TANZIA Buriani Abbas Kleist Sykes

Kwameh,
Huwezi kuelewa hii historia mpya.

Wengi hamkujua kuwa kadi no. 1 ya TANU ya Julius Nyerere aliandikiwa na Ally Sykes na kadi no. 2 ni Ally Sykes no. 3 Abdulwahid Sykes na no. 7 Abbas Sykes na kadi hizo zilichapwa na Ally Sykes kutoka mfukoni kwake.

Mnajiuliza mbona watu kibao hatuyajui haya?
 
LGF,
Nadhani umekusudia, ''belatedly.''
Nakuitikia, ''Minalfaizin.''

Kitabu changu unakikosea jina kila siku unapokitaja.

 
Mara ulikuwa hotelini Dubai baadaye ulikuwa tanga, which is which

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Burdizzo,
Pole sana inaelekea mandishi yangu yanawakera watu wengi sana.

Historia ile yote ya 1950s Abbas Sykes anakutana na Nyerere nyumbani kwao, anakuja kujuana na Mama Maria, mipango ya kuunda TANU na mengi hukuyaona ulichoona ni kunikamata uongo nifedheheke kuwa mimi sisemi kweli.

BBC siku ile wananipigia simu nilikuwa Dubai na walitaka kujua sisi kama Watanzania tunachukuliaje maradhi ya Mwalimu.

Mwalimu anafariki mimi nipo Tanga.
Ungesoma bila ghadhabu ungeelewa lakini chuki imeziba fikra zako.

Unataabika kuisoma historia hii ambayo wewe hukupata kuijua na sasa unaijua huipendi.
 
Mkuu nina ujumbe wako upo PM
 
Kiranga,
Husemi kweli.

Umeghadhibishwa na ukweli uliopo katika taazia ya marehemu.

Nyerere nimemtaja kwa mnasaba wake halisi katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika akiwa na Sykes brothers wote watatu.

Nyerere hakupata kueleza haya na alipata kutoa kwa mpigo medali 3979 tarehe 27 April 1985 katika viwanja vya Ikulu wakati anaacha urais.

Wazalendo wote unaowasoma katika makala za historia ninazoandika hata mmoja hakuwamo katika orodha ile.

Leo unasoma yale alionieleza marehemu kuhusu mchango wa kaka zake Abdul na Ally kwa Nyerere binafsi kwa TAA na TANU.

Hujapendezewa sasa unajibaraguza ati nimemfanya Nyerere nguzo ya kila kitu.

Nashangaa hujajiuliza ikiwa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ni hii vipi Abdul Sykes na nduguze walifutwa katika historia ya TANU?

Hujapendezewa kusoma kuwa Nyerere alipata kuishi nyumbani kwa Abdul Sykes na mikakati yote ya kwenda UNO na kuwahamasisha wananchi ilikuwa ikifanyika nyumbani kwa Abdul.

Ukweli huu umekuchoma sana.

Unataabika kujua leo kuwa hawa ndugu watatu hawakumchukua Nyerere kama kiongozi mwenzao bali walimuunga kama ndugu yao.

Iweje katika utunuku wa medali karibu 4000 Nyerere hakuwakumbuka?

Hili jambo linahangaisha nafsi yako kwani unatambua maana halisi ya khiyana hii unaamua kutoa ghadhabu zako kwangu.

Unatamani kumchinja mshenga.

Najua mengi sana katika historia ya TANU.

Huyo hapo kulia ni marehemu Kleist Abdul Sykes.

Tumeishi pamoja maisha yetu toka tu wadogo hadi utu uzima.

Kleist ndiye aliyenieleza urafiki uliokuwapo kati ya baba yake na Earle Seaton Mwanasheria kutoka Bermuda aliyekuwa akiisaidia TAA katika mambo ya sheria na jinsi ya kuwazunguka Waingereza na kuwafikisha UNO.

Hii ilikuwa 1950.

Seaton ndiyo aliyemshauri Abdul Sykes TANU iundwe kwa kutumia katiba ya Convention Peoples Party (CPP) ya Kwame Nkrumah wa Ghana ili Waingereza wasipate sababu ya kuwakwamisha.

Kleist kanionyesha hadi "private dairies," za baba yake.

Abbas Sykes kushoto mengi mengi mengi sana kanisomesha kuhusu harakati za kupigania uhuru.

Kaka usifanye maskhara.
Historia ya TANU naijua.

Tuendelee kuzungumza.

 
Kwa makusudi ama kughafilika, umemdhalilisha Balozi Abbas Sykes kwamba hakuwa na maisha zaidi ya kuwa kivuli cha Nyerere.

Umeniambia sisemi ukweli, hebu twende kimahesabu. Namba hazidanganyi.

Bandiko lako la kwanza limemtaja "Nyerere" au "Mwalimu" mara takribani 43.

Bandiko hilo hilo limemtaja Balozi Abbas Sykes mara takribani 16.

Umemtaja Nyerere zaidi ya mara mbili ya ulivyomtaja Balozi Sykes, katika bandiko la kuenzi maisha ya Balozi Sykes.

Yani umefunika historia ya Balozi Sykes kwa kutupa sana habari za Nyerere, huku ukilalamika wazee wako wanafunikwa hawaandikwi historia yao.

Na wewe umerudia lile lile unalolipinga.

Kisha hujatueleza baada ya Nyerere kufariki Balozi Sykes alifanya kazi gani, imekuwa kama kafa na Nyerere kazikwa naye kama kijakazi wa Farao!

Hujitambui, unafanya kilekile unachokipinga kwa wengine.

Yani hata kama mimi napinga Nyerere kuhodhi ushujaa katika historia ya Tanzania, nikisoma bandiko lako la kwanza naona unaturudisha huko huko kwenye habari za kumfanya Nyerere ndiye subject kubwa hata kwenye tazia ya Balozi Sykes, kama Balozi Sykes hakuwa na maisha zaidi ya kuwa kivuli cha Nyerere.

You are a walking contradiction.
 
Kiranga,
Umechelewa sana.

Kitabu cha Abdul Sykes kipo leo matoleo manne katika miaka 23.

Nyerere ni sehemu ya historia ya wazee wangu.

Nimemweleza na kumfungamanishanao kama inavyostahili.

Historia sasa imekaa vizuri.

Historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika si ile ya mtu mmoja.

Najua mnaumia hili hamkulitegemea.

Hamkutegemea kama iko siku mtamsoma Mufti Sheikh Hassan bin Ameir katika historia ya TANU.
 

Na wewe hujapenda kutajwa Nyerere au hujapenda kuwa Nyerere aliishi nyumbani kwa Abdu Sykes?


Naona hata maana ya "contradiction" huifahamu, pata darsa kuhusu "contradiction" kutoka kwenye Bible...

2 Samuel 24:1​

“And again the anger of the LORD was kindled against Israel, and he moved David against them to say, Go, number Israel and Judah.”

1 Chronicles 21:1​




“And Satan stood up against Israel, and provoked David to number Israel.”



Kitabu hicho hicho, Muandishi huyo huyo "Mungu", baada ya kusoma hapo tuambie aliyetoa amri alikuwa "Mungu" au "shetani"


Kijana hiyo ndio "contradiction".

Kama darsa halijakuingia nikuongeze "Bible" ikufundishe maana ya "contradiction".
 
Ngoja tuongezee mifano mujarab kutoka kwenye Quran.


A contradiction occurs when one statement on a subject excludes the possibility of another. The first one here is a good example. In Surah 19:67, it states that man was created out of nothing. In 15:26, man is created from clay. Since clay is something, we have a contradiction since “nothing” excludes the possibility of “clay.”
 

kuna comment hapo juu naona umeiruka kuhusu Martin Kayamba na uhusiano wake katika kuanzisha African Association iliyoizaa TAA na baadae TANU

unaweza kutoa historia japo kiduchu kuhusu huyu mtu maana inaonekana historia ya mapambano ya kuleta uhuru unaijua kiundani zaidi
 
Safi sana.

Siioni contradiction hapo bali naona "ignorance" kwako kama kwa yule niliekuwa nampa darsa la "contradiction".


Wewe kabla ya kuumbwa ulikuwepo?

Be honest, boy.
 
Riziki zipo za aina mbili, kuna riziki ya halali na kuna riziki ya haramu.
 
Kiranga,
Hapa tutakesha.

Mimi nina faili zima la marehemu.

Mimi nina hazina ya mazungumzo na marehemu yanarudi nyuma takriban miaka 40.

Kama ulitegemea mimi niandike taazia ya kazaliwa mwaka gani kafa mwaka upi ana watoto na wajukuu wangapi haya kwa wengi hayana maana yeyoye.

Katika hayo ningetaka ningeeleza kuwa Abbas Sykes kasoma King's College Budo, Uganda na alikwenda Kampala kafuatana na baba yake.

Hapo Budo marehemu alisoma darasa moja na Kabaka Freddie Mutesa.

Ningekueleza pia Abbas Sykes akiwa kijana mdogo alichukua fedha kwa mama yake Bi. Mruguru bint Mussa akaenda dukani kununua Citroën mpya.

Ningeweza pia nikakuchomekea nikakufahamisha kuwa kaka yake Abdul yeye tayari alikuwa akiendesha Mercedes Ben 220 SE uhuru bado.

Nadhani umeelewa.

Mimi nataka nieleze yale muhimu yasiyofahamika yaliyokataliwa kupokelewa na Mwenyekiti wa jopo la Chuo Cha CCM Kivukoni walipokuwa wanaandika historia ya TANU mwaka wa 1981.

Hutaki habari za Nyerere zikaunganishwa na hawa wazee wangu.

Nashangaa sana imekuwaje ghafla unatokwa na jasho kuwa taazia ya marehemu haikuandikwa vyema na Mohamed Said.

Ati kalamu yangu inamdhalilisha Abbas Sykes.

Mimi Mohamed Said nimdhalilishe Bwana Abbas.

Hivi waliofunika historia ya TANU (si ya Abbas Sykes) huwajui?

Mbona hujasema lolote kuhusu kukosekana kwao mazikoni?

Hivi unajua kama hilo nimeliandika?
Give me a break.
 
Eyce,
Martin Kayamba hakuwa muasisi wa African Association.

Ukitaka habari zaidi za Kayamba msome Daisy Sykes Buruku, "Kleist Sykes The Townsman," katika "Modern Tanzanians," John Illife (Ed.) 1973.

Haya aliyoandika Daisy yeye kayatoa kwenye mswada ambao babu yake aliandika kabla hajafariki mwaka wa 1949.

Katika kitabu hicho utasoma ya Martin Kayamba ambayo yeye mwenyewe hakuyasema.

Katika kitabu hicho utasoma nini Daisy kapokea kuhusu Kayamba kutoka kwa babu yake kupitia kalamu ya Erika Fiah na gazeti lake Kwetu.
 
Ma shaa Allah, wakati huo Marehem Nyerere hata baiskeli hana. Ndio ukweli huo.
 
Abbas Sykes nilipokuwa naongea naye alikuwa anapenda sana kusema watu wa Bara hawatuamini Siri watu wa Pwani na ni vigumu Sana kutusaidia wakati tuna shida. Kwa hiyo lazima tuweke watu wetu katika nafasi za uongozi.
Kwa ajili hiyo nadhani yeye ndiye almost single_handedly amewaweka madarakani watu kama Omar Ali Juma au Mohammed Shein.
Najua hii ni kama kumgombanisha marhemu na watu, lakini hayo ndiyo mawazo yangu.
 
Vitu vya msingi nilivyoandika, kwa ushahidi wa namba, ambavyo hukavikanusha, ni kuwa.

1. Umemuandika Nyerere kuliko Abbas Sykes katika siku ya msiba wa Abbas Sykes. Umemuandika Nyerere takribani mara 43 na Abbas Sykes takribani mara 16.

2. Umeshindwa kueleza maisha ya Abbas Sykes baada ya kufariki kwa Nyerere yaliendeleaje na alifanya nini.

Umemshusha Abbas Sykes na kumfanya kuwa mtu ambaye hakuwa na maisha zaidi ya kuwa kivuli cha Nyerere.

Halafu hapo hapo unalalamika kwamba Nyerere anaandikwa sana kuliko mashujaa wengine walioanzisha mapambano ya kudai uhuru.

Wewe mwenyewe, kwa kujua au kutojua, ni kati ya watu wamaomuandika sana huyo Nyerere kuliko hao mashujaa wengine waliopigania uhuru.

Umeji contradict.
 
Karanga,
Hivi mimi nikukanushe wewe kwa lipi.

Mimi nalalamika.
Nilalamike ili iwe nini?

Unajua kulalamika hadi uwe mlalamishi.

Mimi ni mwandishi si mlalamishi.

Wewe ndiye mlalamishi unataka niandike historia ya wazee wangu utakavyo wewe.

Ulosema katika yote na hakika umenisuuza ni hilo kuwa namwandika sana Nyerere.

Si kuwa namwandika tu hata kumzungumza namzungumza sana.

Nitafute You Tube.

Nimemweleza Nyerere toka siku ya kwanza mwaka 1952 kaletwa nyumbani kwa Abdul Sykes na Joseph Kasella Bantu hadi 1999 anafariki.

Nimemweleza Nyerere kuanzia 1955 wakati anaimbiwa nyimbo za lelemama na shangazi zangu akina Bi. Hawa bint Maftaha katika mikutano ya mwanzo ya TANU Mnazi Mmoja hadi hadi miaka ya mwisho ya maisha yake; jina lake likitajwa...

Subhanallah...

Nimemzungumza Nyerere na Abdul Sykes Zentrum Moderner Orient, Berlin...

Nimemzungumza Abdul Sykes na Nyerere Northwestern University Evanston, Chicago...

Nimemwandikia Nyerere taazia alipokufa...

Ingia hapo chini:
mohamedsaidsalum.blogspot.com.

Fanya "name search," utajua kuwa ushahidi wako wa namba hauna maana yeyote kwani umeelemewa na huo utaokutananao.

Unadhani mie niko hapa kufanya mzaha na wewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…