Uchaguzi 2020 Bungeni: Rais Magufuli amteua Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu, Bunge zima(Wabunge 350) wampigia kura za ndiyo

Hata kama wewe sio chadema au wewe ni mpenda haki, ingekua vizuri ujiulize swali hili, inakuaje baadhi ya wapinzani walijua imepangwa CCM itashinda lakini bado wakaendelea kushiriki mchakato wa uchaguzi mwanzo mpaka mwisho??

Naamini kama wewe ni mpenda haki ungejiuliza hivyo.

By the way, sio kila kitu unachosikia kwenye media ni cha kweli, mengine ni propaganda za wapinzani.
Ningekua na ushahidi au ningeshuhudia hicho ulichokisikia kwenye media, basi ningeunga mkono maoni yako.
 
Yaani hakika nimefurahi mno. Majaliwa ni best PM. Ana busara nyingi, mnyenyekevu na mtendaji.

Hongera sana Mh. Rais kwa kumuamini tena Mh. Majaliwa.
Ana busara saaana aisee na uzuri yeye ni kiongozi wa kwanza ambapo waliochukua form za ubunge jimboni kwake kupitia upinzani walitekwa na kupigwa sana, wakanyanganywa na form zao na jamaa akapita bila kupingwa na wala hakuwahi kukemea tabia hio.

Na baada ya tukio hilo ukawa ndio mchezo wa CCM kupiga wapinzani, kuwanyanganya form na kupita bila kupingwa.

Hakika Majaliwa ana busara saaana yaani kama mfalme Selemani vile.
 
Hata Mbunge wa CHADEMA naye kamkubali? Kwa hiyo anakubaliana 100% kuwa uchaguzi haukuwa na kasoro? Basi. Mbombo ngafu.
 
Hiyo roho chafu inatoka kwa jiwe
 
Obvious choice. Kwanza hatuhitaji kubadilishabadilisha mawaziri wakuu kila baada ya miaka mitano maana ni gharama kuwatunza.

Na wote hawana maamuzi thabiti zaidi ya yale yanayotoka kwa mwenye Nchi.
Sasa aliyeleta mada hii...alitegemea kuna mtu asipige makofi...? Usipopiga makofi, ukirudi nyumbani ukakusanye vyako uende kenya, kama unamazingira fulani hivi unakimbilia ubelgiji......
 
Huyu dingi sina shida nae, mwenye kuleta matata ni yule mwenye kichwa kama kabyureta
 
Wote kijani ulitegemea kura ya hapana hapo.
Maana ubunge ni wa CCM na sio wa mbunge akienda kinyume kufurushwa ni lazima
 
Mkuu nimeshaomba toba nisamehewe. Sikuwa najua kilichotokea huko jimboni kwake. Ninatamani moderator afute Ile post yangu ya kumsifia. So sad
 
Bunge la Ulaya na Jumuia ya madola itatoa hatma ya haya yote...hizi zote ni mbwembwe tu mtoto bado hajatoka tumboni...unaweza kufanya yote utakayo hata kuwaymtangazia majirani si mbaya!!
 
Mkuu nimeshaomba toba nisamehewe. Sikuwa najua kilichotokea huko jimboni kwake. Ninatamani moderator afute Ile post yangu ya kumsifia. So sad
Kwa kuongezea Majaliwa alimvimbishia Rais Mstaafu kuhusu Ubunge wa Nachingwea. Mstaafu alikuwa anataka atangazwe aliyeshinda ambaye ni Dr. Mmoto wa CHADEMA lakini Maja akagoma akasema wamtangaze wa Kijani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…