Bure Series

Bure Series

MWISHO WANGU

SIMULIZI FUPI - MWISHO WANGU

Nilidhani kubadilisha ndoto zangu na kuvurugikiwa ilihitaji miaka mingi jambo hilo kutokea. Nilidhani kuisha kwa uzuri wangu na kila nilichokianzisha toka nilipokuwa mdogo ilihitajika miaka mingi kama ile niliyokuwa nayo sasa. Nilikuwa msichana mdogo sana na mwenye ndoto kubwa ambazo tayari sasa zilikuwa zimetimia. Kuwa na magari ya kifahari na familia yenye furaha ndicho kitu nilichokiwaza katika muda wote wa maisha yangu. Hatima ya maisha yetu anayeijua ni Mungu na kamwe huwezi kumuona na kumuomba muda zaidi maisha yafikapo tamati, kila kitu huvurugika pale jioni ya maisha yako ifikapo. Milango ya ndoto zako hufungwa na giza nene hutanda mbele, fimbo ya kukuongoza njia hupotea. Mwanga hufifia na woga hukusonga.

Hiyo ndiyo hali iliyonipata, machozi na jasho vikanitoka, aliyekuwa awe msaada wangu akanikimbia na kunisahau. Hata wale niliowadharau mwanzoni na kuwaona hawawezi kuwa chochote kwangu wala kunipa msaada nilitamani sasa wajitokeze lakini haikuwa hivyo. Msichana mrembo nikageuka kuwa kituko mbele ya jamii, maringo yangu yote na elimu yangu havikunisaidia kupata huruma ya wanajamii. Jina nililopewa toka utotoni lilikuwa ni Yasmin, ila kwa mapenzi na upendo mkubwa kwa Tony niliamua kubadilisha dini na kuitwa Anjela. Lakini mapenzi yangu kwa huyu mwanaume yalifanya niringe na kujidai, nilimpenda sana, alikuwa ni mtanashati alikuwa ni mwanaume mwenye pesa zake na niliamini alikuwa akinipenda. Maisha mazuri tuliyoishi mimi na yeye yalinifanya niwaone majirani zangu kama takataka, Tony alinikataza kabisa kujumuika nao na mimi sikuona haja hiyo ya kuwa karibu nao. Niliishi kivyangu, hata marafiki zangu niliwakwepa baada ya kufungwa ndoa na Tony, nia yangu ni kujiepusha nao ili wasijewakamzoea Tony.

Nilimpenda sana Tony wangu. Kwa shida na raha ndio nadhiri tulioiweka kanisani, ndugu wakachukia kwakuwa tu nilikubali kubadili dini, nikajipa moyo kwakuwa mwanzo nimeshaujua. Maisha mzuri, kazi nzuri, mume mzuri na hatimaye furaha yangu ikatimia baada ya kupata watoto mapacha, watoto waliokuja kubadilisha mwonekano wa familia na mategemeo yangu. Leticia na Lucrecia ndo majina ya watoto wetu. Walikuwa wazuri sana, watoto wa kike niliowaota siku nyingi sana, wakwe zangu wakaja kunipa hongera, tukasafiri na Tony hadi Irkepusi huko kwenye kreta ya Ngorongoro ili watoto wakamuone mzee Ole Senteu ambaye ndiye babu yao. Tony alikuwa ni Mmasai, alikuwa ni moja kati ya wamasai wasomi na walioishi maisha ya kimjini sana.

Mimi nilikutana na Tony chuo kikuu cha Dar es Salaam kipindi yeye akiwa anasoma uhandishi wa elektroniki, alikuwa kijana mrefu na mtanashati, sikukwazwa na masikio yake au ndonya kwenye paji la uso wake, nilipenda lafudhi yake na haswa alipokuwa akiongea kingereza. Tulipenya misitu na mabonde mpaka irkepusi na tulifanikiwa kufika, vichanga vikafanyiwa mitambiko na tukaruhusiwa kurudi Dar kuendela na maisha Mzee Ole Senteu akamuasa mwanae awe mwangalifu wa watoto, akamsihi anipende na kuniheshimu. Nasaha zikamkaa Tony na nyumbani tukarudi. Tony aliyenipenda sasa alikuwa hasafiri tena, alikuwa akiwahi kurudi nyumbani na aliwapenda sana watoto kuliko mimi. Alikuwa ni mtu wa safari kwa kipindi kabla sijajifungua lakini baada ya hapo hakutaka kusafiri. Mara zote alikuwa nyumbani akiwabeba watoto wake.

Nilimpenda sana mume wangu, nilimpenda kuliko chochote. Asubuhi ilikuja na usikuwa ukafata, riadha na matarajio yangu yakaanza kuota mbawa, watoto wakakua na sasa wakaweza kusema baba na mama, siku zikaenda na miaka nayo ikatutupa mkono. Tony na safari, safari na Tony, Tony anakwenda Uingereza na watoto wanakaa hata miezi sita. Akirudi utasikia anakwenda Ngorongoro huko umasaini, namwambia Tony twende wote Tony hataki ananambia niende kazini na nikae na nyumba nirudipo. Watoto wakajengwa kisaikolojia na hawakuwa tena wakiniita mama, wao kila mara wakawa wanamuwaza baba yao tu, eti tena wananiita AUNT ANJELA, mh! ndo walivyofundishwa na baba yao.

Miaka minne ikakatika Tony akawapeleka watoto shule ya bweni iliyoko Kenya, nikabakizwa bila watoto,. Nani ataamini kuwa eti toka nilipojifungua mpaka watoto wanakua na kwenda shule sijawahi kufanya mapenzi na Tony? Yeye kila wakati amechoka, injinia yuko kazini hata usiku.

Hisia zangu zikaporomoka na mawazo yakaujaza uso wangu. Akili ikagoma kama mshale wa saa, sina tena wa kumwelezea matatizo yangu. Mawifi niliowategemea wakawa wakali kila mara wananiambia nampa kaka yao presha. Nikaanza kujuta kuitwa Anjela. Bado moyo wa kuwa na Tony kama zamani nilikuwa nao, nilijua tu siku moja Tony atakuja kuwa kama mwanzo pale ambapo kazi zitaisha. Sina rafiki tena, mtaani nilikuwa naringa kama nimeolewa na mfalme, hakuna mwingine zaidi ya mimi. Tony akaniambia niache kazi hataki kuona nikiwa nahangaika na kazi tena. Nikamkatalia, akaingia ndani na kuchukua vyeti vyangu vyote akachoma moto. “Nimekuambia ukae hapa nyumbani kama hutaki tafuta pa kwenda, unahangaika nini wakati pesa ipo, nini cha kukufanya uangaike kuamka saa 11 asubuhi eti unakwenda kazini wakati mimi nafanyakazi? Kaa nyumbani wanangu wanarudi toka shule uwahudumie na unihudumie na mimi, hiyo ndio kazi ya mama yoyoo.” Tony akanikoromea kwa ile lafudhi ya kimasai. Akawa mbogo na mori zikataka kumpanda, mwanamke kumbishia mwanaume kwenye kabila lao haikuwa sahihi, kile kitendo cha mimi kukataa kuacha kazi yeye alikichukulia ni kama dharau.

Lakini haikuwa hivyo, haikuwa rahisi kwa yeye kuchukulia kuwa kawaida kwakuwa tayari alishakasirika. Wakati ananigombeza akaja kaka yake wakawa wanazungumza “yero subai” Tony akamsalimu na kaka yake bado akishangaa inakuwaje nilikuwa naongea na mume wangu huku nimesimama, “Yeba, Keiya” akaitika yule shemeji yangu, Tony akiwa bado anatetemeka mikono kwa sababu ambayo haikuwa kubwa akaitikia tena “Shidai”, Ole Itutu akaniangalia na kunipengea kamasi, Tony akalisikia na kugeuka, nilikuwa nalia lakini Tony hakufanya chochote. Wakaingia ndani na mimi nikaketi pale chini nikijililia. Nikatamani nimpigie Cesilia simu lakini ningeanzia wapi? Marafiki niliowatelekeza kwa kumpata mume leo ningeanzaje. Niajikaza tu, wanangu wakarudi kwa likizo baada ya kuwa shuleni muda mrefu sana, nikajua watakuwa wamebadilika na kuanza kumpenda mama yao, lakini haikuwa hivyo. Walikuwa ni watoto wa kizungu. Wakaja na kuniona kama vile mimi ni mfanyakazi wa ndani, wakanijibu watakavyo na Tony akawa anawaangali tu, sikuwa na mamlaka na wanangu.

Siku ya tatu toka waje Tony akaniambia anawapeleka watoto umasaini ili wakajifunze mila na lugha ya kimasai. Sikuafiki hilo, tuligombana sana na Tony, nia haikuwa mimi kuwakataza watoto kwenda umasaini, hapana, nia yangu ni kwamba nilihitaji kukaa na wanangu angalau nijaribu kuwaonyesha kuwa mimi ndo mama na wanatakiwa wanithamini.

Mawazo yalikuwa ndiyo sehemu ya maisha niliyojichagulia. Kiu ya wanangu ilizidi kuwa kubwa kwani baada ya wao kwenda umasaini sikuwaona tena na niliambiwa kuwa wamesharudishwa shule. Tony alikuwa ni Mnyama kuliko hata Khajat wa kwenye hadithi fulani niliyowahi kuisoma, maumivu yangu yalilingana na Nadia kwenye hadithi ya mwandishi mashuhuri aliyeitwa George.

Nikawa mpweke, lakini bora basi watoto waondoke ila Tony awe karibu na mimi, hiyo ilikuwa ndoto ya mchana, safari za Tony zikazidi, mwaka wa tano Tony hataki kufanya mapenzi na mimi eti amechoka. Nikapekuwa makabrasha yake, nikakuta risiti za ada za shuleni walikokuwa wanasoma wanangu. Nikapekuwa na kukuta namba za simu za ile shule, nikapiga simu kwenye ile shule ndipo nilipopagawa. “hallo” simu ilipokelewa na mwanamke aliyeonekana kabisa kuwa alikuwa anatarajia nimuongeleshe kwa lugha ya kwao. “Am calling from Tanzania, I was asking to speak to my daughters. (napiga simu toka Tanzania, nilikuwa naomba kuongea na binti zangu)” nikajaribu kwa upole na unyenyekevu kuomba japo nisikie sauti ya wale watoto ambao hawakuwa wakimpenda mama yao. “madam am sorry its 6pm now the pupils have already went home. (Madam samahani kwasasa ni saa 12 jioni na wanafunzi wameshakwenda nyumbani)” mwe! Yule dada akanijibu kama vile alikuwa anashangaa. Nikataja mpaka majina ya wanangu ila yule dada akaniambia wao hawana mtoto anayekaa bweni, akaniambia watoto wamechukuliwa na mama yao ambaye ndiye anayewaleta na kuwapitia arudipo kazini.

Nikaomba namba ya yule mama na nikampigia lakini akaniambia nikae mbali na watoto wake. Nikajaribu kumwambia majina ya wanangu kama ndo hao akanijibu ndio hao ila nimuulize Tony nani mama wa wale watoto, nikamsihi anipe niongee na wale watoto, akawaita na nikasikia sauti ya Leticia ikiitikia abee mama, sikuwahi kusikia mwanangu akiniitikia vile, kisha alimwambia njoo umsalimie Aunt Anjela, ila mtoto akasema baba amesema tusipende kuongea na Aunt Anjela..niliumia sana. Nikashangaa na kutahamaki kwanini Tony anifanyie vile.

Kesho yake nikatoroka nyumbani kwakuwa alikuwa amesafiri, nikapanda ndege asubuhi mpaka Nairob nchini Kenya, nikawasiliana na yule mwalimu na akanielekeza shule ilipo, nikaenda na watoto walikuwa bado hawajaletwa kwakuwa walikuwa wanaingia darasani saa 7 siku hiyo. Nikakaa na baadaye niliona gari likiwashusha wanangu, nikawakimbilia, ooh mungu wangu watoto wakasimama hawakutaka kunitazama, wakageuka na kuangalia nyuma, nikashangaa sana Tony kutoka kwenye ile gari na kuja kwa haraka, hakuniuliza kitu, alinipiga kupita kiasi mbele ya wale watoto, yule mwanamke aliyekuwa naye kwenye gari alitoka na kuja pale kisha akamwambia Tony aniache.

“Tony mume wangu, muache tu, hiyo inamtosha.” Yule mwanamke akaonekana kufurahia kilichonitokea.

“We dada, mimi ni mwanamke mwenzio, nilipata shida miezi tisa kubeba watoto hawa na zaidi nimewalea na wewe leo hii unashiriki kunitenga na wanangu, mchukue Tony ila niachie wanangu.” Yule dada akanipandisha na kunishusha. Akanitemea mate na kuondoka. Jamani mimi ni binadamu au takataka. Nikanyanyuka na watu walikuwa wengi pale, damu zilikuwa zikinitoka puani. Nikamuomba mtu anionyeshe hospitali ilipo nikaenda wakanitibu pale na kunifunga vidonda vile kisha nilielekea uwanja wa ndege na kupanda ndege ya kuja dar.

Nilipofika Dar nilikwenda kufata gari yangu niliyokuwa nimeiegesha kwenye maegesho ya pale uwanjani na kuondoka. Nilikuwa nalia kama mtoto. Nikafika ubungo mataa nikiwa mbele kabisa nasubiri foleni iruhusu, machozi yakaujaa uso wangu, nikaona taa ya kijani, kumbe haikuwa ya kijani, ilikuwa ni nyekundu ila niliona vibaya, nikaondoa gari na kukutana na Lori la mizigo. Nilikuja kushtuka wiki mbili mbele, nilikuwa mwenyewe hospitalini, miguu yangu yote ilikuwa imekatwa kuanzia kwenye magoti kushuka chini, nikalia sana. Nikauliza kama kuna mtu amekuja kuniangalia nikaambiwa kuna mtu alipiga simu akasema atakuja kuniona lakini hajawahi kuja. Nikauliza namba iliyopiga wakanijulisha ilikuwa namba ya Tony. Tony hakuja mpaka karibu naruhusiwa ndipo alikuja, akajifanya kunipa pole. Madaktari wakamwambia atoe milioni nne niwekewe miguu ya bandia ila alisema hana pesa.

Nikasema akachukue kwenye akaunti yangu lakini Tony akajibu kuwa ameshazitumia kwenye kitu kingine na kwamba hakuna haja ya kumuhudumia kiwete. Tony akamuhamishia yule mwanamke nyumbani na mimi akanipa chumba kingine. Hiyo haijatosha Tony hakutaka hata kuniogesha, eti akamleta kijana wa kiume awe ananihudumia na kuniogesha. Mh! nilikaa mpaka wiki mbili na nguo moja, sikuweza kujisogeza kwakuwa sikuwa na nguvu, alininyang’anya simu na kunifungia ndani.

Kuna siku nilikuja kuona huo ni ujinga, nikajiburuta mpaka sebuleni, Tony alikuwa amelala sakafuni na yule mwanamke wakichezeana, nilikuwa na kisu nimekificha, niliposogea taratibu nikakipenyeza kile kisu kifuani kwa Tony na kukichomoa haraka, wakati yule mwanamke anataka kukimbia nilivuta dera lake na hapo alianguka nikamchoma kisu cha tumbo na kurudia mara nane, nilirudi tena na kumchoma Tony kisu mara ishirini.

LEO HII NIKO HAPA NASUBIRI RAIS AWEKE SAHIHI KWENYE HATI YA MAHAKAMA ILI NINYONGWE,,,niliishi na watu vibaya naomba kila mtu anisamehe.

MWISHO
 
UMENIUA ASHURA

SIMULIZI FUPI - UMENIUA ASHURA

Ashura .. oooohh.. Ashura … umeniua!!!

Kwa nini umenifanyia hivi Ashura…??? Nilikukabidhi moyo wangu nikiamini kuwa unanipenda. Ndiyo, niliamini hivyo tangu siku ile ya kwanza tulipokutana pale TILDO mwaka 2010, wakati tunarejesha fomu zetu za maombi ya mkopo kwenye ofisi za bodi ya mikopo ya elimu ya juu.

Naikumbuka sana siku hiyo… ulikuwa umevaa baibui la rangi nyeusi, vazi lililoyasitiri maungo yako na kukufanya uonekane mwanamke mwenye staha, nikapendezwa na wewe na Moyoni nikafikiria kukufanya uwe mke, tabibu wangu wa moyo.

Wakati bado napiga hesabu za kukufuata … mara ghafla nikakuona ukichapua hatua kuja mahali nilipo. Sikuwa na uhakika kama ulikuwa unakuja kwangu mpaka ulipofika mbele yangu na kunisalimu, “Kaka mambo?” Siyo siri Ashura… sauti yako iliufanya moyo wangu kuzizima mara tu ilipotua masikioni kwangu. Sauti yako ilikuongezea alama na kukufanya uwe mrembo maradufu, na mara shauku ya kuwa nawe kama mke ikakita barabara kwenye kitako cha moyo wangu.

Kwa kuwa sikutaka kuonekana dhaifu kwa viumbe wa jinsia yako, nilijikaza kiume na kuitikia “powa, inakuwaje?” nilitoa sauti kavu, japo moyoni nililainika kama siagi kwenye kikaango cha moto.

Baada ya salamu ulinieleza shida yako nilikuelewa, tukatoka nje, tukavuka barabara mpaka upande wa pili kwa yule mwanasheria aliyekuwa akitia sahihi na kugonga muhuri kwenye sehemu ya kiapo cha wakili, sehemu ambayo ilikuwa tupu kwenye fomu yako kabla hatujafika kwa yule mwanasheria!

Baada ya kutoka kwa Yule mwanasheria tulivuka barabara na kurejea tena TILDO, ukakusanya fomu yako. Huo ukawa wasaa wa sisi kufahamiana, wasaa ambao baadaye ulituweka kwenye dunia ya mapenzi…mapenzi

mazito!

Tukawa kama jozi ya viatu visivyofanana ila vyenye kurandana, naweza kusema tulikuwa kama mapacha wa hiyari tuliokulia na kuzaliwa kutoka katika matumbo tofauti. Kwa ufupi tuliendana sana.

Tukapanga mengi juu ya maisha yetu ya baadaye, ikiwemo kufunga ndoa licha ya tofauti za kidini zilizokuwepo baina yetu…mpaka hapo naweza kusema; ‘kweli mapenzi ni upofu!’

Siku zikaenda….zikaenda hatimaye ukafika wakati tukayaanza masomo yetu ya elimu ya juu. Wakati wewe ukiwa ‘DUCE’ Chang’ombe mimi nilikuwa ‘MUCE’ Iringa, wote tukisoma shahada ya kwanza ya ualimu.

Umbali kwetu haukuwa kikwazo cha mapenzi yetu, tukaendelea kuwasiliana kwa simu tukijuliana hali na kutiana moyo katika masomo yetu, huku mipango yetu ikiwa palepale kwamba siku moja tufunge ndoa tuishi kama mke na mume..

Katika mazungumzo yetu hayo, mara swali likaibuka, “Tutafunga ndoa ya namna gani ilhali twapishana kwa imani ya dini?”

Nilikusihi ubadiri dini ili tufunge ndoa kanisani, ukalipinga suala hilo kwa sababu ambazo hata mimi niliziafiki. Ulidai kuwa wewe ni yatima ambaye umelelewa na babu na bibi, na ukazidi kudai kuwa babu yako ni kiongozi mkubwa wa kidini, hivyo wewe kubadiri dini ni sawa na kuifungua milango ya laana kutoka kwa babuyo, halikadhalika pia utengano baina yako na nduguzo, nilikuelewa na nikakukubalia kwa sababu siku zote nilitaka uwe mwenye furaha, na katu sikutaka kukuona mwenye huzuni tangu machoni mpaka moyoni.

Kwa sababu ya kukupenda sana, upendo usio kifani nilifikiria na kujishauri sana hatimaye nikaamua kubadiri dini kwa ajili yako, nikaitwa Mustafa baada ya miaka mingi ya kuitwa John…jina nililopewa na wazazi wangu muda mfupi baada ya kuzaliwa.

Ulifurahi sana, jambo ambalo lilinipa faraja kwa kuwa nilitaka kukuona mwenye furaha!

Mwaka wa kwanza wa masomo ukaisha, tukaingia wa pili bila misukosuko kwenye masomo yetu. Muda wote huu ulipita nikiwa siijui hata tupu yako, achilia mbali kukubusu jambo ambalo sijawahi hata kuthubutu baada ya wewe kuniambia kuwa; “Ni dhambi kuikaribia zinaa” hapo nilikuelewa kwa sababu hata mimi nalijua andiko hilo mujarab.

Kwa kuwa mimi ni mwanaume rijali, nilikusihi tuitafute ‘NUSRA’ ili kujiepusha na dhambi ya kuzini, dhambi ambayo ilikuwa ikitukaribia siku hadi siku.

Ashura mpenzi wangu ukanipinga kwa kusema haitawezekana kwa sababu ‘Mshika mbili moja humponyoka’ hivyo tusubiri mpaka pale tutakapomaliza shule. Nilikuelewa na nikazidi kumuomba Alah anijaalie moyo wa subira.

Kwa kuwa Alah si mnyimi wa fadhila, alinijaalia subira mpaka mwaka wa tatu wa masomo yetu ulipoisha. Tukahitimu salama salmin tena kwa ufaulu wa alama za juu. Ashukuriwe Jalali!

Baada ya shule kweli tulifunga ndoa, ndoa ambayo ilinifanya niyagundue mengi kwenye mwili wako. Kwanza; Ashura ulinidanganya kuwa wewe ni ‘bikra’, kumbe si kweli na nilipokuuliza ulidai kuwa; labda ilitoka yenyewe baada ya wewe kuendesha baiskeli kwa umbali mrefu ulipokuwa ukienda kuteka maji kisimani, na ulipoenda kusaga kwenye mashine ambayo ilikuwa kijiji cha pili kutoka kijijni kwenu. Na kwa hili pia nilikuelewa!

Naweza kusema wewe ni mwenye bahati Ashura, ndiyo wewe ni mwenye bahati kwa sababu umejaaliwa mume ambaye ni muelewa na mvumilivu…lakini kwa makusudi kabisa umeamua kuniua!

Kwa nini Ashura…kwa nini….umeniambukiza ukimwi? Wakati unajua fika kuwa mimi ndiye mtoto wa pekee kwa yule mama mjane ambaye alijitoa kwa hali na mali kuhakikisha mwanaye nasoma kwa karo iliyotokana na biashara ya ubwabwa!

Eti unanituliza kwa kuniambia, “I’m sory!” I’m sory ina maana gani baada ya kunichafulia damu kwa virusi?

Mwanamke niliyekupenda, nikakuamini, nikakukabidhi moyo wangu….leo umeniua!! Umeniua Ashura…umeniuaa!!!

MWISHO
 
ULAANIWE

SIMULIZI FUPI - ULAANIWE

Kabla sijakuandikia haya nilivuta kumbukumbu ya miaka kadhaa nyuma Maria. Siku ile tulipokutana kisimani kuteka maji, macho yetu yakatazamana na sote kwa pamoja tukajikuta tukiona aibu.

Haikuwa mara ya kwanza kuonana lakini ile ilikuwa siku maalumu, ukaniomba nikutwishe ndoo ya maji, wakati nainyanyua tyukatazamana tena machoni na kujikuta tukitabasamu.

Haikuwa mara ya kwanza kutabasamu, lakini hii siku ilikuwa ya aina yake.

Siku ambayo nafsi zetu zilishindwa kutunza siri na kwa pamoja zikakiri kuwa zilikuwa zinahitajiana. Nilikwambia nakupenda nawe ukajibu unanipenda pia.

Maisha yetu duni hayakutuzuia kufurahi, nyumbani kwetu tukipika magimbi nilijitahidi kuficha pande moja na kukuletea shuleni, na wewe ulinihifadhia mahindi ya kuchemsha na kuniletea katika kile kisima tulichokutana mara ya kwanza. Nakumbuka hekima zako na jicho lililoona mbali, ulisema tusishiriki ngono kwani mwalimu wa sayansi alidai kuwa ni hatari kwa afya na pia husababisha mimba kabla ya wakati.

Nilikusifu na kisha nikateta na moyo wangu nikisema wewe ni msichana wa kipekee sana kwangu. Msichana mwenye ndoto za maisha.

Darasa la saba likamalizika, sikubahatika kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kama ilivyokuwa kwako. Ulilia pamoja nami na almanusura ugome kwenda shule uliyochaguliwa,

nikakusihi usome ili siku moja tuiendeshe familia yetu vyema, na hapo rasmi nikajikita katika kilimo.

Maria ukaenda shule huku ukisisitiza kuwa unanipenda sana, shule ilikuwa umbali wa vijiji vitatu kutoka kijiji chetu. Nilipouza mazao nilifunga safari na kukuletea pesa kidogo za matumizi, walimu walinitambua kama kaka yako lakini mimi na wewe tulijua nini kinaendelea. Kila nilipokuja ulinisisitiza kuwa unanipenda sana na mimi ni kinga yako dhidi ya wanafunzi wa kiume wanmaokutongoza kila kukicha.

Nilijisikia fahari, elimu yangu ya darasa la saba lakini nina nafasi kubwa zaidi ya hao wanafunzi wenzako. Nikaongeza bidii katika kilimo na wewe ukaendelea kusoma kwa juhudi.

Sifa zako darasani nilizisikia kutoka kwa wanafunzi wenzako, walienda mbali zaidi na kusema kuwa ulipewa zawadi ya mwanafunzi mwenye nidhamu. Hayo yote yalikuwa fahari kwangu, nilikutazama kwa jicho la mke mtarajiwa nawe ukanitazama kama mume.

Mama yangu alitaka nioe baada ya kuwa kilimo kimekaa mkao wa kuniingizia kipato huku ufugaji nao ukishamiri. Nilipingana naye katakata na kumwambia kuwa wakati bado.

Mama alilalamika sana akitaka kumshika mikononi mjukuu wake wa kwanza kabla hajafa lakini haikuwezekana kunishawishi kuoa msichana mwingine tofauti na wewe Maria.

Sikushtuka ulipochaguliwa kujiunga kidato cha tano maana dalili zilikuwepo za kutia matumaini.

Sasa haukuwa umbali wa vijiji vitatu bali mikoa kadhaa ambayo hakika nisingeweza kumudu kuhudhuria mara kwa mara.

Hapo rasmi yakaanza mawasiliano kwa njia ya barua. Nilikuandikia nawe ukaniandikia, kila barua yako haukusita kunikumbusha kuwa unanipenda sana na hakuna mwingine zaidi yangu. Nilizitunza barua zako kama kumbukumbu baada ya ndoa yetu.

Ndoa ambayo tulipanga ifanyike baada ya wewe kumaliza kidato cha sita. Hata mama nilimwambia kuwa nimekaribia kuoa. Akaniuliza namuoa nani sikumjibu upesi!!

Nilichomwambia ni ‘avute subira’

Ulipomaliza kidato mambo yakabadilika, ukalalamika kuwa huwezi kuolewa kabla hujawa na shahada ya kwanza, kama kweli nakupenda ningoje miaka mitatu si haba!!

Ni kweli nakupenda nikalazimika kungoja.

Huku kijijini nilifanikiwa kujenga nyumba yangu ya tofali za kuchoma, basi wasichana kadhaa walijiweka niweze kuwaoa, lakini kwanini nikusaliti wakati moyo wangu ulinituma kwako pekee.

Maria, ninapoyaandika haya sikulaumu wewe bali nailaumu elimu uliyoipokea katika kichwa chako, nalilaumu na hilo jiji lililokupokea.

Sasa ulikuwa na simu hukutaka tena habari za barua, ulitambua kabisa kijijini kwetu mtandao wa simu haukuwa umefika lakini ukanitaka niwasiliane nawe kwa namba yako. Kuupata mtandao nililazimika kunyonga baiskeli yangu vijiji vinne zaidi na hapo ningeweza kusema nawe japo kwa shida.

Kuna siku nilinyonga baiskeli yangu, ikapata pancha tairi zote mbili nikalazimika kuisukuma huku natembea, nilichoka sana lakini kila nilipokumbuka kuwa ni safari ya kwenda kuzungumza nawe nilijawa na nguvu mpya na kisha kukaza mwendo.

Nilipokupigia simu ukazungumza kwa sekunde chache tu, nayakumbuka maneno yako hadi leo ninapokuandikia haya, uliniambia upesiupesi “NIPO KWENYE DISKASHENI NICHEKI KESHO” hata hukuniaga ukakata simu.

Maria, hivi ni kwa sababu sikuwa najua maana ya diskasheni ama ni kwa sababu niliishia darasa la saba basi kila kitu ukaniona sijui na sitakiwi kujua??

Yaani hata salamu yangu niliyokupa kwa furaha hukujibu!!

Hiyo ilikuwa siku ya kwanza kujikuta nakasirika kwa sababu yako!!

Nikaziba pancha na kunyonga kurudi nyumbani, usiku wa kiza kinene.

Lakini hata siku iliyofuata nilijikuta sina hasira na ninatamani kuzungumza nawe, na hapa ndipo nikatambua kuna nguvu ya mapenzi inaniendesha nafsini.

Tulizungumza kwa dakika kumi, niliridhika japo sikusikia ukiniomba msamaha kwa kitendo chako cha kunikatia simu, lakini bado sikujali nilichofurahi ni kuwa tumezungumza, nilitaka kukueleza siku hiyo kuwa mama amelalamika tena juu ya mjukuu. Lakini nilisita na kubaki nalo moyoni nikingoja umalize miaka yako mitatu.

Mawasiliano yetu yakaendelea kuwa ya nadra sana na ile hali yako ya kunikumbusha kuwa unanipenda mara kwa mara ikatoweka, ukawa mtu wa kungojea nikwambia nakupenda nawe unajibu kwa sauti ya chini “NA MIMI PIA”…….siku zikasonga mbele bila mimi kuchoka kukwambia kuwa nakupenda, lakini sasa ulijibu “ME TOO” tena kama unayejilazimisha, nilitamani sana kuuliza lakini imani yangu haikuniruhusu kumfikiria mtu vibaya pasipokuwa na uthibitisho.

Nikaendelea kungoja!!!

Ujenzi wa barabara ulikuja na Baraka katika familia yangu!! Serikali ikatulipa milioni kadhaa, kwa sababu mimi nilikuwa mtoto wa kiume nilisimamia masilahi yale. Nikaikarabati nyumba yangu na kuwa ya kisasa, wasichana wakazidi kujigonga lakini kila nilipowakaribisha nyumbani kwangu walikutana na picha yako kubwa ukutani.

Ulivaa kiheshima sana na ulikuwa unatabasamu!!

Hapo wakakata tamaa, na niliwaeleza kuwa wewe ni mama mwenye nyumba ile.

Umbali hunyausha mapenzi!!

Nikaamua kukufungia safari kuja huko chuoni kwako Dar es salaam. Nikamuaga mama kuwa kuna biashara naenda kuchukua huko. Akanibariki kwani sikuwahi kumwangusha hata siku moja tangu nikose nafasi ya kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza.

Nikaingia jijini, nikajikuta nina utofauti na kila mtu, shati langu kubwa lililochomekewa katika suruali pana ulikuwa utambulisho tosha kuwa nimetoka kijijini.

Hayo sikujali, kwa sababu niliamini kuwa najua kusoma na kuandika pia naweza kuzungumza Kiswahili fasaha basi lisingeharibika neno.

Nikajifanya mjinga na kuuliza huku na kule hatimaye nikakipata chuo chenu.

Chuo kikanipokea kwa namna ya kusahangaza, nikataka kufumba macho lakini nikawakuta wenzangu wakiyakodolea macho mapaja yaliyoanikwa nje na asilimia kubwa ya wasichana, wakati nataka kuduwaa kuhusu nywele za bandia katika vichwa vya akina dada mara nikakutana na wengine wakiwa wameyaanika matiti yao nje. Walikuwa wanacheka kama hawayaoni, na waliponipita nikaona jinsi wanavyoshindana kutikisa matako yao.

“Mungu wee!! Maria wangu ameweza vipi kuwavumilia watu hawa….” Nilijiuliza huku nikiendelea na msako wa kumshangaza Maria, nilikuwa nimenunua kanga na vitenge, gauni kubwa refu kwa ajili ya Maria. Nilikumbuka pia kumnunulia nguo za ndani kwa kumkadiria kiuno chake cha enzi hizo.

Niliulizia juu ya Maria na bado sikumpata, niliambiwa kile chuo kina Maria kama mia hivi.

Nikajihifadhi mahali na kumkodolea macho kila anayepita mbele yangu, sasa sikuyaonea aibu matako na matiti yao, mapaja pia sikuyaogopa.

Majira ya saa mbili usiku nikaiona sura ya Maria ikiwa katika mavazi yale ya ajabu, matiti yake yalikuwa makubwa sana, mapaja yalikuwa wazi na matako yake yalizidi kipimo. Nikanyemelea kwa wasiwasi nikamfikia na kuita kwa wasiwasi.

Naam!! Ukageuka Maria, hakika ulikuwa wewe, ajabu hukushtuka badala yake ulishangaa. Rafiki zako wakakuuliza huyu ni nani, na ukasema tumesoma wote shule ya msingi hakuna la ziada.

Kila mmoja alinishangaa Maria! Ni wewe pekee uliyetakiwa kunifanya niwe na amani lakini hukudiriki kunitetea, nilizomewa sana. Na mara akafika mwanaume aliyevaa hereni katika sikio lake akakutwaa, mkaitana majina ya kimapenzi. Mkakokotana mkishikana viuno.

Maria nilistaajabu sana, niliumia sana na kujihisi sina thamani yoyote ile, ni kama ilikuwa ndoto lakini nd’o uhalisia uliokuwepo. Maria haukuwa wewe niliyekuzoea wakati ule, haukuwa wewe niliyekutwisha maji kisimani. Na wala haukuwa wewe niliyekuwa nakutembelea shuleni.

Siku hiyohiyo nilinunua simu na baadaye nikakupigia, uliisikia sauti yangu na kuitambua. Ukaniambia kuwa wewe ni mchumba wa mtu, na hukutaka maongezi zaidi ya hapo. Ukakata simu kisha ukanipigia tena, nilipopokea alikuwa ni mwanaume, akanikanya nisitishe mawasiliano nawe. Na mara akanitukania mama yangu!! Nikakusikia pembeni ukicheka.

Unakumbuka vyema kuwa nilikupigia baada ya siku mbili na hukupokea simu yangu!! Ukanitumie ujumbe kuwa nakusumbua, basi nilikuwa na shida ya kukueleza kuwa yule mama aliyelilia mjukuu tangu zamani hatimaye alikuwa amekufa bila kumuona mjuukuu wake.

Tazama nilivyokuwa mjinga mimi!!

Tazama nilivyokuwa hayawani!!

Nililazimika kumzika mama yangu huku nikiona haya kuyaaga maiti yake, ni kama alijua siku moja niajuta kuwa na wewe, hakika nimejuta. Yaani miaka yote ya kusubiri mwisho umenisaliti na kuniaibisha mjini???

Nimeamua kukuandikia kwa sababu utasoma na usiposoma wewe atasoma Maria mwingine, muongo, mnafiki na msaliti kama wewe.

Ukiwa unamalizia kuisoma tambua kuwa niliathirika kisaikolojia, nikajikuta namuona kila msichana kama Maria, walipojipendekeza kwangu nilifanya nao mapenzi na kisha kuwatupilia mbali, nikidhani nkuwa nakukomoa huko ulipo kwa kuwakomoa hawa.

Nilifanya kwa fujo huku sura yako ikigoma kufutika katika kichwa changu.

Na hadi kufikia hatua hii napenda kukuambia neno moja ambalo linaniumiza sana…

Sijawahi kukusamehe, na bila wewe kunitenda vile huenda ningeweza kuishi miaka mingi zaidi, lakini mimi ni wa kufa tu!!

Maria kwa maovu yote uliyonifanyia, na kwa kisasi kibovu na cha kipuuzi nilichojaribu kulipa.

Nasikitika kuwa kusema neno hili na liishi nawe daima.

“MARIA bila wewe nisingeukwaa UKIMWI…..nimeukwaa kwa sababu yako!!! Na ulaaniwe kwa adhabu hii uliyonipa mimi na kizazi changu!!!”

MWISHO
 
NILIKUWA NA MPENZI

SIMULIZI FUPI - NILIKUWA NA MPENZI

Mwanzoni sikumpenda kutoka moyoni, nilimpenda kwa kuwa tu alikuwa mrembo haswa..kwa kifupi nilimtamani tu….yaani nilitegemea akinivulia nguo zake tukashiriki tendo hamu yangu itaisha na nitaachana naye. Ndio ningeachana naye kwa sababu sikuona umuhimu wa kudumu na msichana ambaye sijui hata kama nitamuoa. Nilipomwambia tutaoana hakika nilidanganya Alinipenda sana, kadri siku zilivyokwenda alizidisha upendo wake kwangu. Hakuna nilichohitaji kwake akaninyima, aliwahi kumdanganya baba yake kuwa anaumwa akatumiwa pesa ilimradi anipatie mimi nilipomwambia kuwa kuna mtu ananidai na abananisumbua kwelikweli. Alisikitika kusikia vile, akaahidi kunipigania. Haikuwa kweli nilichomwambia juu ya kudaiwa, pesa ile aliyonipa niliitumia kulipia chumba nikafanya uzinzi na Fatuma. Alihadithiwa habari hiyo na marafiki walioniona nikiingia kule, akalia kwa uchungu mbele yangu, lakini neno lake la mwisho likabaki kuwa ‘NAKUPENDA SANA…..WEWE NI MWANAUME WA MAISHA YANGU’……..

Nilijisikia vibaya lakini nafsi nyingine ikanikumbusha kuwa nilikuwa katika mahusiano na msichana yule kwa sababu moja tu…NGONO… na katu hakutaka kushiriki ngono na mimi. Alinikwepa sana hadi nikajisikia vibaya. Nikahisi huenda ana mtu mwingine. Hakika nilidhani kuwa anajihusisha na mtu mwingine ambaye hushiriki naye tendo hilo la ngono ambalo kwangu mimi kilikuwa kitu pekee ambacho kingeweza kuniaminisha kuwa ananipenda kweli. Msichana mrembo kama huyo kamwe asingeweza kuishi bila kufanya mapenzi. Hakika haikuniingia akilini. Wangapi wenye mali zao wanamtongoza, yeye ni nani hadi asiingie majaribuni?? Hapana ni uongo mtupu ananiongopea mimi. Nikaendelea na vimbwanga vya hapa na pale.

Hakuchoka kunibembeleza, hakuchoka kunipenda na hakuchoka kunikumbusha kuwa ni mimi pekee nilikuwa katika moyo wake wa nyama. “Nikipotea jumla nd’o utajua kuwa nilikuwa nakupenda..” aliwahi kunambia neno hilo. Japo lilinigusa lakini sikulitilia maanani. Hatimaye tukamaliza shule, nikategemea kuwa ule muda wa kumfaidi msichana yule kingono ulikuwa umewadia. Lakini haikuwa hivyo, akaendelea kuwa mgumu huku akijitetea kwa sababu zisizokuwa na kichwa wala miguu. Mwanzoni nilidhani kuwa aliogopa kufanya mapenzi kabla hajamaliza shule, lakini ajabu hadi tulipomaliza bado alisimamia msimamo. Sasa nikajikuta katika pepo mbaya, nikaanza kumwonyesha hadharani kuwa nina wanawake wengine. Japo chozi lake liliniumiza sana lakini sikujali. Kwa nini ananinyima penzi binti huyu? Nilijiuliza. Hatimaye nikafikia uamuzi wa kuachana naye.

Lakini siwezi kuachana naye bila kumjua ladha yake. Nilijiapia kuwa jambo hilo haliwezekani hata kidogo, mimi kama mwanaume kamili atanitangazaje kwa marafiki zake, kuwa sijawahi kulala naye tukafanya tendo??? Aibu kubwa!!! Nikampangia shambulizi moja la mwisho na kama ni ubaya uwe ubaya tu. Ilimradi nilishapanga kuachana naye….haitanidhuru lakini lazima nifanye naye tendo Nilimuita nyumbani kwangu, ilikuwa mida ya jioni. Alipofika nilimlaghai hapa na pale nikamgusa matiti yake madogo yaliyosimama wima yakijitahidi kunidhihaki. Na yalifanikiwa hasa hasa kunikebehi. Nikamgusa huku na kule..nilipotaka kumvua nguo akanizuia. Nilikuwa nimekunywa pombe kiasi hivyo sikuwa na aibu, nikaamua kutumia nguvu, niliamua KUMBAKA…..nikaichana sidiria yake, kisha nikaiondoa chupi yake sasa akabaki yu uchi wa mnyama. Alihaha huku na kule asiamini kile kinachotokea mbele yake. Nikamrukia ili niweze kutimiza lengo… Kamwe sikuwahi kumwona binti huyu akiwa katika uoga namna ile…alikuwa amekodoa macho yake….na alikuwa anatetemeka… Akataka kukimbia uchi, nikamdaka mkono nikamvutia pale nilipokuwa.

Sikuwa nahuruma hata kidogo, nilichotaka ni itu kimoja tu..NGONO KISHA AKINICHUKIA NA ACHUKIE. Mara akatokwa na kelele kubwa sana zilizonishtua sana. Amakweli sikuzitegemea. Sikudhani kama amnaweza kufanya tendo lile “ANANIBAKAAAAA, NISAIDIEENI ANANIBAAAKA…..” ilikuwa kelele kubwa haswa, na alifanya kwa kurudia rudia Kelele zikawafikia wasamalia wema, binti akaendelea kupiga kelele. Hatimaye mlango ukavunjwa, wasamaria wakanivagaa na kuanza kunipiga……nilipigwa hadi nikapoteza fahamu. Nilipozinduka nilijikuta na pingu mkononi, pingu iliyounganishwa na kitanda. Nilikuwa na maumivu makali mwili mzima. Nikakumbuka kuwa nilifumaniwa nikitaka kufanya ubakaji.

Pombe zilikuwa zimenitoka na niliona aibu wa kitendo cha kinyama nilichotaka kumfanyia Maria. Baada ya kujitambua vyema na nguvu kunrejea mwilini nilirejeshwa mahabusu. Nikaingia mahabusu nikikabiliwa na kesi mbaya ya ubakaji. SIKU NNE baadaye nilikuja kutolewa……hapakuwa na dhamana lakini ilikuwa barua tu ya kustaajabisha niliyokutana nayo.

“Mpenzi Christopher mwanaume wa maisha yangu…..haikuwa nia yangu kukusababishia kipigo kikali na kuitwa mbakaji… nimefanya haya kwa sababu nakupenda kutoka moyoni…napenda uishi miaka mingi..Chriss ni wewe mwanaume pekee niliyetokea kuvutiwa naye kihisia ukauteka moyo wangu na kujikuta nikiwa mtumwa wa mahaba yako… lakini nina mapungufu makubwa…nina kasoro kubwa ambayo hainipi hadhi ya kulala kitanda kimoja na wewe…..Chriss mimi ningekuwa muuaji iwapo ningekuruhusu unibake….hivi chriss unadhani mpapaso wako haukunisisimua? Nilisisimka haswa na nilitamani nikutimizie kwa hiari kile ulichotaka, labda mimi nilikuwa muhitaji kuliko wewe mpenzi lakini…..lakini nisingeweza kukuua, ….

Chriss ninayo furaha na wala usisikitike kusikia hili, mimi nimefurahi sana kufa nikiupigania uhai wa mwanaume niliyempenda, ninayempenda na ninayekufa kwa ajili yake. Kitanzi hiki kiwe kumbukumbu yako milele kuwa NILIKUPENDA…….C hriss mimi ni muathirika wa gonjwa la UKIMWI niliambukizwa na wazazi wangu …nilizaliwa nikiwa na Ukimwi Chriss, mama kabla ya kufa alinikanya kuwa nisiwe na tabia kama ya marehemu baba ambaye alimuambukiza maksudi kutokana na taba yake ya kutotulia nyumbani, mama akanikanya kuwa ni heri nife peke yangu kuliko kuua yeyote asiyekuwa na hatia. Na huyo mtu ni wewe Chriss haukuwa na hatia na haukustahili kufa..…..laiti kama ungenibaka basi leo hii ningekufa nikiwa MUUAJI… ninafurahi kuwa nakufa kama SHUJAA. Nimeyaadika haya huku kitanzi kikiwa shingoni mwangu, nakufa leo lakini wakuache wewe huru. Huru kabisa, naenda kuungana na mama yangu nimweleze kuwa sikuwahi kuua duniani na nimeamua kuondoka ili siku moja nisije kuua yeyote. Ubaki salama Chris wangu”

Nilijikuta napoteza fahamu tena baada ya kuhakikishiwa kuwa Maria alizikwa baada ya kujinyonga katika chumba chake nyumbani kwao na barua ile ilikutwa chini ya miguu yake iliyokuwa unaning’inia……. nilipozinduka nilikuwa nyumbani kwetu…kila jicho lilinitazama kwa namna yake……wengine kwa hasira wengine dharau na baadhi kwa huzuni. AMA KWA HAKIKA nilikuwa na mpenzi aliyenipenda kwa dhati……. UPUMZIKE PEMA PEPONI Maria…..kamwe sitakusahau mpenzi…….

UJUMBE;

Usilipize baya kwa baya kwa kizazi kisichokuwa na hatia…..

JIFUNZE kupenda kwa dhati lakini HISIA ZAKO ZISIKUFANYE MTUMWA!!!!

SHARE KWA WENGINE

MWISHO!!!
 
USIKU USIO NA JINA

SIMULIZI FUPI - USIKU USIO NA JINA

NDEGE wa angani pekee nd’o walikuwa wakiendelea kulipa uhai anga lililotanda kwa giza nene huku nyota zikishindwa kufua dafu katika kuileta nuru. Anga lilipoanza kutoa miale mikali inayong’ara, ndege walivikumbuka viota vyao na makundi kwa makundi walitoweka anga ikabaki katika hali ya upweke, miale mikali pekee nd’o uhai mdogo uliosalia.

Miale hiyo haikuishia kuleta uhai katka anga pekee, bali ulimurika pia katika chumba kimoja ambacho kilikuwa kimekaliwa na mwanamke. Alikuwa amevaa nguo za kulalia, macho yake yakiwa makavu. Taa ilikuwa imezimwa hivyo ule mwanga ukaibua undugu kati ya macho na sasa.

Ilikuwa yapata saa tisa usiku. Yule bwana aliyemuoa kwa mbwembwe zote na mapenzi miaka miwili iliyopita alikuwa hajarejea nyumbani bado.

Ni kweli alikuwa ameanza tabia za kuchelewa nyumbani lakini siku hii alipitiliza.

Mwanamke akakunja uso wake kwa uchungu mkuu, akajiziba na viganja vya mikono yake. Akatambua kuwa amebanwa na donge la hasira kooni na hawezi kulihimili mpaka atoe kilio. Hapo akaamua kutimua mbio kuelekea chumbani kwake. Akafika akaduwa chumbani kwake huku akitiririkwa na machozi. Akaliendea kabati la nguo ili aweze kuchukua kitambaa atumie kukabiliana na machozi yale.

Mara paah! Kikaanguka kitu kikilia mfano wa sarafu, akainama kutazama ni kitu gani. Hofu ikazidi kutanda.

Ilikuwa pete ya ndoa, pete ambayo kwa mikono yake alimvisha mume wake wakati wanaamuriwa kuwa mume na mke. Pete hiyo imetolewa kidoleni sasa na kufichwa kabatini. Hapa uvumilivu ukamshinda akakimbilia kitandani, akajirusha na kuanza kugalagala huku akilia kilio cha uchungu mkubwa, lakini alijitahidi sana kuizuia sauti ile isipenye na kukifikia chumba kilichokuwa kinafuata, kwani hakutaka huyo mtu katika chumba kile aweze kutambua kuwa alikuwa katika kulia.

Kilio hiki kilikuwa na mengi ndani yake, alijiuliza iwapo huo nd’o ulikuwa uhitimisho wa safari ya ndoa yake, alijiuliza kama hiyo ni talaka alikuwa ameandaliwa kwa vitendo. Kama sio kwanini aitupe pete yangu humu, kwanini anachelewa kurejea nyumbani? Alijiuliza bila kupata majibu.

Mawazo tele aliyokuwanayo yalimfanya asisikie mchakato wowote wa mtu kutembea katika korido kisha kukifikia chumba na kugonga mlango. Mlango ulipogongwa kwa mara ya pili ndipo akili zikamkaa sawa. Akajifuta machozi kwa kutumia shuka, kisha akaenda kufungua bila kuuliza aliyekuwa mlangoni ni nani.

Alitambua tu kuwa lazima atakuwa mumewe na hakika ilikuwa hivyo, mwanamke huyu alimtazama mumewe kidoleni akidhani atakutana na pete na kujitoa mawazo kuwa huenda aliifananisha tu ile iliyodondoka.

Kapa!! Hakuona kitu.

“We Felista…..” mumewe aliita huku harufu ya pombe ikitambaa mle chumbani.

Mungu wangu ameniita jina langu!!

Mwanamke yule alitahamaki, haikuwa kawaida hata kidogo kwa mume wake kumuita kwa jina hilo na badala yake alizoea kumuita mpenzi, mahabuba na majina mengineyo yanayotangaza huba.

Leo hii anamuita Felista!!! Tena we Felista!!

Kama mbwa vile!!!! Mshikemshike.

Felista hakuitika lakini yule mwanaume mlangoni hakujali akapiga hatua moja mbele, hakika alikuwa amelewa na alitaka kukosa muhimili, kama lisingekuwa kabati basi angepiga mweleka na kusalimiana na ile marumaru pale chumbani.

Akiwa ameegemea kabati mwanaume yule ambaye ni kwa mara ya kwanza alirudi nyumbani akiwa amelewa alianza kubwabwaja maneno machafu sana kwa mkewe, maneno ambayo hata Malaya na hawara pia akiambiwa yanaweza kumkera, lakini maneno haya aliambiwa mwanamke wa ndoa iliyobarikiwa kabisa.

Maneno yakazidi mwanamke naye akazidi kukasirika, mwanzoni alipuuzia lakini ikamtoka yule mwanaume kauli mbaya sana ambayo ilibadili usiku ule na kuwa usiku wa kukumbukwa.

Usiku wa sintofahamu na huenda usiku mrefu kupita yote katika maisha yao.

Usiku usio na jina!!!

*****

URAFIKI wao ulianzia ufukweni mwa bahari, Felista na rafiki zake waliokuwa wanasoma shule moja walipokuwa wakicheza na mchanga wa bahari, mara warushiane mchanga mara wamwagiane maji. Mchezo ukiwa umewanogea mara Felista akamponda mwenzake na kiatu chake chepesi, bahati mbaya kusudio lake likashindikana baada ya kiatu kile kukwepwa na mlengwa kisha kikamfikia mwanaume mmoja aliyekuwa ufukweni pia.

Bila kufikiria mara mbili mwanaume yule ambaye labda kwa sababu zake binafsi alikuwa akingoja litokee jambo ili aweze kuwakabili wasichana wale ambao mmoja wao tayari alikuwa amemjibu vibaya alipojaribu kumweleza juu ya mapenzi. Mbio mbio mwanaume yule akaenda kumkabili Felista ambaye alikuwa ameduwaa akiwa amejiziba midomo yake kwa mshangao mkubwa.

Mwanaume yule akamfikia Felista na kuanza kumkaripia pasi na kumpa nafasi ya kuomba msamaha ama kujieleza vyovyote vile. Felista aliyekuwa anatetemeka alimuona mwanaume mwingine akijongea mahali pale.

“Frank, acha hasira kaka. Mtoto wa kike huyu halafu si unaona watu wanavyokushangaa…..jifanye hakijatokea kitu. Halafu na wewe binti waambie wenzako kama michezo mkafanyie mbali, si unaona hapa watu wamekaa sawa eeh!” sauti ilisihi. Yule kijana aliyekuwa anazidi kupandwa za jazba akapiga kite cha hasira kisha akakubaliana na yule rafiki aliyemsihi.

Felista na rafiki zake wakatafuta eneo jingine, si kwa minajiri ya kucheza tena la! Kila mmoja kuvaa nguo na kutoweka. Ufukwe ushakuwa gundu tena.

Wakati wanaondoka pale, Felista alimwona yule kijana aliyewasuluhisha baada ya yule kijana mjeruhiwa wa ajali ya kiatu kumkabili.

“Asante kaka.” Alimwambia baada ya kumkaribia.

Wakazungumza kidogo kisha wakati wanaagana kwa kushikana mikono akasikia kama kuna kitu anapewa mkononi, akaufunga mkono vyema kisha akaondoka na rafiki zake.

Alipoufungua mkono baada ya kufika mbali alikutana na kadi ya biashara ikiwa na namba za simu na eneo la ofisi zinapopatikana.

Bahati nzuri ofisi za huyu msuluhishi zilikuwa zinahusika na jambo ambalo Felista alikuwa akisomea katika masomo yake chuo kikuu cha Dodoma. Hivyo alimtafuta kwa lengo la kuulizia kama ataweza kupata nafasi ya kufanya mazoezi yake kwa vitendo katika ofisi hizo. Huo ukawa mwanzo wa mazoea yao, kisha urafiki na baada ya kumaliza chuo walikuwa wachumba.

“Nakupenda Gervas.”

“Nakupenda Felista”

Maneno haya waliambizana kwa mara ya kwanza mjini Dodoma. Yakadumu hadi walipofanikiwa kufunga ndoa.

Ndoa iliyobarikiwa na pande zote mbili bila kinyongo chochote kile. Kila mmoja akiwa amemuelezea mwenzake juu ya siri zake na historia za miaka ya nyuma bila kificho.

Maisha ya ndoa yakaanza rasmi!

Upande wa mawifi palikuwa shwari kabisa na hata mashemeji walimpenda Felista naye alijitahidi kuwapenda pia.

MIAKA miwili ikakatika upendo ukaanza kupooza, ulipooza kwa sababu Felista alikuwa hajaongeza zao lolote katika ukoo wa Gervas wala katika nyumba waliyokuwa wanaishi jijini Dar es salaam.

Gervas aliahidi kuwa atavumilia mpaka mwisho, neno hilo lilimpa faraja sana Felista, akajipa imani kuwa akipata upendo wa mumewe basi hawa wengine wanabaki kuwa wa ziada tu. Hakuumiza kichwa kuhusu wao.

Lakini alitilia maanani ule usemi usemao, ‘damu nzito kuliko maji!!’ na hapo akakumbuka kuwa mume wake si ndugu yake wa damu na hakuna damu yoyote ambayo inawaunganisha. Akajiwekea tahadhari hii kichwani.

HAKIKA baada ya mwaka mwingine, mume wake akaanza kubadilika, akawa anawasikiliza dada zake sana, kuna maneno fulani hivi ambayo japo Felista hakuwa anayafahamu lakini aliamini maneno hayo ndiyo chanzo cha kila kitu kuwa shaghalabaghala. Akajaribu kujiimarisha ili aweze kuwa kinara katika nyumba lakini haikuwezekana kabisa tayari wale wana’damu’ moja walikuwa kitu kimoja.

Alitamani kuikimbia nyumba lakini asingeweza kurudi nyumbani bila kupewa talaka, akatamani kuiomba talaka yake lakini kibaya zaidi mume wake hakuwa amewahi kumtamkia kuhusu talaka hata siku moja. Hili kwake likawa tatizo, akawa anaishi utumwa katika nyumba yake.

Ugeni wa mawifi ukawa haukatika nyumbani kwake, wakifika wanagawana jiko mawifi hawataki chakula cha mama mwenye nyumba. Wanajipikia wao wenyewe, salamu wanajibu kwa kujilazimisha tu na maisha yanaendelea.

Felista alipomuuliza mumewe akajibiwa kuwa ajitahidi kuwazoea mawifi zake. Hilo nd’o lilikuwa jibu pekee aliloweza kutoa mume, tena katika namna ya kupuuzia tu.

Mawifi wote waliopita walikuwa micharuko na wasumbufu lakini wifi aitwaye Sarah huyu alikuwa wa aina yake alionyesha ushirikiano wa hali ya juu kwa Felista, alimsaidia kazi za ndani na kuna wakati walipika wote jikoni. Alimpa moyo kuwa hiyo anayopitia ni mitihani tu kutoka kwa mwenyezi Mungu na ipo siku itapita na maisha yataendelea.

Wifi huyu wa ajabu, kila walipokuja mawifi wakorofi yeye alikuwa akijiondokea kabla hawajafika. Jambo hili lilimshangaza sana Felista lakini moyoni akaamini amepata shujaa wa kweli wa kumpigania, aliamini kuwa wifi yule anawachukia na kuilaani tabia wanayofanya wadogo zake. Hata ambapo wifi yule hakuwa ndani ya nyumba yake, alikuwa akimpigia simu usiku na wakati wowote ule kwa lengo la kumfariji, alimueleza kila kitu kilichokuwa kinatokea. Alijaribu kumsihi aongee na kaka yake ili aweze kuwa kama zamani, wifi Sarah akakubaliana na Felista na kumwahidi kuwa ataongea na kaka yake vizuriu kwa kina juu ya hilo.

Hakika siku iliyofuata Felista alipokea ujumbe kutoka kwa Wifi Sarah kuwa mambo yanaenda vizuri amemsema kaka yake kwa kirefu na bila shaka amemuelewa.

Juma lililofuata furaha kiasi ilirejea ndani ya nyumba. Felista akakiri kuwa wifi Sarah ni wifi wa kweli kabisa.

Muda ukazidi kusogea na tabia ikawa ileile, wakija mawifi wakorofi na mama mkwe basi Sara anajiondokea. Na maisha yakaendelea.

Baada ya miezi kadhaa wifi sarah alishika ujauzito. Hakumficha Felista alimueleza ukweli kabisa juu ya jambo hilo. Felista alimpongeza huku moyoni akiumia sana na kutamani ile mimba ingekuwa ya kwake, wifi Sarah akaanza kuwa mkorofi, uvivu ukamtawala na akawa mtu wa kulala tu kutwa nzima.

Mimba bwana!!!........ Felista alijisemea huku akitabasamu, aliamini kuwa ni mimba imemfanya kuwa vile wifi yake mkarimu kabisa. Hakutaka kumkera na kila lililokuwa likitokea kwake aliisingizia mimba ya wifi yake.

Mara usumbufu wa mimba ukaongezewa na usumbufu wa mumewe, akaanza tena kuwa mkorofi ndani ya nyumba. Zile tabia zake za zamani zisizotabirika zikaanza kujirudia. Mara akapitiliza zaidi na kuanza kulala sebuleni siku nyingine.

Mara akilala chumbani hataki kuguswa na mkewe, Felista alilia sana lakini nd’o lilikuwa tatizo tayari. Mshauri mkuu alikuwa ni wifi yake lakini huyu naye mimba ilikuwa imemfanya awe mtukutu na msumbufu. Hivyo mchezo ukawa hivi.

Kutwa ni usumbufu na vimbwanga vya wifi na usiku ni karaha za mume wa ndoa. Hapa sasa Felista alikonda barabara. Wazazi wake na ndugu zake wengi walikuwa mkoani Kagera hivyo hakuwa na pa kupumulia, akijaribu sana kuitafuta furaha basi ni siku ambayo alikuwa akienda kutengeneza nywele saluni. Huku aliweza kuburudisha akili yake kwa kusikia maneno ya wanawake wenzao wakipigana vijembe wao kwa wao.

Baada ya kurejea nyumbani zilikuwa karaha tupu.

Hadi miezi tisa ije kumaliziaka nitakuwa nimebakia kama sindano!! Felista alijisemea kwa masikitiko makuu.

Mzigo wa ndoa ulikuwa unamuelemea, afadhali basi angekuwa anafanya kazi mahali walau shilingi mbili tatu zingekuwa katika hifadhi yake lakini hakuwa kazini, mume alikuwa hajamruhusu kufanya kazi bado kwa kauli ya kwamba bado haijapatikana kazi ambayo inamfaa. Mume amesema mke angebisha nini?

Maisha magumu yakaendelea kuishi katika nyumba ya Felista.

MWANZONI Gervas alikuwa anafanya vimbwanga vyote lakini katu hawezi kulala nje ya nyumba yake bila taarifa. Lakini hili nalo likaibuka kutokea pasipofahamika.

Baada ya yule wifi mtukutu kutoweka pale nyumbani na kuonekana kuwa walau nyumba itakuwa na amani kidogo, jambo jingine likazuka. Gervas naye akaanza kuchelewa kurudi nyumbani.

“Afadhali Wifi angekuwepo maana alikuwa anamkaripia akichelewa kurudi….ona sasa” alilalamika mwenyewe huku akiitazama saa ya ukutani. Ilionyesha kuwa ule ulikuwa usiku wa saa nne. Akaendelea kungoja hadi akapitiwa na usingizi.

Siku hiyo alillalasebuleni na mumewe hakurejea kabisa.

Aliporejea siku iliyofuata Felista alijiandaa kumkabili na kupambana naye amweleze alilala wapi. Bahati ikawa mbaya upande wake, mumewe hakumjibu kitu. Alivua nguo zake alizokuja nazo akajitupa kitandani na kusinzia hoi!!

Kizungumkuti hakika!!

Ina maana hatambui tena umuhimu wangu!! Ina maana hakumbuki kama aliwahi kusema atanipenda milele….alijiuliza Felista biula kuupata muafaka.

Mienendo mibovu ikaendelea kuchukua hatamu, ikafikia kipindi Felista akaiomba talaka yake.

Neno hili likamshtua Gervas, hakuwahi kulitegemea. Wakati Felista alidhani kuwa itakuwa kazi rahisi lakini Gervas hakuwa tayari. Akaahidi kubadilika kabisa, akasingizia msongo wa mawazo unamsumbua.

Lakini wakati wote huu kuna jambo ambalo Felista alikuwa akiliona machoni mwa mumewe.

Aliuona uongo waziwazi…uongo usiopingika kuwa kuna kitu anaficha lakini hana mapenzi tena. Hakumpenda Felista.

Hakumpenda kwa sababu alikuwa tasa.

Felista akarudisha moyo nyuma akampokea tena Gervas.

*****

BAADA ya miezi kadhaa, Felista bila kujua kwanini amepata wazo hilo alijikuta tu akifunga safari ya kwenda hospitali kwa mara nyingine kuangalia tatizo lilikuwa nini hadi hapati mtoto. Hakumweleza mumewe kama ataenda hospitali siku hiyo.

Aliuacha funguo mahali ambapo wote wawili wanafahamu kuwa huwa wanahifadhi. Akaenda zake hospitali.

Akaongea kwa kirefu na daktari, akamweleza hata yasiyomuhusu juu ya namna anavyodharauliwa na fdamilia ya mume wake. Daktari akamchukua vipimo na kuingia maabara. Baada ya hapo akaketi na kumweleza kila kitu juu ya kizazi chake, majibu haya alikuwa akiambiwa kila siku iendayo kwa Mungu na madaktari tofauti tofauti. Lakini huyu kuna moja la ziada alimweleza Felista. Lilimtingisha kidogo Felista lakini alilipokea kwa tabasamu hafifu kana kwamba alilitambua hapo kabla.

Alizungumza sana na daktari. Kisha wakaagana.

Alipofika nyumbani alikuta nyumba ikiwa na uhai, kulikuwa kuna kilio cha mtoto mchanga. Akiwa anastaajabu alipokelewa na tabasamu kali la wifi Sarah. Felista akastaajabu, kumbe ilikuwa imepita miezi lukuki tangu waonane, sasa Sarah alikuwa na kichanga.

Hakuwa mkorofi tena. Hakuwa na tabia zake za kununa. Felista akakiri kuwa ni mimba tu iliyokuwa inamsumbua wifi yake mzuri.

Wakakumbatiana na kubusiana mashavuni. Ilikuwa furaha tena katika familia ile.

Felista alitaka kumshirikisha Sarah juu ya kilichojiri hospitali, lakini akaona ni mapema sana kumweleza mzazi huyu aliyejikita katika kukilea kichanga chake.

FELISTA akafikia maamuzi ya kumweleza mume wake na liwalo na liwe.

Hapa ndipo ukafika ule usiku usiosahaulika kamwe, usiku wa kizaazaa. Ule usiku ambao haukuwa na jina.

Ilikuwa saa tisa usiku ambapo mlango ulifunguliwa, mume wake aliyekuwa amelewa kwa mara ya kwanza akaingia ndani huku akiyumba yumba.

“We Felista wewe….mpuuzi mpuuzi malaya usiyekuwa na nidhamu….ni wewe uliyeniomba talaka yako sio….sasa nasema andika hiyo talaka tisa mkubwa wewe mimi nitaweka sahihi. Andika naachwa kwa sababu sizai, kwa sababu ya umalaya wangu andika upesi wewe changudoa mzoefu….” Alibwabwaja Gervas. Felista akapokea kama pigo kali maneno yale. Hakuamini kama yanatoka kwa mume wake. Akatamani kulia kwa nguvu lakini kifua kilikuwa kinambana.

“…Tena ikiwezekana uondoke usiku huu umwachie mwanamke anayeweza kuzaa nyumba yake hayawani wewe, mwenzako mbona amezaa upesi tu…wewe unanikalishia makalio humu ndani unamaliza sofa zangu kunguru usiyefugika wewe…rudi kwa mama yako mwambie umalaya wako umekuponza na sikutaki tena….hiyo pete yako vua nitamvalisha mwingine.”

AKILI hapa ikamchemka Felista, yaani ina maana wifi Sara amezaa na mume wangu? Alijiuliza.

Halafu ananiita mimi malaya wakati ameniambukiza UKIMWI huyu mwanaharamu!!! Alilaani Felista huku akikumbuka majibu aliyopewa na daktari hospitalini. Hapa sasa ujasiri ukamshinda akataka kuuliza lakini mume akaendelea kuropoka.

“Sara wewe ndiye mke wangu asante kwa bebi boi uliyeniletea…asante sana kwa zawadi hiyo…nakupenda Sara wee…mwaaaah!!” alizidi kubwabwaja kilevilevi.

Felista akalipata jibu kuwa kumbe kuna sintofahamu katikati. Akatazama kushoto akakutana na chupa ya soda. Alairukia kwa hasira akaitwaa na kuituliza katika kichwa cha mume wake, mlevi yule akalainika na kutua sakafuni.

Haikutosha akaendelea kumtwanga nayo hadi akahakikisha mikono imechoka. Kisha mbio mbio akakimbilia jikoni akatwaa kisu.

Akakimbilia chumbani kwa wifi Sara.

“Sara wewe ni nani katika nyumba hii.” Akamuuliza kwa ghadhabu, huku akiwa amekificha kisu chake kwa nyuma.

“Mama mwenye nyumba kwani vipi?” akajibu kwa dharau na hili likawa kosa kubwa sana, laiti angejua angejitetea kuliko kujibu jeuri.

Felista akamvamia na kuzamisha kisu chote mbavuni kwa ujasiri akakichomoa tena na kukizamisha katika chemba ya moyo.

Wifi feki Sarah kimya!!!

Akakitazama kile kitoto kilichokuwa kimesinzia akataka kukimalizia lakini huruma ikamwingia. Akatimua mbio chumbani kwake akakuta Gervas ametulia vile vile.

Akahaha bila kujua ni kipi anafanya pale chumbani. Akajigonga huku na kule kisha akafanikiwa kutuliza akili akachukua pesa katika mifuko ya mumewe, akaongezea na ya kwake kisha akatoweka.

ASUBUHI alikuwa safarini kuelekea Mwanza, akili ilikuwa haijatulia kabisa kutokana na kilichotokea.

Safari nzima aligubikwa na mkasa mzito sana ambao aliamini akimshirikisha mama yake anaweza kupata afueni. Mkasa wa kumfuga mke mwenza akidhani ni wifi yake...

Hakika alifika Mwanza, na kumsimulia mama yake kila kitu. Hakujua na wala hakusema kama alikusudiia kuua.

SIKU MBILI baadaye wakatangaza tukio la mauaji ya kutisha jijini Dar es salaam.

Mwanaume kwa kupondwa pondwa kichwani na chupa, mwanamke kwa kuchomwa kisu na mtoto mdogo kwa kukosa chakula.

Ni taarifa hii iliyoondoka na akili za Felista na kumfanya mwendawazimu milele…..taarifa ya kuhusika katika mauaji ya watu watatu

Mama yake mzazi pekee nd’o aliweza kusimulia mkasa ulivyokuwa kabka mwanaye hajawa na wazimu kichwani, wazimu wa kuvua nguo na kukimbiza watu hovyo. Hapakuwa na la kumshtaki kichaa huyu. Simulizi ya mama yake ikabakia kuwa simulizi inayogusa jamii, hasahasa wanandoa zenye utata na vijana ambao walikuwa hawajaingia katika ndoa bado.

Ikapita miezi kadhaa, yule kichaa Felista akabeba mimba mtaani, hakujulikana aliyembebesha mimba ile. Kilio kikazuka upya na watu wakaanza kujiuliza je? Tatizo alikuwa mumewe ama???

Nani angejibu iwapo mume ni marehemu na mke ni kichaa?? Yule aliyemjaza mimba pekee ndiye ajuaye na ule UKIMWI aliojiambukiza ndio utakaomuumbua...

Hongera sana mkuu kwa simulizi..
 
Back
Top Bottom