, lakini tuliomba kibali cha kutembelea ambapo nakiri ujenzi wake umekwenda mara tatu ya alivyoacha Magufuli (Rais John Magufuli wa awamu ya tano),” amesema Msukuma.

Katika hatua nyingine ametaja hoja ya kupanda kwa bei ya mafuta Tanzania akitaka Serikali ichukue hatua za dharura kama ilivyofanya katika mazao ya wakulima, lakini ameonya bila kufanya hivyo wakati wowote mafuta yatapanda tena.
Wahuni tu hawa in Polepole's Voice.
 
Sasa kama wakati wa uhai wa Mwendazake lilifika zaidi ya 50% halafu mwaka baadaye ujenzi unfikia 41% hupati picha ya kilichokuwa kinaendelea? Lilibomolewa au?
Nani aliwahi kutoa hizi taarifa za kwamba Bwawa limefika 50%? Acha uzushi wewe.

Mwisho nani hajui kwamba Serikali ya Mwendazake ilijaa uongo,kupika data na Takwimu? Ni mjinga tuu kama wewe ndio ungeweza muamini Mwendazake.

Mwendazake alizindua zaidi ya mara 3 Bomba la mafuta la Uganda lakini hakuna hata greda 😆😆..
Sgr ya km 200 tuliambiwa ingeanza mwaka 2018 hadi leo hii imekwama 😬😬
 
Sasa kwani kuna tatizo ripoti ikisema hivyo?

Ndio maana ya serikali kujibu hoja,Sukuma gang mmja keshaelewa sababu za kuchelewa wala hazihusiani na Serikali ya mama bali wapigaji waliokuwa wamewekwa na kiongozi wa malaika wa Sukuma gang.
Kama kawa
Kaburu gang wewe
Ujumbe ukufike
haya weka tusi lako hapo chini
 
Nani aliwahi kutoa hizi taarifa za kwamba Bwawa limefika 50%? Acha uzushi wewe.

Mwisho nani hajui kwamba Serikali ya Mwendazake ilijaa uongo,kupika data na Takwimu? Ni mjinga tuu kama wewe ndio ungeweza muamini Mwendazake.

Mwendazake alizindua zaidi ya mara 3 Bomba la mafuta la Uganda lakini hakuna hata greda 😆😆..
Sgr ya km 200 tuliambiwa ingeanza mwaka 2018 hadi leo hii imekwama 😬😬
Mwendazake ndio nani?
 
Back
Top Bottom