Buriani Amina Chifupa!

Status
Not open for further replies.
[/ATTACH]


mungu akulaze mahala pema peponi dada yetu na mungu tunakuomba usitufitinishe baada yake.


pia wape subira na uvumilivu na moyo wa kuyakabili majaribu jamaa zake na hasa mwanawe na mumewe
 

Attachments

  • salayachifupa.jpg
    21.9 KB · Views: 188
  • mpakanjiawatoto.jpg
    6.5 KB · Views: 83
kuna taarifa kuwa baada ya kuua Epyana Malecela na kumfanya yule dada kuwa zezeta na leo hii Amina kututoka then kuna asilimia kubwa ya watu wanaoamini kuwa EMANUEL NCHIMBI ni hatari zaidi

Hii topic inaweza kutolewa au inaweza ikafanyiwa moderation humu lakini kwenye BLOG ya AMINA iko open kwa kila mtu kuijadili

http://aminachifupa.wordpress.com/
 
Saikosisi,
Sielewi unachozungumza kabisa!....Ngoma hutibiwa popote una maana gani? tiba gani unayozungumzia hapa... kama sii kuamini ili kuridhisha imani yako kuwa marehemu alikuwa na ngoma. Hivi jamani lini mtakuwa na subira kidogo kuliko utunzi wa ngonjera ktk maisha ya watu.

Wewe ulikuwa ukimjua marehemu ama unafanya kusimuliwa na watu?..maanake ndio zenu Wabongo mwanamke asiwe mzuri -kosa, lazima awe Malaya ama ana ngoma!

Ugonjwa Haujulikani!... Mpankanjia na baba ya Marehemu wamesema hivyo tena kwa watu wa karibu sana, leo hii magazeti ya udaku yameshaanza kuzua maradhi kama vile kweli..Tupeni jina la dakrari aliyesema marehemu alikuwa na ugonjwa wa kisukari!...
maanake wengine hapa tunao jamaa zetu wenye kisukari na haijawahi kutokea nama hiyo.
 
Kwa habari zaidi someni maandishi yaliyokuwa highlighted hapo chini!

MAELFU ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiongozwa na viongozi wa juu wa serikali jana waliuaga mwili wa Mbunge wa Viti Maalum wa CCM, marehemu Amina Chifupa nyumbani kwao Mikocheni.

Shughuli ya kuanga mwili wa marehemu iliyoongozwa na Rais Jakaya Kikwete, ilianza saa 7.00 mchana na kukamilika baadaye jioni, ilighubikwa na huzuni kubwa.

Watu wengi walishindwa kujizuia na kuangua kilio wakati wa kuaga huku wengine wakisema Tanzania imepoteza kijana shupavu ambaye hakuogopa kusema kile ambacho hakina maslahi kwa nchi.

Familia yake imesema marehemu alikuwa na magonjwa mengi ya ajabu yaliyoshindikana kupata tiba ya kitalaam.

Baba wa marehemu, mzee Hamis Chifupa, alisema magonjwa hayo yalimuanza tangu Mei 8 mwaka huu.

Kuhusu taarifa kuwa mwanawe alikufa kwa kisukari Mzee Chifupa alisema marehemu hakuwa na rekodi ya kuumwa ugonjwa huo.

Mume wa marehemu Mohammed Mpakanjia alisema alifanya mambo yote kama muislam na amesikitishwa huku akiwa haamini kama kweli Amina amekufa. Alisema kutengana kwao si chanzo cha kifo bali matakwa ya Mungu.

Watu wengi walijitokeza nyumbani kwa marehemu, akiwamo mwanasiasa mkongwe Mzee Rashid Kawawa, Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad, Meya wa jiji la Dar es Salaam, Ayub Kimbisa, na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Salum Londa.

Akitoa nasaha zake, Maalim Seif aliwataka vijana zaidi wajitokeze kupinga vita dhidi ya dawa za kulevya kama ilivyokuwa enzi za marehemu aliyekuwa mstari wa mbele kupiga vita biashara ya dawa za kulevya.
Alisema CUF walikuwa wakiunga juhudi zake siku zote na kwao wamempoteza mtu muhimu. Londa aliwataka vijana kuiga mfano wa marehemu na kufanya kazi kwa bidii katika nyanja tofauti ili wapate mafanikio.

Source:- http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=191

Pia ktk gazeti hilo hilo someni Kipande kinachosema - Watanzania wamlilia Chifupa, Bunge laahirisha kikao.
Mtaipata picha kamili wapi tumetoka na tunakwenda wapi!
 
Na Zitto Kabwe ( Mmh!!!)

AMINA, umetangulia kwa Mola. Umetutoka tukiwa bado tunakuhitaji. Taifa lako ambalo ulianza kulitumikia ukiwa kijana mdogo linakulilia. Nchi imezizima, hakuna anayeamini.

Safari hii ni yetu sote, wewe umeanza. Msalimie Bibi Titi. Unakumbuka nilikuwa nakwambia kupitia kwako namwona Bibi Titi?

Wengi wanadhani wanakujua. Umeondoka bila kuwaonyesha kuwa wanakujua ndivyo sivyo. Kila mtu anasema chake kutokana na ama amesikia nini au amekuona katika nini.

Unakumbuka ulipochaguliwa kuwa mbunge watu walisemaje? Eti hata Amina naye kawa mbunge? Utafanya nini bungeni. Haikukuchukua mwaka ukawaonyesha tofauti. Ukafanya yale ambayo wengi kwa kweli yalitushinda kufanya. Ukaanza vita kubwa na ngumu ambayo hujaimaliza mpaka unaingia kaburini leo. Hata hivyo si lazima umalize vita uliyoianza. Edward Mondlane wa Frelimo alituaga kabla hajaona mwisho wa vita aliyoanzisha ya kumng’oa Mreno Msumbiji. Kina Samora wakamaliza vita hiyo. Umeianza vita, tutaimaliza. Umetupa changamoto.

Swali lako la mwisho bungeni lilihusu wizi wa mitihani. Hukupata bahati kuliuliza. Uliuliziwa na jirani yako, Ruth Msafiri, wa Muleba Kaskazini. Najua kama ungekuwapo ni aina gani ya swali la nyongeza ambalo ungeuliza. Nilikuangaza kule unakokaa sikukuona. Lakini nilijua utarudi muda si mrefu. ???????????????????????????????

Amina ulikuwa mwepesi kujifunza na wala hukuona aibu kuomba msaada, tena bila kujali itikadi ya chama ya unayemwomba msaada. Mimi nilikutana nawe kwa mara ya kwanza pale tulipoitwa na Mheshimiwa Spika kuhesabu kura za kumthibitisha waziri mkuu. Tukapeana namba za simu na kupoteana tukiwa tunasalimiana pale tunapoonana tu. Sikutegemea hata siku moja kama utakuwa karibu yangu kiasi tulichofikia. ???????????????????????????????Niseme kweli, hata mimi nilikuwa najiuliza utafanya nini bungeni wewe, nikijisemea kuwa wewe ni kilaza tu.

Rafiki yangu, na pia rafiki yako kipenzi, Omar Ilyasambe, kwa sasa yupo masomoni nchini Marekani, alinitahadharisha nisiwe kama watu wengine wanaokutafsiri kwa ujumla. Akaniambia nikupe muda wa maongezi na msaada kwa yale ninayoyajua. Urafiki ukaanzia hapo. Urafiki wa kujifunza na kujadiliana mambo mengi ya nchi yetu.

Nakumbuka ulikuwa unanilaumu kwa kuwa mkali kwa serikali yako ya CCM na kwamba wakati mwingine nazidisha. Nilikwambia ndiyo kazi yangu katika upinzani. Ulinielewa. Tulijadiliana maswali yetu na maswali gani ya nyongeza kuuliza. Tulijadiliana kuhusu masomo yako na masomo gani ya kuchukua katika juhudi zako za kutafuta elimu.
???????
Tulibishana sana kuhusu ni wapi ukasome shahada yako ya kwanza. Wewe na Omar mkitaka uende kusoma nje, mimi nikitaka usome hapa hapa nchini ili pia ufanye kazi zako za ubunge. Niliwashinda na kweli ukaanza kusoma. Ukajitahidi kusoma kwa bidii sana. Walimu wako watakukosa.

Amina, ulikuwa na malengo makubwa sana katika maisha yako. Ulianza kujiandaa kuongoza umoja wa vijana wa chama chako katika matayarisho ya kupata mafunzo thabiti ya uongozi. Mapema kabisa ulianza kupambana na vikwazo, lakini hadi unaanza kuumwa, zote uliona ni changamoto tu za maisha ya kisiasa. Siku uliyoanza kuumwa ulikuwa uende Lindi kufanya kazi za vijana, lakini pia kujiandaa na changamoto za uchaguzi mwakani. Masikini umeondoka na ndoto yako. Inauma sana kukupoteza.

Wakati tunaokujua tukitafakari kuhusu kifo chako, hatuoni tumempoteza mbunge tu, tunaona tumepoteza mpiganaji mahiri. Mpiganaji wa mstari wa mbele katika vita ya kunusuru taifa kutokana na ubadhirifu wa mali za umma. Wakati mwingine tunaona tumepoteza kamanda mwema, mwenye uwezo wa kupata habari zote za adui na kushauri njia bora za kukabiliana na adui.

Amina, maisha yako yana tafsiri nyingi. Umepitia mambo mengi sana. Ulitaka kuandika kijitabu kuhusu maisha yako ili watu wakujue vizuri. Wakati tunajiandaa ?????????kukusanya vya kukusanya, ukawa mgonjwa. Umeondoka kabla hujakamilisha azima yako. Bado watu hawakujui. Tutakamilisha kazi yako ili vizazi vijavyo vijue kuwa kulikuwa na kijana kiongozi mahiri mwenye msimamo thabiti.

Amina niseme nini kukuelezea wakati tunakupumzisha pumziko la kudumu? Maneno hayaji, vidole vinatetemeka. Tutakukumbuka. Ucheshi wako na umahiri wako katika kuhakikisha unapata unachokitaka.

Usiku wa tarehe 6, Mei ulinipigia simu ????????kuniambia kuwa Mkwawa anakuita, na kwamba Mwalimu Nyerere ananipa salamu. Mimi naomba uwape salamu. Uwaambie nchi yao ipo inaendelea, na kwamba huna uhakika ndoto yao ya kujenga taifa imara itafikiwa karibuni. Waambie Mkwawa na Mwalimu kuwa siku hizi ili uwe kiongozi ni lazima upande mabegani mwa mwingine na kumwangusha na wala si uwezo wa mtu.

Amina, nakutuma kwa Bibi Titi, mwambie kuwa juhudi zake za kutaka mwanamke, tena mwanamke wa Kiswahili kuonekana ana uwezo wa kuwa kiongozi, bado zinaendelea, na wewe umeziacha zinaendelea. Umefanya kazi yako, umewaachia kijiti wengine wafanye pia.

Nenda Amina, nenda kapumzike. Umetuonyesha kuwa vijana tunaweza. Tumejifunza, hatutakuangusha.


My take

No comment
 
Habari zenu Ndugu WanaJamboForum,

Kwanza nianze kwa kusema Mungu ailaze roho ya Marehemu Amina Chifupa Mpakanjia Mahala Pema Peponi Amen!


Amina tutakukumbuka kama kijana mtanashati, jasiri, mwerevu, mchangamfu na mjenga hoja! CCM umetuachia pengo kubwa sana katika vijana wetu shupavu kama wewe, lakini kama isemavyo, 'Akitakacho Mungu hashindwi, kwani Dunia ni yake". Rest in Peace!

Okey! On the other side:-

Kwanza nauliza kwanini Serikali haikumpa ulinzi wakati Amina Chifupa alivyosema kwamba atafichua majina ya watu wenye kudeal na madawa ya kulevya na vinginevyo, wakamwacha aende bila ulinzi, na najua Serikali walijua kwamba anajua hao watu, wakamwacha aende hivi hivi bila ulinzi, na wanajua kitu chochote kinaweza kufanyika wakati huo?

Pili kama walijua ugonjwa wa marehemu, kwanini wasingempeleka kuu ya Taifa ya Muhimbili, wakaenda kumweka kwenye hospitali ya Jeshi, Jamani!! Hospitali ya Jeshi?????????!!!!????.. Na wanakuja na excuse ya Kisukari.... ivi kuna mtu anaweza kufa na kisukari.. embu nielimisheni kama nimekosea, lakini kuna watu wengi wanavisukari lakini hawawafi kwa kuoza mwili na mwili kuwa ganzi, kama sukari imepanda mpaka juu unapewa dawa, na ikiwa chini kuna description unapewa ili iwe wastani.. na ikipita viwango unakufa..

Hii ni sumu kabisa inaonekana... Mimi binafsi na wenzangu tunajaribu kufanya 'invetigation' katika hili swala, na kwa wengine wanaofanya investigation msisite kutueleza hapa kwenye forum and likewise!!

Kitu kinachonisononesha ni Mtoto wake Amina, anakua bila mama! Duh... Mungu awape nguvu famlia na Amina waweze kupita majonzi na uchungu wakati mgumu kama huu..

Pia naona wapinzani, viongozi , wasanii, na watu mbalimbali waliyokuja hapo kwenye nyumba ya marehemu kutoa salamu zao za pole kwa familia ya Chifupa.

Kuna habari hii nimesoma kutoka gazeti la 'Wapinzani wetu' kuhusu kifo cha Amina, Soma Chini Kwa Habari Zaidi!!

Simanzi: Kifo cha Amina Chifupa

Na Happiness Katabazi

KIFO cha Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Chifupa, kilichotokea juzi katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, jijini Dar es Salaam kimelitikisa taifa.

Habari ambazo gazeti hili limezikusanya kutoka sehemu mbalimbali nchini zinaonyesha kwamba msiba wa mwanasiasa huyo kijana umebadili kabisa mwenendo wa mambo kitaifa.

Uamuzi wa Spika wa Bunge, Samuel Sitta kutangaza kuahirishwa kwa Kikao cha Bunge la Bajeti kwa siku nzima jana kwa ajili ya kutoa fursa kwa wabunge kushiriki kumuomboleza mwanasiasa huyo, unatokana na namna tukio hilo lilivyogusa hisia za watu wengi.

Viongozi takriban wote wakuu kitaifa, akiwamo Rais Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu Edward Lowassa, viongozi wakuu wastaafu wa kitaifa, wanasiasa wa vyama mbalimbali vya siasa, wafanyabiashara na wananchi wengine kwa ujumla, kila mmoja kwa wakati wake alionekana akiwa ameguswa na tukio hili kubwa la kwanza la aina yake.

Jijini Dar es Salaam jana, hali ilikuwa ni ya majonzi makubwa na katika maeneo mbalimbali habari kuu iliyokuwa ikizungumzwa ilikuwa ni hiyo ya kifo cha mwanasiasa huyo ambaye tangu alipoingia bungeni Desemba mwaka juzi, alitokea kuwa mjengaji makini wa hoja.

Kikubwa kinachoonekana kuwaumiza vichwa watu wengi ni mazingira ya kifo chake, kila mmoja akiwa hataki kuamini iwapo kweli mwanasiasa huyo alikuwa amekumbwa na maradhi makubwa ambayo hatimaye yamechukua maisha yake.

“Nini hasa kimemuua Amina jamani, ni kisukari kweli? Ni kitu gani hasa?” ndilo swali kubwa ambalo limekuwa likiulizwa na watu wengi kutoka sehemu mbalimbali nchini.

Nyumbani kwa baba yake mzazi, Hamisi Gabriel Chifupa, hali ilikuwa ni tete kuanzia usiku ya kuamkia jana na kwa jana nzima maelfu ya watu waliokuwa katika hali ya simanzi na kwikwi za kuomboleza walifika katika eneo hilo kufarijiana.

Vilio vya hapa na pale, huzuni na mshtuko wa kutoamini kilichotokea uliendelea kutawala eneo hilo na hata maneno yaliyozungumzwa na baba mzazi wa Amina na aliyekuwa mumewe, Mohammed Mpakanjia, kwa nyakati tofauti jana, yalikuwa yakionyesha dhahiri hali ya kutoamini au kuelewa vyema ni kitu gani hasa kilikuwa kimemtokea.

“Amefariki…alianza kuugua tangu Mei 8, alikuwa na homa kali na baadaye ikajulikana alikuwa na kisukari ambacho sijui kilitokea wapi kwa kuwa sisi tulikuwa hatujui. Wataalamu wamejaribu sana kuokoa maisha yake lakini imeshindikana,” alisema mzee Chifupa.

Kwa upande wake, Mpakanjia jana alasiri akizungumza huku akibubujikwa machozi alikaririwa akisema; alikutwa akiwa na kisukari ambacho jitihada za madaktari kujaribu kushusha kiwango cha sukari yake waliyokuwa wakiielezea kuwa haikuwa ya kawaida kwa mtu aliye hai zilishindikana.

Vilio na simanzi viliongezeka majira ya saa 7:57 mchana wakati mwili wa Amina ulipowasili nyumbani kwa wazazi wake, Mikocheni.

Ni hakika watu wengi walikuwa hawaamini kifo cha Amina lakini baada ya kuwasili kwa jeneza hilo baadhi ya wananchi walisikika wakisema wameamini kufariki kwa Amina baada ya kuona jeneza hilo.

Jeneza hilo baada ya kuingizwa ndani ya uzio wa nyumba hiyo, ulisomewa dua iliyoongozwa na Mufti wa Tanzania, Sheikh Shaban bin Simba kwa muda wa dakika tano, kisha likaingizwa sebuleni ambapo mwili huo unalala hapo hadi leo asubuhi kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Lupembe-Ihenjo, wilayani Njombe kwa mazishi.

Baba wa marehemu alisema uamuzi wa kumzika huko unatokana na uamuzi wa Amina mwenyewe ambaye alipata kueleza miaka mingi nyuma kwamba alitaka atakapokufa azikwe huko.

Mama yake Amina alisikika akilia huku akisema: “Alipata ujauzito nikampeleka Hospitali ya Mwananyamala akajifungua salama, hivi karibuni ameugua tukampeleka Hospitali ya Lugalo kumbe mwanangu ndiyo anakufa.”

“Binafsi yangu yanasema kifo cha Mbunge Chifupa, nakihusisha na masuala ya kishirikina kabisa na kama nitakuwa natenda dhambi Mungu anisamehe,” alisema muombolezaji mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, baba wa marehemu alisema hausishi kifo cha mwanae na imani za kishirikina wala mapambano yake dhidi ya dawa za kulevya, bali anaamini ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kuwataka vijana waendelee alipoishia.

Kwa upande wake, Mpakanjia alisema haamini kilichotokea, ila kikubwa kinachomsikitisha ni mwanawe ambaye bado anahitaji mapenzi ya mama yake na kuongeza kwamba amemwacha katika wakati mgumu.

Ilipotimia saa 10:34 jioni, ujumbe wa wabunge 32 waliomwakilisha Waziri Mkuu na wabunge wengine uliwasili nyumbani kwa mzee Chifupa ukiongozwa na Spika, Samuel Sitta.

Sitta, alisema Bunge lililazimika kuahirisha kikao chake kwa ajili ya kuomboleza kifo hicho.

Alisema ujumbe huo umekuja na ujumbe wa simanzi kutoka kwa wabunge wote na Waziri Mkuu na kusema kwamba, hakika Bunge limepata pigo kubwa kwa kumpoteza mbunge huyo.

Aidha, alisema Mbunge wa Singida Kusini, Mohamed Misanga, ndiye atakayeongoza wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo kwenye msafara wa mazishi kijijini Lupembe.

Akitoa salamu za pole kwa niaba ya serikali, Waziri wa Usalama wa Raia, Bakari Mwapachu, alisema serikali imepokea kwa mshituko mkubwa taarifa za kifo cha mbunge huyo aliyekuwa mstari wa mbele kupambana na mambo mbalimbali hususan yaliyowahusu vijana.

“Njia pekee ya kumuenzi marehemu ni kutekeleza kwa vitendo yale yote aliyoyapigania..tulimpenda lakini Mungu amempenda zaidi,” alisema Mwapachu ambaye alitoa ubani wa sh milioni moja kwa niaba ya serikali.

Aidha, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Dk. Emmanuel Nchimbi, alisema kwa niaba ya Baraza Kuu la umoja huo amesikitishwa na msiba huo na kumtaka Mpakanjia na mzee Chifupa, kukubali kwamba ni kazi ya Mungu ambayo haina makosa, hivyo wakubaliane na hali halisi.

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohammed, alisema kambi yake ilipata faraja kuona mbunge wa CCM kijana shujaa akiingia bungeni na kuiomba familia iwe na moyo wa uvumilivu.

“Kila kifo kina upya wake na uchungu wake. Nasema kifo hiki ni kipya kwa sisi wahusika wa taifa hili, kilichobaki sote pamoja tuige na kuendeleza yale yote mazuri aliyoyaacha,” alisema Hamad Rashid.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria msiba huo ni Waziri Mkuu mstaafu, Rashid Kawawa, Dk. Salim Ahmed Salim, John Cheyo, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, Mama Maria Nyerere na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali (Taarifa zaidi zimo ndani).
 
Ninaanza kwa kusema kuwa ninapingana na wote wanaosema kuwa tukae kimya na kuwa usifanyike uchunguzi wowote kuhusu kifo cha huyu mtanzania shupavu aliyesimama kidete kupigania maslahi ya walio wengi.
Ninaungana na wenzangu waliopendekeza kufanyike uchunguzi huru na tena wa kisayansi ili kumaliza mtimanyongo katika sakata hili.Tumeshapoteza watu wengi katika staili hii ya "ghafla bin vuuu!!" nitaanza kuwataja mmoja baada ya mwingine.

1). Edward Moringe Sokoine (former waziri mkuu jamhuri ya muungano TZ)
-Tuliambiwa na kulazimishwa kuwa alikufa peke yake(eti mtu mmoja tu)
katika ajali iliyohusisha msafara wa magari pale dakawa nje kidogo ya
mji wa Morogoro.Kama kawaida ya Watanzania tulikubali ili yaishe!

Hebu soma kidogo tu habari hii hapo chini uone jinsi huyu mtu
alivyoipenda nchi yake(patriot)

http://www.ippmedia.com/ipp/guardian/2007/04/12/88230.html

2) Horace Kolimba ( former Katibu mkuu CCM taifa)
-Naye masaa machache baada ya kuhojiwa na kamati maalum ya CCM
kule dodoma, alikolimbwa na watu wasiojulikana!!! na tukaambiwa kuwa ilikuwa shinikizo la
damu.
Kama kawaida ya watanzania tulikubali ili yaishe!

3) Major General Imran Kombe (former mkuu wa usalama Taifa)
Naye aliuwawa kwa kupigwa risasi na polisi nje kidogo ya mji wa moshi
pale maili sita na baadaye serikali ilisema kuwa eti polisi
"walimmchanganya" Major General Kombe na jambazi maarufu wa magari "ernest
white" hivyo ilikuwa bahati mbaya tu!.
Kama kawaida ya Watanzania tulikubali ili yaishe!

4) Stan Katabalo ( an investigative reporter of "Mfanyakazi" newspaper)
-Naye baada ya kuibua issue ya "Loliondo Gate" iliyohusu uuzaji wa
sehemu ya mbuga ya wanyama kule Arusha kwa mfanyabiashara wa
kiarabu katika mazingira ya rushwa naye alikatika ghafla bin vuuu.
Na kwa mara nyingine tena Watanzania tulikubali ili yaishe!

5) Ipyana Malechela ( former Mwenyekiti wa vijana-CCM,Dar)
-Baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa vijana -UVCCM Dar.
Alionyesha nia ya kugombea uenyekiti wa vijana -UVCCM kitaifa! Na hili
halikuwapendeza "mamluki" na siku chache tu baadaye alialikwa
kwenda Leaders' Club kwenye tamasha la michezo la kumpongeza kwa
kuchaguliwa kwake.Kifo kilimkuta masaa machache kabla ya tamasha hilo
ambalo alikuwa awe mgeni rasmi.
Hapa tuliambiwa kuwa kifo chake kilisababishwa na "natural causes"
Kama kawaida ya Watanzania tulikubali ili yaishe!

6) Amina Chifupa.
- Hapa tena hata la kusema ninashindwa! familia inasema kisukari;wengine wanasema "alisomewa albadir";wengine wanasema ni ngoma!..
Ila yote tisa kumi ni kwamba kifo chake kinatatanisha! na tunaheshimu tamko kutoka kwa familia yake, ila ieleweke kuwa yeye mwenyewe alishasema kuwa "maisha yake yapo hatarini" hasa baada ya kuanza kuibua hoja nzito na maarufu bungeni na sote tumeona nini alimaanisha kwa kauli yake hiyo!
Hivyo basi ndugu zangu watanzania tutaendelea kukubali yaishe mpaka lini?
Hii orodha ambayo nimeitaja hapa mnataka ifike wapi ndio mjue kuwa kuna haja ya kuchukua hatua katika mambo haya?
Hivi kweli kisukari,albadir,shinikizo la damu,ngoma,kipapai,wendawazimu,kurukwa na akili,natural causes,kizunguzungu, na malaria huwapata watu tu pale wanaposimama kidete kupambana na wala rushwa au kufichua maovu au kutetea wanyonge?
Kwa nini wananchi hatushinikizi kuwepo na uchunguzi huru na hasa wa kitaalam kutoka nje ya nchi pindi mambo kama haya yanapotokea?
Au ndiyo kusema kuwa tumeshazoea ule wimbo wetu wa " tukubali ili yaishe"!

Hii staili ya ghafla bin vuu lazima tuanze kupambana nayo!..
kamwe hatuwezi kuendelea kuangalia watu wakiangamia namna hii..!
na kwakweli watu kama akina Dr.Slaa(mbunge Chadema),Lucas Selelii(mbunge CCM-Nzega), na Anna Kilango waangalie sana hayo
magonjwa ya ajabu ajabu ambayo hutokea wanapoamua kuihoji serikali au kukemea maovu.
 
Uchunguzi ni muhimu.. Maswali ni mengi kuliko majibu... Watanzania hawahitaji maneno matupu... Hata kama hayo yote yanayosemwa ni kweli... Hata leo mtu akigongwa na gari, akipigwa risasi, ama akanywa sumu, kama alikua an augua malaria ama alikua na ngoma akipimwa ataambiwa alikua na ..... lakini sasa utaasema hajapigwa risasi? Kwani wangapi wanaugua na wapo? je, ugonjwa wake ulikuja baada ya kutaka kufanya PRESS CONF?

Naungana na Mwanakijiji, UCHUNGUZI TU
 
Halisi umepata PM yangu? Tupigie kelele.. wembemkali naomba ruhusa kutumia maneno yako hapo juu kuongezea katika wito wa kutaka uchunguzi ufanyike.
 
Duh!
Mmeona jinsi Lowassa alivyokwepa swali kule Mwananchi?...
 
watu wenye ngoma hufariki kwa TB,Malaria,Typhoid, etc etc. Kitaalamu hawezi kusema mtu amekufa kwa ngoma.

Kutokana na maneno-maneno, ingepaswa mwili wa marehemu Amina Chifupa ufanyiwe uchunguzi kuona kama kifo chake, au maradhi yaliyosababisha kifo chake, yalikuwa triggered na SUMU.

Hao wanaodai kwa utamaduni wa kitanzani mwili/maiti haipaswi kuchokonolewa wamepotoka. Imani na mawazo ya namna hiyo inaweza kuficha uhalifu/maovu ktk jamii. Haya mashaka kwamba huenda marehemu alipewa sumu hayapaswi kupuuzwa kwa kutumia mila zilizopitwa na wakati.
 
hivi walionesha mwili wake unavyoonekana? maana sumu ina dalili nyingi...... au ndo alizikwa bila watu kuuona mwili wake?
 
Jokakuu,
Unajua hawa walioleta dhana hiyo ndio wachawi wenyewe. Uislaam haukatazi kabisa mwili kufanyiwa uchunguzi..Na hata sheria ya kuzika maiti haraka imetokana na sababu muhimu ambazo zinahusiana na kuomboleza kwa muda mrefu hali kuna ibada nyingine muhimu hapa zinasimama. - Mathaln kutafuta riziki ktk maendeleo ya nchi ama jamii na wakati mwingine mnaweza kuwa vitani n.k. Maiti isiwe kizuio cha mambo mengine muhimu ktk maisha yenu ya kila siku - Ametoka kwa bwana na bwana kamchukua!...
Lakini pamoja na sababu zote hakuna inayohusiana na kuzuia kufanyika kwa uchunguzi wa kisayansi.

Sisi wenyewe ndio wachawi na katika kuziba uchawi tumezua aya ambayo inafunga kabisa nafasi ya kugundua sumu ama kukubali kwamba a crime was committed.
 
Mkandara,
unajua hii minongono ya watu kuuwawa kwa sumu siyo mizuri kwa mustakabali wa taifa letu. ndiyo maana mimi naunga mkono wanaopendekeza uchunguzi wa kina wa kisayansi ufanyike.

watu wanadai ati marehemu aachwe "apumzike." What about wale wanaotuhumiwa kwamba wamempa sumu marehemu? Hivi kama madai hayo siyo ya kweli tutakuwa tunawatendea haki kweli kwa kuachia hali iendelee kama ilivyo?

Hao wanaopinga uchunguzi wanaonyesha hali fulani ya uwoga-uwoga. Hilo nalo linachochea hizi tuhuma za foul play.
 
Jokakuu,
Nimezipata hanari kuwa jana pale kwa marehemu kila mtu alitaka kumjua EN ni nani?... yaani minong'ono yote ilikuwa kuhusu huyu jamaa!...

Haya kuna kundi ambalo linaamini kuwa mmewe marehemu alikuwa zungu na ndiye aliyempa Marehemu majina ya wahusika. Mkewe alipokwenda kutoa habari hizo nje ndipo ugonvi ulipoanza na inasemekana kuwa kamati ya Mafia ilifkia Uamuzi wa kumwondoa huyu binti na jamaa Mpakanjia alikuwa ktk deal!..
Hizi zote ni dhana ambazo zimesambaa mjini na hakuna hata mtu mmoja anaye amini kuwa marehemu kafa kwa maradhi ya kawaida.
 
hivi walionesha mwili wake unavyoonekana? maana sumu ina dalili nyingi...... au ndo alizikwa bila watu kuuona mwili wake?

ndio maana nikasema dini inaplay big part katika hili suala zima. yeye ni muislam na dini hairuhusu kuonyesha mwili hivyo mzee.
 
Kada Mpinzani,
usitake kuongeza maneno yako ktk vitu usivyovifahamu.
Dini haikatazi kuutazama mwili ila inakataza kuufanya mwili wa marehemu kama maonyesho!
Ndugu na jamaa waliweza kuona mwili, madaktari na hata wakoshaji maiti kwa hiyo ni swala la daktari na wahusika sio kila mtu kuumbua maiti!
sasa unafikiria watu wakisha ona maiti na kuona kuwa imebadilika ndio watafanya nini kama sio kwenda kuanzisha udaku!..
 

ok, Mzee Mkandara nimekupata.
Mbona kwa dini hapa mimi ndio mwenyewe, nadhani labda nimekosea kuandika au wewe umekosea kusoma. Nilichomaanisha kuonyeshwa mwili hadharani hiyo haiwezekani kama wanavyofanya wenzetu ( kitu ambacho sio kibaya ) na hivyo ndugu wa karibu sana pamoja na familia ndio huwa wenye uwezo wa kuuona mwili tu, ikiwa pamoja na kuoshwa, kama alikuwa na hereni wakati wa kifo basi atavuliwa na wanawake wenzake. hicho ndicho nilichokusudia kusema, lakini si vinginevyo ! nadhani mzee mwanakjj alidhani kama wanaoyesha mwili hadharani ili watu waweze kujua kama kulikuwa na dalili za sumu ( which is true and i totally agree ) na ndipo nikamjibu kwa kifupi kutegemea atapata ujumbe niliotarajia kuufikisha.
 
Sawa, lakini kweli wakionyesha mwili hadharani ndio hizo dalili ya sumu zinaweza onekana ama wataalam ndio wanatakiwa kuuona (kuuchunguza) mwili na kutoa taarifa hizo!..

Navyojua mimi maana ya kuonyesha mwili kwa wakristu ni kutoa rambirambi (respect) za mwisho sasa ikiwa watu wanakwenda pale na akili mbili sijui kama tutakuwa tunamtendea haki marehemu!.... Nimeyaona hayo ktk maiti za wale waliokufa Detroit... kuna watu walidai kwa nini maiti ya mwanamke haikuonyeshwa!

Come on guys wakuonyeshe wewe ili?....huu ni udaku tu hii tamaduni sii yetu sisi waswahili na naweza kusema watu wengi huwa hawaendi kutoa respect bali dukuduku la kujua maiti imeharibika kiasi gani, tofauti na wenzetu wazungu.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…