Kufuatia kifo cha Mbunge Amina Chifu, maswali mengi yamejitokeza hapa Dar es Salaam pamoja na vitongoji chungumzima vya Tanzania yetu, kweli kuna wengi waliosema kuwa alipwa na shoku kubwa baada ya kuachwa na mumewe hali iliyosababishwa kupata presha.
mbunge huyo aliyekuwa kipenzi cha vijana wengi nchini na watu wa rika nyingine, alijijengea umaarufu mkubwa aliposimama bungeni na kueleza jinsi tatizo la dawa za kulevya linavyoiharibu jamii. Alisema yuko tayari kujitolea kuwasaidia polisi kuonyesha vilipo vijiwe vya wauza dawa za kulevya mkoani Dar es Salaam, katika jitihada zake za kupambana na tatizo hilo ambalo limekuwa likiota mizizi nchini.
Lakini wengi wao wanasema ni "mchezo mchafu" aliochezewa huyo binti mdogo ba baadhi ya vingunge ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hasa huyu Emmanuel Nchimbi.
Lakini all in all, watu wengi wanarudi tena kwa bw.Nchimbi kama ilivyokuwa wakati wa kifo cha Ipyana Malecela kwamba alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wakiwania cheo cha mwenyekiti a vijana, kijana wa mzee Malecela aliondoka kana kwamba pamba inavyotekea kwa sekunde na moto.
Kwa nini watu wanamuhusisha nchi na kifo cha Amina?
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa unasadikiwa kuwa Marehemu Amina tayari alishajijengea mizizi tosha ya kuhakikisha kua anakuwa mwenyekiti wa umoja wa Vijana ka kufanya kampeni nzito, hali ambayo ilimkatisha tamaa bw.Nchimbi ambae indaiwa tayari ameshakuwa na mtu wake mfukoni.
Ilidaiwa awali Marehemu Amina alikwenda kuomba ushauri wa kutaka kugombea nafasi hiyo kwa Nchimbi na huyu bwana alimueleza bayana kabisa marehemu kwamba bado hajapevuka kisiasa kushika nafasi hiyo nzito kwa Vijana wa CCM.
Hali ambayo Amina alipingana nayo na kumuhakikishia kwamba yeye amekomaa na kama bado badi atajivunza humo ndani atakaposhika nafasi hiyo, huku Nchimbi akimpiga mkwara kwamba tayari nafasi hiyo ina mwenyewe tangu maka 2005.
Marehemu Amina baada ya hapo alitoka katika mazungumzo hayo kwa nguvu mpya, kasi na hari kuhakikisha kuwa anafanya kampeni kabambe kabla ya muda kuhakikisha anachukua nafasi hiyo.
Iliyobaki huku nyuma ni Nchimbi na kundi lake kuhakikisha kwamba huyu binti wanammaliza kisiasa, ndiyo majungu yalipoanza kwa kuhusishwa kwake kutembea nje ya ndoa na mbunge kabwe zitto wa Chadema.
Baada ya saka hilo, Amina aliahidi kumwaga mchele hadharani pale katika ukumbi wa idara ya habari maelezo, kisa cha mumewe kumuacha na ilidaiwa kwamba alikuwa anataka kumtaja bwana Nchimbi, lakini kutokana na ushauri wa wazee wake aliamua kusitisha uamuzi wake, lakini alitumia simu yake ya mkono kumtumia bwana Nchimib ujumbe mfupi ulisomeka;
Ujumbe huo ulisomeka; Alichounganisha Mwenyezi Mungu binadamu hawezi kukitenganisha. Nakuheshimu sana kama kiongozi wangu, Mwenyekiti wangu, Naibu Waziri, M-NEC, M-CCM, mkubwa wangu kiumri, mbunge na kadhalika. Nimesikitishwa sana na jitihada za kutaka kuvuruga ndoa yangu, nakutakia kila la heri, lakini usisahau malipo ni hapa hapa duniani na kila mwenye kufanyia wenzake mabaya na yeye hulipwa kwa ubaya. Nampenda sana mume wangu na ntailinda ndoa yangu kwa gharama yoyote cko tayari kumpoteza, mi ni zaidi ya mwanamke. Asante sana, kila la heri na kazi njema katika kulifanikisha hilo, wizara yako nyeti sana, ina mambo mengi sana. Bye
Hakika hatujui Bw. Nchimbi alimjibu nini Amina, lakini baada ya hapo hatukumsikia tena Amina,massage hii ya Amina ni ushahidi tosha Nchimbi alikuwa hana mahusiano mazuri na huyu bwana Nchimbi.
Inadaiwa kuwa bana Nchimbi sasa hivi ni miongoni mwa watu wanaodaiwa kuogopwa kama ukoma na wabunge wenzake hata mawaziri kwa ukalumanzila,lakini hakuna mwenyewe ushahidi wa kutosha,Je Amina ametolewa kafara? wanasiasa wakubwa wa Marekani wanasema Politics is of the heart as well as of the mind,many people don't care how much you khow until they khow how much you care.
Tuangalia historia kidogo ya Amina aliyegombea ubunge baada ya kujipatia umaarufu kutokana na utangazaji katika Radio Clouds FM tangu alipokuwa mwanafunzi miaka ya mwisho ya 1990, alikuwa amedai kuwa Naibu Waziri huyo alikuwa na mipango ya kumchafua katika siasa kutokana na nia aliyoitangaza ya kutaka kugombea uenyekiti wa taifa wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).
Amina alikuwa pia ameomba ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), kupitia Kundi la Vijana katika Uchaguzi Mkuu wa CCM utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Katika Bunge la Bajeti linaloendelea sasa mjini Dodoma, Spika Samuel Sitta, alitangaza Jumanne wiki iliyopita kuwa mbunge huyo kijana ni mgonjwa, lakini hakueleza alikuwa akisumbuliwa na nini. Juni 22, mwaka huu, Amina aliuliza swali bungeni kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, akitaka kufahamishwa hatua gani zinazochukuliwa na serikali katika kudhibiti uvujaji wa mitihani.
Amina hakuwapo bungeni siku hiyo na swali lake ambalo ni la mwisho kwake katika Bunge hilo tukufu alilolitumikia kwa takriban mwaka mmoja na nusu, liliulizwa kwa niaba yake na Mbunge wa Muleba Kaskazini, Ruth Msafiri (CCM).
Anakumbukwa pia kwa tukio lililomsibu bungeni mwaka jana wakati alipoagizwa na Spika Sitta kutoka nje ya ukumbi kutokana na kuvaa suti ya kike na kofia ya pama bila glovu kama kanuni zinavyoagiza. Anakumbukwa pia kwa siku zake chache bungeni kwa kupenda kuvaa vilemba na nguo za mngaro.
Katika mahojiano yake na Radio Clouds FM katika kipindi cha Jahazi mapema Mei mwaka huu, Amina alisema anaamini anao uwezo wa kushika moja ya nafasi za juu za uongozi, ukiwamo urais.
Asilimia kubwa ya wanasiasa hupenda kupanda hadi kuwa rais. Mimi kwa sasa ni mdogo, sina uzoefu na sijakuwa kwenye siasa kwa muda mwingi, najifunza, lakini muda ukifika naweza, maana kila binadamu ana ndoto.
Mtu lazima ujiwekee malengo makubwa ili ufanikiwe. Kama utafikiria kujenga nyumba utajenga, kama ukifikiria kununua gari utanunua, hivyo hivyo kwa vitu vingine utakavyokuwa umejipangia
lazima watu waishi kwa malengo mbalimbali makubwa, alisema Amina katika mahojiano hayo na kuongeza kuwa hata kama hutayafanikisha angalau uliyafikiria.
Amina ambaye pia alikuwa anasoma katika Chuo Kikuu Huria (OUT), alisisitiza katika mahojiano hayo kwamba dunia ya sasa inahitaji wasomi zaidi. Dunia ya sasa inahitaji usome zaidi. Mfano bungeni ukigeuka hivi kuna profesa, ukigeuka hivi daktari, imenipa changamoto na mimi natamani siku moja niitwe kwa majina hayo, alisema.
Katika mahojiano hayo ya mwisho hadharani na umma, Amina alisema sasa hivi yeye ni mwanasiasa, hivyo lazima awe mstaarabu na ajiheshimu na kuongeza kuwa Amina wa miaka mitano iliyopita alikuwa amebadilika na watu hawakupaswa kutarajia kumuona akifanya mambo ya ajabu.
Ukiondoa masuala ya kijamii na kisiasa, Amina pia alikuwa mkereketwa wa michezo na mara ya mwisho alisafiri na timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars, kwenda Msumbiji, katika mechi ya awali ya Kombe la Mataifa ya Afrika mjini Maputo, Oktoba mwaka jana.