Buns za nyama

Buns za nyama

farkhina

Platinum Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
14,568
Reaction score
16,917
Mahitaji
Nyama ya kusaga kg 1/2
Karot 1 kubwa kata ndogo ndogo
Pilipili mboga 1 kubwa kata ndogo ndogo
Thomu
Tangawizi
Bizari ya pilau
Ndimu
Chumvi kiasi
Pilipili manga

Namna ya kutaarisha
1)Chemsha nyama weka chumvi,tangawizi,thomu,bizari ya pilau,ndimu na pilipili manga

2)weka karoti na pilipili mboga

3)changanya vizuri kwa mwiko hadi ichanganyike vizuri... wacha hadi uwive na ikauke vizuri..

4)weka pembeni ipoe..

Buns

Unga kg 1
Chumvi kiasi
Siagi 4 tablespoon
Samli 4 table spoon
Ufuta...
Hamira 1 tablespoon
Baking powder 1tea spoon
Yai 1...tenganisha kiini na ute

Namna ya kutaarisha
1) Changanya unga, chumvi, siagi, kiini cha yai, samli, hamira na baking soda
2) Tia maji hadi uchanganyike vizuri kama ukitaarisha chapati
3) Kanda unga wako hadi uwe laini
4) Weka sehemu ya joto for 30minutes ili uumuke kidogo
5) Kata kata madonge na kila donge tengeneza uwazi ili uweke nyama yako ndani
6) Weka kwenye trey alafu pakaa ute wa yai katika maduara uliotengeza alafu nyunyizia ufuta juu
7) Weka sehemu ya joto kwa dakik 30- 45
8) Washa oven na uweke trey yako ya buns moto 300 -350

Buns za nyama tayari kwa kuliwa

1384768238322.jpg
1384768252066.jpg
 
Nimekuja mammy

Mwisho wa mwaka huu tutapikaa mpaka restaurant zitahamia majumbani

Home made,taamuu
 
Nimeamua kuongezea hiii...
Badala ya kutengeneza maduara waweza pia tengeneza rose rolls...
 

Attachments

  • 1384790863836.jpg
    1384790863836.jpg
    97.8 KB · Views: 239
  • 1384790877278.jpg
    1384790877278.jpg
    11.3 KB · Views: 152
Unatuma posts nzuri sana. Ushauri wangu baadhi ya majina ya vitu unavyopika jaribu kutumia lugha rahisi iliozoeleka kwa wabongo mfano buns ni skonzi, shrimp ni prons,
 
Unatuma posts nzuri sana. Ushauri wangu baadhi ya majina ya vitu unavyopika jaribu kutumia lugha rahisi iliozoeleka kwa wabongo mfano buns ni skonzi, shrimp ni prons,

Ahsante kwa ushauri.....shukraan
 
Back
Top Bottom