Bure Series

ASANTE MAMA WA KAMBO





  • SIMULIZI FUPI - ASANTE MAMA WA KAMBO





    SHAMRA shamra zilizidi kurindima kwa fujo katika ukumbi wa Sabasaba wilayani Temeke, hakika maharusi walikuwa wamependeza na utakuwa mchoyo wa kuzaliwa usingewapongeza waliotumia ubunifu wa hali ya juu kuupamba ukumbi ule nao ukapambika.



    Kila mmoja alitabasamu bila kujalisha linatoka moyoni ama ni la kuzugia!!



    Wanawake walipiga vigelegele na wanaume walipiga mbinja kila muda ambapo msema chochote aliamuru!!



    Naam!! Ilikuwa sherehe ya aina yake ya kuwaunganisha Maria na Christian kuwa mwili mmoja!!!



    Chris alikuwa mwenye furaha sana alipopewa nafasai ya kusema chochote, alizishukuru pande mbili akianza na ule upande wa ukweni akawashukuru kwa zawadi ya mke mwema…..kisha akageukia upande wa pili na kuwashukuru wazazi wake waliomkuza na kumpa elimu dunia pamoja na ile ya darasani!!!



    Hatimaye msema chochote (MC) akamkabidhi kipaza sauti Maria!!





    Ukumbi mzima ulitambua kuwa Maria hakuwa akitabasamu kutoka moyoni lakini bado hakuna aliyejua kwanini alikuwa katika hali ile.



    Maria akashika kipaza sauti mbele ya umati na kuanza kuzungumza.



    “Imekuwa safari ndefu sana hadi kuifikia siku hii ya leo…nikimtoa mwenyezi Mungu katika safari hii ninaye mtu mwingine muhimu katika dunia hii wa kumshukuru!! Ni mtu mmoja tu nasisitiza pasipokuwa na unafiki wowote!!



    Namshukuru mama yangu…mama yangu wa Kambo” akasita kidogo ukumbi nao ukawa kimya!! Kimya kikuu…Maria akaendelea.



    “Asante sana mama wa kambo kwa MATUSI YOTE uliyonitukana maana ulinifanya niyazoee, awali nilikuwa nakasirika sana ukinitukana, ukimtukana marehemu mama yangu, ukinitukania baba yangu. Naam ukaniimarisha zaidi hata nilipokuwa nafanya kazi za ndani sikuhangaishwa na matusi kutoka kwa watoto wa bosi wangu!! Niliyapuuzia tu!!! Maana kila tusi ulikuwa umenitusi tayari



    Asante kwa KUNILAZA NJE asante sana kwa jambo lile, nikalizoea giza, mbu wakaizoea damu yangu!! Ukaniimarisha na hata nilipokosa pa kulala nikiwa mtaani stendi ilikuwa sehemu sahihi kwangu na nililala bila hofu. Mama wa kambo siwezi kusahau kukushukuru kwa kunilisha chakula ambacho watoto wako walilalamika kuwa ni kibaya ama kimeharibika. Ulikuwa sahihi mama maana hata kule majalalani sikuhangaika tena kila kinachoitwa chakula mimi nilikula. Unadhani ungenidekeza ningeweza vipi?



    Siku uliyoamua rasmi kunifukuza ukinizushia kuwa nakujazia choo na kukumalizia godoro bila sababu za msingi ni hivyo hivyo niliwahi kufukuzwa na mabwana wengi walaghai. Lakini sauti zao na yako zilifanana hivyo sikuogopa chochote kitu!! Nikabaki kuwa imara huku nikihesabu kuwa haya ni mapito tu!!



    Kulala bila kula kwa siku mbili hadi tatu katika nyumba yako lilikuwa jambo la kawaida sana hivyo niliweza kumvumilia Chriss wangu alipokuwa hana pesa. Alinishangaa sana kwa uvumilivu wangu lakini leo atambue kuwa bila wewe nisingeweza kumvumilia.



    Ulininyima elimu mama wa kambo!! Vyema sana ukanifanya niishi kwa kutumia nguvu zangu tu na akili ya ziada lakini si vyeti!! Sikuwa mtu wa kuchagua kazi, nilibeba kokoto, nikafanya ubaamedi, nikafua nguo za watu, nikafagia barabara na kazi zote zile ambazo zilihitaji watu kama mimi nisiyekuwa na elimu!! Asante mama wa kambo!!!



    Sijaisahau ile siku uliyonimwagia maji ya moto na kuondoka na ngozi yangu usoni, tazama ulinisaidia sana hakika, wanaume hawakunitamani!! Ndio…nani wa kumtamani na kumthamini mwanamke asiyekuwa na mvuto.



    Ulifanya la maana sana mama maana maumivu niliyoyapata kuondokewa na wazazi wangu, maumivu niliyoyapata kwa mateso yako, ni heri hayo yalitosha na ukaniepushia maumivu ya kudanganywa na wanaume wakware kisa uzuri wangu kisha wanitelekeze pasi na msaada. Ni heri waliidharau na kuichukia sura yangu hadi nilipokutana na Chriss. Hakujali sura akayajali maumivu yangu na akaamua kunipooza!!!



    Hata lile kovu uliloniachia kwa kunichoma na mkaa wa moto pajani, yeye hakujali pia. Unadhani ni wanaume wangapi wanaweza kuwa na ujasiri wa Chriss??



    Nasema nawe ewe mama uliyevaa nguo nyeupe pee!! Umeketi katika kiti cha tatu kutoka kushoto, mama usiyekuwa na haya uliyenitukana huku ukisema kamwe kuwa sitaolewa!! Nimezisikia tetesi kuwa wale wanao wawili wa kike uliowabatiza cheo cha umalikia walijazwa mimba na kuzaliwa nyumbani, sijui kama ni kweli kuwa yule mwanao wa kiume alinibaka ukanitusi mimi kuwa namfunza tabia mbaya nasikia na yeye ni teja na kila leo anakuibia vitu nyumbani!!



    Natoa shukrani kwako kwa mabaya yote uliyonitendea, natoa shukrani kwako kwa moyo wako mgumu unaodhani kuwa niliyasahau yale yote na leo hii umeketi upande wa ukoo wangu ukisubiri kunipa zawadi ya kunipongeza kwa sababu nimeolewa.



    U mnafiki ewe mama, u mkatili katika maana halisi ya kuitwa mkatili.



    Nayasema haya ili niwe na amani, nayasema haya bila unafiki wala tabasamu bandia la kuigiza!!!



    Nilijua itafika siku ya kusema nd’o maana sikusema katika siku hizi zote.



    Ewe mama wa kambo umenipa zawadi nyingi sana tena za kudumu, siihitaji zawadi yako siku hii ya leo. Sihitaji chochote kitu katika maisha yangu kutoka kwako!! Umenipa vingi na vinatosha sana!!!



    Asante sana mama wa kambo!! Mama mbaya unayesababisha hata wale mama wa kambo wenye utu waonekane kuwa si lolote na si chochote kitu!!!”



    Maria alimaliza kuzungumza huku machozi yakiondoka na nuru yake asiweze kuona mbele tena.



    Mama yule ambaye ukumbi mzima ulikuwa ukimtazama alibaki akiwa ameinama kama anayesikiliza kwa makini yale aliyokuwa akielezwa na Maria. Watu walingoja sana anyanyuke waweze kuibaini walau sura yake. Lakini hakunyanyuka, aliyeamua kumgusa bega mara kadhaa kwa kumsukuma ndo aliihitimisha safari yake sakafuni.



    Mama yule hakuwa na fahamu zake!!!



    Zikafuata hekaheka za kumpepea lakini fahamu hazikurejea.



    Maria naye alifanya harakati hizo huku akiipuzia shela aliyokuwa ametinga. Hali ilikuwa tete na ukumbi wa sherehe ukageuka kuwa ukumbi wa hekaheka!!



    Wakati mama yule anakimbizwa hospitali, Maria alipata fursa ya kukwapua bahasha ambayo ilikuwa mikononi mwa mama wa kambo kabla hajaanguka!!



    Akaifungua na kukutana na kipande cha karatasi.



    “Sina zawadi yoyote ya kukupa Maria, japo ni wewe wa kunipa mimi zawadi kubwa ya msamaha. Hakuna nikitegemeacho tena duniani zaidi ya msamaha wako!! Siwezi kujieleza nikaeleweka kwa yote yaliyotokea miaka hiyo lakini waweza kunielewa! Ninauhitaji msamaha wako kabla sijafa Maria. Nililelewa na mama wa kambo nikanyanyaswa na kupewa kila aina ya mateso, sidhani kama ilikuwa sahihi kulipizia kwako nakiri mbele yako kuwa nilikosa na leo hii nitaomba msamaha mbele ya umati. Nisamehe Maria!!”



    Alipomaliza kuusoma ujumbe ule alihitaji kumwona yule mama na kumweleza kuwa amemsamehe tayari lakini akakutana na taarifa kuwa MAMA WA KAMBO AMEFARIKI TAYARI!!!



    Maria alijikuta katika mkanganyiko wa huzuni na amani!!



    “ASANTE MAMA WA KAMBO!!” akajisemea.



    FUNZO:



    Hata wale watu unaohisi ni wabaya katika maisha yako, jifunze kutoka kwao.



    Na utakuwa imara zaidi katika maisha yako iwapo ukijifunza kutoka kwa watu wanaokukatisha tamaa. Kaa kimya, inama kama kondoo, waache wanyanyue midomo yao juu na kukusema. Kama wanakusema kwa chuki zao usijali, na wakisema la ukweli lichukue kama funzo.



    WAPENDE ADUI ZAKO LAKINI HAKIKISHA HAWAJUI KAMA UNAWAPENDA AMA UNAWACHUKIA!!! Utafaidi kutoka kwao mkiishi hivi!!



    MWISHO!!!
 
MTENDA HUTENDWA





  • SIMULIZI FUPI - MTENDA HUTENDWA





    Umaarufu wake pale chuo cha ualimu Butimba Mwanza, maumbile yake na sauti yake ilikuwa mitego tosha kwa wanaume kujisogeza karibu yake walau wapate kumsabahi kwa sababu yeye hakuwa na utaratibu wa kumsalimia mtu yeyote mpaka umuanze, na ilikuwa nadra sana kukujibu kwa maneno mara nyingi alitumia kichwa au kope zake kujibu salamu hizo, ndio waweza kusema kwamba ungekuwa wewe usingemsalimia lakini kiukweli alikuwa mzuri sana wa kuweza kukuvutia hata wewe, watu walimchukia lakini moyoni walimsifia kwamba alikuwa mrembo wa chati za juu sana.



    Umaarufu wa kipekee wa binti huyu ulimfanya awe kama nembo ya chuo kwa wanafunzi, yaani ili uaminike kweli unasomea pale Butimba basi swali la kwanza la uthibitisho lilikuwa, “Unamfahamu Angel??”. Ukiwa



    unamfahamu basi kweli unaaminika unasoma chuo kile.





    Hakuwa na pesa lakini alivyokuwa anaishi maisha ya juu mh! hutakaa huamini kwamba huko kwao analalia kitanda cha kamba na jamvi ndio godoro lake, huku ikimlazimu kusubiri giza liingie ndio aweze kuoga nyuma ya nyumba yao iliyoezekwa kwa nyasi kasoro chumba cha baba yake ambacho kiliezekwa kwa bati dogo lililochakaa.



    Alizaliwa miaka ishirini na moja iliyopita kwa njia za kijadi na kupewa jina la Nyangoko alilokuwa nalo hadi anajitambua na baadaye kujijua na kugundua kuwa lile jina halikuendana na maumbile yake ya kupendeza lakini hakuwa na uwezo wa kulibadilisha lakini licha ya kushindwa kuibadilisha hali hiyo alitumia lazima pale chuoni na ole wako uthubutu kumwita jina hilo (Nyangoko) kama unataka usonywe hadi ujihisi upo uchi basi mwite Nyangoko badala ya Angel (enjo) au malaika kama alivyojibatiza mwenyewe na kulazimisha watu wamjue hivyo kwa hapo chuoni.



    Angle alikuwa wakipekee!!!!



    Watu walikuwa wanajiuliza kama alilazimishwa kusomea ualimu ama kufeli ndo kulimsukumia njia hiyo, hakika hakuwa akifanania!!!!!



    Mguu wa bia uliobebwa na paja lenye unene wa haja, hipsi ambazo zilikuwa zikijibana vyema kwenye nguo zake na kuleta mvuto kumtazama, alijua kutembea vyema hivyo nyama za makalio yake zilitingishika vyema pia. Mwenye macho aliona!!





    ****





    Deogratius au Mtu pori kwa wengi walivyomzoea sio tu kwa jinsi alivyokuwa mshamba hapana pia alikuwa anatoka Morogoro lilipotoka kundi lililovunjika la muziki wa kizazi kipya la watu pori lililopata umaarufu mwishoni mwa mwaka 2006.



    Licha ya ushamba wake labda uliochangiwa na umaskini au mazingira aliyokulia Deo bado alikuwa na hisia kali za kimapenzi kama binadamu wengine na kikubwa zaidi alikuwa ameangukia katika kumpenda binti mwenye maringo na mikogo yote pale chuoni (Angel) na aliamua kuchuana vikali na Steward mtoto wa diwani kata ya nyamagana katika kumuwania Angel. Mchuano huo ulikuwa kama kituko kwani dharau aliyoonyesha Angle kwa Deo kwa mwanaume mwingine angekata tamaa au angempiga vibao yule binti.





    “Hivi Deo ndugu yangu una marafiki????” siku moja katika maongezi yake na Deo aliulizwa



    ‘”Ndio ninao tena wengi tu mbona…..kwanini



    umeuliza hivyo ???’’ alijibu kwa furaha





    “Basi rafiki zako wanafiki ``





    Kwa nini unawaita wanafiki nani huyo mnafiki ???





    "Deo hivi rafiki zako hawajakwambia huna hadhi ya kuwa na mimi? kaulize vizuri wakueleze" lilikuwa ni jibu alilopewa Deo siku alivyomwandikia kaujumbe Angle wakiwa darasani, darasa zima lilimcheka Deo.



    Mtu mmoja tu ndio hakucheka nae ni Steward, hakupendezwa hata kidogo na dharau za Angel kwani aliamini Deo alimpenda Angel kweli tofauti na yeye aliyetaka kuonja ladha ya mrembo huyu kitandani kisha aachane naye . alijisikia vibaya pia kwa kuwa Deo alikuwa mwanaume na kijana mwenzake pia hivyo kuaibishwa kwa Deo ilimaanisha aibu kwa wanaume wote.





    * * * *





    Furaha aliyokuwa nayo siku hiyo hakuna aliyejiuliza kuna nini, Angel kwa mdomo wake alikuwa amemkubalia Deo kimapenzi , alikuwa amekiri makosa yake na kuomba msamaha na alimwomba waonane jioni hiyo guest moja pale jirani na chuo gharama juu yake Angel, kwa Deo hiyo ilikuwa furaha kubwa sana na hakuhitaji hata Angel aombe msamaha kwani alimwona yupo sawa tu na hana hadhi ya kumuomba msamaha.





    Saa moja jioni tayari Angel na Deo walikuwa ndani ya chumba kimoja katika nyumba ya kulala wageni (guest), wote walikuwa na furaha huku Deo akiwa na hamu kubwa sana ya kuonja penzi la mwanamama huyu kwa malengo mawili tofauti, kwanza kuitafuta heshima alitambua wazi kwa kufanikiwa tu kulionja penzi la mwanadada huyu ataheshimika kwa tendo hilo la kumpiku mtoto wa diwani kwa kimwana huyu, pili aliamini kuwa Angel alikuwa anamfaa sana kuishi naye kama mke siku moja.





    "Kaoge basi mpenzi wangu tupumzike kidogo nina hamu na wewe kweli," akiwa amebana pua Angel alimwambia Deo aliyekuwa pembeni yake, neno mpenzi ni kama lilipiga shoti akili ya kijana huyu kutoka shamba, kama mwizi haraka haraka akazama maliwatoni akimwacha Angel akisugua paja lake lililokuwa wazi kwasababu ya kinguo kifupi alichovaa. Paja lile sio tu lilikuwa laini bali pia ni kama liliongea lugha ya mahaba ambayo mwanaume akiisikia lazima atetereke.





    "Atajua mimi ni nani na kamwe hatajutia usiku huu, tena ngoja cha kwanza nimalizie humuhumu nikaanze nae cha pili" alijisemea Deo huku akiendelea kujiosha mwili wake na kisha kujichua, alijihakikisha kabisa kuwa alikuwa ametakata mwili wake tayari kwa kugusana na mrembo Angel. Deo alikuwa kama mjinga ndani ya bafu, mara ajaribu staili atakazotumia akifika pale kitandani.





    Baada ya kumaliza kuoga na kujifuta mwili wake vyema tukio ambalo lilichukua kama dakika kumi na tano, sasa Deo alitoka bafuni tayari kwa mapambano aliyokuwa amepania sana.





    "Angel, Angel!"Deo aliita lakini chumbani hapakuwa na mtu wakati anatoka bafuni, Angel hakuwa pale ndani Deo aliangaza kama kuna chumba cha ziada pale ndani lakini hapakuwa na chumba kingine, akili yake ilisimama kwa muda hadi alipokutanisha macho yake na kikaratasi cha kalenda pale kitandani ambacho hakika kilimvutia kukisoma, kwa haraka haraka akakichukua.





    “Au ametekwa mtoto wa watu…….dah!!!” alijiuliza Deo kabla ya kusoma yaliyoandikwa pale katika ile karatasi. Cha ajabu na kweli hapakuwa na maandishi yoyote yale zaidi ya tarehe mojawapo kuwa imezungushiwa duara nayo ilikuwa tarehe moja (1) ya mwezi wa NNE. Siku hiyo ya tukio.



    Deo alijiuliza nini maana ya ujumbe ule. Mara ghafla akili yake ikapiga kama radi na kuleta majibu. Majibu yaliyomfedhehesha





    "Ayaaaa leo siku ya wajinga mh!........ mi mjinga namba moja duniani,..yes!! mimi ni mjinga namba MOJA" aligutuka Deo baada ya kujiuliza na kupata maana halisi ya hiyo tarehe, mfadhaiko ulimkumba na kujikuta akivaa nguo zake kwa aibu kubwa japo alikuwa peke yake pale ndani. Alitazama kushoto na kulia hapakuwa na mtu. Hisia zake zilizokuwa juu sana zikafifiua na kupotea kabisa.





    "Nitawaambia nini sasa washkaji ????? " alijiuliza Deo huku akivaa nguo zake.



    Hakika alikuwa ameumbuka!!!!





    * * *





    Kwa furaha tele Angel alichukua tax iliyompeleka hadi ukumbi wa bwalo la magereza ambapo aliahidiwa na Steward kwamba amemwandalia zawadi kubwa sana siku hiyo. Tabasamu halikumuisha usoni kutokana na kituko alichomtendea Deo.





    "Yaani ile ndio dawa yake hapo hatanisumbua tena nina uhakika….pumbavu kweli unadanganyika kijingajinga tu…..wapi na wapi mimi kulala na yule mlugaluga, yaani kweli kabisa aende kuninukia kimbuzimbuzi mimi!!!” alikuwa akijiwazia hivyo Angel wakati teksi ikiwa inazidi kuiacha barabara nyuma na kuelekea anapotaka Angel. Wakiwa wamekaribia kufika Angel alimwomba dereva apunguze mwendo ambapo alianza kujipamba uso wake hadi akapendeza kama ilivyo ada akajipulizia na marashi.



    Kwa mikogo na manjonjo aliwasili ukumbini na mshehereshaji (MC) aliwanyanyua wageni wapatao 50 kumpokea mgeni rasmi ambao bila kinyongo walisimama na kuanza kumpigia makofi huku vigelegele pia vikisikika kuwatambulisha kina dada waliokuwa pale, kwa kitendo kile Angel alizidisha mikogo huku akitembea kama vile mlimbwende wa kimataifa alijisikia sana mrembo huyu.



    Baada ya kufika na kuchukua nafasi yake kama alivyokuwa ameelekezwa na binti aliyewekwa kwa shughuli hiyo Steward alichukua kipaza sauti na kuanza kuzungumza.



    "Ndugu wageni waalikwa mabibi na mabwana nachukua fursa hii bila kupoteza muda kumruhusu mpenzi wangu Angel mbele yenu afungue pazia hili na atoe zawadi yake niliyomwandalia kama ishara ya upendo wangu kwake, najua zawadi hii yaweza kuwa ndogo sana kulinganisha na pendo la dhati analonionyesha kwangu lakini naamini ataifurahia,baada ya kuifungua ndipo sherehe itaanza rasmi, napenda kutamka mbele yenu hakuna msichana nampenda kama Angel" aliongea Stewart kisha MC akamwongoza Angel kwa mbwembwe pamoja na fujo za Dj hadi kwenye pazia kubwa ili afungue na kutoa zawadi yake



    "Kama sio gari mh!..........au kibajaji maana Sterwad naye….au ndo lile kabati kutoka Denmark alilokuaga ananiambia" alijiwazia Angel huku akizidi kutembea kwa mikogo kuelekea kwenye pazia. Aliamini alikuwa ni msichana mwenye bahati kupita wote duniani. Alitembea kwa pozi zote za kuzaliwa na za kuiga kwani aliamini ni wengi walikuwa wanamwonea wivu, hivyo alifanya kuwakomesha.





    “Nawatakoma mwaka huu????!!!!!” alizidi kujishaua.





    “Ntahesabu hadi tatu halafu atatufungulia pazia letu mwanadada mrembo Angel….sote tusimame ” Mc alisherehesha, kweli baada ya kuwa amehesabu hadi tatu, Angel akiwa na furaha tele alitelemsha lile pazia "1/4 HAPPY FOOLS DAY" ndio maneno makubwa aliyoyakuta mbele ya ukuta uliokuwa umezibwa na lile pazia



    "Aibuuuuuuuu" ukumbi mzima ukazomea wanawake wakaanza kumshushua kwa kutumia maneno, bila kuteleza akajikuta ameanguka chini alitamani azimie lakini hakuzimia, aliombea ardhi ifunguke aingie ndani yake lakini ndio kwanza ardhi ilikakamaa watu wote bila huruma wakaondoka wakamwacha hapo.



    Alihaha huku na kule kama mfa maji!!! Aibu ikawa imechukua hatamu. Alikuwa amesahau kabisa aliyomtendea Deo muda uliopita sasa ilikuwa zamu yake!!! Naye ametendwa!!!!



    Tena mbele ya umati mkubwa zaidi!!





    Amakweli USILOPENDA KUTENDEWA NAWE USIMTENDEE MWENZAKO
 
HUYU NDIYE BINTI YANGU







  • Mama mmoja mzee alisimulia kisa hiki cha Kweli "Kizuri".
    Alisema : Nilikuwa na watoto watatu,wote wameoa ... Basi nikamzuru yule Mkubwa Na Nikataka Nilale Kwake, Ilipofika Asubuhi Nikamwambia Mkewe Aniletee Maji Ya Kutawadhia... Akanipa Maji Nikatawadha Vizuri,Nikasali Kisha Yale maji Yaliyobaki Nikayamwaga Katika Kitanda Nilicholala... Mke wa Mtoto Wangu Aliponiletea Chai ya Asubuhi Nikamwambia "Ewe Mwanangu,Hii Ndio Hali Ya Watu Wazima,Nimekojoa Kitandani".
    Mke Akakasirika Na Kunifokea Na Kunitolea Maneno Makali,Kisha Akaniambia nioshe Mashuka Niyakaushe Na Nisirudie Tena Kufanya hivyo.
    Nikajifanya Naficha Hasira Zangu Za Kuambiwa Vile,Nikaosha Tandiko na Kulikausha.,Kisha Nikaenda Kulala Kwa Mwanangu Wa Pili.
    Kule Kwa Mwanangu Wa Pili Nako Nilifanya Vilevile,Mkewe Nae Akanijia Juu,Akapiga Kelele Sana Na Kumueleza Mume wake ambaye ni Mwanangu na Hakumkemea.
    Nikaenda Na Kwa Mwanangu Mdogo,Huko nako nikafanya Vilevile,Mkewe Aliponiletea Chai Asubuhi Nilimwambia Kuwa Nimekojoa Kitandani.
    Yule Binti Akasema "Hii Ndio Hali Ya Watu Wazima,Mara Ngapi Sisi Tulikojolea Nguo Zenu Tukiwa Watoto?.. Kisha Akachukua Zile Nguo Na Kuziosha Na Kuzisafisha".
    Yule Mama Akasema,Kuna mwenzangu Amenipa Hela nikamnunulie Mapambo ya Wanawake na sijui Kipimo Chake ila Ana Mwili kama Wako,Nipe Kipimo Cha Mkono Wako.
    Bibi Akaenda Sokoni Kununua Dhahabu na Mapambo,Kisha akawaita watoto wote watatu na wake zao waende nyumbani kwake.
    Akawaeleza kwamba yeye ndio alimwaga maji kitandani Na Wala Haikuwa Mikojo.
    Kisha Akachukua yale Mapambo na Dhahabu na Kumkabidhi Yule Mke wa Mtoto wake Mdogo na Kusema "Huyu Ndiye Binti Yangu Ambaye Nitaenda Kwake Hata nikiwa Mkongwe,nitamalizia Umri Wangu Kwake."


    MWISHO
 
TAFAKARI NJIA ZAKO








  • Mchungaji mmoja alijibadili na kuwa omba omba katika viunga vya kanisa alilokuwa akitarajia kutangazwa jumapili hiyo kama ni mchungaji mpya wa kanisa lile akitokea mji mwingine.
    Alitembea kuzunguka lile kanisa akiwa amevaa nguo kukuuu zilizochanika chanika huku akipishana na watu waliokuwa wakiingia kanisani. Ni watu watatu tu ndio waliomsalimia.
    Wengine wote hawakutaka hata kumuangalia mara mbili, walipitiliza moja kwa moja na kuingia kanisani.
    Aliwaomba watu msaada wa chakula au hela ya kula hakuna hata mmoja aliyempa chochote.
    Akaenda katika malango ya kanisa na kukaa katika ngazi akaweka chombo chake ili aguswae atoe msaada lakini hakuna hata mmoja alietoa hata senti moja.
    Akainuka na kwenda mbele kabisa ya kanisa, akakaa benchi la kwanza kabisa, mzee wa kanisa akamwambia aondoke pale na akakae nyuma kwa vile ile sehemu ni ya watu maarafu (VIP).
    Akaenda nyuma ya kanisa na akakaa benchi la mwisho kabisa lilikowa halina watu, maana wote walionekana kulikwepa. Akiwa amekaa akawa anasikiliza matangazo ya wiki kutoka kwa mzee wa kanisa.
    Akasikiliza wageni wapya wakitajwa na kukaribishwa katika kanisa ila hakuna hata mmoja aliyemkaribisha kwa kuwa nae alikuwa mgeni mazingira yale.
    Akaendelea kuwatizama watu waliokuwa wakimuangalia na kutoa mshangao ambao ulikuwa na tafsiri kwamba hatakiwi mahala pale.
    Baadae kiongozi wa kanisa akaenda pale mbele kutangaza jambo la muhimu. Akasema kwamba anayo furaha kumtambulisha mchungaji mpya mbele ya waumini wote.
    Waumini wakasimama na kutizama huku na huku wakiwa wanapiga makofi. Yule ombaomba akasimaa kutokea kule nyuma na kuanza kutembea kuelekea mbele ya aisle.
    Kufikia hapo watu wakaacha kupiga makofi na kanisa likawa kimya wote wakimtizama yeye...akatembea mpaka madhabahuni na kuchukua kipaza sauti. Akasimama pale kwa dakika kadhaa, akakohoa kidogo na kunukuu mistari kutoka kitabu kitakatifu cha Mathayo 25:34-40 akaanza
    "Kisha mfalme atawaambia wale walio mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika, nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitizama, nalikuwa kifungoni mkanijia...Ndipo wenye haki watakapomjibu wakisema, Bwana ni lini tulikuona una njaa, tukakulisha au una kiu, tukakunywesha? Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha? Au u uchi tukakuvika? Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa au kifungoni tukakujia?
    Na mfalme atajibu, akiwaambia, AMIN AMIN NAWAAMBIA. KADIRI MLIVYOMTENDEA MMOJAWAPO WA HAO NDUGU ZANGU WALIO WADOGO, MLINITENDEA MIMI"
    Baada ya kunukuu hayo, kwa masikitiko na uchungu mwingi moyoni mwake akajitambulisha mbele yao kwamba yeye ndiye mchungaji mpya wa kanisa lile na kuwaeleza ni nini amejifunza kutoka kwao asubuhi ile.
    Wengi wakaanza kulia huku wameinamisha vichwa vyao chini.
    Akawaambia "Leo naona ni mkusanyiko wa watu, ila sioni kanisa la Mungu. Dunia inayo watu wengi wa namna yenu, tunaleta mazoea hata kwenye ibada sasa, kimsingi Mungu tunaemuabudu hayupo mioyoni mwetu. Wakristo mnatakiwa muwe wanafunzi wa Yesu kristo wa kufuata mafundisho na kutenda mema kama yeye alivyofanya. Lini mtaamua kuwa wanafunzi wa Yesu!?
    Baada ya kusema hayo akaahirisha ibada mpaka jumapili inayofuata baada ya kutimiza neno la Mungu kupitia vitendo.
    ______________________________
    _____________


    Basi wewe uliye mkristo, zitafakari njia zako, kwenda kanisani kila Jumapili haitoshi, tuishi katika misingi ya kweli ya ukristo huku tukiwa na moyo wa kuwasaidia wale wote wasiojiweza.
    Mwenyezi Mungu atubariki, tuishi vema sawasawa na vile yeye apendavyo.



 
KONDOO WA IDDY








  • Jamaa mmoja alielekea sokoni kununua kondoo Kwa ajiri ya sikukuu ya Iddy. Pindi alipokuwa akirudi nyumbani,kondoo wake akakimbia. Yule jamaa akamfukuzia mpaka yule kondoo akaingia katika nyumba moja ya mama mjane mwenye watoto yatima. Baada ya watoto kumuona kondoo kaingia ndani, wakafurahi na kuanza kuimba: [emoji207]Kondoo wa eid ! kondoo wa eid ! kondoo wa eidi !. Mama yao alikuwa chumbani, akawajibu wanae: Hakuna kondoo wa eid. Muhusika wa kuwanunulia kondoo wa eidi hivi sasa yupo mchangani.{Akikusudia baba wa watoto hao aliye fariki na kuwaacha watoto na mke}. Pindi yule mama alipo toka sebuleni,kweli akakuta kuna kondoo na watoto bado waendelea kushangilia. Ghafla yule jamaa mmiliki wa kondoo akafika katika nyumba ile, akapiga hodi na kukaribishwa. Lengo lake lilikuwa ni kumchukua kondoo wake aliye mkimbia. Lakini kutokana na hali halisi aliyo ikuta kwa watoto wale, Kwanza kabisa nyumba yao ilikuwa ikionesha ya kwamba wahusika ni fukara mno,lakini vile vile furaha waliyo kuwa nayo watoto wale , ilimfanya yule jamaa awaonee huruma watoto wale na kujisikia aibu kumchukua yule kondoo !!! Akamwambia yule mama: Hii ni sadaka yangu kwenu, Kwa ajili ya Eid. Yule mama akafurahi sana na watoto wake kwa kupata kitoweo cha iddi. Yule jamaa ikambidi arudi nyumbani kwake na kuchukua fedha nyingine, ili aweze rejea kwa mara nyingine sokoni na kununua kondoo wa iddi.
    Baada ya kufika sokoni, akakuta kuna gari ndio inashusha kondoo wengine. Akasubiri mpaka walipo maliza kuwashusha wale kondoo. Baada ya hapo akaanza kuchagua kondoo munasibu kwa ajili ya iddi. Kuna kondoo mmoja alipendezwa nae. Lakini alikuwa ni mkubwa na kanona kulikoni kondoo wa mara ya kwanza. Kutokana na hivyo akawa na khofu,je fedha yangu niliyo nayo itatosha kumnunua
    kondoo huyu??? Wacha nimuulize muuzaji.
    Mteja: "Ebwa ee kondoo huyu ni kiasi gani?"
    Muuzaji: "Hebu chagua vizuri,ndiye uliye ridhika nae?."
    Mteja: "Naam nimeridhika na huyu, Anauzwa kiasi gani?"
    Muuzaji: "Kondoo huyu nitakupatia bure, Kwani baba yangu aliniuSia ya kwamba, Pindi nitakapo fika sokoni na hawa kondoo,Mtu wa kwanza kuchagua kondoo nisimuuzie, bali nimpatie bure ikiwa ni sadaka !!! kutokana na hivyo kondoo huyu ni bure kwako,hongera ndugu yangu."
    Jamaa akarudi nyumbani na kondoo wake akiwa na furaha ya hali ya juu.


    FUNDISHO!!!
    [emoji841]Hivi ndivyo yalivyo malipo ya wema na sadaka,malipo yake huwa si yenye kuchelewa.Tatizo ni kwamba sisi wanaadamu Baadhi ya nyakati huwa hatuyahisi malipo hayo.
    [emoji841]Sadaka hizo hazito punguza katika mali zetu, bali itakuwa ni sababu ya kuongezeka mali zetu
    [emoji843]Kumbuka kutoa ni moyo si utajiri[emoji843]


    MWISHO
 
BABA YANGU YUKO WAPI?








  • "Akiwa na miaka kumi na minane, Kijana Junior alianza kuzitambua shida alizokuwa akipitia mama yake,hii ni baada ya kumaliza darasa la saba na kukaa nyumbani kwa muda baada kukoswa hela za kuendelea na masomo yake ya elimu ya sekondari, hapo ndipo Junior alipomkalisha vizuri mama yake na kumhoji kuhusu baba yake, na haya ndo yalikuwa maelezo ya mama Junior alipomsimulia mwanae"


    "Mwanangu,, Baba yako alinipa ujauzito baada ya kumaliza darasa la saba, baada ya kuligundua hilo nilimfuata na kumuambia ukweli alikataa japokuwa alikuwa anajua kuwa muda mwingi aliutumia kuwa na mimi,, ilipita wiki moja tu nikasikia amefunga ndoa na mwanamke mwingine, ni kitu kilichoniuma haswa na huwa kinaniuma mno katika maisha yangu kila ninapokumbuka,,

    **************

    "Mimba yangu ilizidi kuwa kubwa sana, nilijitahidi kujihudumia mwenyewe kwakuwa bibi yako hakuwa na uwezo hata kidogo maana kila nilipokuwa namfuata baba yako kumuomba hela alikuwa ananifukuza na ninapopiga simu yake alikuwa akimpa mwanamke wake anapokea simu yangu, nilijaribu kuuliza kwanini kanifanyia hivyo, nikabaini kuwa alikuwa ananitumia tu kwa starehe zake kwani alikuwa na mwanamke mwingine pembeni, pia alikuwa akiwaambia marafiki zake kuwa hawezi kunioa mimi mtoto wa maskini ataoa tajiri mwenzie, kingine kinachonifanya hata nisitamani kuolewa na mwanaume mwingine, wakati nakuzaa wewe nilijifungua kwa shida sana kwani nilifanyiwa upasuaji na kutolewa mfuko wa uzazi, kwahiyo siwezi kuzaa tena, na hakuna mwanaume ambaye atakubali kuoa mwanamke ambaye hatamzalia mtoto,, sikutaka kukwambia yote haya kwakuwa sikutaka umchukie baba yako.... Yote kwa yote usimchukie baba yako kwani bado ni baba yako tu.

    Alizungumza mama Junior, wakati huo wote Junior alikuwa kimya kabisa akimsikiliza mama yake kwa makini kwani alikuwa akiongea huku analia na kumfanya Junior naye ashindwe kuvumilia na kujikuta akidondosha machozi...

    *********************

    "Junior alishusha pumzi nzito huku akiinuka na kumsogelea mama yake akaanza kumfuta machozi na kumbembeleza hadi aliponyamaza,,

    "Usijali mama yangu kuhusu mimi kusoma, najua kuna matajiri wengi Duniani ambao hawajasoma, hivyo nami nitakuwa tajiri siku moja na nitakuja kukutunza pia"

    Alizungumza Junior huku akimuachia mama yake na kuingia chumbani kwake na kuanza kupangapanga nguo zake,,,,

    *******************

    "Hatimae kulipambazuka,Junior aliamka asubuhi sana siku hiyo na kubeba begi dogo lililokuwa na nguo na kuanza safari,, kwakuwa hakuwa na hela yoyote alitembea kwa mguu kutoka Sengerema hadi kamanga, alipofika hapo alishindwa kuendelea na safari yake kwani hakuwa na hela ya kukata ticket kwa ajiri ya kuvuka,,kwakuwa usiku nao tayari ulikuwa umeshakuwa mkubwa, hatimae aliamua kutafuta sehemu ya kulala, alifungua begi lake na kuchukua shuka lake na kujifunika huku usingizi mkubwa ukimchukua,,

    "Alikuja kushtuka usiku sana baada ya baridi kali sana kumpiga, alishangaa alipojikuta akiwa na nguo alizokuwa amevaa tu, hapakuwa na begi wala shuka alilokuwa amejifunika, bila shaka vibaka walikuwa wamepita navyo, Baridi ilizidi kuwa kali sana kiasi cha kumkosesha usingizi kabisa Junior, alianza kumkumbuka mama yake na kuanza kujilaumu kwa kuondoka bila kumuagaa, wakati anawaza hayo aliona moto umbali kidogo na alipokuwa akajikuta akitamani kuupata, alianza kupiga hatua hadi alipoukaribia, alishangaa kukuta kijana mmoja tu akiwa amekaa huku akianika nguo zake zilizokuwa mbichi muda huo, Junior aliangalia pembeni akaona mtumbwi mdogo, bila shaka jamaa yule alikuwa ametoka ziwani kùvua, Junior alimsalimia jamaa yule akaitikia huku akimkaribisha Junior kwani alizani mvuvi mwenzie...

    ********************

    "Junior aliutumia muda huo kuusogelea moto ule na kuanza kupiga story mbili tatu na yule jamaa ambaye alionekana kuwa mchangamfu sana.,

    "BHEBHE NGALU, MISHAGA WELAGHA"

    "Ni Sauti iliyomshtua Junior kutoka usingizini ikimtaka kuamka, Junior hakuwa na jinsi aliamka japo giza bado lilikuwa limetanda juu ya anga, bila shaka ilikuwa saa tisa au kumi usiku..

    **********************

    "Twende ukanisaidie kuvuta nyavu rafiki yangu, si unajua nipo peke yangu baada ya wenzangu kuzama,, kwahiyo boss wangu hadi atafute vijana wengine tena napata shida sana kufanya hii kazi peke yangu"

    alizungumza Jamaa yule na kumfanya Junior kuingiwa na uwoga kidogo kwani alikuwa hajawahi kufanya kazi hiyo ila hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali

    "Waliingia ndani ya mtumbwi na kuanza kukata mawimbi hadi ziwani, Junior ilibidi awe mkweli, alimwambia jamaa yule kuwa ndo mara yake ya kwanza, jamaa akatabasamu kidogo,

    "Hata mimi nilijifunza, hebu niangalie mimi ninavyofanya nawewe ujaribu"

    Alizungumza jamaa yule na kumfanya Junior kuangalia kwa makini, ndani ya dakika kadhaa Junia alikuwa ameshajua na kuanza kumsaidia yule jamaa, Mungu si Athumani wala Dossa,, siku hiyo walipata samaki wengi sana hadi yule jamaa akashangaa, Asubuhi wakaenda kukabidhi wale samaki kwa boss wao ambaye naye alishangaa sana kwani mzigo siku hiyo ulikuwa mkubwa sana zaidi ya siku zote, na kwakuwa hapakuwa na wafanyakazi wengi ilikuwa ni rahisi kwa Junior kuajiriwa na kampuni ile iliyokuwa inasimamiwa na mzungu,,,

    *****************************

    "Ilipita wiki moja Junior tayri alikuwa mvuvi hodari sana kitendo kilichomfahisha sana boss wake na kuzidi kumsifikia huku akimuahidi kumuongezea mshahara wake, muda wote huo Junior hakuweza kuwasiliana na mama yake ambaye alitafuta hadi akakata tamaa na kuzidi kuchanganyikiwa akajikuta analazwa hospital, mwezi ulipita na Junior kupewa mshahara wake wa kwanza, siku alipopokea mshahara cha kwanza alinunua simu na namba ya kwanza kuisave ilikuwa ni namba ya mama yake,,baada ya kuisave alijaza vocha na kuipigia namba ile, mama yake alipokea kwa kuuliza nani mwenzangu huku sauti yake ikiwa imechoka sana,,

    "Ni Mimi mwanao Junior mama"

    baada ya sauti ile,alisikia vigeregere vya mama yake na kuwafanya hadi waliokuwa wanamhudumia kushangaa kwani mama Junior alipona ghafla, shangwe zile zilimfanya Junior kuamini kuwa mama yake anampenda mno na ndo pekee anayemtegemea maishani mwake,waliongea mengi sana huku akimtumia mama yake nusu ya mshahara wake"

    "Siku zilizidi kwenda huku Junior akiendelea kugawana na mama yake mshahara hivyohivyo,, miaka ilisogea huku Junior akipandishwa kazi na kukabidhiwa ofisi yake kutokana na uaminifu wake kazini na utendaji kazi wake"

    "Siku moja Junior akiwa ndani ya gari yake mpya aliyokuwa amenunua akirudi nyumbani kwao, alishangaa akisinamishwa na mzee mmoja aliyekuwa akitembea kwa mguu huku akiwa amepauka sana na kumuomba lift kwani nae alikuwa anaenda Sengerema, Junior hakuwa na kutu moyoni mwake,alimpa lift mzee yule na kuanza kupiga nae story moja mbili,,mzee yule alijikuta akifunguka na kumsimlia maisha aliyopitia;

    "Kijana wangu, wakati nikiwa kijana kama wewe nilioa mwanamke ambaye alikuwa mtoto wa kitajili haswa, wazazi wake walitupa kila kitu hadi kazi pia walinipa,nimeishi na mwanamke yule bahati mbaya nikaugua tezi Fulani ya kizazi,madaktari wakaniambia sitakuwa na uwezo wa kumbebesha mimba mwanamke,, kilichoniuma zaidi ilipita miaka miwili nikaona mke wangu tumbo limejaa,nilipomuuliza akanijibu kwa dharau kuwa hawezi kuishi na mwanaume suluari,kiukweli niliumia sana nikaamua kumuacha ila ndo hivyo sikutoka na kitu kwani mali zote zilikuwa za mwanamke,niliingia mjini na kuanza kutafuta kazi lakini sikupata kazi ya maana zaidi ya kazi ndogondogo za kunipatia chakula,, kwa sasa nimezeeka nimeona nirudi nyumbani nikafie kwenye mashamba ya wazazi wangu kwani hapa nilipo nina kansa pia na siku zangu za kuishi zinahesabika,nani atanizika huko mjini wakati sina ndugu hata mmoja,bora hata ningekuwa na watoto"

    alizungumza mzee yule nakumfanya Junior kutokwa na machozi kwani aliikumbuka simulizi ya mama yake,

    "ukimya ulitawala kwa muda hatimae Junior akafanikiwa kufika mbele ya nyumba fulani ambayo ndo kwanza ilikuwa imekamilika, alisimamisha gari na kushuka, wakati huo mama yake alikuwa jikoni, alipomuona mwanae alikimbia kwa furaha na kumkumbatia huku akishangaa gari ilivyokuwa inang'aa, wakati anashangaa ile gari mara aliona mtu akishuka,,,

    "karibu mzee huyu ndo mama yangu"

    alizungumza Junior ila alishangaa mzee yule akiwa amemkodolea macho mama junior wakati huo mama junior nae akiwa amemtolea macho mzee yule

    "Junior baba yako huyooooo"

    alipiga kelele mama junior wakati huo yule mzee alimwangalia mama Junior

    "Sarah huyu ndo mwanangu,nisamehee mama"

    baada ya kutamka maneno yale yule mzee alianguka hapohapo, Junior aliwahi akambeba na kumuingiza ndani ya gari na kumpeleka hospital, alikaa nje na mama yake wakiwa na hamu ya kujua maendeleo ya baba yake ambaye siku zote alikuwa anatamani kumfaham, baada ya muda waliitwa na dokta,,,,

    "Kwanza niwape pole, kiukweli mgonjwa wenu hatuko naye tena duniani kwani ameugua kansa kwa muda mrefu sana ambayo imeathiri mapafu,bora mngemuwahisha ingesaidia"

    Junior alilia sana baada ya majibu Yale, siku ya kwanza kumfahamu baba yake,ndo siku baba yake anafariki,,,,,,,,


    _____Nini umejifunza hapa?


    MWISHO
 
MUNGU ANAWEZA







  • Kijana mmoja alisafiri kwa meli na rafiki zake, wakiwa katikati ya safari yao meli ilianza kuzama.


    Watu wengi pamoja na rafiki wa yule kijana walikufa maji wakati wanajaribu kujiokoa kwa kuogelea, lakini yule kijana alifanikiwa kushika ubao ulioelea majini akaanza kuelea nao, maji yalimpeleka hadi kisiwa cha mbali sana ambako hakukuwa na watu wala wanyama isipokuwa wadudu tu! Alifika ufukweni amechoka sana na asiyeamini tukio lililotokea, akaishi huko

    kwa kula matunda.


    Aliweza kujenga ka-kibanda kwa shida sana maana hakuwa na shoka wala panga, hatimaye akaanza maisha mapya. Aliishi muda mrefu kisiwani na tayari alishazoea mazingira yale ya shida japo shida haizoeleki.


    Mara zote nyakati za jioni aliwasha moto kwa kupekecha vijiti. Siku moja kama kawaida yake aliwasha moto nje karibu na kibanda chake, aliota moto muda mrefu hatimaye akapitiwa na usingizi.


    Alilala hapo hapo hadi usiku wa manane aliposhtushwa na joto kali lisilo la kawaida. Kumbe moto ulishika nyasi za kibanda chake na kibanda chote kikaungua moto.


    Alilia sana na kumlaani sana Mungu kwa mateso hayo akisema "Hivi Mungu nimekukosea nini mpaka unitese hivi? Pamoja na shida zote hizi bado unaniongezea shida nyingine, umeteketeza makazi yangu ilhali nimejenga kwa shida, Hukuridhika kunitenga mbali na familia yangu nilipoishi kwa raha? Hukuridhika kuwaua rafiki zangu wote baharini? Kwanini Mungu umekuwa mkatili hivi? Bora nife tuu maana nimeshachoshwa na hizi shida!" akaendelea kulalamika na kumlaani Mungu hadi kukapambazuka.


    Ilipofika asubuhi aliiona meli ikija kwa mbali kuelekea alipo, alishangaa maana hakuna meli yoyote inayoweza kwenda kisiwa kile labda kama imepotea njia. Meli ilipofika ufukweni yule kijana akaifuata, alienda moja kwa moja hadi kwa kapteni.


    Kapteni akamwambia "tuliona moto mkali sana usiku tukahisi ni meli inawaka moto tukasema tuje ili tutoe msaada..kwa kweli tumetembea masaa mengi sana hadi kufika hapa, mshukuru Mungu maana ametumia moto kutuleta hapa" yule kijana kusikia hivyo alilia sana, akajilaumu kwa jinsi alivyo mnung'unikia Mungu.


    Akaelewa kuwa Mungu ana njia nyingi za kuleta msaada kwa mtu. Akapiga magoti akatubu huku akimshukuru Mungu. Safari ya kurudi nyumbani ikaanza.


    FUNDISHO:


    Wakati mwingine Kuna mambo mabaya huwa yanatokea katika maisha yetu yanayotufanya tuone kama Mungu ametusahau.


    Tunamnung'unikia na kumlaumu Mungu bila kujua kuwa Mungu ana njia nyingi sana kutuletea msaada. Njia za Mungu huwa zinaonekana kama ujinga fulani, lakini kiukweli ujinga wa Mungu ndiyo akili kubwa ya mwisho ya mwanadamu.


    Tunasahau kuwa mabaya tunayokutana nayo yanafanya kazi kwa Manufaa ya hatma zetu.


    Unaweza fukuzwa kazi usijue kumbe ndio unaelekea katika kazi bora zaidi, unaweza kuachwa na mtu uliyempenda sana ukadhani ndiyo mwisho wa maisha kumbe Mungu amekuandalia mtu mwingine mwenye mapenzi ya dhati mtakayefikia malengo ya kujenga familia, unaweza kukataliwa na kutengwa na ndugu kumbe Mungu amekuandalia watu-baki watakaofanikisha ufikie malengo yako pasipo masimango ya ndugu, hata rafiki wanaweza kukusaliti kumbe Mungu amewaondoa makusudi ili kukuepusha na mabaya waliyoyapanga juu yako.


    Sasa usimlaumu Mungu ukadhani anakuzidishia matatizo, hapo anatafuta njia ya kuyaondoa hayo matatizo.


    Mshukuru Mungu kwa Kila Jambo, kwakuwa hajawahi kukuwazia mabaya. Anakuwazia mema sikuzote.


    Tafadhari Share kama umeipenda na marafiki zako wajifunze.....
 
I LOVE YOU BABA








  • Siku moja baba mmoja alikuta gari yake aina ya Hammer nyeusi,,ikiwa imechorwa chorwa kwa jiwe,, aliyefanya hivyo ni mtoto wake. baba huyi alipatwa na hasira sana na kuamua kupiga vidole vya mwanawe mpaka akaumia na baadae akampeleka hospitali. Lakini baada ya kufanyiwa uchunguzi daktari akasema kuwa hakuna uwezekano ila ni kuvikata tu hivyo vidole. Basi mtoto akakatwa vidole vyake vyote. Sasa akiwa wodini amelazwa na anaendelea na matibabu akamuuliza baba yake swali lifuatalo. " eti baba hivi vidole vyangu vitaota tena vingine?" Baba badala ya kujibu swali akaanza kulia sana na kumkumbatia mwanae. Akawa na mawazo sana na akarudi nyumbani ili baadae arudi tena hospitali. Alipofika nyumbani akaanza kukagua gari lake na kuangalia pale ambapo mwanae amechora ndipo akakuta kumbe mwanae aliandika maneno yafuatayo. " I LOVE YOU BABA" akiwa na maana nakupenda sana baba. Basi pale baba akazidisha kilio. Aliporudi hospitali akamkuta mwanae na baada ya kumsalimia akaambiwa tena na mwanae ILOVE YOU DAD. Baba kwa uchungu akamjibu mwanae kwa kusema I love you too my son. Akauliza mtoto. Baba uliona ripoti yangu ya shule nilikuwa naongoza somo la hisabati, ila kwa sasa sitasoma tena hisabati mpaka vidole vyangu vitakapoota kwa sababu kwa sasa siwezi kuandika. Baba akaendelea kulia..


    MWISHO
 
WASHUKURU "MABUNDI"



Twende sasa moja kwa moja kwenye kile ambacho nimekusudia kukushirikisha wakati huu. Nimefikiria kukusimulia kisa maarufu sana duniani. Ndiyo, ni kisa maarufu na kimesimuliwa kwa miaka nenda rudi. Lakini leo nimeamua nikusimulie kwa namna ya pekee ambayo haijasimuliwa na watu wengi. Siyo kwamba natia swaga! Hasha, nakupa kitu ambacho ulikuwa unakikosa, pengine ulitamani kukisikia. Sasa msimuliaji nipo hapa, weka umakini.
Hiki ni kisa cha kijana mmoja mdadisi sana aliyeamua kufanya utafiti. Utafiti wenyewe ulikuwa ni kuchukua yai la tai na kumuwekea kuku ili aone nini kitatokea! Baada ya majuma matatu alianguliwa tai mzuri sana.
Tai huyo alilelewa na kuku pamoja na vifaranga wa kuku. Alikula na kuchakura kama kuku. Pia aliruka umbali mdogo kama kuku na kufanya kila kitu alichofanya kuku.
Ilikuwa baada ya muda mrefu kupita, ndege mmoja mwenye busara alikuwa akipita akamuona tai akiwa na kundi la kuku akila, kucheza na kufurahia maisha ardhini!
Yule ndege alimfuata tai na kumweleza kuwa; "Wewe ni tai, mfalme wa anga. Hustahili kuishi ardhini kama kuku. Hebu ruka uende zako ukafurahie juu pamoja na tai wenzako"
Yule tai akajitazama, kisha akacheka kwa dharau akisema kuwa yeye ni kuku, kama kuku wengine! Hivyo, haiwezekani awe mfalme wa anga.
Yule ndege aliondoka kwa maskitiko makubwa sana. Alijua uwezo mkubwa alionao tai, ila amechagua kuishi maisha yasiyo stahili. Hakuwa na namna nyingine ya kusaidia. Ilibidi aende zake.
Baada ya siku chache, yule ndege alirudi tena akirudia wimbo ule ule. Kwa bahati mbaya wimbo ulifikia kwenye masikio ya tai yaliyozibwa na nta!
Hatimaye yule ndege alichoka akaamua kwenda zake moja kwa moja.
Siku moja, bundi alikuwa anapita katika harakati zake. Mara akamuona tai akiwa anachakura kama kuku. Bundi akamshangaa sana tai. Hakuishia hapo, aliamua kumfuata na kumweleza nafasi aliyonayo, lakini tai alibaki anazubaa!
Bundi aliamua kumnyakua tai na kuruka naye mbali juu ya mawingu. Akiwa katikati ya anga umbali mrefu sana toka ardhini, aliamua kumuachia yule tai bila msaada.
Mara, tai akaanza kushuka chini kuitafuta ardhi! Wakati huo alianza kutapa tapa huku akipiga kelele kuomba msaada. Wakati akitapa tapa, akagundua kuwa ameweza kuruka. Tangu hapo hakurudi tena ardhini kuishi kama kuku. Aliungana na tai wenzake na kuanza kuishi akiwa mfalme wa anga.
*******
Una kitu cha kujifunza hapa. Ukiachilia mbali jinsi unavyoweza kushindwa kuelewa uwezo mkubwa ulioko ndani yako, hebu tafakari nafasi ya bundi kwenye hatua zako za mafanikio!
Mabundi ni sura mbaya! Bundi ni nuksi, tena bundi hapendwi. Wapo watu maishani mwako, ambao wanakufanyia ubundi. Ukiangalia kwa mtazamo mfinyu, unaweza kudhani kwamba, wapo kwa ajili ya kuuchukua uhai wako ama kukuangamiza!
Lakini ukitafakari kwa kina,utajua kwamba, wapo kwa ajili ya kukusaidia kufika mahali ambapo hukudhani kwamba ungeweza.
Inaweza isiwe rahisi, maana wanaweza kukuweka kikaangoni. Lakini wanakukomaza ili uwe imara. Sasa kwanini usiwapigie makofi? Wapongeze, hata ikiwezekana, washukuru!
Washukuru mabundi maishani mwako, maana hawata kuacha vile ulivyo.
*******




Asante kwa muda wako kusoma makala hii. Naomba unisaidie kushare ili wengine watambue u muhimu wa mabundi maishani mwao
 
UMEPOTEZA NDOTO ZANGU









  • UMEPOTEZA NDOTO ZANGU



    Akiwa anaendesha gari Mr.Lee alitekwa na mawazo sana, Biashara,familia sambamba na majukumu mengine ndiyo yaliyoifanya akili yake iwe bize kuchanganua hayo huku ikisahau kama yupo barabarani akiendesha gari.
    Kufumba na kufumbua macho yake yalishindwa kuushawishi ubongo wake kuwa yamemuona mutu akikatisha barabara katika zebra kisha kuchukua maamuzi, badala yake alijikuta anashituka ghafla na kubana breki bila hata kukwepesha gari. Mara alifumba macho huku meno akiwa ameyang’ata, kwa mbali ngome za masikio yake yalisikia sauti ya kishindo kidogo cha kugonga kitu, huku sauti ile ikiwa imesindikizwa na sauti nyororo ila yenye uhalisia wa maumivu ndani yake.
    Ghafla ufahamu ulimrejea na kugundua amemgonga mtu.alifungua mrango haraka na kutoka kwenda kumtazama. Masikini Mr. Lee wala hakuamini macho yake baada ya kumwona dada mrembo aliyekuwa akifanya mazoezi kwa kuendesha baiskeli amelala chini huku damu nyingi zikimtoka eneo la kichwani. Alimfata haraka na kuanza kumuinua huku akimsemesha, alifanya hayo huku akitaza kila upande ili aombe msaada kwa watu wamsaidie kumuinua amkimbize hospitali , huwenda akaokoa maisha yake. Alipoona watu wapo mbali kidogo aliamua ajaribu kumuinua yeye mwenyewe.
    Alipoanza kumuinua yule mwanamke mrembo alimshika mkono Mr. Lee na kujitahidi kuzungumza. Mr. Lee alipoona mwanamke yule anataka kuzungumza alichutama kando huku wakiwa wameshikana mikono na kumsikiliza kisha mwanamke aliyazungumza haya
    “umepoteza ndoto zangu,naondoka na jeraha moyoni mwangu. Nilisoma kwa shida sana kutokana na hali duni ya wazazi wangu, sikukata tamaa kwakuwa nilikuwa nina ndoto maishani mwangu.tazama upepoteza ndoto zangu. Wazazi wangu walinisomesha kwa kujinyima huku wakiamini ipo siku nitakuwa msaada kwao, maombezi yao kila siku juu yangu ili nifanikiwe na nije kuwasaidia siamini kama kweli yameishia hapa. Umepoteza ndoto zangu. Nina wiki moja tu tangu nilipoajiriwa kwenye kampuni kubwa na kusaini mshahara mnono, sijaonja hata harufu ya mshahara huo wala matunda ya elimu yangu niliyoipigania hadi kufikia level ya Masters.
    Sijui wazazi wangu, ndugu zangu, na marafiki zangu watalipokeaje hili kwakuwa nilikuwa ni mtu mwenye matumaini makubwa ya kuja kuwasaidia siku za usoni, umepoteza nguvukazi ya Taifa maana serikali ilikuwa ikinitanbua kutokana na elimu yangu. Tazama umepoteza ndoto zangu wala siwezi kupona tena.ni uzembe tu wala siyo kingine maana hii ni zebra.
    Hujanipoteza mimi pekee bali umetupoteza wawili, nina mtoto tumboni, sijui mume wangu ambaye nimetoka kufunga naye ndoa miezi mitatu iliyopita ataipokeaje taarifa hii.
    Hata hivyo huwenda siyo kosa lako, huwenda siku zangu zimetimia, haustahili kulaumiwa wala kuadhibiwa juu ya hili. Ila mwanangu, mwanangu, mwanangu…..”
    Alipokwisha kuzungumza hayo dada yule alikata roho huku akiwa ameshikana mkono na Mr. Lee. UMEPOTEZA NDOTO ZANGU ni maneno ambayo aliyatilia mkazo sana ila haikuwa na jinsi, hatima ya maisha yake iliishia pale. Mr. Lee hakuamini kitendo kile, alijikuta anapiga magoni anaangua kilio kizito huku akiwa amejiinamia. Aliijutia sana nafsi yake, akiwa bado amejiinamia huku akilia alitamani dada yule apone kisha ampe hata nusu ya utajiri wake.
    Mr. Lee alipoinua uso na kumtazama dada yule kwa mara nyingine huku akilia, alishangaa kuona watu wamejaa wamemzunguka wakiwemo polisi. Walimshika wakamfunga pingu na kuongoza kwenye gari la polisi. Kabla hajapanda kwenye gari aligeuka na kumtazama dada yule, alishuhudia mwili wake umechukuliwa kwenye machera ukielekezwa kupakiwa kwenye gari la wagonjwa. Aliutazama mwili ule hadi unapakiwa na kufungwa mlango “UMEPOTEZA NDOTO ZANGU” ni neon la mwisho yalilojirudia kichwani mwake kisha akajinenea moyoni “NASTAHILI KUHUKUMIWA” na kuingia ndani ya gari.

    MWISHO

    ****************

    FUNZO:

    Kwa upande wangu ingawa simulizi hiyo amezungumziwa dereva wa gari ambaye alikatisha maisha ya msichana mwenye ndoto za kufika mbali, ila wapo wengine ambao si madereva na wanatenda hayo. Mfano wanaume kuwapa ujauzito wanawake na kushindwa kuendelea na masomo kisha kuwatelekeza wakilea wenyewe, wafanyakazi kuwasababishia wafanyakazi wenzao kufukuzwa kazi kutokana na wivu, kulogana kisa mtu anafanya vitu vya maendeleo, na vingine vingi. Siku zote kumfanyia mtu kitu ambacho hastahili kufanyiwa au kitu kile ukifanyiwa wewe hupendezwi nacho ni dhahili unatenda unyama ambao mwanadamu hastahili kutendewa.
    Yatupasa tuwe makini kwa kila jambo,tutafakari kwa kina kabla ya kutenda. uzembe wako mdogo sana unaweza ukamgarimu mwenzio kwakiasi kikubwa na kumpotezea dira kabisa kwa kitu alichokuwa anakitumainia.
 
  • HUYU NDIYE MAMA YANGU





  • SIMULIZI FUPI: HUYU NDIYE MAMA YANGU



    Kwa: wanawake wote!!



    TETESI zilizokuwa zimezagaa mtaani zilinitatanisha sana, nilijua kuwa kila nilipokuwa napita basi watu walinyoosheana vidole na kusema lolote ambalo waliweza kusema.



    Ni kweli sikujua rasmi ni maneno gani walikuwa wanasema lakini hayakuwa mazuri.



    Ningeweza vipi sasa kuwazuia watu kusema wakati walikuwa wamepewa vinywa ili waweze kusema. Niliyaishi maisha yangu bila kujishughulisha na maneno yao, ilikuwa ngumu lakini niliweza.



    Nilijua kilichokuwa kinawachanganya zaidi ni maisha yangu duni, kulalia mkeka pamoja na kuwa na sufuria mbili ndogo.



    Nilitabasamu na kujiuliza ikiwa wanapenda niwe na maisha bora basi na waninunulie vitu wanavyotaka niwe navyo na hapo watakuwa na haki ya kusema lolote.



    Nilizisikia tetesi eti wananiita mimi mshirikina, wengine wakazusha eti mimi ni jambazi na nimejenga majumba mengi ya kifahari.



    Nikatabasamu na kumega tonge la ugali nikalichovya katika mlenda wangu nikalimeza likadondoka tumboni kunipa shibe mimi siku ziendelee.



    Sikujua wenzangu kuwa maisha yasiyowahusu yalikuwa yanawanyima amani kabisa na ikafika siku ya siku ile naamka tu nakutana na lundo la watu mlangoni kwangu.



    Nikajiuliza je litakuwa ni tatizo la kodi au? Lakini kodi yote nilikuwa nimelipa, kama ni usafi nilikuwa nafanya kila inapofika zamu yangu, sasa ni kitu gani kimewaleta pale katika mlango wangu.



    Nikatoka nje na hapo nikakutana na mikono iliyobeba mawe, mapanga na marungu!!



    Moyo wangu ukapiga kwa nguvu sana, nikajiuliza ni kitu gani tena hiki kinanitokea mimi. Nikiwa bado sijapata jibu kijana mmoja mbabe wa umbo akawatuliza wenzake kisha akazungumza.



    “Akilimali unashutumiwa kwa wizi wa kuvunja na kuiba kwenye duka la mzee Yahaya, hatupo hapa kwa ajili ya shari bali kuzirudisha pesa zote ulizochukua katika meza iliyopo pale…” kabla hajamalizia mama mmoja mfupi mweusi akadakia, “Unamweleza nini sasa wakati anajua ni meza ipi inayozungumziwa mbona unambembeleza….”



    Yule kijana akaendelea!!



    “Tupatie hizo pesa nasi tutakupeleka polisi tu lakini kama hautoi pesa hata polisi haufiki tutakuua hapahapa huu mtaa haujawahi kuwa na wezi kabla haujahamia hapa Akilimali. Ni kitu gani hiki unatuletea katika mtaa wetu……” alizungumza kwa jazba. Kisha mwanamke mwingine naye akadakia.



    “Hata mtu hajulikani dada, baba, wala kaka yake mtu gani huyu asiyekuwa hata na mama wa kumtembelea walau tumjue….”



    Alipomaliza kuzungumza palikuwa kimya. Nilijua kuwa jambo lililokuwa mbele yangu halikuwa dogo hivyo nilitakiwa kuwa mtulivu na mwenye busara haswa!!



    Nikajikohoza wakatulia kunisikiliza. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kuzungumza mbele ya kundi la watu kama vile.



    “Niliisubiri hii siku kwa hamu ya kuzungumza nanyi katika umoja huu, nisingeweza kumfuata kila mmoja na kuzungumza naye japokuwa niliyasikia maneno yenu sana tu wanaume kwa wanawake wakubwa kwa wadogo. Imekuwa heri imekuwa siku hii, kabla sijaanza kuzungumza nawahakikishia kuwa sina pesa ya mtu na nikimaliza kuzungumza natoa ruhusa kwa yeyote anayeweza kuua na aniue mimi… sina chochote cha kusema ni urithi, mkeka wangu huu atakayeona yafaa basi ataupeleka katika kituo cha watoto yatima wanahitaji sana kwa ajili ya kujihifadhi usiku, na sufuria zangu hizi ziende hukohuko. Ewe mwanamke uliyeupaza mdomo wako eti wataka kumjua mama yangu napenda nikuelezee juu ya mama yangu wewe na wenzako wote wamsikie na kumjua.



    Mama yangu ni kahaba muda kama huu amelala hoi kitandani kutokana na suluba ambazo nyinyi wanaume mmepa usiku wa manane, mlioutumia mwili wake na kuacha kumlipa, mama yangu yupo jalalani sasa amechanganyikiwa kutokana na ugumu wa maisha na baadaye wajinga wajinga kati yenu waka,mbaka akakumbwa na kichaa cha mimba yupo majalalani anakula makombo yenu mama yangu yu hai anaishi, anaishi katika nyumba zenu mama yangu ni mtu mbaya sana mama yangu ni yule mama wa kambo ambaye haoni kama ni haki yule mtoto mdogo pale nyumani akitabasamu walau kwa sasa moja tu, anamuonea na kumkosea haki zake pasi na sababu mama yangu ni mbaya kiasi hicho na sidhani kama mngetamani kumuona, yupo mama yangu na anaishi na muda huu ninaozungumza na mimi yupo hospitali akitoa mimba ya ambaye angekuja kuwa mdogo wangu, simpendi mama yangu na kama hamuamini basi muende hospitali sasa mtamkuta akiwa na mwanaume anayejiita daktari wakishirikiana kumuua mdogo wangu, wakati mwingine simlaumu mama yangu ila nawalaumu nyie wanaume washenzi na mapanga yenu mnaowaingilia na kuwajaza mimba kisha mnawakataa. Mnagoma hata kuzihudumia hizo mimba mlizowajaza na wengine hata pesa ya kutolea hiyo mimba hawatoi eti mama yangu aitafute hiyo pesa ya kufanyia mauaji yeye mwenyewe.



    Nikasita kuzungumza nikawatazama na sasa sikuweza kuyazuia machozi yangu, nikajifuta kidogo kisha nikaendelea kuzuingumza.



    “Ni huyu ndiye mama yangu, mama ambaye kwenu mnamuita changudoa bila aibu mnamnunua, ni huyu huyu mnayemuita baamedi kila kukicha mnambughudhi kumshika sehemu zake nyeti hovyo na kumwagia bia zenu huku mkimtukana matusi ya nguoni, wengine mnafikia hatua hadi ya kumtukania mama yake… naam! Yule mama yake baamedi ambaye mnamtusi ndiye mama yangu, mmenijalia hapa na mapanga na marungu nazungumza nanyi viumbe mnaojipatia sheria mikononi, mnataka kumjua mama yangu wakati mama zangu mnaishi nao katika nyumba zenu mnawaita mahausgeli mnawanyanyasa na kuwaumiza sana nafsi zao, mama zao walikwishatangulia mbele za haki walitangulia pamoja na mama yangu lakini bado nina mama wengi sana duniani. Mama yangu ni yule mwanamke unayemuita mke wako kipenzi na kila siku unampiga bila huruma, mama yangu ni yule hawara yako mpumbavu anayejua kuwa umeoa nab ado anadai kuwa anakupenda, mama yangu ni yule binti wa miaka 18 nambaye bila aibu wewe mzee mwenye rungu na miaka yako 45 unashiriki naye mapenzi hivi wazazi wake wataajisikiaje umewahi kujiuliza?? Nasema na nyinyi mbona mpo kimya, nasema na nyinyi mama zangu nasema na nyiyi kaka zangu tuliozaliwa tumbo moja, nasema na baba zangu, nasema na wajomba na wadogo zangu… mkitaka kumjua mama yangu mnyanyue mikono yenu juu kisha mmwombe mwenyezi Mungu awarudishe katika matumbo mliyotokea kisha mzaliwe tena na huyo atakayewazaa NDIYE MAMA YANGU! Na baada ya hapo mkiishusha mikono yenu myashike mapanga na marungu yenu mniue mimi ndugu yenu. Naam! Natamani kufa ili nikaishia na mama zangu huenda huko ni sehemu sahihi zaidi….”……..



    Nikashusha pumzi zangu kisha nikainama huku machozi yakiyafumba macho yangu, sikuweza kuona mbele na nilikuwa nimejiandaa kwa kila kitu!!



    Baada ya dakika moja machozi yakiwa yamepungua niliunyanyua uso wangu juu, na sikukuta mtu zaidi ya yule mama aliyenihoji juu ya wapi yupo mama yangu!!



    Nilishuka chini na kumfikia alikuwa amepiga magoti, nikamyanyua na kisha kumkumbatia.



    Huku akiwa analia akaniambia maneno machache.



    “Akiliamali kijana wangu naomba msamaha wako na ninaomba kuanzia sasa niwe mama yako wa hiari.”



    Nilimkaribia zaidi na kumkumbatia yule mama na hapo nikamwambia WEWE NI MAMA YANGU!!!





    JIFUNZE:



    Ndugu yako si yule tu ambaye mnachangia damu ama tumbo moja. Bali ni yeyote yule ambaye anaweza kuwa nawe wakati wa machozi, kicheko.



    MWISHO
 
  • MKOMBOZI





  • SIMULIZI FUPI : MKOMBOZI

    MTUNZI : W. LYAMBA



    Katika kijiji cha Matare wilaya ya Mugumu Serengeti, bwana Wambura alikamatwa kwa kesi ya kusingiziwa na kuhukumiwa kwenda jela miaka mitatu.

    Huku nyuma akiacha mke na watoto wanne waliokuwa wanasoma. Hukumu hiyo ilimtesa sana kichwa chake, alitamani kila mtu anayemhisi kuwa ana makosa aingie katika moyo wake na kuupata ukweli.

    Alilia na umaskini wake, lambda angepata wakili mzuri angeweza kumtetea, kumkosa wakili kukahalalisha kifungo hicho!!

    Alikwenda gerezani huku akiumia sana rohoni. Aliyaanza maisha mapya kwa shida sana, akawa mnyonge kila mara na mwili ukapoteza afya kiujumla.

    Huko gerezani alifanikiwa kupata rafiki aliyekuwa na cheo ama jukumu la uzikaji wa wafungwa hasahasa ambao hawakuwa na ndugu ama ambao ndugu zao huwa hawajitokezi pale gerezani.

    Mzikaji alijaribu sana kumtia nguvu Wambura na kumwaminisha kuwa hiyo ilikuwa hatua tu ya maisha anapaswa kuizoea na siku moja ukweli utajulikana tu! Bwana Wambura maneno ya mzikaji hayakumuingia kabisa.. alizidi kunyong’onyea.

    “Siwezi kuvumilia kukaa gerezani miaka mitatu…..kama unajali kilio changu nisaidie nitoroke kwa namna yoyote ile ndugu yangu!!” Wambura alimsihi mzikaji.



    SIKU MOJA mzikaji akamwambia Wambura kuwa msaada umepatikana. Lakini yataka moyo!!

    “Nipo tayari kwa lolote ilimradi tu nitoke humu!!” alijibu kwa msisitizo huku akimtegea sikio mzikaji.

    “Msaada pekee wa kukutorosha humu ndani ni kwa njia ya jeneza… yaani mfungwa akifa mimi nakuunganisha naye kwenye jenerza…..” akashusha pumzi kisha akaendelea “Wewe ukisikia kengere ya msiba, njoo mara moja kwenye chumba cha maiti, utakuta tayari sanduku liko katikati ya chumba linakuwa halijafungwa, funua kifunioko ingia ndani yake ulale pembeni ya maiti kwani sanduku huwa kubwa la kutosha kila aina ya maiti na hata miili miwili inaingia. Kisha nitakuja na kulipigilia misumari. Baada ya muda tutalipakia kwenye gari na kutoka kwenda nje ya gereza makaburini nikiongozana na baadhi ya wafungwa na maaskari magereza.

    Tutakuzika huko lakini baada ya dakika 20 hadi 30 nitarudi kukufukua. Hautaweza kushindwa kupumua kwa dakika hizo, utatoka ukiwa huru.”



    JAPOKUWA wazo lilikuwa zuri lakini lilimtisha sana Wambura. Hata hivyo akaona afadhali afanye hivyo kuliko kukaa gerezani miaka mitatu bila kosa.



    Siku moja akasikia kengere ya msiba. Akafanya kama alivyoelekezwa na mzikaji. Akaenda na kuingia chumba cha maiti. Kweli akalikuta sanduku, akiwa na hofu kuu akaingia na kulala pembeni ya maiti iliyokuwepo. Mara akasikia mtu ameingia na kulipigilia msumari sanduku. Muda mfupi baadaye sanduku likainuliwa na kuwekwa kwenye gari.

    Gari ikatoka nje ya gereza hadi makaburini. Sanduku likashushwa na kuwekwa kaburini na kuanza kufukiwa.

    Wambura alijitahidi sana kuvumilia japo hofu ilizidi kutanda. Alimtegemea sana mzikaji na alianza kumuona mkombozi wa maisha yake.

    Kama alivyoambiwa, akasubiri dakika kumi, ishirini.. zikapita kimya!!

    Dakika thelathini kimya. Joto nalo likazidi kuongezeka.

    “Nitavumilia hadi afike…” alijisemea kisha akajiongezea kauli ya ujasiri.

    “Kama nilitakiwa kuishi gerezani miaka mitatu kivipi dakika kadhaa za hapa kaburini”



    KWA kuwa alishakaa gerezani kwa muda kiasi akatamani kujua aliyekufa ni nani… ni kwewli aliogopa kuitazama maiti lakini aliona kama inatisha zaidi ikiwa imefunikwa vile kuliko ikiwa wazi.

    Akaifunua upande wa usoni… Kwa kuwa kulikuwa na giza nene alikodoa sana macho kuitazama.

    LAHAULA!!! MACHO YAKAKUTANA NA SURA YA MZIKAJI!!!

    MZIKAJI ALIKUWA AMEKUFA NA AMEZIKWA NA AHADI ZAKE ZA UKOMBOZI!!



    ________________

    FUNZO::

    Usimtegemee sana mwanadamu katika maisha yako, kwanza ni dhambi!!

    Pili mwanadamu anakumbana na vikwazo kama unavyokumbana navyo wewe hadi kumwendea yeye. Hivyo kumpatia maisha yako ni kuzidi kuyaweka hatarini zaidi!!

    Umeonewa umesingiziwa unanyanyaswa….. mwachie Mungu afanye maamuzi…

    _______________

    Haya mzikaji aliyetegemea atamfukua naye ni maiti…… tazama mateso atakayoyapata hadi kufa kwake…..

    Bila shaka atatamani kurudi gerezani kwa miaka mingine kumi lakini haitawezekana tena!!!
 
MAUTI YALIBISHA MLANGONI







  • MAUTI YALIBISHA MLANGONI



    Daktari Mogiri alifungua mlango polepole na kutoka nje. Alinikuta nimeketi kwa fomu ndefu hapo nje ya wodi nikisubiri. Nilikuwa nimejishika tama na kuzama katika luja ya mawazo. Ni kweli kwamba mshika tama huwa analo moyoni.nilimwangalia kwa macho ya atiati nikitazamiakusikia mengi kumhusu mke wangu Zuhura. Sikujua kilichomtendekea tangu aingizwe mle ndani ya chumba cha upasuaji, masaa matano yaliyopita. Kumbe kweli usilolijua ni kama usiku wa manane.

    Akilini mwangu, yaliyotendeka yalikuwa yangali mbichi mno. Nilitoka kazini mapema alasiri hiyo na kurudi nyumbani kwani sikuwa na kazi nyingi ya kufanya. Nikafululiza hadi mlangoni na kubisha bila kupata jibu.wanenao husema kuwa kimya kingi kina mshindo. Nilifungua mlango polepole na kuingia ili kugundua kilichonisubiri. Lo! Ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni.

    Zuhura alikuwa kalala sakafuni, akigaaga na kufurukuta kwa uchungu na kutoa sauti ya maumivu. Aliye na macho haambiwi tazama. Nilielewa fika kuwasiku zake za kujifungua zilikuwa zimewadia. Kasha akajikazana kutamka,



    “Nisaidie jamani.” Kisha akanyamaa ghafla na kuendelea kufurukuta. Fimbo ya mbali haiui nyoki kwa hivyo, niliwaita majirani walionipa usaidizi wa kutafuta rukwama ili kumpeleka hospitalini. Ilikuwa nadra na adimu kama wali wa daku kuona magari katika sehemu tuliyoishi. Sehemu ya Ngomani. Kama wakaazi wa pale, tulizoea maisha hayo na haikuwa ajabu kumwona akipanda au kuabiri ‘gari’ letu- rukwama. tulimpeleka kwa zahanati ya kipekee hapo mjini na kupata kuwa muuguzi hakuwepo. Nikawa nimechanganyikiwa nisijue la kufanya jirani mmoja aliposhauri tumkimbize Zuhura katika hospitali ya wilaya.





    Hospitali ya Afueni ilijulikana kote kwa kuwa ya bei ghali. Lakini nilishawishika na kukubali kwani maisha ya Zuhura ilikuwa muhimu kuliko pesa. Tukaandamana hadi kule. Hisia za uchovu na kutamauka tayari zilianza kuninyemelea nikawa nafuata wenzangu tu kama bendera inavyofuata upepo au maji inavyofuata mkondo. Moyo wangu ulijaa ukunjufu kwa ukarimu walionionyesha.

    Nikawa nimeketi hapo nikisubiri matokeo ya daktari waliokuwa wakimhudumia. Takribani miaka mine sasa tangu tufunge ndoa, Zuhura alibaki tasa asiweze kupata motto hata mmoja. Mara nyingi nilimsikia akimlilia Muumba wake na kusali. Hatimaye maombi yake yalijibiwa na sasa tulikuwa tukitarajia mwana wetu wa kwanza. Tayari nilikuwa na cheche za matumaini. Penye nia pana njia eti. Hata nikakisia kuwa atakuwa msichana na tungemwita Zawadi. Pengine kama ishara kuwa Maulana alitupa zawadi baada ya miaka. Nilisahau kabisa onyo la wahenga eti usikate kanzu kabla motto hajazaliwa.

    Daktari Mogiri akanisongelea na tukaanza majadiliano. Mazungumzo ya kiume kama alivyoyataja. Mara kwa mara niliwaona wauguzi wakipitapita kushoto-kulia wakiendelea na shughuli zao. Daktari alikuwa amemaliza kazi yake muhimu mle ndani.

    “Unatarajia mtoto wa jinsia ipi? Mbona? Mtamwita nani? Utampa Zuhura zawadi gain kwa kazi aliyofanya?” aliniuliza maswali chungu nzima. Maswali yenyewe yakatuongoza katika ulimwengu wa gumzo. Tukazungumza na kupitiza wakati bila hata kugundua. Hata chembechembe za wasiwasi nilizokuwa nazo zikanitoka kabisa. Nikajihisi huru, kiumbe mpya na nikavaa piku la tabasamu.

    Ndipo sasa daktari akaamua kunipasulia mbarika hatimaye. Akanidokezea kuwa Zuhura alikuwa amejifungua motto wa kiume mwenye buheri wa afya. Singejizuia tena.licha ya kuwa usiku ulikuwa umeingia, nilirukaruka kwa furaha kupindukia ungedhani mwenda wazimu. Nikatamani majirani wote waliomleta Zuhura wangalikuwepo lakini walikuwa washarudi makwao kushughulikia jamii zao. Nikaanza kuwazia jina la motto wetu nikiwa katika hali ya kurukaruka bado.



    “Tutamwita Bahati” Nilisema kwa nguvu huku nimemkumbatia daktari kwa furaha macho yangu nikiwa nimeyafumba.

    Daktari alikuwa akinitazama tu kwa wakati wote huo pasi na la kusema. Lakini nilipoanza kuuelekea mlango wa chumba alimolazwa mke wangu, alinisitisha na kunizuia. Akaniomba kusubiri lakini furaha iliyonijaa ikanifanya kuwa kiziwi. Nikajitia pamba masikioni nisisikie la mwadhini wala la mteka maji msikitini.

    Akanivuta kando kidogo na kunidokezea kuwa Zuhura mwenyewe alifuja na kupoteza damu nyingi hivyo basi asingeweza kuishi! Kwa kifupi, aliniambia kuwa mke wangu alikuwa amea…sikuyaamini macho na masikio yangu. Maneno hayo yalinifanya kiuwa chakaramu zaidi. Yalinikata maini, yakanikera na kunikereketa ajabu. Uso wangu uliokuwa na furaha ulibadilika ghafla na kufinga. Kwa nguvu kama za tembo na hasira za mkizi, niliuendea ule mlango bila kumjali yeyote wala chochote. Alinifuata na kujaribu kunivuta nyuma huku akiniliwaza. Juhudi zake zikangonga mwamba.

    Sikujua kuwa daktari ni watu wenye vipawa vha kuwapumbaza watu namna hiyo! Kwa muda wote huo, daktari alikuwa amejua ukweli na kunificha kwa kunishirikisha katika mazungumzo. Pengine hayo ni baadhi ya mafunzo wanayopewa wanaposomea fani ya udaktari lakini ubunifu wa ya Mogiri ulishinda wote. Niliajabia ubunifu wake!





    Niliingia kwa fujo na rabsha kama mfungwa aliyeachiliwa huru. Wauguzi wakashtuka na kujaribu kunizuia. Daktari akaingia na kuagiza nionyeshwe mtoto. Nikaelekezwa hadi alikokuwa. Mtanashati ajabu na mwenye afya ungedhani kutoka mbinguni. Alilala kwa utulivu asijue mamake alikokuwa. Laiti angejua. Lakini kuonyeshwa mtoto haikunisaidia wala kinutuliza. Nani angekilisha,akivishe na kukilinda siku zote? Unyama upi huo kuingizwa katika ulimwengu na kuachwa na mwenyeji wako hata kabla ya kumwona ana kwa ana? Nilijihurumia, nikamhurumia malaika wa Mungu. Machozi yakanidondoka kama mtoto na nikayaacha kumwagika bila aibu.

    Kwa mwongozo wa daktari, nilifululiza hadi alikolazwa Zuhura. Msichana mrembo aliyeumbwa akaumbika alikuwa amelala kwa upole na utulivu asijue hata wakati wa kuamka. Alikuwa amefunikwa vizuri hata usingedhani ni maiti. Ikanifanya kutoamini na kuanza kumwamsha. “Zuhura, amka umwone Bahati mwana wetu.”





    Akawa haoni, hasemezi,hatikisiki. Kimya kikajiri. Niliinama kando yake na kumtikisa tena mara hii kwa nguvu machozi zaidi yakinitoka. Nikamshauri ainuke twende kwetu tusherehekee kuzaliwa kwa mtoto wetu. “Zuhura” niliita mara ya mwisho kwa nguvu na pumzi ikaniishia.

    Sauti nyororo ya Zuhura aliyekuwa amelala kando yangu usiku wote ilinigutusha kutoka usingizini ikinijuza kuwa kumekucha. Miale ya jua nayo ilikuwa imeshachomoza nje. Furaha iliyoje kupata kuwa hiyo ilikuwa ndoto ya ajabu.
 
NJOZI







  • SIMULIZI FUPI : NJOZI



    Jua lilikwisha zama lakini bado nyuma liliacha mikia yake ya uchengu wa mwangaza uliopinganisha rangi tofautitofauti kama ishara ya heri njema kwa wote walioipenda siku hiyo.Hadi kufikia wakati huo, bado tulikuwa baharini tukikamilisha shughuli zetu za uvuvi. Kweli ilikuwa siku njema. Tulibahatika kuwavua samaki wengi mno. Pengine kwa sababu unyavu wetu ulikuwa ungali mpya. Tulifurahia na kuchangamkia jambo hili hata tukawa tunapiga soga kwa ucheshi mwingi tukiisukuma mashua yetu kufelekea ukingoni mwa ziwa kwani kilicho na mwanzo kina mwisho.

    Mara kwa ghafla bin vuu, upepo mkali ukaanza kuvuma kwa nguvu kama za tembo. Mawimbi yakawa yameanza kujitunga tayari ziwani. Yalionekana yakijibeba, yakijiinua na kujibwaga tena kwa nguvu. Mawingu mazito tena meusi ti yakuogofya na kutisha yalikuwa yamekusanyika angani. Dalili ya mvua ni mawingu.





    Kuona vile,sote tuliingiwa na wasiwasi kama wa kuku mgeni. Mambo yalikuwa yakitambarika kila muda ulipozidi kuyoyoma. Ndiyo sasa tulikuwa tumefika katikati ya ziwahilo. Kwa utaratibu, mashua yetu ilianza kuongeza uzito hadi ikawa nzito kama nanga.isitoshe, Samaki tuliokuwa tumewavua pia walichangia uzito kuongezeka.

    Liloogofya zaidi ni kuwa hapakuwa na wavuvi wengine ziwani. Wote walikuwa washatoweka, wakatokomea na kuvogomea katika peo za macho yetu. Walikuwa wamerudi viamboni mwao kujiunga na jamaa zao. Nyoyo zetu zilitututa kwa nguvu kwa hofu. Upepo mkali ukaanza na kwa umbali tuliona miti zikiinama kusalimu amri. Lililonijia akilini ni tukio lililomkumba Yesu na wafuasi wake kama nilivyopata kuona kwenye sinema awali. Yesu alionekana kuunyosha mkono wake na kuamuru mawimbi kutulia na ghafla yakapoa. Nami bila kusita niliunyosha mkono wangu kama Yesu na kuyaamuru kutulia, jambo lililowafanya Nguviu na Suluhu kuangua vicheko licha ya hali iliyotawala. Lakini hakuna kilichobadilika. Pengine hatukuwa na imani dhabiti katika Bwana.





    Badala yake, mashua yetu ikaanza kuingia na kuzama majini. Tulijaribu kupunguza kiimo cha mashua yetu kama hatua ya kwanza. Ungeona namna walivyoruka, kuogelea na kupotelea majini kwa furaha, ungedhani ni wafungwa wameachiliwa huru baada ya hukumu ya kifo. Uzani ukapungua kidogo na tukarejelewa na cheche za matumaini.sote watatu tukawa tunasukuma mashua yetu kwa furaha. Tukaamua kufanya chapuchapu kuiondoa mashua yetu humo ziwani kwani giza lilikuw limeanza kutawazwa angani. Tena tulitaka kuondoka kabla mvua kuanza kunyesha. Wahenga huonya eti tahadhari kabla ya hatari.

    Sikuona wala kujua namna Suluhu alivyorudisha unyavu majini. Alitugutusha alipoanza kucheka na kuitana tumpe usaidizi wa kuuvuta unyavu huo kwani ulikuwa na windo nono. Nani asingefurahi? Tena umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu na aidha kidole kimoja hakivunji chawa. Sote tukauangana na kuanza kuburura hadi hapakuwa na dalili zozote za wavu kusonga.

    Sululu alisonga mbele zaidi na kuburura kwa nguvu zake zote na lo! Samaki mkubwa alijitokeza kwa rabsha,fujo, vurumai na kishindo na kisha kuzama ghafla na kufanya mashua yetu kutingizika. Kumbe mkia wake ulikuwa katika sehemu ya chini ya mashua yetu ndani ya maji. Hili tuligundua kwa namna mashua yetu ilivyorushwa. Tukawa majini tukipigania maisha yetu. Kwa mara ya kwanza nikakutana na kifo ana kwa ana. Tulianza kupiga mayowe kutaka usaidizi lakini vilio vyetu viliambulia patupu.

    Ikawa kila mtu na mzigo wake kwani mvua kubwa ilikuwa ishaanza kunyesha. Ngurumo za radi zilisikika na nguo zetu zikaloa chepechepe. Tukawa sasa ni kuogelea, haswa mimi niliyesalia na wiki moja tu kukalia mtihani wangu wa kitaifa wa kidato cha nne. Mashua yetu ilisombwa na maji na kuenda mbali mno. Potelea pote! Heri uzima kuliko mashua. Tulikuwa tumeogelea na hata kukaribia sana ukingoni.

    Lakini kila mara maji yalituzidi nguvu. Kumbe tulijiingiza katika ziwa bila mbinu toisha za kuogelea. Susulu alichelewa kupiga mayowe kwani tulipomsikia akifanya hivyo, tayari alikuwa akisukumwa na maji. Alikazana kutufikia na kutupa mkono wake lakini nguvu zilionekana kumwisha hadi akwa anapelekwa tu kama gogo. Tulijaribu kadri ya uwezo wetu kumfuata lakini wapi! Alikuwa keshakwenda zake. Msomaji, hisia zetu baada ya hapo zilikuwa hazielezeki.





    Tulipokuwa mita chache tu karibu na ukingo wa ziwa, Nguviu naye alilalama eti mguu wake ulikuwa umekamatwa na kitu kisichojulikana. Nikainua kichwa zaidi juu ya maji na kutamka kwa shida nikimwarifu kujikaza kufika ukingoni ili suluhisho lipatikane. Huo haukuwa wakati wa kusema mengi kwani maji yaliingia kinywani. Lakini aliendela kunung’unika zaidi.

    Nilionekana kujua kuogelea zaidi. Nikamwambia aushikilie mguu wangu mmoja nami niogelee hadi mwisho kisha nimvute. Japo ilikuwa ngumu kuogelea katika hali hiyo, nilijaribu na kufika ukingoni salama. ‘Mungu hamwachi mja wake.’ Nilisema kwa sauti. Mimi ndiye nilitangulia na kuona kipande cha gogo. Nikafurahi na tabasamu hafifu ikaonekana usoni mwangu.





    Bila kukawia, nililipanda gogo lenyewe na nikawa sasa namshawishi Nguviu kuunyosha mkono wake niukamate, kasha nimvute pia. Cheche za matumaini zilizotoweka awali zikarejea tena. Nguviu aliukaribia mkono wangu kwa utaratibu. Akaunyosha wake, nikaukamata na kuanza kumvuta.

    Mara tu aliponipa mkono wake wa pili, alivutwa ghafla na mara hii akazama zii. Nilikuwa tu nimeanza kupiga mayowe wakati lile gogo nililopanda lilizama pia na kunitumbukiza majini. Kumbe alikuwa ni mamba niliyemkanyaga kwa wakati huo wote! Kila kitu kikawa giza totoro kwangu.Nilipiga usiahi mkali na kujaribu kufungua macho. Ndipo nikagutuka kutoka usingizini. Nilikuta darasa zima linanizomea huku Susulu na Nguviu wakifa kwa vicheko vilivyopenya angani kana kwamba walikuwa na fununu ya kile nilichoota. Nduru ndiyo ilimfanya mwalimu wa Bayolojia kugundua kuwa nilikuwa nikilala darasani wakati wote tangu alipoanza kufunza alasiri hiyo. Nilijua kilichonisubiri baada ya kipindi kukamilika.
 
KILIO CHA VALENTINE







  • KILIO CHA VALENTINE

    (Aibu Kusimulia)

    ‘’Ni aibu kufikiria, itakuwa kusimulia?’’ Sauti ya Latifa ilisikika kupitia simu, ni dhahili alikuwa akilia.

    ‘’Pole sana ndugu yangu lakini aibu hadi simuni, tena ukitumia jila la kificho?’’Nilijaribu kumpooza kwa kuingiza utani kwenye maongezi yetu kumbe nilikuwa kama nimechochea kilio chake.

    Akakohoa na kuonesha kapaliwa mate, kisha akatulia na kuendelea kuongea safari hii sauti yake ilionesha huzuni na uchungu aliokuwa nao achana na aibu aliyokuwa nayo tangu awali.

    ‘’Jina feki ni kwako Michael, kwa Mungu na wahusika tunaolijua tukio hili ni jina halisi hata ningejiita kiumbe wa kutoka sayari ya mbali kuna watu duniani, Mungu na malaika zake wanalijua hili’’

    Alimeza mate na kutulia kwa muda (nadhani alikuwa akijaribu kufuta machozi yaliyokuwa hayakomi) kamasi zilisikika zikirudishwa zilikotoka.Kisha akaendelea.

    ‘’Michael ni aibu, aibu ambayo kama si ile hadithi ya ‘Siri Yenye Mateso’ ambayo ilinionesha kuwa kuna mambo ya aibu na kuumiza duniani basi nisingethubutu kukuambia suala hili’’ Nilikumbuka kile kisa kilichoandikwa na ndugu yangu Moringe Jonasy ingawa sikuona kama kulikuwa na kisa cha kutaajabisha na kuonewa aibu kwa binadamu wa zama hizi.

    ‘’Ile hadithi ilikuwaje?’’

    ‘’Umesahau Michael au unataka kunichora tuu?’’

    ‘’Hujakisoma?’’ Sauti yake sasa ilikuwa ni ya kulaumu.

    ‘’Nini, mtu kuzaa na shemeji yake? Daktari kuzaa na mgonjwa wake? Au familia kupata watoto wa jinsia moja?’’ Nilijaribu kukumbuka visa vya kile kitabu ambacho nilikuwa mmoja wa wahariri wake.

    ‘’Na kisa cha fumanizi la mwalimu?’’ Alinikumbusha akionekana kurejea kwenye ule ukawaida wake, sauti za kwikwi na kamasi kupandishwa kila muda zilikuwa zimekoma.

    ‘’Ahh sasa waogopa fumanizi, Latifa? comeon Latifa hiyo imekuwa kawaida sasa au ni fumanizi la baba na mwana?’’ Nilijaribu kumfanya aone tatizo lake lilikuwa la kawaida hiyo yote ilikuwa katika kumrejesha kwenye hali ya kuona tatizo lake si la kiwango cha juu sana duniani ,kama alivyokuwa amenitumia ujumbe mchana wa siku ile, ujumbe ambao niliupuuza baada ya kuona ulitoka kwenye namba nisiyoielewa, namba ya nje ya nchi, ilikuwa ni Vatcan.

    ‘’Bora ingekuwa hivyo Michael, si fumanizi la baba na mwana lakini ni fumanizi la rafiki’’Aliongea na kutulia akitaka lile aliloliongea liniingie lakini ni kama alivyotegemea niliangua kicheko ambacho kilinifanya nitokwe na chozi.

    ‘’Nilijua utacheka Michael, na yeyote ambaye ningempigia simu hii na kumweleza hili’’Aliongea kwa sauti ya kumaanisha na kunifanya nitafakari zaidi nikimuua mbu aliyekuwa akiifaidi damu yangu kwenye bega langu la kushoto.

    ‘’Lazima nicheke Tiffah kwani ajabu kwa marafiki kufumaniana?’’ Nilimuuliza nikimalizia kicheko changu kilichonitoa chozi pale kwenye ufukwe pweke wa ziwa, kwa mbali nikiona mwanga wa taa za wavuvi na zile za magari machache ng’ambo ya ziwa lile nchini Malawi.

    ‘’Mie siyo punguani wa kuogopa fumanizi la rafiki yangu na kuyatamani mauti Michael, kisa hiki ni tofauti na visa ulivyozoea kuviandika kwenye hadithi zako ni kisa cha ajabu ambacho nafsi yangu inaamini ni vyema kuufikishia ulimwengu jambo hili’’

    ‘’Naam nieleze hicho kisa nami nilie kama uliavyo maana najikuta nazidi kuchekeshwa’’

    ‘’Hujui Michael ni kisa kirefu kilichojaa mambo ya kustaajabisha ngoja nikusimulie tuu kama utalia ama utacheka ni uamuzi wako kwani ni kawaida watu kuchekeshwa na yanayoliza na kulizwa na yachekeshayo, cha msingi na cha lazima nakuomba uuandikie ulimwengu juu ya jambo hili ukikiweka kisa katika hadithi na uhalisi wake’’

    Hiyo ilikuwa ni sehemu ya maongezi kati ya rafiki yangu Michael na binti aliyejitambulisha kwa jina la Latifa, Michael ni rafiki yangu kipenzi ambaye alikuwa na kisa cha kweli cha ‘’Meseji kutoka kwa Marehemu Mchungaji’’ lakini kwa bahati mbaya alikutwa na matatizo yaliyomweka kitandani hadi leo.Matatizo mwendelezo wa kisa kile cha ajabu ambacho Valentine ya mwaka jana nilipoenda kumtembelea na kumweleza lengo langu la kuandika hadithi ya ‘’Chozi langu Valentine’’ akanipa simu yake na kunionesha sehemu ya kisa chake alichoanza kuandika juu ya binti huyo akikipa jina la K ilio cha Valentine na kunipa rekodi ya mazungumzo yake ambayo yeye aliyaandika kama yalivyokuwa lakini baada ya kuyasikiliza nikaamua kuandika kisa hiki kwa namna ninayoiweza zaidi kwani kuandika hadithi kwa mtindo wa Daiolojia huwa kunanipa tabu sana.

    Michael alininisisitiza Valentine ya mwaka huu kisa hiki kiwafikie wasomaji na iwe zawadi kwao nami nimeamua kukileta kwa namna niliyoona itamvutia hata Latifa kama yu hai kuko Ulaya.

    _______________

    Tarehe kumi na nne ya mwezi wa pili mwaka 2010 ilikuwa ni siku muhimu na ya kuvutia sana kwa vijana wawili wapenzi Sarah na Credo waliokuwa wanafunzi katika chuo kikuu cha Tumaini Iringa.Si tuu kwa kuwa ilikuwa ni siku ya wapendanao duniani kwote lakini siku hiyo ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya wapenzi hao.Wakiwa na furaha ya kuadhimisha siku hiyo kwa pamoja kwa mara ya pili kwani mara ya kwanza ilikuwa mwaka uliopita wakiwa si wapenzi ingawa tukio hilo liliwaunganisha na kuwafanya wawe wapenzi.

    Baada ya sherehe hiyo kufanyika kwenye ukumbi mdogo uliokuwa ng’ambo ya chuo cha Ruaha, Sarah na Credo waliachana na rafiki zao na kuelekea nyumbani ama tuseme vyumbani kwao walikokuwa wamepanga.Walipoachana na rafiki zao waliopanda daladala ama kutembea kwenda kwao kwa miguu kama walivyofanya akina Sarah, walikumbatiana na kupena mabusu kabla ya kuendelea na safari yao kuelekea nyuma ya Chuo cha Ruaha palipokuwa na makazi ama tuseme malazi yao huku wakiwa wameshikana mikono kimahaba.

    Kitu ambacho hawakukijua ama walikijua na kukisahau ama kukipuuza kutokana na vipombe walivyorashia vinywani mwao kuitoa ile aibu ya kusherekea na kuchangamka kunogesha sherehe yao iliyofana kutokana kuwa katika siku ambayo kwa waanzilishi ilikuwa ni ya wapendanao ila kwa sie wanamapokeo ni siku ya zinaa na ngono.Walipita kwenye kichaka kidogo kilichokuwa kikikaribia kona ya ukuta wa chuo na kuwakuta watu watatu waliokuwa wamekaa kwenye mawe wawili upande huu mmoja upande wa pili wa barabara ile iliyokuwa na majani mabichi yaliyonyeshewa na kimvua kidogo kilichokuwa kimenyesha jioni ya siku ile, kichaka kilichojulikana kwa uhatari wake kutokana na uwepo wa mateja.

    Ilikuwa ni saa saba usiku, na akili zao zikawaambia kuwa wale walikuuwa ni wavuta bangi tuu walioamua kuutumia usiku ule kwa kuwa na kitu wakipendacho, bangi.

    Naam hawakukosea watatu wale walikuwa wakivuta bangi na walianza kuzivuta muda mrefu tangu kile kimvua kilipoacha kunyesha na sasa walikuwa wamependana na bangi na bangi ilikuwa imeuzidi upendo wao na kuziteka akili zao.Walitenda akili zilivyowaambia na kwa bahati mbaya kila mmoja alizifuata, huyu alipowaza kuimba pambio waliimba wote, huyu alipowaza kulia walilia wote na mengine mengi waliyoyatoa waliyafanya kwa umoja wao.

    Sauti za wapenzi wale wakiimbiana nyimbo za mapenzi na kucheka kimahaba kutoka mbali ziliwafanya watulie kuwasikiliza, ulikuwa ni wimbo mmoja wa Kenny Rodgers aliokuwa akiuimba Credo ndio uliomfanya Sarah ajikute ajisahau kabisa kama walikuwa barabarani kwenye usiku ule uliokuwa na giza zito.Joto la huba lilijidhihirisha kupitia kiganja kilichofumbatiwa na kile cha mpenziwe.

    ‘’Simameni’’Sauti nzito ya kilevi iliyojaa amri ilisikika kutoka kwa mmoja wa wale waliokaa upande mmoja wa barabara wawili.

    ‘’Habari zenu mabraza’’

    ‘’Shikamooni’’ Sauti zao zilisikika kwa zamu huku Sarah akionekana mwenye uoga.

    Nywele zilimsimama kwa woga akizidi kujisogeza kwenye mwili wa mpenziwe ambaye naye alianza kuiona ile hatari waliyokuwa wameisogelea.

    ‘’Kaeni’’ Sauti ilitoka upande wa pili wa ile barabara.

    Waligwaya, na hilo ndilo walilolitaka wale wavuta bangi kwani waliwavamia na kuwaweka kwenye himaya yao, wawili wakimdhibiti Credo na mmoja akimdhibiti Sarah aliyekuwa akiomba msamaha kwa wale wahuni ambao hawakutaka kumsikia wa kumjali zaidi ya kumtaka anyamaze.

    Waliwaongoza hadi kwenye kichaka kikubwa kilichokuwa kilimani ambako huko walikutana na wahuni wengine ambao wao walikuwa wabwia unga.Hapo wakalazimishwa kuvuta bangi kitu ambacho Credo hakukikubali na kutaka kupambana nao kitu ambacho kilikuwa kosa kubwa sana kwani aliwafanya wale mabwana wachane na mpenziwe na kuanza kumpiga.

    ‘’Sarah kimbia’’ alimwambia mpenziwe huku akiendelea kupokea kipigo kizito kutoka kwa wale mateja na wavuta bangi wenye nguvu lakini kabla Sarah hajafanikiwa kuunyanyua mguu akimbie kutokana na hofu na ule upendo aliokuwa nao kwa mpenziwe alikamatwa na mmoja wa wale wavuta bangi wenye nguvu na kudhibitiwa kikamilifu akishuhudia kitu kilichomuumiza moyo wake.

    Kitu ambacho hakuweza kustahimili kukitazama kwani mpenziwe alivuliwa suruali yake na kuingiliwa kimwili na vijana wawili wavuta bangi waliowakuta pale barabarani na wakawaleta pale.

    Alifumba macho asiuone ule unyama lakini masikio yake yalizisikia sauti za kilio cha maumivu alichokitoa mpenziwe huku maneno ya kashfa , dhihaka na ya kukolea utamu kutoka kwa wale vijana wawili waokuwa wakipokezana kwa zamu yakimuumiza nafsi yake na kujikuta akitokwa na machozi na kilio ambacho kilizuiwa na yule mvutaji aliyemdhibiti kwa kumziba mdomo wake.

    Dakika ishirini za mateso na maumivu ya mwili na akili kwa wapenzi wale wawili zilikuwa kama muongo wa mateso mfululizo.Waliachiwa na kutakiwa kukimbia bila kugeuka huku wale walevi wa bangi na unga walipotelea kilimani wakikimbia na kucheka vicheko vilivyozidi kuzikata nyoyo za wapenzi wale ambao sasa badala ya mwanaume kumsaidia mwanamke safari hii mwanamke akawa akimsaidia mpenziwe kutembea kwani alikuwa akishindwa kutembea vyema.

    Waliofika walipopanga , ambapo Credo alikuwa akikaa peke yake na Sarah akikaa na rafiki yake na kwa Credo kukiwa kama kwake hivyo waliingia moja kwa moja kwa Credo na akachemsha maji na kumwogesha akimkanda.Baada ya hapo akampa dawa ya kutuliza maumivu iliyopunguza maumivu ya mwili lakini nafsi zao ziliumia sana kuliko hata maumivu ya mwili.

    Palipokucha palikucha na taarifa za Credo kuwa na homa ambayo wengi walijua ilitokana na uchovu wa kushereheka usiku uliopita.Walifanya siri ya wawili , siri iliyowaumiza peke yao kwani walijua kuvuja kwa siri hiyo ni aibu na mateso ya nafsi zao.

    Walifanikiwa kuifanya siri hiyo ikadumu hadi pale Credo alipopona na kuendelea na masomo kama kawaida .Kupona kwa Credo kulikuwa faraja kwao ingawa ile aibu haikukoma mioyoni mwao lakini ambacho hawakukijua kupona kwake ulikuwa ni mwanzo wa aibu nyingine kubwa iliyotisha.

    Wiki mbili baada ya Credo kupona Sarah alitamani tunda, tunda alilolipenda akalila na kulitamani zaidi kabla ya tukio lile la aibu lakini siku walipoamua kulila tunda ilikuwa ni msiba mwingine kwani Credo akahakikisha kile alichokuwa akikiwaza wakati akijiuguza.Aliwaza kwani licha ya kushikwa na kuguswa hapa na pale katika kuugua kwake alijikuta akili ikishtuka lakini mwili uligoma, siku zote uligoma katika usiri lakini siku ile uligoma kwenye usiri wa wawili ambao walianza kuuzoea ingawa usiri huo kwa Credo ulikuwa ni kama utumwa kwake kwani alijua lazima kulikuwa na siku ambayo usiri huo utapotea hasa siku akija kumkosea mwenye siri yake.

    Tofauti na alivyotegemea jambo lile lilimuumiza na kuonesha kumuumiza sana Sarah ambaye licha ya kuona kwa macho yake, hakuwa tayari kukubaliana na hali ile na kuwa mvumilivu akijaribu kila siku kwa mwezi mzima, kimya miezi miwili kimya mitatu hadi mwaka ulipoisha bado mwili wa Credo ulikataa kufanya kile akili yake ilitaka.

    Hadi walipohitimu Sarah aliondoka akiwa mnyonge na mwenye hofu sana, kitu ambacho kwa Credo ni kama alikuwa amekisahau, alijiweka mbali na Sarah na kumtaka atafute mwanaume asiye na tatizo kama lake.Sarah hakutaka kukubalina na jambo hilo akitaka kumsaidia mpenziwe kwa kutafuta tiba hospitalini jambo ambalo Credo hakulitaka akimwambia kuwa ule ulikuwa ni mwisho wake kuwa mwanaume sahihi kwani hakukuwa na matarajio ya kupona.

    Walipoachana chuoni ulikuwa ni mwisho wa mawasiliano yao kwani Credo alibadili namba za simu huku akiacha kuwasilina na marafiki ambao aliamini kuwa Sarah angehangaika kutafuta mawasiliano yake kupitia kwao.

    Huo ukawa mwisho wa Credo na Sarah, Sarah akiachiwa maumivu makali hadi pale alipopelekwa na wazazi wake nchini Afrika ya kusini alipobadili mazingira na marafiki kidogo kidogo yale maumivu yalipungua na kujikuta akisahau kumbukumbu za tukio lile zikija mara chache tofauti na hapo awali.

    Credo alipotoka Mjini Iringa aliingia jijini Arusha ambako ndiko kwao kabla ya kujizamisha jijini Dar es salaam ambako na huko alikutana na rafiki yake wa siku nyingi ambaye alikuwa akifanya kazi kwenye kampuni moja kubwa. Akipokea mshahara mnono ambao uliweza kumsitiri yeye na rafiki yake wa siku nyingi ambaye aliingia pale jijini kwa minajili ya kutafuta ajira akiwa na shahada yake ya Uandishi wa habari.

    Rafiki yake alikuwa amepanga nyumba ya vyumba vitatu na sebule, chumba kimoja wakikifanya ofisi yao na viwili vya kulala kila mmoja na cha kwake.Mara kwa mara rafiki yake alikuwa akitembelewa na nduguze hali iliyowafanya wakawa wanalala pamoja wakimpisha mgeni.

    Katika siku walizokuwa wakikaa pamoja waliburudika kwa kile rafiki yake alichokikusanya akimsaiidia kuendeleza ofisi ambayo Credo aliitumia kuandaa vipindi vingi ambavyo aliamini siku moja angekuja kuviuza kwenye vyombo mbalimbali vya habari.Kuna nyakati rafiki yake alikuwa akitembelewa na mpenzi wake aliyekuwa akifanya kazi nje ya nchi wakati mwingine rafikiye akija na vimada wengine alikuwa akiokota katika ulevi.

    Pombe ina mengi ya kushangaza na kustaajabisha lakini inapowekwa vingine huleta vioja vilivyo na hatari kubwa, ndivyo ilivyokuwa usiku mmoja walipokuwa wakinywa pombe Credo alifanikiwa kuitia pombe hiyo kitu kilichoamsha hisia za ajabu kwao kabla ya kuwaingiza kwenye ulimwengu wa ajabu.

    Huo ukawa mwanzo wa tendo chafu lichukizalo mbingu na nchi, tendo ambalo walilifanya kila walipopata nafasi.Credo akawa mke na rafikiye mume, pale walipofika wapenzi wa rafikiye Credo alibaki kuwa rafiki wa kweli akiwaita hao wanawake ni shemeji zake huku moyo wake ukiumia.Hali ilindelea hivyo hadi siku binti aliyejipa jina la Latifa alipoingia nchini kimya kimya siku ya Valentine ,ilikuwa ni usiku uliofanana na ule wa miaka kadhaa iliyopita pale Iringa kwani kijimvua kilikuwa kimetoka kunyesha na kutengeneza umande palipokuwa na nyasi na kuweka vidimbwi pale palipokuwa na bonde.

    Saa kama zile za tukio lile la kuaibisha pale Iringa , siku hiyo tukio hilo la kuaibisha lilifanyia chumbani kwa rafiki yake Credo na hakuonekana kulionea aibu hadi pale waliposhtushwa na kilio cha Latifa pale dirishani na kukurupuka , lakini walikuwa wamechelewa.

    Latifa aliumia sana , mtu aliyemwita shemeji alikuwa mke mwenzake si kwa kusikia bali kwa kuona kwa macho yake.Aliwaita na kuwauliza kulikoni huku akitokwa machozi Credo alieleza kila kitu akiomba msamaha kuwa ndiye mkosaji na alianza mchezo ule baada ya tukio lile pale Iringa kuumaliza uanaume wake akifanya tendo hilo na watu mbalimbali pale Iringa.Siku ile alikuwa amemtilia madawa kwenye kileo na kumsisimua mwili rafiki yake na amekuwa akifanya hivyo mara nyingi hadi alipoona tukio lile limezoeleka kwenye kichwa chake.Dawa hiyo alikuwa ameipata kwa shoga mwenzake mmoja pale Iringa na alikuwa akiitumia mara nyingi aliomba msamaha na kuhitaji msaada wa kutoka kwenye uchafu huo.

    Ndipo Latifa alipovaa ujasiri wa kuondoka nao hadi Italia kwenye hospitali moja wakipata matibabu ya kimwili na kiakili.Na baadaye akaelekea kwenye mji/nchi ya Vatican na kupiga simu ile kwa Michael mwandishi mwenzangu wa hadithi ambaye bado yupo kitandani akipigania uhai.

    Naam hiki ndicho kilio cha Valentine ambacho leo nimetimiza ahadi yangu kwa Michael kukileta kiwe funzo kwenu wasomaji wangu.

    Mwisho.
 
USIKIVU NI TIJA








  • SIMULIZI FUPI: USIKIVU NI TIJA







    Bwana Makalanga ni kijana anayependa sana kujituma katika kile alichokuwa anakifanya na hii ndo siri kubwa ya mafanikio yake. Bwana Makalanga kipindi alipokuwa anasoma alimuomba sana Mwenyezi ili amjalie apate kazi nzuri na hatimaye mke mwema mara baada ya kumaliza masomo yake.

    Bwana Makalanga mara baada ya kumaliza elimu ya chuo kikuu alifanikiwa kupata kazi katika moja ya kampuni ya mitandao ya simu hapa nchini kama msimamizi wa masoko. Baada ya mwaka mmoja maisha ya upweke yaani ya kukaa peke yake bila msaidizi aliyashindwa na hivyo akaanza kutafuta mke ili aweze kusaidiana katika mambo yake amabayo yeye alihisi anahitaji msaada.

    Mungu ni mwema kila wakati, bwana Makalanga alifanikiwa kupata mwanamke ambaye baadae alifunga naye ndoa na baada ya muda walipata watoto wawili,wote wakiwa wakiume.Mke wa Makalanga naye alikuwa ni mfanyakazi katika kampuni moja inahusika na uchimbaji na ununuaji wa madini, hivyo kwa kuwa walifanikiwa kununua gari kila siku asubuhi walikuwa wanatoka pamoja nyumbani kwenda kazini kwa kutumia huo usafiri wao.

    Mke wa bwana Makalanaga alikuwa anapenda sana kudeka,yaani kila wakati alipenda kumuona mumewe akiwa anamkumbatia ,anamlisha na hata kumuogesha,japo haikuwa rahisi sana kwa bwana Makalanga kuyatimiza hayo yote ila kila wakati alijitahidi kumfanya mkewe awe mwenye tabasamu na furaha wakati wote.

    Mrs Makalanga hakuishia hapo,zaidi na zaidi alipenda sana kufunguliwa mlango wa gari na mumewe lakini kwa upande wa bwana Makalanga hakuona umuhimu wowote wa yeye kumfungulia mlango wa gari mke wake ilihari mkewe ana mikono ya kumwezesha kufungua mlango mwenyewe,hivyo bwana Makalanga aliona ni kama usumbufu tu. Mke wa bwana Makalanga wala hakuchoka kumwimiza mumewe jinsi gani anavyojisiksia fahari akiafunguliwa malango wa gari wakati wa kuingia na kutoka ila hasa alipenda sana kufunguliwa na mumewe pindi wanaporejea kutoka kazini lakini bado bwana makalanga wala hakulitimiza hilo na aliona ni kama mambo ya kitoto na ya kuapoteza muda tu.

    Siku moja muda mfupi baada ya kumwacha mkewe kazini,majira ya asubuhi bwana makalanga alipata simu ya

    kushtusha kwani aliambiwa kuwa mkewe amepata ajari akiwa anavuka barabara na kufariki papopapo, bwana Makalanga aliumia sana sana kwani upendo wake kwa mkewe ni mkubwa sana,wafanyakazi wenzake walimfariji kuwa hiyo ni kazi ya Mungu hivyo yampasa kuvumilia kwani hakuna njia nyingine na hata akilia haitasaidia kumfanya mkewe kuwa hai tena.

    Siku ya mazishi ilipofika,mwili wa marehemu uliletwa kutoka hospitali kwa kutumia gari la hospitali ambayo mwili wake ulihifadhiwa,ndugu na jamaa walimtaka bwana Makalanga kufungua mlango wa gari ili mkewe atoke na aingizwe kwenye jeneza teyari kwa mazashi, baada ya kuambiwa hivyo bwana makalanga alilia sana kwa uchungu mkubwa sana kiasi cha watu wote kumshangaa kwa nini alilia sana kipindi anaufungua mlango wa gari ili kuutoa mwili wa marehemu.

    Baada ya mazishi,bwana Makalanga aliamua kuwaeleza ndugu na jamaa kwa nini alilia sana kipindi anaufungua mlango,aliwaambia alimkumbuka sana mkewe kipindi cha uhai wake alivyokuwa akimwambia amfungulie mlango akiwa hai lakini hakufanya hivyo na matokeo yake amekuja kufanya hivyo kipindi akiwa amekufa teyari.bwana Makalanga alijilaumu sana kwa nini hakumskiliza mkewe hata kwa siku moja tu, lakini lawama zake hazikuwa na nafasi tena wakati huo .
    MWISHO.
    Je umejifunza kitu? kama ndio usiache kumwambia mwenzako kuwa na tabia ya usikivu, kwani kitu kikishatokea hauwezi tena kurudisha muda nyuma ili usikie na kisitokee tena.
 
DAU LA MNYONGE







  • SIMULIZI FUPI : DAU LA MNYONGE

    MTUNZI : MWL DAMIAN CHIKAWE



    (hiki ni kisa cha kweli)

    Jina lake halisi (yaani jina alilopewa na wazazi wake) ni Ayubu Twisana,lakini akiwa kazini kwake anatambulika kama Mwalimu Twisana kwa upande wa waalimu wenzake na kwa wanafunzi wanamtambua kama "Chaunoko". Mwalimu Twisana ni mtoto pekee wa Mzee Twisana,akiwa na umri wa miaka saba kipindi anaaza shule ya msingi waalimu wote walimpenda sana kwa jinsi alivyokawa ana nidhamu akiwa darasani na hata nje ya darasa,kila wakati walitamani kuwa naye karibu ili asijiingize katika makundi ya wanafunzi wahuni,na hii ndio desturi ya waalimu wengi ,huwa wanapenda sana kuona mwanafunzi anakuwa na bidii,furaha ya mwalimu ni kuona pale ambapo wanafunzi wanafaulu vizuri.

    Ayubu Twisana 'Mwl Twisana' alikuwa mwanafunzi pekee aliyefaulu katika darasa lake na kuendelea na Elimu ya sekondari,wazazi wake walifurahi sana,waliuza kila kitu walichonacho ikiwemo baiskeli na mbuzi wao ili wapate pesa ya kumpeleka mtoto wao shuleni.

    Ayubu alifanikiwa kuanza Sekondari,na muda wote alikuwa anapenda kujifunza kwa bidii sana ili siku moja akawasaidie wazazi wake,hali ya umaskini ya nyumbani kwake ndio iliyomfanya apambane sana katika masomo na katu wala hakuwahi kujihusisha na masuala ya mapenzi ingawa wasichana wengi walikuwa wakijiringisha kwake kutokana na umahili wake darasani. Kijiji kizima kilimpenda sana na hata baadhi ya wazazi wengine walisikika wakiwaambia watoto wao "kwa nini musiwe kama mwenzenu Ayubu?".

    Miaka ilisonga na hatimaye Ayubu alimaliza elimu ya sekondari na kubahatika kupata alama za kumfanya aende kidato cha tano na sita.

    Pia huko nako alifanikiwa kupata alama za kwenda chuo kikuu,ila hakuweza kwenda huko kwani hakuwa na pesa za kuendelea na chuo kikuu na badala yake alienda chuo cha Ualimu ngazi ya diploma. Baada ya miaka miwili alifanikiwa kumaliza na akarudi kijijini kwao akisubiri apangiwe ajira.Mabinti wengi walitamani kuolewa na Ayubu,ila Ayubu wala hakuwa teyari kwa wakati huo kwani malengo yake yalikuwa bado hayajatimia na mpaka wakati huo Ayubu wala hakuwahi kumjua mwanamke.

    Ajira zilipotoka, Ayubu naye alipata na akapangiwa kituo cha kazi.Wazazi wake walifurahi sana na waliamini angalau shida zao zitakoma kwa kiasi fulani.

    Ayubu 'mwalimu Twisana' alikuwa mwalimu mchapa kazi sana,alijitahidi kwa kadri ya uwezo wake ili kuhakikisha nidhamu ya wanafunzi inarudi kwani aliikuta shule ikiwa na mazingira mabovu sana na wanafunzi pia hawakuwa na nidhamu.Kutokana na Juhudi zake baada ya muda Mwalimu Twisana alipewa kitengo cha nidhamu na huko ndiko lilikozaliwa jina la Chaunoko na pengine furaha yake ya kuwa mwalimu kuisha kabisa.Alipambana na wanafunzi wahuni wote, wanafunzi wengi walimchukia sana na hata baadhi ya wazazi wa wanafunzi hao walimchukia pia kwani walidhani anawaonea watoto wao.

    Siku moja alipoamka asubuhi alikuta nywele zake zote za kichwani zimenyolewa,pia alikuta ujumbe kwenye karatasi uliosomeka hivi "wewe si wa kwanza wala wa mwisho,walikuwepo wakaondoka na watakuja wataondoka,achana na watoto wetu,hill ni dogo tu,ukiendelea kuna baya zaidi litakupata".Mwalimu Twisana hakujali hilo aliendelea na kazi yake kama kawaida.Wanafunzi wahuni wakishirikiana na wazazi wajinga walifanya kila ubaya kwake lakini walishangaa kumuona mwalimu Twisana haachi kuwaadabisha wanafunzi.

    Wazazi walimtega mtego wao wa mwisho ambao huo waliamini hachomoki.Waliamua kumtumia mwanafunzi wa kike ili aonekane kama anashiriki naye mapenzi na hatimaye wamtie nguvuni.Ama kweli waliodhamiria hutenda!

    Siku moja majira ya usiku,Mwalimu Twisana alikwenda bafuni kuoga.Bafu lilikuwa nje ya nyumba hivyo alivyoenda kuoga aliacha mlango wa chumbani kwake wazi kwani alipanga chumba kimoja na alikuwa akiishi peke yake. Akiwa bafuni,huo ndo muda waliotumia wanakijiji kutimiza adhma yao,walimchukua msichana na kumvua nguo na kubaki na chupi tu kisha wakamwingiza chumbani kwake na kumwambia ajilaze kitandani kwake.

    Mwalimu Twisana akiwa hana hili wala like maskini wa Mungu alipomaliza kuoga alitoka bafuni,ile anataka kuingia tu ndani alishangaa sana kuona mkululo wa watu wakimwambia asimame.Alitii wito,mzee mmoja akasema

    "mimi ni Mwenyekiti wa mtaa huu,huyu ni mgambo wetu wa kijiji,na hawa ni wazazi ni wazazi wa binti anayeitwa Mariamu,wanamtafuta tangu jana ila kwa bahati nzuri tumepata taarifa kuwa yupo kwako na we we ndio unamrubuni kimapenzi,sasa tumekuja kupekua chumbani mwako ili tumchukue binti yetu"

    Huku akishangaa maelezo hayo marefu yaliyotolewa na mzee,mwalimu Twisana kwa kujiamini aliwaambia waingie ndani waangalie mtu wao,alijiamini kwa sababu aljiua ndani kwake hakuna mtu yeyote aliyemwacha.

    Walipoingia ndani,Mwalimu Twisana hakuyaamini macho alihisi ni macho ya mtu mwingine wala si yake,alishangaa kumkuta huyo binti akiwa kitandani kwake na chupi tu.Alihisi chumba kinatikisika ,yule mzee akasema "ndo huyu tumemkuta,unasemaje sasa mwalimu hii ndio kazi yenu inavyowatuma mfanye?"

    Mwalimu Twisana akasema "kwanza hata siwaelewi mnachokisema,huyu mtoto sijui ameingiaje humu"

    Yule MZEE 'Mwenyekiti' akaamrisha akamatwe mwalimu na apelekwe polisi.

    Mwalimu Twisana alifunguliwa kesi ya kushiriki ngono na mwanafunzi,hata walipofika mahakamani siku ya kesi yao mwalimu alijaribu kujitetea kwa kila namna ila hakueleweka kwani hata yule binti alitoa ushahidi kuwa amelala mara nyingi tu kwa mwalimu huyo,si walimpanga bwana!!

    Hakimu alitoa hukumu ,mwalimu alihukumiwa kwenda jera miaka 30.Maskini!!binadamu wakikuandama huna chako,labda uwe na Mungu ndani yako!,wazazi wa mwalimu Twisana walisikitika sana na hata kijijini kwake walisikitika sana!

    Ama kweli dau la mnyonge haliendi joshi,na likienda joshi basi Mungu tu ameamua! Hakika ng'ombe wa maskini hazai!!.Mwallimu Twisana alitegemewa kuwa mkombozi wa familia yake lakini leo hii anajikuta anaenda jera kwa kosa ambalo hakulifanya,upendo wake kwa wanafunzi uligeuka chuki na majanga dhidi yake,alipigania wanafunzi wafanye vizuri lakini akaonekana ni tatizo kwao. Hakuna alichopata kwenye kazi yake hiyo isipokuwa madeni tu mwisho wa mwezi lakini alifanya yote hayo kwa upendo wake kwa wanafunzi ili nao wafanikiwe lakini mwisho wa siku anakuwa kama mshumaa "unatoa mwanga kwa wengine huku wenyewe ukiteketea"



    Mwisho.

    Taja Ulichojifunza chochote,like,share and coment
 
    • NJIA PANDA YA KUZIMU - 1





    • SIMULIZI FUPI : NJIA PANDA YA KUZIMU



      Umasikini wa kutisha, majukumu yaliyonizidi umri na dharau zisizomithirika kutoka kwa watu waliotuzunguka zilinifanya nijisikie mpweke sana, mama yangu aliniambia kuwa licha ya yote hayo yanayotutokea nijitahidi sana kupambana na jinamizi la tamaa.

      Mama alinionya kabisa nijiepushe na tamaa.

      Maneno ya mama yaliniingia na kunikaa japo kuna muda nilijikuta nikitamani vitu ambavyo vilikuwa nje ya uwezo wangu.

      Nilitamani kuwa na msichana mrembo anizalie mtoto naye mama apate mjukuu wake wa kwanza kabisa. Tena si mjukuu kwa njia za mkato la. Nilihitaji mama apige vigelegele harusini nikiwa naveshana pete na mke wangu.

      Lakini yangewezekana vipi haya pasi na pesa.

      Pepo za pesa zilivuma na kuwafuata wenye nazo ili utimie ule usemi kuwa ‘mwenye nacho ataongezewa’.

      Umasikini wetu ukanifungua akili na kukitambua kipaji changu, nikatambua kuwa nilikuwa nao uwezo wa kuandika tungo za hadithi ambazo zilivutia kusomwa na rika lolote lile.

      Mama yangu hakuwa shabiki wa kusoma, si kwa sababu hakupenda nilichokuwa naandika bali kwa sababu hakuwa akijua kusoma.

      Nilipokuwa namsimulia nilichokiandika alinitia moyo na kuniambia kuwa siwezi kujua huenda ni maajabu ya Mungu kunitunuku kipawa kile ili nije kuibeba familia yangu.

      Siku zikakatika huku nikijikatia tamaa na kile kipaji changu.

      Na hatimaye nikiwa katika dakika za mwisho kujihesabia kuwa kipaji kile si mali kitu. Nililetewa taareifa na rafiki yangu ambaye alipenda sana kuzisoma kazi zangu, aliniambia kuwa kuna shindano limetolewa magazetini, gazeti lile linatafuta mtunzi na mwandishi wa hadithi.

      Nilizipokea taarifa zile katika namna ya kawqaida sana, kwa sababu nilitambua wazi kuwa matangazo mengi ya kazi huwa washapatikana wafanyakazi na pale wanatoa tangazo ili kutimiza wajibu tu.

      Rafiki yule akanisihi sana nishiriki.

      Nikamwambia kuwa nitajaribu, akanieleza kuwa kule wanahitaji simulizi ambazo zimechapishwa tayari. Akanitoa hofu kuwa atanisaidia kufanya kazi ile.

      Ikaanza kwa kukata tamaa lakini mambo yakaanza kuwa kama yanavyotakiwa.

      Tulishiriki watu mia mbili na zaidi katika shindano lile.

      Sikuamini pale walipokatwa watu mia walioshindwa eti mimi nikabaki katika ile orodha ya washiriki waliofanya vizuri na nilikuwa nafasi ya saba kwa ubora kati ya watu mia moja.

      Ni hapo ari ikarejea, katika kuendelea na shindano ikatakiwa simulizi nyingine mpya na sio ile iliyoshindanishwea awali.

      Nikajikunja na kuandika simulizi nyingine tena.

      Ikaingizwa katika mashindano nikafanikiwa kuingia katika hamsini bora safari hii nikiwa nafasi ya kumi kati ya washiriki wote.

      Mama yangu alikuwa akiniombea sana dua kila siku, na kunitia moyo kuwa nifanye kwa akili zote na ikiwa nitashinda basi umasikini tutaupungia mkono wa kwaheri.

      Baada ya kubaki watu hamsini kwa mara ya kwanza tukakutana na mmiliki wa gazeti lile ambaye alikuwa mtu mkubwa sana hapa nchini Tanzania.

      Lilikuwa jambo la kipekee sana kuzungumza naye ana kwa ana, akatueleza kuwa kati ya watu hamsini alikuwa akihitaji watu watano tu.

      Akaelezea kuwa safari hii ni yeye ambaye atazisoma simulizi zote hamsini na kutambua ni nani bora kati ya wote.

      Akatutamanisha zaidi kwa kutueleza kuwa hao watu watano watakaoshinda basi watapata kazi moja kwa moja katika ofisi yake, watapangishiwa nyumba jirani na ofisi na gharama zote zitakuwa juu yake. Na kubwa zaidi ni mshahara mnono.

      Mate yalinitoka mpenzi msomaji, nilikuwa naihitaji sana pesa kuliko kitu kingine kwa wakati ule. Nilikuwa nina haja ya kuifanyia kitu jamii na familia yangu.

      Bwana yule akatueleza aina ya simulizi ambazo anazipenda.

      Akasema anavutiwa na simulizi zinazobeba uhalisia zaidi. Akasema hapendelei simulizi ambazo ni dhahania zaidi ambazo hata ufikirie vipi ni kitu ambacho hakiwezi kutokea katika nchi yetu.

      Akatusihi tujitahidi kuandika vitu ambavyo vina uhalisia na nchi yetu, matukio ambayo yanatokea katika jamii zetu na kadhalika nchi jirani.

      Baadaye alitoa fursa ya kupiga picha ya pamoja, kwangu mimi ile ilikuwa hatua kubwa sana katika maisha yangu.

      Picha zikaoshwa kidigitali na kila mmoja kupatiwa yak wake.

      Niliifikisha picha ile kwa mama yangu kana kwamba ni mshahara, tulipatiwa pia fulana zenye tangazo la shindano lile.

      Mama alinikumbatia kwa nguvu sana na kisha kumshukuru Mungu kwa muujiza ule anaoutenda.

      Nilimweleza mama juu ya simulizi ambayo inatakiwa katika fainali ile.

      ‘’Simulizi zipo nyingi mwanangu, tatizo huwezi kujua mwenzako atakuwa ameandika simulizi kuhusu nini, pale bondeni kwa mzee Hoja kuna binti anasemekana ana historia hiyo nasikiaga tu juu juu yaani kama ungempata yule ingekufaa lakini sikushauri kabisa uende huko maana sina uhakika lakini kuna tetesi za ajabu ajabu..huko usiende. Tafuta machokoraa andika kuhusu wao, wana mengi sana watoto wa mitaani, tena ikiwezekana unaiita simulizi hiyo CHOKORAA….’’

      ‘’Hapana kuna mwandishi tayari ameandika kitabu kinaenda kwa jina hilo….’’ Nilimkatisha mama kuhusiana na hilo, ‘’kwani huyo binti sijui kuna nini nikizungumza naye si ninamwambia kama nikishinda nampatia pesa kidogo au..’’

      ‘’Martin wewe yule nimekwambia achana naye, kama na hao machokoraa ni ngumu kaandike kuhusiana na wagonjwa wa kansa ama wenye ukoma…..’’ mama alitoa wazo jingine.

      ‘’aah mi mambo ya hospitali sitaki mama najua huko kila mmoja ataenda…’’

      ‘’sawa kama hautaki mambo ya hospitali chagua mengine ila sio kwa mzee hoja na binti yake yule, achana naye tuheshimu waswahili waliosema lisemwalo lipo… sawa mwanangu..’’

      Mama alimaliza kisha akanipongeza tena na kunitakia heri. Nikaingia jikoni nikajipakulia chakula nikala kisha nikaingia chumbani kwangu kulala.

      ------

      WANASEMA kuwa ni heri usimkanye mtu jambo kwa sababu utampa shauku ya kulijua. Na hapohapo wanasema mtu mzima dawa.

      Mimi nilitamani kufanya kitu kizuri, nilizitamani zile pesa alizoahidi mkurugenzi yule.

      Bila kumshirikisha mama nilienda maeneo ya nyumbani kwa mzee Hoja nikiwa na lengo la kumuona huyo binti.

      Kweli nilimuona na kusalimiana naye nikizuga kuwa namtafuta mtu fulani pale, yule binti wa kuitwa Nasra akanieleza kuwa nimekosea nyumba labda.

      Nikaingilia pale alipoishia yeye na kisha nikamueleza bayana kuwa nilikuja kumtafuta yeye na si kitu kingine pale.

      Alipigwa na bumbuwazi, nikamtoa hofu na kumueleza kuwa mimi ni mwandishi chipukizi na nilikuwa nimekuja kuzungumza naye ikiwezekana tufanye biashara.

      ‘’biashara gani tena kaka yangu’’

      ‘’Nahitaji simulizi ya maisha yako, siijui hata kidogo lakini kama inafaa niipeleke katika mashindano. Ikifanikiwa kushinda mimi nitakupatia pesa kiasi nami nitabaki nazo kiasi. Halafu kila mwezi nitakuwa nakulipa…’’ nilimweleza kwa pupa kana kwamba tayari nimezipata zile pesa.

      Nasra akanitazama kisha akatabasamu kidogo.

      ‘’Kweli unayoyasema ama unataka kitu kingine tu…’’

      ‘’Sihitaji kitu kingine dadangu we kama inawezekana hata sasa hivi nisimulie tu…’’

      ‘’Hapana kwa sasa hivi, tufanye kesho jioni tukutane kisimani nitakusimulia kidogo halafu keshokutwa nitamalizia, ujue mama hapendi nimsimulie mtu kilichonitokea lakini nahitaji pesa kwa sasa ikiwa hautaniongopea utakuwa umenisaidia sana. Ila sharti moja tu kabla sijaanza kukusimulia unanilipa pesa kidogo..’’ alizungumza kwa sauti ya kunong’ona. Sasa hapo pa kumlipa mi sikuwa na kitu chochote lakini nililazimika kumkubalia tu.

      Tukaagana nikaenda kwa yule rafiki yangu na kumweleza juu ya siri ile. Sikumficha kitu kuhusu Nasra.

      Na yeye akasema kuwa aliwahi kusikia tetesi kuwa kuna historia pale ya ajabu.

      ‘’Hayo maajabu nd’o nayataka.. Ramso nataka ushindi kumbuka nikishinda mimi, umeshinda wewe, ameshinda maza na watu wengine wengi tu. Na ili kushinda inabidi kuandika kitu cha kipekee…’’

      ‘’Sawa sasa hapo kinahitajika nini zaidi’’ akaniuliza swali nililokuwa nikihitaji.

      ‘’Nasra anahitaji kifuta jasho kabla hajaanza kunisimulia.’’

      ‘’Duh sawa sipo vizuri lakini chukua hii elfu thelathini utampatia ilimradi tu asimulie ukweli mtupu….’’ Alizungumza huku akinipatia kiasi kile cha pesa. Nilimshukuru sana na kumuahidi kuwa kesho yake nitamtafuta baada ya kuzungumza na Nasra ili nimpe mustakabali wa simulizi ile….

      Tukaagana huku tukicheka kwa furaha sana, tuliuona ushindi ukiwa unakaribia.

      Sikumweleza kitu chochote mama yangu, nilimpatia shilingi elfu kumi kwanza. Akaduwaa ni wapi nilikuwa nimetoa nikamweleza kuwa muda utafika zitakuwa zimezagaa humo ndani pesa za kutosha. Nikamweleza kuwa nimeandika simulizi moja nzuri sana najua nitashinda.

      ‘’Isijekuwa ulienda kwa mzee Hoja we mtoto…’’ aliniuliza bila kutilia maanani. Nikatikisa kichwa kukataa.

      Nikalala huku nikimuwaza Nasra.

      Niliwaza ahadi nilizompatia na kuhisi utekelezaji wake utakuwa mwepesi tu, nitamlipa hadi atafurahi mwenyewe. Kwa tetesi nilisikia kuwa mshahara tutakaopewa washindi si chini ya milioni moja na laki mbili, hapo laki ya kwake halafu nabaki na milioni moja, au nampa hata laki mbili… ujue milioni parefu sana.

      Ndugu msomaji nilijipigia mahesabu makali sana hakika, nikasahau kuwa si vyema kupigia mahesabu pesa ambayo haijaingia katika mkono wako.

      Hatimaye usingizi ukanipitia nikiwa namuwaza Nasra na jinsi alivyokuwa akienda kunipatia ushindi.

      Siku iliyofuata sikucheza mbali na kisima, nikiwa na daftari langu tayari kabisa na kalamu.

      Hatimaye Nasra alifika akiwa na ndoo yake ya maji.

      Tulisalimiana na kisha tukakaa chini ya mti ni hapa alipoanza kunisimulia mkasa wake.

      Mkasa ambao sikujua kabisa kuwa utanichota mtama na kisha kuanza kuniburuza kuelekea nisipopajua.

      Naam wanasema pia USILOLIJUA halitofautiana hata kidogo na ule usiku mnene wa kiza.



      Niliona kama Nasra alikuwa akiteka maji taratibu sana nikaona ni heri nimsaidie upesi upesi ili nianze kuusikiliza mkasa wake aliotaka kunisimulia mkasa nilioamini kuwa utakuwa mkasa wa aina yake ambao utaniwezesha kushinda lile shindano na hatimaye kupata kazi inayoingiza kipato kikubwa.

      Hatimaye nilichokingoja nilikipata….. nasra akaanza kuusimulia mkasa wake kwa sauti tulivu kabisa huku uso wake ukitawaliwa na tabasamu hafifu sana.

      ‘’Nitakuwa muongo nikisema eti mume wangu hakunipenda, hakika alinipenda na kunijali haswa.

      Kila nilichotaka alikuwa ananipa kadri ya uwezo wake, ambacho hakuweza kunitimizia basi alinieleza wazi kuwa hawezi lakini atajaribu kunitimizia.

      Sijui wanawake tuna matatizo gani, tuna tatizo la kutoridhika yaani likiisha hili jema tunataka jema jingine.

      Baada ya yote yaliyotokea nikajikuta nikianza kumlalamikia mume wangu kuhusiana na suala la ndoa isiyokuwa rasmi, yaani yeye aliwajua wazazi wangu lakini mimi hakuwahi kunitambulisha kwao. Na kamwe hatukufunga ndoa iliyotambulika….. nililalamika sana lakini alikuwa anatabasamu na kunieleza kuwa ni kitu gani nilikuwa nakosa…’’ mwanadada Nasra alianza kuusimlia mkasa wake katika maneno yale nami nikawa makini sana kumsikiliza. Nikatikisa kichwa kumaanisha kuwa nilikuwa nimeelewa aendelee kusimulia. Nilikuwa ninayo haraka ya kujua ni kitu gani kilimsibu katika mkasa huu.

      ‘’Wanawake tukiamua jambo fulani liwe hivi kutokana na hisia zetu basi jambo hilo huwa, sisi sio wepesi wa kupuuzia mambo kama ilivyokuwa kwenu wanaume… ndo maana ni rahisi sana wanawake kugombana kuliko wanaume kwa sababu tunaloliwaza tunataka liwe….. basi nikanuia kuwa nitaenda kuwaona wazazi wa mume wangu kilazima. Na dawa pekee ilikuwa chumbani, kila siku ambayo nilipanga kuchota siri kadhaa kwa mume wangu basi nilikuwa nakiandaa chumba vizuri, nisijisifu ndugu mwandishi lakini japokuwa sikuzaliwa Tanga lakini nilikuwa mkorofi sana pale linapokuja suala la chumbani, nilijua kukiandaa chumba nacho kikaandalika, nilijua namna ya kumfanya mwanaume afanye lile ambalo awali hakukusudia. Na wanasema kuwa wanawake huhisi waume zao wanatoka nje ya ndoa lakini kwa tiba niliyoitoa chumbani nikiwa na mgonjwa wangu yaani mume wangu hakika wasiwasi ulikuwa mbali nami najua wapo wengi wataalamu kunizidi lakini hawapatikana kirahisi hadi kumfikia mume wangu. Nilikuwa najiamini sana, basi kila tukiwa watupu nilifanya namna zote za kumchimba mume wangu hadi pale nilipoipata ramani rasmi juu ya wapi ni kwao na ni kwa jinsi gani naweza kufika… nilijiona mjanja sana kwa kufanikiwa kule sikujua kama nilikuwa najiingiza katika matatizo makubwa. Ni bahati yangu sana eti leo naongea nawe unaandika mwandishi……’’ akavuta pumzi na mimi nikamsogezea ile ndoo ya maji akachota kwa kutumia kikombe alichotumia kuteka maji, kisha akapiga mafunda kadhaa na kushusha pumzi. Kisha akaendelea

      ‘’Nikafanikiwa kumlaghai mume wangu kuwa ninaenda nyumbani baba yangu mdogo anaumwa, kwa jinsi alivyonipenda aliniruhusu huku akinibusu shavuni na kunieleza kuwa ananipenda sana na hapendi baya lolote liweze kunitokea.

      Maneno yake hayakuyabadili maamuzi yangu, nikapanda gari na kuondoka kuelekea wilaya ya Kilindi mkoani Tanga ni huku ambapo mume wangu wakati tukiwa katika faragha aliropoka kuwa wazazi wake wote wawili walikuwa wakiishi…. Tena akaongezea ambalo hajaulizwa akasema ana muda sana hajaenda kuwasalimia. Sikuitilia uzito kauli hii mimi nilitaka kuwaona wazazi wa mume wangu, eheee kabla sijasahau mwandishi. Wakati huo nilikuwa nina mimba ya miezi miwili. Niliona si heri kuzaa bila wazazi wa upande wa pili kunitambua, hakuna kitu nilikuwa naogopa kama kurudi nyumbani kwa baba na mama yangu huku nikiwa nina mtoto waanze kunilea mimi na mwanangu. Nadhani hili lilinisukuma zaidi, mama yangu mzazi nilimuaga kuwa naenda kwa wakwe zangu lakini kisirisiri asimuulize mume wangu… mama akanikubali mtu mwingine niliyemuaga alikuwa ni rafiki yangu Rahma, huyu alikuwa mstari wa mbele kunikejeli kila siku kuwa mimi ni mjinga ninaishi na mwanaume nisiyepajua kwao.

      Nikaondoka….. ndugu mwandishi umewahi kusafiri na kisha ukafikia njia panda…’’ aliniuliza, nikatikisa kichwa kumkubalia kuwa nimewahi na ninazifahamu njia panda nyingi tu.

      Akainama na kisha akafunua kichwa chake, nilishtuka kukiona. Naye alijua kuwa nitashtuka, akakifunika kisha akanitazama huku akitabasamu.

      ‘’Hujaona nywele hata moja katika kichwa changu na unaona makovu ambayo ni mabichi, hayo hayatakauka kamwe na ninajua hujaamua kutema mate chini lakini najua kuwa ninanuka sana tu. Najua hili kiuwazi…. Haya yote niliyafuata mwenyewe nilipojikuta katika njia panda ya kwenda kuzimu….. nikajiuliza wapi ni sahihi na wapi si sahihi kumbe pote kusini, kaskazini, mashariki na magharibi zilikuwa njia za kuelekea kuzimu. Nikachagua njia mojawapo nikaifuata eti njia ya kwenda kwa mama mkwe wangu na baba mkwe, watu walionielekeza waliniuliza mara mbilimbili, una uhakika bibi Shuku ni mama mkwe wako nikawajibu kiujasiri huku wengine nikiwaletea nyodo. Kuna mwanaume mmoja alinisihi sana eti nisiende kwa bibi Shuku bali niende kulala nyumbani kwake, aisee nilimtukana sana mwanaume yule yaani nilimtusi sana nilihisi amenichukulia kiwepesi sana kuwa mimi ni msichana nisiyekuwa na uelekeo. Baada ya matusi yale yule mwanaume aliguna kisha akaniambia ‘asante sana dada yangu ila sikuwa na nia mbaya kabisa’ sikujibu lolote nikamsonya na kuondoka zangu.

      Nikatembea na kwa mbali nikaliona lile jumba la kifahari ambalo nilielekezwa kuwa ndipo nyumbani kwa bibi shuku. Nikatabasamu na kutambua kuwa kumbe wote walikuwa wakinionea wivu kwa sababu ukweni kwetu wana uwezo kifedha, nikapiga hatua hadi nikafika. Nikapokelewa mizigo yangu na watoto wadogo. Nikaambiwa kuwa mama mkwe yupo ndani, wakaniongoza nikaingia.

      Nilipoingia nikasikia nikiitwa jina langu huku nikikaribishwa, nikashangaa wamenijuaje hawa wakati sijawahi kufika, au Mohamed aliwatumia picha zangu, nilijiuliza. Mohamed ni jina la mume wangu ndugu mwandishi.

      Lakini nilipogeuka nikakutanisha macho yangu na Rahma, huyu alikuwa rafiki yangu kipenzi jijini Dar es salaam ambaye alikuwa akinisisitiza kila siku kuwa nisiwe mjinga nifanye nijuavyo nifike ukweni kwetu ajabu sasa namkuta ukweni hakunishangaa, aliendelea na mambo yake na hapo yule mama mkwe ambaye alikuwa amegeuka upande mmoja na kunipa mgongo aligeuka.

      Mwandishi niliishiwa nguvu, nikataka kukimbia nilipogeuka kutazama wale watoto wawili wanaofanana walionisindikiza pale ndani zilikuwa ni paka mbili nyeusi zikinitumbulia macho kwa ghadhabu. Nikapiga mahesabu lipi ni jambo jepesi kuendelea kutazamana na yule kiumbe wa kuitwa mama mkwe wangu ama kukabiliana na wale paka ili nipite pale mlangoni.

      Nikaamua kuwakabili paka, ile napiga hatua moja mbele paka akaruka juu na kunitia kucha katika uso wangu huku akitoa milio ya ajabu kama kitoto kichanga.

      Maumivu yale yakanifanya nipoteze uelekeo nikakimbilia upande ninaodhani kuwa ni sahihi kumbe la.

      Nikahisi kukumbatiwa na kitu chenye joto sana, nilipofumbua macho vizuri nilikuwa mikononi mwa kiume wa ajabu kabisa ambaye niliambiwa kuwa ni mama mkwe wangu…. Mwandishi nikatamani nipoteze fahamu lakini sikupoteza fahamu. Niliendelea kutambua nilichokuwa nakiona, kile kiumbe kilikuwa kina sura mbaya na kilikuwa kikitokwa na harufu kali ya mkojo, kinywa chake kilikuwa kinatoa harufu mbaya wakati huo kiumbe kile kilikuwa kinacheka…….’’ Alisita Nasra akatazama juu kama anayekumbuka kitu.

      Na hapo akaanza kutetemeka huku akinyanyua mikono yake juu kama mtu anayejizuia asipigwe na kitu fulani.

      Hofu ikaanza kuniingia na mimi nikatazama nisione kitu chochote kile.

      ‘’Wanakutaka wanakutaka….wewe’’ Alianza kuzungumza yule dada huku akiwa na hofuu kuu, nikajikuta namuuliza.

      ‘’Wanamtaka nani na wanamtaka wapi’’ niliuliza kiuoga

      ‘’Wanakutaka wewe.. wanakutaka NJIA PANDA YA KUZIMU….’’ Alinijibu huku akitetemeka.

      Jibu lile liliniogopesha sana, nikajikuta naachia kalamu na daftari ili niweze kukimbia maana hali haikuwa shwari kabisa.

      Ile napiga hatua kukimbia mara Nasra akaidaka suruali yangu kwa nguvu sana, nilijaribu kurusha rusha miguu ili aniachie lakini hakuniachia alikuwa anaunguruma sana muungurumo wa ajabu.

      Nikafanya kuufungua mkanda wa suruali ili initoke nikafanikiwa lakini sikuweza kwenda mbali. Sana yule Nasra ambaye nilikuwa najitoa katika mikono yake nilishangaa kumuona akitoweka akiwa amebeba ndoo ya maji kichwani.

      Nikageuka nitazame ni kitu gani kilikuwa kimenishikilia kama sio Nasra.

      Nikakutana tena na sura ya Nasra.

      Nasra amenishika nisiondoke na Nasra anaondoka akiwa amebeba ndoo ya maji.

      Nilikuwa nimepatikana jamani, haya mambo nilikuwa nikisimuliwa tu na kuyaona katika filamu sasa nilikuwa matatani.

      Huyu nasra aliyenikamata nisiondoke alikuwa anatabasamu tu. Na mara upepo ukavuma na kichwa chake kikawa wazi kile kitambaa alichokuwa amejitanda kikatoweka.

      Mamaaa macho yangu ambayo awali yaliona majeraha tu katika kichwa cha nasra sasa hayakuwa majeraha tupu bali kuna wadudu walikuwa wakiibuka na kutoweka, nilisisimka vibaya mno.

      Na nikiwa nimeishiwa nguvu kabisa, nasra aliyebaki alizungumza.

      ‘’karibu sana mwandishi njia panda ya kuzimu.. tunakuhitaji sana huko.’’ Sauti ilikuwa ile ile ya nasra.

      ‘’Nasra… nisamehe, naomba unisamehe…’’ nilimsihi lakini badala ya kujibu sasa alifyatuka na kunichabanga kofi kali usoni.

      Sikuona nyota nyota badala yake niliona vitu kama vichwa vya mbwa mwitu, na akili iliponikaa sawa niliona fisi wawili wakiwa mbele yetu. Hakuwa amenishikilia tena dada yule.

      ‘’tunaenda au unabaki…’’ aliniuliza.

      ‘’nabaki siendi huko siendii niache..’’ nilimjibu huku hamaniko likiwa limenishika vibaya mno.

      ‘’haya mi naondoka nakuacha na hao hapo rafiki zetu…’’nasra alinijibu huku akiondoka na kuwaendea wale fisi.

      Nikageuka ili niwaone wale marafiki alioniambia, nikakutanisha macho yangu na mto si mto ziwa si ziwa lakini kikubwa zaidi niliwaona mamba wakisogea taratibu kuja eneo ambalo tulikuwepo.

      Ndugu msomaji, sikusubiri nasra anielekeze nini cha kufanya nilikimbia nikampita nisijue hata ni wapi nilikuwa naenda.

      Nasra akaniambia nipande juu ya mgongo wa fisi mmoja. Nilikuwa muoga lakini alipopanda na mimi nikapanda.

      Kukosa kwangu umakini wa kuiga kila alichokuwa akifanya nasra nikajikuta nakaa tu utadhani ile ni taksi. Fisi akakimbia nikaanguka chini vibaya mno na wakati huo mamba wakizidi kusogea, nilipoanguka na wao wakaanza kukimbia kwa kasi kunifuata pale nilipokuwa.

      Nasra alikuwa anaondoka zake akiwa ameshikilia masikio ya fisi wake.

      Mamba wale walionyesha waziwazi kuwa walikuwa na njaa kali walikuwa wakisukumana huku na kule ili kuniwahi….

      Nikapiga kelele kumuita mama yangu mzazi nikisahau kumuita Mungu wangu…..

      Nilipofumbua macho mamba walikuwa wamebakiza mita chache tu kunifikia……

      Na hapo likatokea jambo la ajabu kabisa lililonimaliza nguvu zaidi…..



      Nikageuka ili niwaone wale marafiki alioniambia, nikakutanisha macho yangu na mto si mto ziwa si ziwa lakini kikubwa zaidi niliwaona mamba wakisogea taratibu kuja eneo ambalo tulikuwepo.

      Ndugu msomaji, sikusubiri Nasra anielekeze nini cha kufanya nilikimbia nikampita nisijue hata ni wapi nilikuwa naenda.

      Nasra akaniambia nipande juu ya mgongo wa fisi mmoja. Nilikuwa muoga lakini alipopanda na mimi nikapanda.

      Kukosa kwangu umakini wa kuiga kila alichokuwa akifanya Nasra nikajikuta nakaa tu utadhani ile ni taksi. Fisi akakimbia nikaanguka chini vibaya mno na wakati huo mamba wakizidi kusogea, nilipoanguka na wao wakaanza kukimbia kwa kasi kunifuata pale nilipokuwa.

      Nasra alikuwa anaondoka zake akiwa ameshikilia masikio ya fisi wake.

      Mamba wale walionyesha waziwazi kuwa walikuwa na njaa kali walikuwa wakisukumana huku na kule ili kuniwahi….

      Nikapiga kelele kumuita mama yangu mzazi nikisahau kumuita Mungu wangu…..

      Nilipofumbua macho mamba walikuwa wamebakiza mita chache tu kunifikia……

      Na hapo likatokea jambo la ajabu kabisa lililonimaliza nguvu zaidi…..

      Yule fisi alinigeukia na kisha akanikazia macho. Nilipomtazama nikawa naona ile sura ya fisi ndani yake ni kama palikuwa na sura ya mtu. Na kabla sijajiuliza zaidi mara yule fisi akafungua mdomo wake.

      ‘’We fala si upande tuondoke au unataka kuliwa na mamba…’’

      Mama yangu, nilihamaki, yaani fisi ana sura ya mtu nab ado anaongea. Yule fisi alinisogelea kisha akanikanyaga teke kwenye mbavu zangu halafu akaongea tena, sasa alinitukania mama yangu.

      Ebwana eeh duniani kuna mambo ndugu msomaji lakini baadhi ya mambo uyasikie tu yaisikukute wewe.

      Nilipanda katika mgongo wa yule fisi mtu nikamshika masikio akatoka mbio kali sana hadi tukampita fisi wa Nasra, hata sikujua ni wapi tunaenda ila nilikuwa juu ya usafiri wa fisi mtu.

      Kadri tulivyozidi kwenda tulizidi kuingia gizani na hali ya hewa ilizidi kubadilika na kuwa joto sana.

      Hatimaye yule fisi alisimama na kuniamrisha nishuke upesi huku akilalamika kuwa mimi ni mzito sana. Ipo siku na mimi nitambeba yeye.

      Kusikia kauli ile nikatambua wazi kuwa sasa nilikuwa nipo katika hatua za mwisho kabisa za ubinadamu wangu na muda si mrefu nitakuwa mnyama tena mnyama mwenyewe fisi.

      Mapigo ya moyo yalipiga vibaya sana, na nilikuwa najutia kutosikiliza maneno ya mama yangu mzazi juu ya hofu yake katika familia ile.

      Nilishuka nikawa nimechutama nikitazama huku na kule katika giza lile, ile fisi ikaondoka zake lakini haikufika mbali mara ikarudi kwa kasi na kuniparamia pale nilipokuwa ikaniangusha chini.

      ‘’mpumbavu wewe umeniumiza mgongo yaani, umenirukia utadhani mimi chuma, shenzi kabisa..’’ fisi ile iliendelea kuniralua ikanichania nguo zangu nikabakia na nguo za ndani tu, ikaning’ata huku ikinipiga matteke, sikuweza kukabiliana nayo kutokana na hofu niliyokuwanayo lakini hali ilivyokuwa tete nikajisemea kuwa nisipokuwa makini yule fisi ataniua tena ataniua vibaya kwa sababu alikuwa ananing’ata kwa nguvu na mateke aliyorusha hayakuwa na masihara hata kidogo.

      Nikajikaza nikasimama wima na kusema kama kweli nakufa basi nitakufa na shingo ya yule fisi, nilikuwa nimekasirika na nilijiona kuwa muda wowote ule nitakuwa mfu.

      Nikamtegea yule fisi alete mdomo wake, pale chini nilipokuwa nilifanikiwa kuokota jiwe.

      Kweli fisi akajileta, aisee nikamtandika jiwe moja la mdomo.

      Fisi mtu akatowa yowe huku akikimbia kuelekea alipojua yeye mwenyewe. Na hapo mwanga ukatokea na kujikuta kumbe nilikuwa nimezungukwa na lundo la viumbe wa ajabu. Viumbe hawa nimewahi kuwaona katika filamu za kinaijeria na katika masimulizi ya kutisha.

      Bila shaka hawa walikuwa ni misukule. Walikuwa wakinipigia makofi na nisijue katika nyuso zao walikuwa wanatabasamu ama vipi.

      Na mara msukule mmoja uliofanania kwa mbaali na jinsia ya kike ulianza kunisogelea huku ukiwa umetanguliza mikono yake mbele. Mikono myeusi michafu yenye kucha chafu pia.

      ‘’Ni mimi nimekupatia lile jiwe, naomba uwe mume wangu..’’ kiumbe yula alizungumza huku akitetemeka na akizidi kunikaribia. Nikaanza kusogea nyuma, ilikuwa afadhali fisi anayezungumza kuliko kiumbe huyu aliyetaka eti niwe mume wake.

      Nilichanganyikiwa sana. Wakati narudi nyuma nilijikuta naanguka chini na kiumbe yule akanifikia.

      ‘’Naitwa Manka’’ akajitambulisha jina lake huku akitokwa na mate machafu mdomoni.

      ‘’Mwachee’’ mara sauti kali ya kike ikaamrisha, yule binti akakimbia na kuniacha pale, wale wenzake wakawa wanamzomea.

      Nilipogeuka nikakutana na mwanamke mweusi sana lakini huyu akiwa na mavazi ya kawaida.

      Akanipungia mkono na kuniita, nikasimama na kumsogelea huku nikiwa katika hofu bado. Nikamfikia akanielekeza mahali nikaketi, akamaliza akaita jina ambalo sikulikamata mara moja.

      Akajongea pale msichana mmoja ambaye hakuwa kama wale viumbe wengine.

      ‘’Utaongozana naye na kumfundisha biashara yetu….’’ Alimweleza kisha akaondoka na kuniacha nikiwa na binti yule.

      Bila kuzungumza lolote yule binti alichukua maji maji na kuanza kunimwagia kichwani, nilipojaribu kujitikisa akasonya kisha akanitandika kwenzi kali kichwani. Nikashtuka na kutaka kusogea pembeni akaninasa kibao kikali usoni na hakuonekana kujali lolote kabisa.

      Yaani ananipiga huku akiendelea kunimwagia yale majimaji ya baridi sana.

      Baada ya hapo akanishika mkono na kisha akanipeleka hadi mahali palipokuwa na sufuria likiwa na mifuko laini ya plastiki.

      Akaleta ndoo na kuanza kuchota maji yaliyofanana na damu akawa anbajaza katika ile mifuko na kufunga huku mimi nikitazama na baada ya hapo akaanza kunifundisha namna ya kufunga mifuko ile.

      Nilijitahidi huku nikiwa naogopa sana. Hatimaye tulimaliza kujaza maji yale yaliyofanana na damu katika mifuko ipatayo hamsini.

      Akanipatia sufuria moja nikajitwisha kichwani na yeye akachukua sufuria jingine, tukatembea hadi mahali fulani. Akanishtukiza kofi kali mgongoni. Na wakati nashtuka nikajikuta katika eneo lililonifanya niduwae.

      Nilikuwa Kariakoo mtaa wa shule.

      ‘’utafanya kile ambacho nafanya, hayo uliyobeba ni maji ya kandoro… utauza kama ninavyouza ole wako usite kuuza…’’ alizungumza dada yule huku akiendelea kupiga mdomo watu wanunue maji yake….

      Nilikuwa namfuata nyuma tu, mara abiria mmoja akaniita. Nikaenda akachukua mfuko mmoja.
 
NJIA PANDA ZA KUZIMU - 2

Akanilipa shilingi mia moja, Mungu wangu eeh yule mtu alikunywa yale maji yanayofanania na damu kabisa, alikunywa huku akinilalamikia kuwa huenda yale maji hayajachemshwa.

Akanywa ule mfuko mmoja akamaliza akaongeza mwingine, nilitamani kusema neno lolote lakini huwezi amini kila nikitaka kusema sauti inakwama kabisa. Na sauti inapokwama yule dada ananigeukia na kunitazama kwa jicho kali sana.

Tulizunguka kule Kariakoo kwa takribani masaa manne kama sikosei tukawa tumemaliza kuuza yale maji ambayo si maji bali uchafu unaofanana na damu.

Hapa naomba niseme kitu mpenzi msomaji, yaani tangu nifanikiwe kuwa huru tena haya maji yanayoitwa ya kandoro siwezi kunywa nipo radhi kubaki na kiu lakini sio kunywa maji yale. Simaanishi na wewe hapo usinywe la hasha lakini wanasema kuwa usiloliona huwezi kuliogopa.

Mwenzenu niliona…

Wale watu ambao mchana walinunua uchafu ule na kunywa kama maji ndio haohao ambao usiku walikuwa wanaletwa kwa ajili ya kulima mashamba. Na walikuwa wanalima kweli.

Kidogo kidogo nikazoeana na yule dada na hapa ndipo nilipoyajua machafu mengi ambayo yananikera hadi leo kwa sababu hayataki kutoka katika kichwa changu.



Kule tulipokuwa hapakuwa na saa hivyo nitakuwa muongo nikielezea tukio kisha niseme ilikuwa saa fulani, yaani ile ilikuwa ni dunia ya wenyewe siku ambayo wa kujiita malikia ambaye bila shaka alikuwa ndiye yule mama mkwe wake Nasra akiamua tu hakuna kulala basi siku hiyo hamtaliona giza. Na siku watu wakimkera analeta giza hata siku tatu.

Kuna siku tulienda kariakoo kuuza yale maji mfanowe damu, tukarejea na maji kama pakiti tano hivi tukamueleza kuwa watu hawajanunua sana maji siku hiyo kuna mvua kubwa ilikuwa imenyesha.

Akatuuliza kwa upole sana ikiwa tunafahamu nini maana ya mvua, tukakubali kuwa tunaifahamu mvua vizuri.

Akacheka kidogo kisha akatuuliza nini maana ya mvua.

Tukabaki kimya tusijue ana maana gani kutuuliza lile swali, tulipokosa jibu akatuambia atatupa jibu baada ya muda mchache.

Akaondoka na kuingia ndani akaufunga mlango wake wa maajabu ambao unaonekana wakati wa kufunguliwa na kufungwa tu. Nyumba haionekani wala vilivyomo ndani. Yule dada aitwaye Adella ambaye ndiye ali9kuwa mwalimu wangu katika maisha yale mapya aliwahi kunieleza kuwa ndani ya ile nyumba kuna vito vingi sana vya thamani na samani zenyewe pia ni nyingi.

Baada ya kuingia ndani anga ilianza kutanda na kuwa nyeusi, tukadhani kuwa kama kawaida alikuwa ametupa adhabu ya kuleta giza siku tatu. Lakini hili halikuwa giza, mara ngurumo zikasikika na hapo mvua kubwa ikaanza kushuka.

Cha kushangaza mvua hii ni kama ilikuwa ikinyesha na kuingia katika beseni, yaani9 kila ilivyokuwa inanyesha maji yalizidi kuongezeka kwa kasi. Na wakati huo ile anga ikisogea taratibu ili ikutane na maji yale, Adella hakuwa vizuri sana katika kuogelea lakini mimi nilikuwa mtaalamu nilijitahidi sana kumsaidia Adella ili asinywe maji yale ambayo yangeweza kumsababishia kifo ikiwa angekunywa sana. Nilijaribu sana lakini baadaye tulikuwa tunaikaribia anga iliyokuwa inatema maji kwa wingi.

Sasa hapo sikuwa na namna yoyote nilifumba macho kukisubiri kifo, Adella naye alikuwa kimya akitumbua macho kuitazama ile anga ilivyokaribiana na uwepo wetu.

Ilikuwa hali ya kutisha sana.

Ghafla yale maji yakaanza kukauka tukaanza kushuka chini kwa kasi.

Tulipotua ardhini palikuwa pakavu kabisa na pembeni alikuwa amesimama yule malkia akiwa na beseni dogo tu.

‘’hiyo ndo maana ya mvua, je imenyesha mvua kubwa na ya kutisha kama hiyo…’’ alituuliza huku akitabasamu na kuondoka zake.

Ndugu msomaji, uchawi upo kama hauamini ni bora uamini tu lakini kamwe usijiingize katika shirki kwa sababu haimpendezi Mungu hata kidogo.

Yaani ardhi ile ilikuwa kavu kabisa na wenzetu walikuwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.

‘’alituweka kwenye beseni’’ yule dada akaniambia likiwa ni neno lake la kwanza kunieleza kisha akaendelea.

‘’asante sana kwa kuniokoa wewe ni rafiki yangu kuanzia sasa..’’ aliniambia kwa sauti iliyojaa upole.

Na neno lile ndilo lililozua kizaazaa.

Neno lile likaujenga ukaribu zaidi baina yetu akaniahidi kuwa ipo siku tutatoka na kuishi duniani kama mtu na mke wake.

Mapenzi yakanza katika ardhi nisiyoielewa.

Adella alikuwa akinieleza mambo mengi sana ambayo amewahi kuyafanya, yalikuwa ya kutisha sana lakini aliniambia kuwa wanaotakiwa kutishika ni wale ambao wanaishi duniani sio mimi kwa sababu muda wowote ule nitatumwa kufanya kazi. Na nisijidanganye kuwa itakuwa rahisi kutoroka.

‘’Hivi wewe unadhani kwa nini ukiwa kariakoo haukimbii ukatoroka au huwa hauzioni gari za kwenda Temeke zimejaa pale shule ya uhuru… nikupe onyo yaani usije ukathubutu kutoroka kwa njia nyepesi kama hizo utajikuta matatani sana… acha kabisa Martin…’’ alinipa maonyo ya ajabu ajabu.

Ni kama vile alikuwa amenitabiria kuwa kuna kazi naenda kupewa katika siku hizo za karibuni.

Tulikuwa kama pacha vile na yule malkia alionyeshwa kupenda tunavyofanya kazi kwa ushirikiano.

Siku hiyo alituita na kutueleza kuwa kuna sherehe kubwa sana inatarajiwa kufanyika ndani ya siku saba zijazo akatueleza kuwa kila kitu kipo lakini hakuna msanii mzuri ambaye atatumbuiza katika hizo sherehe.

Na hapo akatuagiza kwenda kutafuta msanii ama wasanii wawili ambao watatumbuiza katika hiyo sherehe. Nilistaajabu sana lakini kwa sababu yule ADELLA alikuwa mkongwe hakustaajabu.

Na siku hiyo alinieleza kuwa ukiwa mzembe tu na usiyejishughulisha unaishia kuwa msukule ama unauzwa na ukiuzwa unaweza kuishia kuliwa nyama ama kufanywa kiti.

Maneno ya adella yalinichanganya sana kwa sababu yalikuwa mengi na yalikuwa yanatisha.

Usiku tuliondoka kama kawaida tulipofika mahali akanizaba kibao kikali sana mgongoni na kujikuta tupo katika ukumbi ambao nilikuwa naufahamu vyema na msanii aliyekuwa anatumbuiza pale jukwaani nilikuwa namfahamu, nilishtuka sana kujikuta ndani ya ukumbi ule na nilihisi kuwa muda si muda nitakutana na watu ambao nilikuwa nawafahamu.

Adella aliniacha nikiwa katika kona moja ya ukumbi, akajichanganya na baadaye nikamuona akimtuza yule msanii, alimrushia matawi matawi watu wakawa wanapiga kelele kumpongeza.

Hatimaye yule msanii akamuamuru adella apande jukwaani.

Adella akageukia upande niliokuwa nimesimama na kunifanyia ishara ya dole gumba, yule msanii alimkumbatia adella huku mapigo ya muziki yakiendelea.

Sijui ni mimi pekee niliyeliona tukio lile ama kila mtu aliona, huenda niliona mimi mwenyewe maana wangeona watu wengine lazima wangepiga kelele tu.

Wakati anamkumbatia adella alimfunga msanii yule kitu kama hirizi nyekundu kiunoni. Walipoachana akabaki na ile hirizi.

Akili zangu ni kama zilikuwa zinarejea hivi, nikajiona mjanja sana kuwa siwezi kuendelea kuishi maisha yale.

Nikajichanganya na kutoka nje ya ukumbi, huko nikaanza kuzubaa ni wapi nielekee kwa sababu sikuwa na nauli na pale nilipokuwa paliwa ni umbali mrefu sana hadi kufika nyumbani.

Siku hii ndipo nilizidi nkukiri kuwa ikiwa wewe ni mjanja basi kuna mjanja zaidi yako.

Nilizurura hapa na pale naingia hapa natokea kule na kujikuta nikiwa palle nilipoanzia awali.

Muda ulizidi kwenda hadi pakakucha, naziona gari najishauri kupanda lakini sipandi, natembea hadi huko na kurudi palepale,.

Kama ni adhabu basi ile ilikuwa ni adhabu kubwa sana, nawaona watu ninaowafahamu nikiwaona nakimbia na kujificha wakiondoka najishangaa ni kwanini sikiwakimbilia na kuwaeleza yote yaliyonitokea.

Hatimaye njaa ikaanza kuniuma, mchana jua kali akili inakuwa nzito kufanya maamuzi. Ilikuwa baada ya siku mbili nikiwa naishi kama kivuli nazurura huku na kule na hakuna anayenijali. Hatimaye baada ya siku mbili nikapata mwanamke wa kwanza kabisda kunisaidia.

Huyu alinichukua na kuniuliza nilikuwa nina matatizo gani, alikuwa ni mama mtu mzima anayejiheshimu, alinieleza kuwa amekuwa akiniona pale kwa siku mbili. Akanipeleka hadi nyumbani kwake, nikasema kuwa hatimaye nilikuwa nimepata msaada thabiti, alinipatia nguo nikabadilisha na kisha akanipatia chakula, baadaye akanieleza kuwa yeye ni mjane na watoto wake wote wameenda shule hivyo kwa wakati huo alikuwa akiishi mwenyewe.

Nilimpa pole na kumsihi kuwa anisaidie nauli niende nyumbani kwetu akaniahidi kuwa siku inayofuata nitaenda nyumbaji. Nyumba yake ilikuwa nzuri ya kupendeza sana hakika alikuwa amejipanga mama yule.

Usiku alinionyesha chumba ambacho ningelala ili siku ifuatayo niende nyumbani.

Nikaingia na kujifungia nikasinzia.

Baadaye usiku mnene nikahisi joto kali sana, nikatoa shuka, bado joto kali, nikatoa nguo nikaona si vibaya nikilala mtupu.

Ndugu msomaji katika hili uwe makini, hali kama hii ikikutokea usiku muite MUNGU wako akusimamie. Mimi nilichukulia kuwa hali hii ilikuwa ya kawaida sana kumbe nilikuwa nawekewa lile joto ili nivue nguo kwa hiari.

Nilipobaki mtupu nikasinzia, eti bila sababu nikaanza kumuota yule mama aliyenisaidia, nikamuona akinikumbatia huku akiwa yu uchi wa mnyama, nikawa naifurahia hali ile joto nalo likazidi. Baadaye nikajikuta nipo katika kuzini na mama yule.

Nilipokuja kushtuka nilihisi kuna harufu kali ya marashi pale chumbani. Na nilikuwa natokwa jasho haswa…..

Nilitapatapa huku na kule kisha nikalala tena hoi.

Asubuhi na mapema nilimsikia yule mama akiniita, nikavaa nguo zangu na kutoka nje hadi alipokuwa.

Alinipokea kwa tabasamu zito kisha akanieleza kuwa yeye alikuwa anataka kutoka akanipatia nauli na kunieleza kuwa nikifika nyumbani nimsalimie mama yangu.

Nikaipokea nauli, akanifungulia mlango nikatoka nje.

Ebwana eee, ukisikia wabaya watu wanyama wanasingiziwa ndo hii.

Nilijikuta nipo katika ardhi ileile ya maajabu.

‘’ulienda kwa huyo mama kufanya nini siku mbili zote hizi..’’ ilikuwa sauti ya adella akiniuliza kwa hasira kali. Nilikuwa nimepigwa na bumbuwazi nisijue ni kitu gani cha kujibu.

Yaani akili haikuwepo kabisa, yaani kumbe kumuamini kote kule yule mama alikuwa ndo yule malikia.

Nilitamani kusema neno lakini kabla sijaongea lolote adella aliita jina la kitu nisichokijua, kisha yeye akaondoka zake.

Mama yangu, akaja yule fisi mtu alikuwa amevimba kwa hasira.

Kumbe adella alimwamrisha aje kunisulubu.

Fisi akafanya kweli, safari hii haikuwa kama mwanzo, sikuona jiwe wala fimbo ya kumchapia.

Fisi akanirukia na kupitisha meno yake kwenye paja langu… maumivu makali yakanipitia.

Nilipagawa sana………

Akanifuata tena na kuniangusha chini kisha akanibamiza na kichwa chake katika mbavu zangu.

Nikashindwa kupumua vizuri.

Yule fisi akarudi nyuma tena kisha akanifuata kwa nguvu sana, nikajua kuwa kwqa namna yoyote ile alikuwa anakuja kunimalizia…

Nikafumba macho huku nikiuma meno kwa nguvu..



NIKIWA nimetulia pale nikikisubiri kifo changu mara nilisikia kilio kikali sana cha mwanaume ambaye alikuwa katika maumivu makali sana. Nikajikuta nikifumbua jicho langu kutazama. Nilimuona yule fisi mtu akigalagala chini huku akijitupa huku na kule.

Na baada ya hapo akatulia tuli huku akianza kuvimba kwa kasi kubwa na kelele kubwa zikiendelea kupigwa na yule fisi mtu.

Uvimbe ule ukaanza kuisababisha ngozi yake ianze kutatuka kana kwamba hapo awali ilikuwa imeshonwa na uzi wa kawaida.

Ilitatuka na baadaye kikasikika kishindo kikubwa sana wakati fisi yule akipasuka na kusambaratika vibaya mno.

Matone mazito ya damu ya moto kabisa yalinirukia, na hapo nikasikia tena mluzi mkali sana ukipigwa.

Ghalfa zikasikika shwangwe na hapo ukawa uwanja wa kugombania vilivyogombaniwa, misukule wale wachafu kabisa wakaingia katika ukumbi wa kuwania mabaki ya kupasuka fisi yule.

Walifika kwanza kwangu na kunigombania huku wakinilamba zile damu kwa matamanio, kucha zao zilikuwa zinaniumiza lakini nilitulia tuli kwa sababu sikujua naweza vipi kujiokoa kutoka katika hali ile.

Niliwaona misukule wengine wakigombania utumbo, wengine waligawana ngozi. Na baadaye msukule mmoja ukapita na kichwa cha yule fisi, kichwa ambacho kilikuwa na sura ya mtu kabisa.

Nikiwa nimeganda pale kama barafu mara alifika mbele yangu yule mama mweusi ambaye alikuwa akiitwa kwa cheo cha malikia.

‘’hicho kisichana chako kinachojifanya kukupenda kilitaka ufe leo nimekuokoa naomba utambue hilo….’’ Alizungumza vile kisha akatoweka.

Dakika mbili mbele ADELLA akasimama mbele yangu akitokea anapojua yeye mwenyewe.

‘’Martin nina ujauzito wako….’’ Alinieleza. Nikatumbua macho na kujiuliza ni lini mimi nilishiriki zinaa na binti yule. Lakini hakuonekana kutania kabisa alikaa akisubiri nijibu alipoona kimya akaendelea.

‘’Tambua kuwa mimi ni mzazi mwenzako…na utaniona Martin utake usitake…’’ alimaliza kusema hayo akaondoka zake. Akarejea alipotambua yeye mwenyewe.

Nilibaki kustaajabu ni kitu gani kile, huyu mama anadai kuwa ameniokoa yeye Adella alitaka nife sasa anakuja Adella anasema ana ujauzito wangu na anaenda mbali zaidi na kusema iwe isiwe lazima tutaoana. Niliduwaa sana.

Baada ya hali ya hewa kutulia, aliagizwa mtu kuja kunipa majukumu na hili jukumu la sasa nilitakiwa kwenda nikiwa mwenyewe bila kuambatana na Adella.

Niliagizwa kwenda kumpa motisha yule msanii wa mziki ili aweze kuhudhuria tamasha katika siku ile maalumu ambayo ilitajwa bila mimi kuitambua.

Alikuwa yule msanii ambaye Adella alianza kumwandaa tayari.

Nilijiuliza nitaanzia wapi bila adella lakini ilikuwa na sikutegemea nikapewa masharti yote ya kufuata. Niliona kuwa ni masharti magumu. Lakini nilipopigwa kibao na kujikuta natokea nyumbani kwa yule msanii ndipo niligundua kuwa mwanadamu ni kiumbe hatari sana, ishi na Mungu kila wakati ili kupambana na mambo haya, lakini bila nguvu zake jamani huko majumbani kwetu kuna mengi sana yanatokea.

Nilifika nyumbani kwa yule msanii, sijui nilikuwa naendeshwa na akili ya nani jamani. Haikuwa akili yangu kabisa, nilikuwa ninalo dumu lililokuwa na maji yale yanayofanania na damu. Nilifika kama nilivyoagizwa nikaliendea jokofu na kulifungua kisha nikaweka lile dumu ndani yake.

Nilikuwa nahofia sana yule mwandishi akisimama itakuwaje. Nilidhani ataniona lakini nilihakikishia kuwa hataamka mpaka nitakapoamua….

Baada ya kuweka maji yale kwenye jokofu nikawasha jani fulani hivi likafuka moshio kidogo kisha nikalizima.

Hivi umewahi kupatwa na kiu kikali sana usiku, ukakurupuka na kwenda kunywa maji.

Binafsi sijui kama ni kila tukio la aina hii linakuwa na maana mbaya ama la lakini naelezea ambacho nilishuhudia tu.

Baada ya moshi ule yule msanii alianza kuhangaika, wakati huo nimesimama nyuma ya mlango ambapo mimi namuona na yeye hanioni. Alisimama na kwenda katika jokofu, akachagua lile dumu langu.

Akafungua na kuweka katika glasi na kugida kwa fujo maji yale yafananayo na damu. Aligida kwa wingi mno, kisha akarejea kulala. Nikaliendea jokofu na kuchukua dumu lile likiwa limesalia na damu ile kiasi.

Kisha nikatoka nje nikapokelewa na fisi mtu mwingine, safari hii sikuuliza nikapanda mgongoni nikamshika masikio tukaondoka kwa kasi hadi kambini.

Na huko nikakuta nimeandaliwa sherehe fupi kwa kufanikiwa zoezi lile.

Nilipokuwa na adella nilikuwa nakula ugali na mboga za majani lakini siku hii nilikaribishwa chakula ambacho kwao wanakiita chakula bora sana.

Zilikuwa nyama nisizozielewa kabisa, na pia palikuwa na maji yafananayo na damu.

Nilikaribishwa kwa shangwe lakini sikuweza kula. Zile sura zilikuwa ngeni kabisa machoni pangu sikuwa na yeyote niliyekuwa namfahamu.

Mara bila mimi kusema neno lolote walianza kucheka kwa sauti ya juu na kisha mmoja wao akawanyamazisha wenzake na kuanza kuzungumza na mimi.

‘’NDUGU mwandishi, yaani ukakosa vitu vyote vya kuandika katika ulimwengu wenu mchafu huo ukaona uanze kutupekua na sisi ili utuandike…. Unajiamini kitu gani wewe kijana….’’ Alinipiga piga begani. Na hapo akaendelea.

‘’ukaona kutuandika haitoshi umekuja huku hata mwezi mmoja bado umempachika mimba binti yetu mchapakazi, hizo gharama za kule mtoto utaziweza mwandishi… ama una uwezo wa kumlipia mahari……’’ alinisanifu na wala hakuwa ameniuliza, akaendelea kunitazama machoni huku akichukua pande la nyama, ni hapo nikaliona lilikuwa limeambatana na sikio la mwanadamu, akarusha lote mdomoni huku akijilamba mikono yake akatafuna na kumeza kisha akatabasamu na kuendelea.

‘’unaotuona hapa sisi ni wazee wa huu ufalme na tumezipata taarifa kuwa umemjaza mimba malikia mtarajiwa wa ufalme huu…. Kwa hiyo wewe umetoka zako huko duniani na ghafla unataka uwe mfalme huku usipopajua.. una jeuri gani wewe……’’ akacheka kidogo na kuendelea, ‘’tumeipanga zawadi yako kwa hiki ulichoamua kufuata huku, tunataka tukupe zawadi ya mengi ya kushuhudia ili ukirejea huko ulimwengu dhaifu uwaandikie na wao wayasome na kutambua kuwa hawawezi kukabiliana na sisi ikiwa wataendelea na huo udhaifu…… kazi uliyoianza ni nzuri sana lakini kuna ugumu fulani, yule msanii amegoma kuja kwenye tamasha letu. Tunahitaji umlete kinguvu sasa maana tumejaribu kistaarabu imeshindikana…… tunahitaji umtumie mama yake mzazi…… na shughuli hiyo ifanyike ndani ya siku nne utuletee majibu, tunakurudisha duniani kwa siku hizo nne kwa ajili ya kuifanya hiyo kazi.. usijidanganye kuwa utatutoroka kwa sababu ulimwengu wenu dhaifu upo katika mikono yetu, ni wapi utakimbilia. Pia tutakuwa nawe kwa ajili ya kukupa maelekezo, sherehe yetu haitanoga bila kuwa na msanii. Ukimaliza hili tutafikiria namna ya kukupunguzia adhabu kwa sababu tangu uje huku haujaadhibiwa ujue… hebu’’ akasita na kisha akazungumza kabila nisilolijua. Na hapo akaletwa bwana mmoja asiyekuwa na mikono na mguu mmoja. Nilikuwa namfahamu kabisa sura yake haikuwa ngeni, aliwahi kuwa mwanasiasa maarufu.

‘’huyu hapa tumekula mguu na mkono na tutamla hadi amalizike kwa sababu alijifanya mbishi na mjanja mjanja’’ alinieleza. Halafu akaletwa mwanamke.

‘’unamuona huyu na mimba yake, hii mimba ina miezi thelathini hadi sasa, hatutamuachia kirahisi azae anajua alichotufanyia, ataumwa uchungu lakini hatajifungua…..’’ alinieleza na kisha akarejea tena katika mazungumzo.

‘’tunakuagiza kuifanya kazi, kaifanye kazi na hautakuwa na ugomvi na sisi lakini ukileta kujua sana hakika utateseka sana na huo si mkwara tupo makini na tunachokifanya.. tunakurudisha duniani uende kwa mama mzazi wa huyo msanii, ni kipi utamfanya ama kipi utatakiwa kufanya ukifika duniani tutakutumia majibu…. Simama ‘’ aliniamrisha nikasimama………

Kama nilidhani mambo magumu yalikuwa kumuona mwanadamu akimla mwanadamu mwenzake, nilikuwa najiongopea kuna mengine magumu zaidi yaliyokuwa yakinisubiri.

Kuna jambo moja tu msomaji nilikuwa nalisahau kila siku, nilikuwa namsahau ama sikuwahi kumtegemea Mungu. Ni vile sikukuzwa katia misingi hi indo maana niliteseka sana, na huenda haya yalinitokea ili nije kukuandikia wewe usome kisha ujifunze……









Katika kipengele kimojawapo katika masimulizi haya nilisema kuwa wabaya watu jama wanyama kama paka na fisi hawa wanatumwa tu hawana ubaya wowote.

Na hawa watu wabaya hawazaliwi na roho mbaya bali mazingira na matukio yanayowatokea maishani husababisha wawe na roho mbaya.

Mimi nilishiriki kutimiza matakwa ya watu hawa wenye roho mbaya.

Nilifungwa akili jamani, hadi sasa hivi sijui ilikuwaje hadi nikashindwa kabisa kutoroka. Acha niamini kuwa nilifungwa akili katika kiwango cha juu sana…

Nilitupwa duniani, nikajikuta nipo katika chumba kimoja kilichokuwa na meza na viti viwili huku pia pakiwa na kitanda na godoro.

Kwa kifupi kilikuwa ni chumba ambacho angeweza kuishi kijana ambaye bado hajaoa. Sikuwa nafanya kazi yoyote, lakini kila siku nilikuwa nakuta chakula pale ndani, kilikuwa chakula kizuri sana kwa kutazama, wakati mwingine kuku, pilau, nyama ya mbuzi na kadhalika.

Ilikuwa baadaye sana nilipoambiwa kuwa zile hazikuwa nyama za kuku wala mbuzi bali nilikuwa nalishwa mizoga ya fisi na wakati mwingine nyama za watu ili niwe na roho mbaya.

Naam, ile roho ikajipandikiza na nikajikuta nayazoea maisha yale kwa juma moja tu.

Na hapo nikaingia kazini.

Mama wa yule msanii alikuwa ni mjamzito, ujauzito ule ulikuwa una miezi ipatayo nane na nusu. Muda wowote ule alitakiwa kujifungua.

Ni hapo ndipo nilipofanya nilichoagizwa, nilimfuatilia yule mama alipokuwa akifanya maozezi ya kutembea, nikapishana naye na kisha nikachota mchanga katika hatua alizoacha barabarani. Nikaenda na ule mchanga ndani kwangu, usiku wakaja wazee kuuchukua huku wakiniambia kuwa nimefanya kazi nzuri.

Ni hapo yalifuata mateso makali kwa yule mama, wanasema uchungu wa mwana aujuaye mzazi, sasa jiulize ule uchungu unakuja lakini mtoto hatoki.

Walimwengu wana mapana jama.

Niliagizwa niende kumshaurti yule msanii ambaye alikuwa ni mtoto mkubwa wa mama yule. Niliamriwa nimshawishi aende kwa waganga kwa sababu hospitali pekee haitoshi.

Kweli nikaenda kumsalimia yule mama pale hospitali nikijifanya mimi ni jirani mwema, baadaye nikamvuta yule bwana na kisha nikamuelezea kuwa hata mimi mama yangu aliwahi kupatwa na tatizo kama lile, nikamsihi sana kuwa lile si tatizo la kawaida na asipokuwa makini basi mama yake ataaga duniani.

Nani kama mama……. Kusikia kuwa mama atapotea akanishika mkono na kuniuliza ni kipi anatakiwa kufanya.

Kitendo cha kunishika mkono likawa ni kosa kubwa sana kwake.

Akajikuta akinisikiliza kila nilichokuwa nasema.

Hatimaye baada ya siku mbili nikamfikisha kwa mganga ambaye alikuwa mwenzetu pia.

Akamchanganyia madawa, akampa na maelekezo.

Ile tunarudi hospitali mama alikuwa amejifungua tayari mtoto wa kike.

Yule msanii akanishukuru sana lakini nikamwambia kuwa aende kumshukuru yule mganga.

Kweli akaenda na huo ukawa mwisho wake kuishi duniani.

Niliumia sana mpenzi msomaji, kwani nilikuwa duniani wakati wakitangaza kuwa msanii yule amekutwa akiwa amekufa kitandani kwake bila kuwa na kovu hata moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…