Bungeni: Mwenyekiti PAC amtaka Kangi Lugola kutoa maelezo kuhusu sakata la ufisadi katika ununuzi wa sare za Jeshi la Polisi nchini

Bungeni: Mwenyekiti PAC amtaka Kangi Lugola kutoa maelezo kuhusu sakata la ufisadi katika ununuzi wa sare za Jeshi la Polisi nchini

Na sa hivi itakua vijana wa usalama wanawapenyezea wabunge wa ccm/cdm vimeo vya Kange akiwa madarakani ili wakaviongee vzr huko bungeniikurano yao.
Akiangalia clip zake wakati ni Waziri sijui anajisikiaje........
Hapa duniani kuwa Ogopa na kuwa makini na

Power,popularity,prestige,property na pomposity......

Hayo yote ndiyo yanamtafuna saizi

dodge
 
Word
Ukiona mtu anataka aonekane ni zaidi ya wote, halafu anaweka na mbwembwe nyingi kuonekana zaidi ya wengine, weka alama ya kuuliza.

Ile kuweka viraka vya bendera ya Taifa mpaka kwenye mashati, kama vile yeye ni mtanzania kuliko wengine. Kutembea ameshikilia ilani ya CCM kama vile yeye ni mwanaCCM kuwazidi wengine, ni dalili ya uovu anaotaka kuuficha kwa mbwembwe nyepesi nyepesi.

Mwigulu naye kuvaa skafu ya bendera ya Taifa kama vile yeye ni mtanzania zaidi kuliko wengine, ni jambo kujiuliza.

Mwalimu hakuwahi hata kuvaa kofia yenye bendera ya Taifa - ina maana akina Lugola na Mwigulu wamemzidi utaifa hata Baba yetu wa Taifa!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na sa hivi itakua vijana wa usalama wanawapenyezea wabunge wa ccm/cdm vimeo vya Kange akiwa madarakani ili wakaviongee vzr huko bungeniikurano yao.

dodge
Daah aisee na hivi alikuwa anawazingua zingua police,lazima nayeye wamlipue
 
Kuna ufisadi kamati ya kudumu ya bunge bado inauficha. Ni hawa hawa waliungana na wezi wenzao kusema hawana imani na prof. Assad.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuwe makin naona ccm inatutoa kwenye reli kuhusu matumizi ya mkopo uliositishwa!spin doctoring hapa naiona!!!!!Wameamua kumtoa kafara tu kupata umaarufu kwa jiwe kuelekea vugu vugu la uchaguzi!!!
 
Mwenyekiti nae asituchoshe. Alikuwa anasubiri Kangi atumbuliwe ndo aje na huu Mkwara? Nnachokiona, huyu ni mwenyekiti ambae ameamua ku side na Serikali, so she is dancing according to the tune!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa ndiyo linapo anzia tatizo la viongozi wetu, hili sakata halikuanza leo hii bali ni kipindi cha nyuma nakumbuka wakati Lugola akimtuhumu CAG kuwa ni muongo hao hao wajumbe wa kamati hii walikuwa wanamshangilia
BAADA ya Kangi Lugola, kuwekwa chini ya ulinzi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa madai ya ufisadi, sasa kuwekwa kikaangoni bungeni. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).



Kaboyoka ametoa hoja hiyo wakati akizungumza bungeni jijini Dodoma, jana tarehe 29 Januari 2020, huku akimtuhumu Lugola kwamba alilipotosha bunge kuhusu ununuzi wa sare hizo.

“Kwa hiyo Kangi alilipotosha bunge kwa kuapa kwamba, atatoa nguo kama sare hazipo, inamaana hasomi hata taratibu,” amesema Kaboyoka.

Mwenyekiti huyo wa PAC amemkalia kooni Lugola, akimtaka aeleze sare hizo zilinunuliwa kutoa wapi pamoja na gharama zilizotumika kununua sare hizo.

“Huyo aliyepewa tenda alipatikanaje, sare zililetwa kutoka wapi, kiasi cha fedha iliyotumika ni ngapi? “ amehoji Kaboyoka.

Kaboyoka amesema Lugola akitoa maelezo hayo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) atafuatilia sakata hilo, ili kujua kama idadi ya sare aliyoitoa, inaendana na idadi halisi iliyopo.

“Kuanzia hapo ndio CAG aweze kwenda stoo kujua kuna nini kutokana na zile ripoti, aone kwamba zile sare ziliagizwa mia na zimekuja mia, kinyume na hapo CAG hawezi kutoka akaenda kwenye stoo akaangalia kitu ambacho hana nyaraka zinazoonyesha kilichomo,” amesisitiza Kaboyoka.

“Nanyanyua mikono juu itakapofika jioni kama mimi nasema uongo kwamba hakuna sare hewa, najivua nguo, kamati ya mambo ya ulinzi na usalama na maofisa ya CAG twende stoo kuu tukaangalie makontena 15 na magodauni 5 yamesheheni sare za vitambaa. Nauweka uwaziri wangu rehani kama mimi nasema uongo,” Lugola aliapa bungeni.

Lugola pia alimtuhumu Profesa Mussa Assad, aliyekuwa CAG kwamba alisema uongo katika ripoti yake, juu ya ununuzi wa sare hizo.

“CAG amelihusisha Jeshi la Polisi na kashfa ya sare hewa, na kwamba sare hizi ni za bilioni 16.6. Kwa heshima na taadhima kwa moyo mkunjufu, kwa mikono yangu meupe nikiwa kama waziri makini, ambaye naitakia mema nchi hii, natetea rasilimali za Watanzania na tumuogope Mungu, sijawahi kuona mtu muongo kama CAG,” alisisitiza Lugola.

Kwa sasa Lugola anakabiliwa na kashfa ya kuingia mkataba wa kifisadi wa vifaa vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, ambapo anahojiwa na TAKUKURU.

Lugola anahojiwa na TAKUKURU baada ya Rais John Magufuli kuiagizataasisi hiyo kuchunguza mkataba huo, kwa ajili ya kujua wahusika ili wachukuliwe hatua.

Chanzo: Mwanahalisi
View attachment 1340857

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Takukuru wamemkamata lugola Kwa tuhuma za ufisadi, rais amemteua lugola kuwa Wazir wa mambo ya ndani

Lugola;- sijawahi muona MTU muongo kama CAG (kipind hicho ni proff Assad) wabunge wa ccm wampigia makofi na kumshangilia

Magufuli;- lugola achunguzwe kwa ufisadi-waimba mapambio wana msifia magufuli

Kutokana na hizo statement tatu inaonyesha kama taifa hatujui tunachotaka
 
Hapa ndiyo linapo anzia tatizo la viongozi wetu, hili sakata halikuanza leo hii bali ni kipindi cha nyuma nakumbuka wakati Lugola akimtuhumu CAG kuwa ni muongo hao hao wajumbe wa kamati hii walikuwa wanamshangilia

Sent using Jamii Forums mobile app
Sihivyo rais alimchagua kuwa waziri akiwa ametoka kutuhumiwa kufanya ufisadi unafki ni janga LA taifa
 
kabla hujateuliwa na Rais basi ni vyema ukajitathimini wewe mwenyewe kwanza kama unatosha, kama una upungufu wa maadili bora kukataa kuliko kuadhirika.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha ya usanii kwenye utumishi wa uma huwa hayadumu
Mkuu hi Sentesi yako ni nzito,ingekuwa imetolewa na Ballack Obama,Tony Blair ingekuwa ni ya kimataifa ila kwa kuwa ni ya Avacacado...... 😀 😀 😀
 
Kama vile namuona yule afande anavyomsubiri pale segerea akampatie chumba chake. pole sana Kangi na karibu segerea.
 
Watamuua vibaya huyu mzee... Sijui kafeli wapi maskini ya Mungu

Jr[emoji769]
Ila napata mashaka na kwamba mtu akiondokewa na mke kuna madhara kama ataanza kuruka na milupo!
Baada ya Kangi kufiwa haikuchukua muda mrefu akaanza vituko vya kukatika katika mauno hadharani. Nadhani alipata mmakonde akamkatia mauno hivyo kila akisikia midundo anajisikia kunengua.
Nampa pole sana muzee!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom