Nimesoma article mbili zinazoniashiria mimi kudhani kuwa Amina alikuwa anaumwa muda mrefu na alikuwa anajuwa kuwa atakufa hivi karibuni. Article ya kwanza ni habari iliyoandikwa kwenye
Habari Leo ya Ijumaa tarehe 29 June, 2007. Kwenye habari hii aya ya 7 hadi ya 9 inasema hivi
Maneno niliyoweka rangi yanaonyesha kuwa Amina alianza kuumwa muda mrefu yaani mwezi wa nne akingali na bado hajapewa talaka na mumewe ambayo ilitokea siku ya May 6, 2007. Na katika kuumwa huko inanyesha Amina alijuwa kuwa hatapona na ndiyo maana akamkumbushia babu yake kuhusu kiwanja cha kuzikwa.
Article ya pili ni eulogy ya Amina iliyoandikwa na Mheshimiwa Zitto kwenye gazeti la
Tanzania Daima la tarehe 28 Juni .Paragraph ya tatu kutoka mwisho kwenye eulogy hiyo inasema hivi:
Siku hiyo ya tarehe 6, Mei ndiyo Amina alipopewa ile talaka yake. Sentensi niliyopigia rangi (kama ni kweli yalikuwa maneno yake) inaonyesha kuwa alikuwa anajua kuwa sasa uhai wake unafikia ukingoni.
kichuguu.
maneno ya Zitto usiyape nafasi alikuwa wapi kuyasema siku zote?
tutayaamini vipi? tumeshuhudia misiba mingi mara inapotokea wanakuja watu na kujifanya wanamjua sana marehemu na alikuwa mtu wao wa karibu.
huyo Zitto alisema jambo la Amina hatalizungumza anamuachia spika. sehemu nyingine akadai alikuwa na ushirikiano na Amina kwenye shughuli kazi tu yaani bunge.story ya leo kuwa yeye alikuwa mshauri wa elimu wa marehemu wakati yeye mwenyewe elimu yake ya kuungaunga mara kakimbia Zanzibar University mara kashauliwa na Kitila mkumbo asome, mara kafanyiwa dissertation na Bint Lwamo. nk
mara anajitia kuwa alipewa kazi na marehemu ya kuandika kitabu cha maisha ya marehemu, huo ni uongo mkubwa, marehemu angeandika kitabu baada ya kufikia malengo yake ambayo Zitto Historia haitamsahau kwa kuwa sehemu ya sababu ya kuzuia marehemu asifike malengo yake.watakuja hata wazazi wa waheshimiwa na kudai kuwa marehemu alikuwa mlezi wa NGO zao na aliacha usia kuwa sehemu ya mali yake iende kwenye NGO zao. tuwe makini na kauli za kujikomba. tuliziona sana kwenye msiba wa Mwalimu.
KICHUGUU.
Kuhusu marehemu kusema azikwe wapi hilo ni jambo common sana kwa waislam tena tunafundishwa kuwa muislam usilale bila kuandaa sanda yake, hilo ni funzo kubwa tunalofundishwa ili tusipate muda wa kusahau kuwa kuna kifo.