Black BackUp
JF-Expert Member
- Aug 5, 2019
- 717
- 666
Kama alimtaja mungu katika kujitetea hapo mwanzoni alipokua waziri wa mambo ya ndani ili aonekane mwema bhaaasi achukuliwe hatua
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ok, nilidhani ni yule wa masjid Taqwa Kisarawe!Itakuwa siyo huyo, ninaomuongelea ni former CAG Professor Assad aliyepikiwa majungu na mpishi mmojawapo ni Lugola.
Ukombozi umekaribia ila kikwazo ni kile chama chenye wagonga meza wengi mjengoni.Kama Lugola kapiga kwenye sare za jeshi wacha apige tu maana huu ni ujinga. Nchi huru ya miaka 60 inaagiza sare za jeshi lake nje ya nchi kama huu si uwendawazimu ni nini?.
Yaani at the expense ya jeshi letu, tunatengenezea nchi nyingine ajira badala ya kuzitengenezea humuhumu kwa ajili ya watu wetu!
Alimkalia kooni mcha Mungu, CAG Professor Assad, Lugola afanye haraka akamuombe msamaha ili roho ya Assad ikunjuke, bila hivyo ataendelea kuwa na wakati mgumu sana.
Alimdhulumu Assad kwa kujihami yeye na Allah anasema, hazidishiwi mwenye kudhulumu isipokuwa hasara.
Karibu
BAADA ya Kangi Lugola, kuwekwa chini ya ulinzi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa madai ya ufisadi, sasa kuwekwa kikaangoni bungeni.
Kaboyoka ametoa hoja hiyo wakati akizungumza bungeni jijini Dodoma, jana tarehe 29 Januari 2020, huku akimtuhumu Lugola kwamba alilipotosha bunge kuhusu ununuzi wa sare hizo.
“Kwa hiyo Kangi alilipotosha bunge kwa kuapa kwamba, atatoa nguo kama sare hazipo, inamaana hasomi hata taratibu,” amesema Kaboyoka.
Mwenyekiti huyo wa PAC amemkalia kooni Lugola, akimtaka aeleze sare hizo zilinunuliwa kutoa wapi pamoja na gharama zilizotumika kununua sare hizo.
“Huyo aliyepewa tenda alipatikanaje, sare zililetwa kutoka wapi, kiasi cha fedha iliyotumika ni ngapi? “ amehoji Kaboyoka.
Kaboyoka amesema Lugola akitoa maelezo hayo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) atafuatilia sakata hilo, ili kujua kama idadi ya sare aliyoitoa, inaendana na idadi halisi iliyopo.
“Kuanzia hapo ndio CAG aweze kwenda stoo kujua kuna nini kutokana na zile ripoti, aone kwamba zile sare ziliagizwa mia na zimekuja mia, kinyume na hapo CAG hawezi kutoka akaenda kwenye stoo akaangalia kitu ambacho hana nyaraka zinazoonyesha kilichomo,” amesisitiza Kaboyoka.
“Nanyanyua mikono juu itakapofika jioni kama mimi nasema uongo kwamba hakuna sare hewa, najivua nguo, kamati ya mambo ya ulinzi na usalama na maofisa ya CAG twende stoo kuu tukaangalie makontena 15 na magodauni 5 yamesheheni sare za vitambaa. Nauweka uwaziri wangu rehani kama mimi nasema uongo,” Lugola aliapa bungeni.
Lugola pia alimtuhumu Profesa Mussa Assad, aliyekuwa CAG kwamba alisema uongo katika ripoti yake, juu ya ununuzi wa sare hizo.
“CAG amelihusisha Jeshi la Polisi na kashfa ya sare hewa, na kwamba sare hizi ni za bilioni 16.6. Kwa heshima na taadhima kwa moyo mkunjufu, kwa mikono yangu meupe nikiwa kama waziri makini, ambaye naitakia mema nchi hii, natetea rasilimali za Watanzania na tumuogope Mungu, sijawahi kuona mtu muongo kama CAG,” alisisitiza Lugola.
Kwa sasa Lugola anakabiliwa na kashfa ya kuingia mkataba wa kifisadi wa vifaa vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, ambapo anahojiwa na TAKUKURU.
Lugola anahojiwa na TAKUKURU baada ya Rais John Magufuli kuiagizataasisi hiyo kuchunguza mkataba huo, kwa ajili ya kujua wahusika ili wachukuliwe hatua.
Chanzo: Mwanahalisi
View attachment 1340857
ukianza kuchagua video maana yake device yako ni Tecno
Ohoooo !!!
Tunatumbua lini sasa yule kangi wa magogoni ?CCM wote ni WAKANGI
Kitakachomfika Afande Kangi hata uchunguzi haujakamilika naogopa kukisema. Tusubiri tuone!
Hahaha hata wa Syria wanasubiri Asaad ajitumbue, au afe lakini mambo bado sana, ingawa wao wameonyesha wazi kwa kupigana naye.Tunatumbua lini sasa yule kangi wa magogoni ?