barabaraya18
Senior Member
- Sep 18, 2006
- 106
- 8
Mwanakijiji, tafadhali usiliendeleze jambo hili; kubaliana na ufafanuzi wake tusonge mbele.
Sababu za kupelekwa kuzikwa kijijni hapo kwa wajomba zake zilitokana na kurudia kwa kauli yake ya kuzikwa eneo hilo alipoanza kuumwa mwezi uliopita. Akizungumza na HabariLeo baada ya dua iliyofanywa na Sheikh Hussein Chifupa (kaka wa marehemu), babu wa Amina, Solomon Mkali-Moto Mbanga (88), alisema alipokea taarifa kwa mshituko lakini anakumbuka kwamba mjukuu wake alichagua mahali pa kuzikwa kutokana na upendo wake kwake.
Alisema alichagua kuzikwa mita 30 tu kutoka usawa wa nyumba yake (babu) katika Kitongoji cha Ihanjo ili watu wa nyumbani kwake watakapopita wawe wanamuona mara kwa mara.
"Mjukuu wangu alichagua sehemu ya kuzikwa na akasema nikizikwa hapa ndugu zake watakuwa wanamuona mara kwa mara na alirudia tena kuniambia sikumbuki mwezi, lakini kati ya mwezi wa nne na watano walikuja na mumewe hapa kunisalimia akanikumbusha sehemu ya yeye kuzikwa na akasisitiza sana, akisema anajisikia kuumwa na kama akifa nikumbuke sehemu aliyochagua kuzikwa," alisema babu huyo.
Usiku wa tarehe 6, Mei ulinipigia simu kuniambia kuwa Mkwawa anakuita, na kwamba Mwalimu Nyerere ananipa salamu. Mimi naomba uwape salamu. Uwaambie nchi yao ipo inaendelea, na kwamba huna uhakika ndoto yao ya kujenga taifa imara itafikiwa karibuni. Waambie Mkwawa na Mwalimu kuwa siku hizi ili uwe kiongozi ni lazima upande mabegani mwa mwingine na kumwangusha na wala si uwezo wa mtu.
Awali, akisoma dua mara baada ya mwili wa marehemu kuwasili kijijini hapo, Sheikh Chifupa alisema jamii inapaswa kufuta fikra za kujenga maswali kwamba ni kwa nini amekufa Amina, kwani kufanya hivyo ni kufuru mbele za Mwenyezi Mungu. "Ninaiomba jamii isizue balaa kufuatia kifo cha mdogo wangu Amina.
Mwenyezi Mungu ametwaa kiumbe wake nasi sote ni nafsi lazima siku moja tutaonja mauti kama ndugu yetu huyu. Tusihusishe kifo hiki na CCM wala na mtu yeyote, bali tumuombee apokelewe kwa heri," alisema.
Nimesoma article mbili zinazoniashiria mimi kudhani kuwa Amina alikuwa anaumwa muda mrefu na alikuwa anajuwa kuwa atakufa hivi karibuni. Article ya kwanza ni habari iliyoandikwa kwenye Habari Leo ya Ijumaa tarehe 29 June, 2007. Kwenye habari hii aya ya 7 hadi ya 9 inasema hivi
Maneno niliyoweka rangi yanaonyesha kuwa Amina alianza kuumwa muda mrefu yaani mwezi wa nne akingali na bado hajapewa talaka na mumewe ambayo ilitokea siku ya May 6, 2007. Na katika kuumwa huko inanyesha Amina alijuwa kuwa hatapona na ndiyo maana akamkumbushia babu yake kuhusu kiwanja cha kuzikwa.
Article ya pili ni eulogy ya Amina iliyoandikwa na Mheshimiwa Zitto kwenye gazeti la Tanzania Daima la tarehe 28 Juni .Paragraph ya tatu kutoka mwisho kwenye eulogy hiyo inasema hivi:
Siku hiyo ya tarehe 6, Mei ndiyo Amina alipopewa ile talaka yake. Sentensi niliyopigia rangi (kama ni kweli yalikuwa maneno yake) inaonyesha kuwa alikuwa anajua kuwa sasa uhai wake unafikia ukingoni.
kichuguu.
maneno ya Zitto usiyape nafasi alikuwa wapi kuyasema siku zote?
tutayaamini vipi? tumeshuhudia misiba mingi mara inapotokea wanakuja watu na kujifanya wanamjua sana marehemu na alikuwa mtu wao wa karibu.
huyo Zitto alisema jambo la Amina hatalizungumza anamuachia spika. sehemu nyingine akadai alikuwa na ushirikiano na Amina kwenye shughuli kazi tu yaani bunge.story ya leo kuwa yeye alikuwa mshauri wa elimu wa marehemu wakati yeye mwenyewe elimu yake ya kuungaunga mara kakimbia Zanzibar University mara kashauliwa na Kitila mkumbo asome, mara kafanyiwa dissertation na Bint Lwamo. nk
mara anajitia kuwa alipewa kazi na marehemu ya kuandika kitabu cha maisha ya marehemu, huo ni uongo mkubwa, marehemu angeandika kitabu baada ya kufikia malengo yake ambayo Zitto Historia haitamsahau kwa kuwa sehemu ya sababu ya kuzuia marehemu asifike malengo yake.watakuja hata wazazi wa waheshimiwa na kudai kuwa marehemu alikuwa mlezi wa NGO zao na aliacha usia kuwa sehemu ya mali yake iende kwenye NGO zao. tuwe makini na kauli za kujikomba. tuliziona sana kwenye msiba wa Mwalimu.
KICHUGUU.
Kuhusu marehemu kusema azikwe wapi hilo ni jambo common sana kwa waislam tena tunafundishwa kuwa muislam usilale bila kuandaa sanda yake, hilo ni funzo kubwa tunalofundishwa ili tusipate muda wa kusahau kuwa kuna kifo.
Nashukuru Mama Lao kwa ufafanuzi wako.
Wanaofanya hivyo mnawajua, mnaweza kuwakemea straight forward kwani kipindi cha kumrushia madongo/kumsimanga kilikuwa kile cha Kashfa ya Zitto vs Amina na walifanya kila waliloweza. Inasikitisha nyakati hizi za majonzi watu kuzigeuza nyakati za kufanya wafanyayo. Binafsi sipendezwi lakini nikiri kuwa si jukumu langu pekee kukemea watu wa aina hii. Aidha wale wanaofungua topic za Amina hivi au Amina vile wanakuwa wanakiuka utaratibu.
Hoja za kukandia ama vinginevyo thread mama ya Kashfa nzito Zitto vs Amina ipo kwa ajili ya kufanya vile na wale wenye kuomboleza nakuombeni changieni thru Just in: Amina Chifupa afariki
Vinginevyo Moderators wataonekana wabaya pale watakapoamua kufanya wanavyoona ni sawa. Ni suala la ubinadamu na kuzisoma nyakati.
Shukrani kwa wale walionielewa na pole kwa ambao kunielewa inaweza kuwa ni ngumu.
For JF Management
Invisible
Kwa hiyo wewe unaona ni sawa "kumsimanga"?Jamani tuwe na ubinadamu...Biinti wa watu alale salama. I am not happy na hivi vijembe. And waht are getting out of all this?????????????/....hizo threads ulizozitaja zinafaa na kutosha kuwasilisha simanzi au vijembe.
....zikifunguliwa nyingine itakuwa multiplication of threads,na hazita-serve the purpose inavyotakiwa.
....zaidi ya hivyo..ni mawazo tu...si unajua watu tumetofautiana!
Kwa hiyo wewe unaona ni sawa "kumsimanga"?Jamani tuwe na ubinadamu...Biinti wa watu alale salama. I am not happy na hivi vijembe. And waht are getting out of all this?????????????/
Admin thread zimechanganyika mno my request ni kupost zile
zinazomuenzi -kama yale mashairi, etc peke yake
Ikishindikana kabisa change heading ya Just in..to Buriani Amina.
Pls pls chonde chonde jamani. Tusiwaseme vibaya marehemu nawaomba sana sana.
Ni wewe huyo?