Bungeni: Mwenyekiti PAC amtaka Kangi Lugola kutoa maelezo kuhusu sakata la ufisadi katika ununuzi wa sare za Jeshi la Polisi nchini

Bungeni: Mwenyekiti PAC amtaka Kangi Lugola kutoa maelezo kuhusu sakata la ufisadi katika ununuzi wa sare za Jeshi la Polisi nchini

Kama alimtaja mungu katika kujitetea hapo mwanzoni alipokua waziri wa mambo ya ndani ili aonekane mwema bhaaasi achukuliwe hatua
 
Kama Lugola kapiga kwenye sare za jeshi wacha apige tu maana huu ni ujinga. Nchi huru ya miaka 60 inaagiza sare za jeshi lake nje ya nchi kama huu si uwendawazimu ni nini?.

Yaani at the expense ya jeshi letu, tunatengenezea nchi nyingine ajira badala ya kuzitengenezea humuhumu kwa ajili ya watu wetu!
Ukombozi umekaribia ila kikwazo ni kile chama chenye wagonga meza wengi mjengoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Walaa yazidu dhwaalimiina illaa khasaarah"
Alimkalia kooni mcha Mungu, CAG Professor Assad, Lugola afanye haraka akamuombe msamaha ili roho ya Assad ikunjuke, bila hivyo ataendelea kuwa na wakati mgumu sana.

Alimdhulumu Assad kwa kujihami yeye na Allah anasema, hazidishiwi mwenye kudhulumu isipokuwa hasara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna jinsi sheria ifuate mkondo wake,Akipatikana na hatia akanyee Debe tu.
 
"Walaa yazidu dhwaalimiina illaa khasaarah"

Sent using Jamii Forums mobile app
Karibu
Screenshot_2020-01-29-22-39-47.jpeg


dodge
 
Alimshambulia CAG Assad!
Alafu kwenye hotuba yake bungeni alikuwa a mb anasema "tumuogope Mungu" wakati huyo Mungu mwenyewe anayemtaja kinafki hamuogopi
Malipo hapa hapa, CAG kalipiwa Kiaina!
FaizaFoxy

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ova
BAADA ya Kangi Lugola, kuwekwa chini ya ulinzi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa madai ya ufisadi, sasa kuwekwa kikaangoni bungeni.



Kaboyoka ametoa hoja hiyo wakati akizungumza bungeni jijini Dodoma, jana tarehe 29 Januari 2020, huku akimtuhumu Lugola kwamba alilipotosha bunge kuhusu ununuzi wa sare hizo.

“Kwa hiyo Kangi alilipotosha bunge kwa kuapa kwamba, atatoa nguo kama sare hazipo, inamaana hasomi hata taratibu,” amesema Kaboyoka.

Mwenyekiti huyo wa PAC amemkalia kooni Lugola, akimtaka aeleze sare hizo zilinunuliwa kutoa wapi pamoja na gharama zilizotumika kununua sare hizo.

“Huyo aliyepewa tenda alipatikanaje, sare zililetwa kutoka wapi, kiasi cha fedha iliyotumika ni ngapi? “ amehoji Kaboyoka.

Kaboyoka amesema Lugola akitoa maelezo hayo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) atafuatilia sakata hilo, ili kujua kama idadi ya sare aliyoitoa, inaendana na idadi halisi iliyopo.

“Kuanzia hapo ndio CAG aweze kwenda stoo kujua kuna nini kutokana na zile ripoti, aone kwamba zile sare ziliagizwa mia na zimekuja mia, kinyume na hapo CAG hawezi kutoka akaenda kwenye stoo akaangalia kitu ambacho hana nyaraka zinazoonyesha kilichomo,” amesisitiza Kaboyoka.

“Nanyanyua mikono juu itakapofika jioni kama mimi nasema uongo kwamba hakuna sare hewa, najivua nguo, kamati ya mambo ya ulinzi na usalama na maofisa ya CAG twende stoo kuu tukaangalie makontena 15 na magodauni 5 yamesheheni sare za vitambaa. Nauweka uwaziri wangu rehani kama mimi nasema uongo,” Lugola aliapa bungeni.

Lugola pia alimtuhumu Profesa Mussa Assad, aliyekuwa CAG kwamba alisema uongo katika ripoti yake, juu ya ununuzi wa sare hizo.

“CAG amelihusisha Jeshi la Polisi na kashfa ya sare hewa, na kwamba sare hizi ni za bilioni 16.6. Kwa heshima na taadhima kwa moyo mkunjufu, kwa mikono yangu meupe nikiwa kama waziri makini, ambaye naitakia mema nchi hii, natetea rasilimali za Watanzania na tumuogope Mungu, sijawahi kuona mtu muongo kama CAG,” alisisitiza Lugola.

Kwa sasa Lugola anakabiliwa na kashfa ya kuingia mkataba wa kifisadi wa vifaa vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, ambapo anahojiwa na TAKUKURU.

Lugola anahojiwa na TAKUKURU baada ya Rais John Magufuli kuiagizataasisi hiyo kuchunguza mkataba huo, kwa ajili ya kujua wahusika ili wachukuliwe hatua.

Chanzo: Mwanahalisi
View attachment 1340857
ukianza kuchagua video maana yake device yako ni Tecno
IMG-20200131-WA0012.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bams,
Ya Lugula yanaweza kumfika na Jiwe pia. Maana matendo yao yanafanana sana
 
Tunatumbua lini sasa yule kangi wa magogoni ?
Hahaha hata wa Syria wanasubiri Asaad ajitumbue, au afe lakini mambo bado sana, ingawa wao wameonyesha wazi kwa kupigana naye.

Hivyo nanyi muje tukinukishe kwanza, tuache kuamini atashindwa uchaguzi wakati mkijua hilo haliwezekani hata tusipopiga kura nchi nzima atapata kura milioni 20 walizojiwekea.
 
Back
Top Bottom