Bungeni: Spika apiga marufuku wabunge kufanya vituko ndani ya Bunge

Bungeni: Spika apiga marufuku wabunge kufanya vituko ndani ya Bunge

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Tulia Ackson amepiga marufuku Wabunge kufanya vituko kama kupiga magoti au sarakasi wakati wakichangia mijadala mbalimbali ndani ya Bunge.

Sarakasi.jpg

Mbunge Flatei Massay akiwa amepiga sarakasi Bungeni
 
Ccm Hii Imeoza Sana Waliofanya Vituko Wachukuliwe Hatua Haraka
Nina uhakika wa asilimia mia kuwa, yule aliyefanya vituko vya sarakasi, angekuwa ni kutoka chama tofauti na CCM, angetolewa nje na polisi. Na pia, angeweza kutupwa nje ya bunge hata zaidi ya mwaka, na bado angepelekwa kwenye kamati ya maadili!
 
Tulivuta naye sana ndumu kwenye 2007 wakati tunaenda kufanya mazoezi ya sarakasi kwenye kijiwe chao,alikuwa kiongozi wa hilo kundi la sarakasi ,ngoma ,judo na karate kuna vijana wake kama kina Ally na D2 walikuwa vizuri sana ila hapo ndumu ni 24hrs ,zoezi,ndumu ,ugali.

Inawezekana hapo ashaivuta kwenye toilet za bunge.
 
Bunge Live... Kila mmoja anatafuta namna ya kuonekana kwa wanachi wake.
 
MH. Tulia;

Usanii unaoanza kuota mizizi Bungeni hauashilii Afya ya Bunge la watu wenye maadili na ustaalabu mbeleni salakasi na kupiga magoti, kesho kutakua na kituko cha mtu kulia, sijui kama mkakati wa kutengeneza vichwa vya habari maana kesho tutasahau umuhimu wa tuzo ya Samia itakuwa Mbunge aliyepiga magoti bungeni na suruali yake, ikiendelea mwingine atadai kukojoa mbele ya watu ilimradi ni vituko mwendelezo.

Wewe ni mtulivu toka Shule lakini pia unaongozwa na hekima na saikologia ya kufukia kinyesi na
na kung'oa uyoga, kupuuza mambo ya hovyo na kuchambua lililo na manufaa.

Ni bunge lako la kwanza kama Spika ukiendeleza upole na utulivu jina lako litakuhukumu. Kemea na Bunge lifuate kanuni . sisi wenzako tunaokuombea ufanye vizuri utatukenyesa ukishindwa kukimudu Kiti.
 
Tulivuta naye sana ndumu kwenye 2007 wakati tunaenda kufanya mazoezi ya sarakasi kwenye kijiwe chao,alikuwa kiongozi wa hilo kundi la sarakasi ,ngoma ,judo na karate kuna vijana wake kama kina Ally na D2 walikuwa vizuri sana ila hapo ndumu ni 24hrs ,zoezi,ndumu ,ugali.

Inawezekana hapo ashaivuta kwenye toilet za bunge.
Huyu atakuwa mvuta ndumu mzuri. Aliibukia bungeni. Wewe sasa. Si ajabu ndio umetoka Kisongo!
 
Back
Top Bottom