Burger mitaa ya Posta

Sahihi kabisa, kitambo sana
 
Mi ndo nlikua natengeneza hiyo mambo na ndo nilikua mtaalam wa kuchoma pizza enzi hizo E.A chef niko peke yangu nimesomea Auguste Escoffier school of culinary Texas USA
Acha fix wewe tushaambiwa mwenyewe kafa, au unatutaarifu toka kuzimu?
Watu mnataka kufanya hata utapeli wa burger?
Nyambaf
 
Katika maisha yote sijawai kula burger😁,
Yaani hata nikiagiza ntatoa mkate tupa kule nakula nyama tu na sallad na chips kiasi🙌
Hongera , maana zile buns ndio tatizo la kufaya mtu aoaongeeka uzito , sababu ni carbs . Kikweli napenda Burger sana, ila only za Burger King , zingine sio mpenzi ndio maana huwa sili, kitu ambacho kinanishinda ni Pizza , huwa sielewi watu wanaipendea nini, nimejaribu zote z Pizza Hut ,Dominos na zingine , sija whi penda hata siku moja.
 
Kwa wenzetu ni vyakula cheap

Kibongobongo wenye uwezo ndiyo
Wanakula

Ova
Yes Sawa tuu na hizi chips Kuku za kitaa, huwa hatuchukulii kama ndio mlo kamili ambao una hadhi , zote hizo ni fast food na haina maana tusile sababu ni cheap na ndio mpka twende The Hyatt and Sherraton ndio tufurahi, asilimia kubwa ya watu tuna penda Chips Kuku za Vitaa , na hizo ndio McDonads and KFC zetu original , sio salama ila ndio tunapenda sababu zina tupa burudani midomoni, sawa sawa na hizo Burger Joints za Ulaya tuu, hatuwezi acha sababu tuu ya kwamba kuna watu wanasema ni cheap na ni ushamba kula huko na ujanja ni kwenda kwa resourant to have a dinner and steak ,tunapenda hivyo hivyo cheap , ndio mana tulipo kuwa wanafunzi milo yetu sisi wengine ndio ilikuwa ni Double Whopper meal with some larger fries and large Strawberry shake , sababu ni quick na una shiba vizuri na kuharibu maumbo yetu kwa kujikuta tumenenepa ovyo na kipindi hicho tukirudi Bongo, kila mtu ana tusifia utasikia "Jamaa alikua States karudi kachana kinoma" kumbe tumejipa magonjwa yasio na sababu kwa unene ,s awa tuu na hizo chips vumbi tuuza kitaa maana hatujui zina kaangiwa kwa afuta ya Trnsformer au ni mafuta yalio tumika mwezi mzima yame kuwa reheated kila saa na kugeuka sumu.
 
Asante sana ,umenipa jibu nililo litafuta miaka mingi shukuran sana . Kikweli haja tutendea haki , alipaswa aachie watoto his recipee ili tujichane some good burgers huku tukimkumbuka ,Mungu amlaze Mahali pema peponi ,Amen
 
Kwa wenzetu ni vyakula cheap

Kibongobongo wenye uwezo ndiyo
Wanakula

Ova

Mungu ana mipango yake, matajiri wana fedha lakini hawali chakula wanachokipenda wanakatazwa na madaktari wao kwasababu ya maradhi ; masikini hawana hela hivyo hawawezi kula chakula wanachokitaka!!
 

What is the difference eating a burger at Kempisky or at street vendors? Tofauti yake ni ambiance basi, lakini contents ni sawa!
 
What is the difference eating a burger at Kempisky or at street vendors? Tofauti yake ni ambiance basi, lakini contents ni sawa!
Kma unavyo sema hakuna tofauti zaidi ya price tuu
 
I agree..well said. Utotoni nilipenda sana wali..ukipewa ugali usiku unaona unaonewa. Lakini siku hizi..wali naweza nipitishe wiki nisile na najiona so normal and so fine. Kadri siku zinavyoenda nakuwa interested na michemsho na vyakula vya mizizi kwa kiasi.
 
Hazikuwa "hamburgers" zilikuwa ni Beef Burgers.
 
What makes you think they were "Beef" and not "Ham burgers"? Watu wameanza kula kitimoto mjini siku nyingi!!
Napajua unapopasema na mwenyewe namjuwa.

To be exact hicho kibanda hakikuwa ilipo Bilicanas, kilikuwa nyuma ya kituo cha mafuta (kipo mpaka sasa, jina limenitoka) mkabla ilikuwa super market ya kwanza Tanzania kama sikosei ikiitwa Afrique, pembeni yake kulikuwa splendid hotel (sasa ni jengo la (extelecomms), usoni mwake kwa kushoto ilikuwa club ya usiku maarufu Margot.

Wakuja unataka kubishana na mwenyeji, mzaliwa wa Dar?

Thubutu enzi hizo Dar nguruwe auzwe kibandani, labda uende kigogo darajani huko.
 
Hazikuwa "hamburgers" zilikuwa ni Beef Burgers.
Labda ukiwa na maana ya kwamba in the middle ilikuw ni beeef , lakini zote ni Hambergers , yani una we ita Sandwich , burger or hamberger.
 
Miaka ya 80s kitimoto imeuzwa sana , nyumba nyingi Oysterbay walikuwa na mifugo tena Nguruwe walikuwa hawakosekani mabandni, nimeona nguruwe kw ara y kwana sio Kijijini ni Oyesterbay .
 
Miaka ya 80s kitimoto imeuzwa sana , nyumba nyingi Oysterbay walikuwa na mifugo tena Nguruwe walikuwa hawakosekani mabandni, nimeona nguruwe kw ara y kwana sio Kijijini ni Oyesterbay .
Mwenyewe ndio huyo walio msema ? Yes nakumbuka ilikua maeno kama kuna uwanja wa parking hivi sikumbuki vizuri , nilikua mtoto enzi hizo , unapelekwa na wazazi hapo na baada ya hapo unapelekwa Snow Cream , kuona kina Micky Mouse .
 
Siku hizi nadhani ndio ingekuwa vigumu zaidi kiti moto kuuzwa vibandani kuliko zamani, lakini hivyo sivyo mambo yalivyo mjini bandali salama . Mkuu wa meza anapatikana sana vibandani katikati ya jiji na sio Kigogo !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…