Buriani Abuu Semhando a.k.a Baba Diana

Buriani Abuu Semhando a.k.a Baba Diana

Jamani ningekua na mamlaka hizi boda boda ningezipiga marufuku!kila siku iendayo kuna watanzaniia si chini ya watatu wanafariki kwa ajali za pikipiki!kila mkoa kuna wodi special ya majeruhi wa pikipiki
 
Jamani mwisho wa mwaka huu...tulieni majumbani.poleni twangapepeta.r.i.p baba d
Sio watu wote ni akina mama wa nyumbani, au akina baba wa nyumbani. Wewe endelea kutulia nyumbani, ila usiku usiwe mgumu kumlipa fadhila!
 
Jamani mwisho wa mwaka huu...tulieni majumbani.poleni twangapepeta.r.i.p baba d
baba diana ni mwanamuziki, sisi ni wafanyakazi... kutulia nyumbani ni sawa na kusema tuache kazi

hebu edit basi ujumbe wako usiwe negative
 
Breaking News - Abuu Semhando Afariki Dunia
Mwanamuziki nyota wa bendi ya Twanga Pepeta, Abuu Semhando aka Baba Diana amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kutokana na ajali ya pikipiki.
Abuu Semhando mwanamuziki nyota wa bendi ya African Stars Twanga Pepeta hatunaye tena baada ya kugongwa na gari wakati akiendesha pikipiki kwenye majira ya saa kumi usiku.

Umauti ulimkuta Semhando wakati akijerea nyumbani kwake akitokea kazini ambapo bendi ya Twanga Pepeta ilikuwa ikifanya shoo eneo la Africana Mbezi Beach.

Mmoja wa wanenguaji wa Twanga Pepeta, Queen Suzi akiongea na Nifahamishe.Com alisema kuwa alikuwa akitaniana na Semhando wakati akipiga tumba lakini hakuwa mchangamfu muda wote.

Msiba upo Mwananyamala nyumbani kwake.
 
May his soul Rest in Peace

Poleni familia ya ASET
 
Habari zaidi zinasema kuwa marehemu aligongwa na gari aina ya Mercides Benz wakati akitoka kwenye onesho la muziki lililofanyika Aficana, maeneo ya Mbezi jijini Dar es salaam. Mara baada ya kugongwa na gari hilo, ambalo lilisimama, marehemu angeweza kupona, lakini alikanywagwa na magari mengine yaliyokuwa yakitokea Mwenge.


...INNA LILLAAH WA INNA ILAYHI RAJUUN,

R.I.P "mkaanga chipsi" wa Twanga Pepeta, Mwenyezi Mungu akusamehe uloyatanguliza, akupe malazi mema ewe Baba Diana,
R.I.P Abuu Semhando!
 
Msiba wa Abou unaumiza sana



1. Leo ni siku aliyokuwa amuoze binti yake wa kwanza
2. Alikuwa ameuandikia uongozi wa Bendi kuwa umpe likizo ya mwezi kwani alitaka asiweko katika jukwaa kwa kipindi. Ni mara ya kwanza yeye kuandika barua ya kuomba
3. Alikuwa mpiga drum wa Remmy Ongala enzi za Super Matimila na mtindo wao wa Talakaka. 1981
4. Katika simu yake ringtone aliyoiweka ni ya wimbo wa Njohole Jazz Band- bendi hii wanamuziki wake karibu wote walikufa pamoja katika ajali mbaya ya gari.


source wanamuziki wa TZ blog.

RIP Baba Diana.
 


...INNA LILLAAH WA INNA ILAYHI RAJUUN,

R.I.P "mkaanga chipsi" wa Twanga Pepeta, Mwenyezi Mungu akusamehe uloyatanguliza, akupe malazi mema ewe Baba Diana,
R.I.P Abuu Semhando!
Hakika sote tu waja wa Mwenyezi Mungu na kwake turarejea. Aamin
 
Inna lillah wa inna ilaihi raji'oon.

May Allah have mercy on his soul
 
May your soul Rest In Peace, Abuu Semhando!
 
Buriani Abou...
ndugu zangu kila mmoja kwa imani yake na ajisogeze karibu na Mungu na kila mmoja awaombee waja waliotangulia mbele ya haki ili wakapate kupumzika kwa amani.

Kumbuka siku ya mwisho ikifika
Kutakuwa na mlio mmoja wa parapanda
Utawakusanya wateule woote
Walioteuliwa kutoka nchi ya Misri
Siku ya mwisho Mungu akitoa hukumu...maneno ya Dakta hayo enzi ya uhai wake
 
34245_1543415664235_1200297381_31541798_6218600_n.jpg

Marehemu Abou Semhando 'Baba Diana' enzi za uhai wake. Hapo ilikuwa katika show ya Old Skul viwanja vya Karimjee ambapo wakongwe wa muziki walikusanyika kutumbuiza

MSIBA MZITO TWANGA PEPETA! - Global Publishers


This world is not our home
 
Back
Top Bottom