Uchaguzi 2020 Bungeni: Rais Magufuli amteua Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu, Bunge zima(Wabunge 350) wampigia kura za ndiyo

Ameshachaguliwa na rais lakini anapigiwa Tena kura na wabunge[emoji16][emoji16].
Sawa angalieni asije akapata kura 0.000.
mkadhani uchaguzi bado unaendelea.
 
Yaani hakika nimefurahi mno. Majaliwa ni best PM. Ana busara nyingi, mnyenyekevu na mtendaji.

Hongera sana Mh. Rais kwa kumuamini tena Mh. Majaliwa.
Busara za kuteka washindani wake jimboni ili apite bila kupingwa?
 
Majaliwa anafaa sana, though hatamaliza miaka 5. Mark these words of mine.
Kama una-fact, iweke mezani; kama ni hisia za ndoto tu ulizokurupushwa nazo leo kitandani, zirudishe hukohuko "uvingini" mwako, sawa?
 
Busara za kuteka washindani wake jimboni ili apite bila kupingwa?
Duu hivi aliteka kumbe? Sina story vizuri hebu shirikisha. Na kama ni kweli huenda ilifanyika purposely na mamlaka ili asifanye kampeni za Ubunge bali asaidie za mamlaka kubwa kama alivyokuwa anafanya. Ila mbona angeshinda tu ubunge bila hata kampeni? Haikuwa na haja ya kuteka kama ni Kweli. Maana CCM 2020 walishinda wote kama ilivyokuwa imepangwa!!!!!
 
Hivi mbatia kumbe alikosa ubunge?,,siku anajishughulisha na kitu gani asee?
Alitumwa Mbeya akatingishe kwa kufanya cinema eti akiahidiwa kuwa chama Kikuu cha upinzani!!!!!. Yaani ndiyo maana ngoja niendelee tu kuwa mpiga kura.
 
JPM kafanya jambo la hekima na busara. PM ni mmoja wa wasaidizi wake wa aminifu kwa kiasi cha kutosha. Ingawa suala la bei ya sukari liliwashinda wote. Hapakuwa na nia ya dhati ya kulishughulikia hasa kutoka kwa PM.
 
Majaliwa anaingia kwenye historia ya Tanzania ya kuwa waziri mkuu wa kwanza aliyepata uwaziri mkuu bila ya kuwa mbunge wa kuchaguliwa na wananchi moja kwa moja. (Majaliwa ni mbunge wa kuteuliwa na NEC!)

Ni aibu kubwa.
Hahahahaha nimesikia makamba anampa sifa eti alipata kura nyingi rwangwa yaaani hawa watu wamechanganyikiwa sijui walipigiwa kura na nani?
 
Majaliwa hana uzuri wowote. Kunachomdaidia ni unafiki. Tendo lile la kumteka mpinzani wake ili asirudishe fomu ulikuwa ni uwendawazimu wa hali ya juu, na ulidhihirisha ni mtu wa namna gani!!
 
Wanaongea ongeaaa.

Wakati wapo wenyewe.

Wanajisahau sijui..
 
Maana CCM 2020 walishinda wote kama ilivyokuwa imepangwa!!!!!
Kama mlijua ilikua imepangwa kuwa CCM itashinda uchaguzi, kwann hamkususia kufanya kampeini za uchaguzi? Na kwann mlijihusisha na upigaji wa kura na kubaki kwenye baadhi ya vituo vya kupigia kura mkilinda kura zenu zisiibiwe, ilihali mkijua tayari kuna mshindi ?

Kifupi, kulikuwa na haja gani ya nyie Chadema kujihusisha na harakati za uchaguzi wakati mlijua tayari CCM imepangwa kushinda??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…