Buriani Amina Chifupa!

Status
Not open for further replies.
Twamuombea kheri na Mungu amwasilishe mahali pema.Ni pengo kubwa kwa vijana na wapiganao na madawa ya kulevya Tanzania.
Inna Lillahi Wainnaillayh Raajioun.
 
Inna llilah Wainna ilah Rajiun!! Sisi ni wa mola na kwake tutarejea
Amina Daima tutakukumbuka kama Shujaa....!!!!


Kwa mshtuko na majonzi makubwa naungana na familia ya marehemu na watz wote kwa ujumla ktk msiba huu mzito wa shujaa huyu kipenzi, mtetezi wa ukweli na haki Tz.

Naam Amina anaingia ktk 'list' ya mashujaa wengi waliokuwa na 'courage' ya kusema ukweli hadharani yale yanayoogopwa kusemwa na wengi.

Kwa cheche zile alizozianzisha za vita dhidi ya madawa ya kulevya amechukua nafasi ya kipekee ktk historia ya tz na Africa kwa ujumla kama Mtetezi,Shujaa na Jemedari wa kutetea ustawi na hali bora ya mamia ya vijana wa kitanzania ambao ni waathirika wa madawa haya haramu ya kulevya.

Daima tutakukumbuka Amina, na Mungu akulaze mahali pema peponi..Amin

CHANGAMOTO...

Kwa wale wote tuliompenda Amina kwa ile courage yake, hii ni changamoto kwetu kuendeleza yale yote mazuri aliyoyasema na kuyatekeleza kwa vitendo.

Kifo chake kisiwe ndio mwisho, au kufifia kwa kampeni za vita ile ngumu dhidi ya madawa ya kulevya na mabaya mengine ktk jamii zetu.
Tumuenzi shujaa huyu KIJANA kwa kuendeleza vita hivi 'waziwazi' na 'underground' baharini na nchi kavu mpaka 'ushindi' upatikane....Tuendelee kumkoma Nyani gilladi...

Tuwakumbuke marehemu wetu kwa kuyataja mazuri waliyoyafanya....'The Prophet s.a.w'

Ombi maalumu kwa viongozi wa kada mbalimbali , Amina aingizwe ktk vitabu vya kumbukumbu ya mashujaa wa nchi yetu.....
'Bwana ametoa...na Bwana ametwaa'. Milango ya mbinguni ikufungukie....

AMINA REST IN PEACE..............YOU WILL ALWAYS BE REMEMBERED
 
Pole Kwa Familia Yake Na Watanzania Wote Popote Duniani Walioguswa Na Msiba Huu,mwenyezi Mungu Ampatie Pumziko La Milele.
 
Mungu ailaze roho ya marehemu pahala pema. "Lisemwalo lipo kama halipo.........."
 

wewe wacha upumbavu wako maana yake nini kumkashifu maiti? mulikuwa munakwenda kufanya uzinzi pamoja? tena inaonyesha ni mwanamke mwenzako? yaani baada ya kumsitiri unatoa aibu za maiti? hakuna hata mtu mmoja aliyekuwa msafi tusidanganyane hapa, aso hili ana lile

Mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu - ameen
 
Kufuatia kifo cha Mbunge Amina Chifu, maswali mengi yamejitokeza hapa Dar es Salaam pamoja na vitongoji chungumzima vya Tanzania yetu, kweli kuna wengi waliosema kuwa alipwa na shoku kubwa baada ya kuachwa na mumewe hali iliyosababishwa kupata presha.

mbunge huyo aliyekuwa kipenzi cha vijana wengi nchini na watu wa rika nyingine, alijijengea umaarufu mkubwa aliposimama bungeni na kueleza jinsi tatizo la dawa za kulevya linavyoiharibu jamii. Alisema yuko tayari kujitolea kuwasaidia polisi kuonyesha vilipo ‘vijiwe’ vya wauza dawa za kulevya mkoani Dar es Salaam, katika jitihada zake za kupambana na tatizo hilo ambalo limekuwa likiota mizizi nchini.

Lakini wengi wao wanasema ni "mchezo mchafu" aliochezewa huyo binti mdogo ba baadhi ya vingunge ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hasa huyu Emmanuel Nchimbi.
Lakini all in all, watu wengi wanarudi tena kwa bw.Nchimbi kama ilivyokuwa wakati wa kifo cha Ipyana Malecela kwamba alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wakiwania cheo cha mwenyekiti a vijana, kijana wa mzee Malecela aliondoka kana kwamba pamba inavyotekea kwa sekunde na moto.
Kwa nini watu wanamuhusisha nchi na kifo cha Amina?
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa unasadikiwa kuwa Marehemu Amina tayari alishajijengea mizizi tosha ya kuhakikisha kua anakuwa mwenyekiti wa umoja wa Vijana ka kufanya kampeni nzito, hali ambayo ilimkatisha tamaa bw.Nchimbi ambae indaiwa tayari ameshakuwa na mtu wake mfukoni.
Ilidaiwa awali Marehemu Amina alikwenda kuomba ushauri wa kutaka kugombea nafasi hiyo kwa Nchimbi na huyu bwana alimueleza bayana kabisa marehemu kwamba bado hajapevuka kisiasa kushika nafasi hiyo nzito kwa Vijana wa CCM.
Hali ambayo Amina alipingana nayo na kumuhakikishia kwamba yeye amekomaa na kama bado badi atajivunza humo ndani atakaposhika nafasi hiyo, huku Nchimbi akimpiga mkwara kwamba tayari nafasi hiyo ina mwenyewe tangu maka 2005.
Marehemu Amina baada ya hapo alitoka katika mazungumzo hayo kwa nguvu mpya, kasi na hari kuhakikisha kuwa anafanya kampeni kabambe kabla ya muda kuhakikisha anachukua nafasi hiyo.
Iliyobaki huku nyuma ni Nchimbi na kundi lake kuhakikisha kwamba huyu binti wanammaliza kisiasa, ndiyo majungu yalipoanza kwa kuhusishwa kwake kutembea nje ya ndoa na mbunge kabwe zitto wa Chadema.
Baada ya saka hilo, Amina aliahidi kumwaga mchele hadharani pale katika ukumbi wa idara ya habari maelezo, kisa cha mumewe kumuacha na ilidaiwa kwamba alikuwa anataka kumtaja bwana Nchimbi, lakini kutokana na ushauri wa wazee wake aliamua kusitisha uamuzi wake, lakini alitumia simu yake ya mkono kumtumia bwana Nchimib ujumbe mfupi ulisomeka;
Ujumbe huo ulisomeka; “Alichounganisha Mwenyezi Mungu binadamu hawezi kukitenganisha. Nakuheshimu sana kama kiongozi wangu, Mwenyekiti wangu, Naibu Waziri, M-NEC, M-CCM, mkubwa wangu kiumri, mbunge na kadhalika. Nimesikitishwa sana na jitihada za kutaka kuvuruga ndoa yangu, nakutakia kila la heri, lakini usisahau malipo ni hapa hapa duniani na kila mwenye kufanyia wenzake mabaya na yeye hulipwa kwa ubaya. Nampenda sana mume wangu na ntailinda ndoa yangu kwa gharama yoyote cko tayari kumpoteza, mi ni zaidi ya mwanamke. Asante sana, kila la heri na kazi njema katika kulifanikisha hilo, wizara yako nyeti sana, ina mambo mengi sana. Bye

Hakika hatujui Bw. Nchimbi alimjibu nini Amina, lakini baada ya hapo hatukumsikia tena Amina,massage hii ya Amina ni ushahidi tosha Nchimbi alikuwa hana mahusiano mazuri na huyu bwana Nchimbi.

Inadaiwa kuwa bana Nchimbi sasa hivi ni miongoni mwa watu wanaodaiwa kuogopwa kama ukoma na wabunge wenzake hata mawaziri kwa ukalumanzila,lakini hakuna mwenyewe ushahidi wa kutosha,Je Amina ametolewa kafara? wanasiasa wakubwa wa Marekani wanasema Politics is of the heart as well as of the mind,many people don't care how much you khow until they khow how much you care.

Tuangalia historia kidogo ya Amina aliyegombea ubunge baada ya kujipatia umaarufu kutokana na utangazaji katika Radio Clouds FM tangu alipokuwa mwanafunzi miaka ya mwisho ya 1990, alikuwa amedai kuwa Naibu Waziri huyo alikuwa na mipango ya kumchafua katika siasa kutokana na nia aliyoitangaza ya kutaka kugombea uenyekiti wa taifa wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).
Amina alikuwa pia ameomba ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), kupitia Kundi la Vijana katika Uchaguzi Mkuu wa CCM utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Katika Bunge la Bajeti linaloendelea sasa mjini Dodoma, Spika Samuel Sitta, alitangaza Jumanne wiki iliyopita kuwa mbunge huyo kijana ni mgonjwa, lakini hakueleza alikuwa akisumbuliwa na nini. Juni 22, mwaka huu, Amina aliuliza swali bungeni kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, akitaka kufahamishwa hatua gani zinazochukuliwa na serikali katika kudhibiti uvujaji wa mitihani.

Amina hakuwapo bungeni siku hiyo na swali lake ambalo ni la mwisho kwake katika Bunge hilo tukufu alilolitumikia kwa takriban mwaka mmoja na nusu, liliulizwa kwa niaba yake na Mbunge wa Muleba Kaskazini, Ruth Msafiri (CCM).

Anakumbukwa pia kwa tukio lililomsibu bungeni mwaka jana wakati alipoagizwa na Spika Sitta kutoka nje ya ukumbi kutokana na kuvaa suti ya kike na kofia ya pama bila glovu kama kanuni zinavyoagiza. Anakumbukwa pia kwa siku zake chache bungeni kwa kupenda kuvaa vilemba na nguo za mng’aro.

Katika mahojiano yake na Radio Clouds FM katika kipindi cha Jahazi mapema Mei mwaka huu, Amina alisema anaamini anao uwezo wa kushika moja ya nafasi za juu za uongozi, ukiwamo urais.

“Asilimia kubwa ya wanasiasa hupenda kupanda hadi kuwa rais. Mimi kwa sasa ni mdogo, sina uzoefu na sijakuwa kwenye siasa kwa muda mwingi, najifunza, lakini muda ukifika naweza, maana kila binadamu ana ndoto.

“Mtu lazima ujiwekee malengo makubwa ili ufanikiwe. Kama utafikiria kujenga nyumba utajenga, kama ukifikiria kununua gari utanunua, hivyo hivyo kwa vitu vingine utakavyokuwa umejipangia… lazima watu waishi kwa malengo mbalimbali makubwa,” alisema Amina katika mahojiano hayo na kuongeza kuwa hata kama hutayafanikisha angalau uliyafikiria.

Amina ambaye pia alikuwa anasoma katika Chuo Kikuu Huria (OUT), alisisitiza katika mahojiano hayo kwamba dunia ya sasa inahitaji wasomi zaidi. “Dunia ya sasa inahitaji usome zaidi. Mfano bungeni ukigeuka hivi kuna profesa, ukigeuka hivi daktari, imenipa changamoto na mimi natamani siku moja niitwe kwa majina hayo,” alisema.

Katika mahojiano hayo ya mwisho hadharani na umma, Amina alisema sasa hivi yeye ni mwanasiasa, hivyo lazima awe mstaarabu na ajiheshimu na kuongeza kuwa Amina wa miaka mitano iliyopita alikuwa amebadilika na watu hawakupaswa kutarajia kumuona akifanya mambo ya ajabu.

Ukiondoa masuala ya kijamii na kisiasa, Amina pia alikuwa mkereketwa wa michezo na mara ya mwisho alisafiri na timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars, kwenda Msumbiji, katika mechi ya awali ya Kombe la Mataifa ya Afrika mjini Maputo, Oktoba mwaka jana.
 
AMINA

Amina ametutoka, kufa ametangulia,
Kama ua amefumba, baada ya kuchanua,
Tunamuombea mwanga, peponi ende ingia,
MSIMAMO ALOWEKA, HAKUNA WAKUCHANGUA
 
Jamani,Kama sio mapenzi ya mwenyezi Mungu.Ninamlaani kwa mabaya yote duniani na mbinguni kwa yeyote kwa njia moja ama nyingine anayehusika na kukatisha maisha ya dada yetu Amina Chifupa.
Amina amekuwa muwazi kwa yale yote aliyoyaona yanafaa na yasiyofaa katika nchi yetu. Nawalaumu sana jeshi letu la polisi kwa kushindwa kumlinda amina kwa sababu ya hatari zote zilizokuwa zikimkabili kwa kuuwawa kwa namna yoyote kama vile sumu na mengineyo kwa sababu kwa kuahahidi kuayataja majina ya wahusika wa madaw ya kulevya.
Anyway MWENYEZI MUNGU AMEWEKE MAHALI MEMA PEOPONI ,AMEEN.
 
NAMLILIA AMINA!

Niliapo naliani, nalia nanyong'onyeka,
Machozi tele usoni, kisimama naanguka,
Hili ni balaa gani, wanandugu kutufika,
Majonzi mengi moyoni, namlilia Chifupa.

Miaka ya ishirini, thelathini hakufika,
Ajulikana nchini, tadhani alizeeka,
Asomjuwa ni nani, ni wengi twahuzunika
Majonzi mengi moyoni, namlilia Chifupa.

Kalamu naweka chini, machozi yatiririka,
Sina nguvu nabaini, mwili wote umechoka,
Nilonayo ni moyoni, ni mengi nayakumbuka.
Majonzi mengi moyoni, namlilia Chifupa.

Mwenyezi Mungu akulaze mahali pema peponi, Amina. Amina!
 
BWANA AMETOA na BWANA AMETWAA...Ni msemo au lugha ambayo inatumika sana kujifariji pale binadamu anapotwaliwa uhai wake.

Je, ni kila binadamu anayefariki hufa kwa mapenzi ya Mungu? Laa hasha...!

Yatasemwa mengi kuhusiana na kifo cha Mrembo, Mpendwa, Kipenzi, Shujaa, Dada na yetu ...Amina Chifupa ... mimi siweki hilo jina ...Mpakanjia ....kutuplease tuliobaki hai..wenye pumzi ya uhai..Lakini KIFO CHAKE KILISHATABIRIWA NAYEYE MWENYEWE kuwa atauawa na NCHIMBI....! wala sio kwa miujiza bali kanusishwa SUMU..! Baba yake ilikiri kuwa CHAMA CHA MAPINDUZI kitalishughulikia swala hilo..na LIMESHUGHULIKIWA...!

MWENYENZI MUNGU AMREHEMU ...AMIN

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Jiji la Dar es Salaam, lilizizima kutokana na taarifa za kifo hicho, watu wakipashana habari kwa haraka hasa kwa kutumia simu za mkononi na ujumbe wa SMS. Wengi walitaarifiwa habari za kifo chake ndani ya nusu saa.

Amina licha ya kuwa na msimamo katika kupambana na dawa za kulevya, pia alikuwa mtetezi mkubwa wa wanawake, vijana, watoto na wanafunzi, kwenye michango yake mbalimbali bungeni. Kwa muda mfupi aliokaa bungeni tangu ale kiapo mjini Dodoma, Desemba 28, 2005, Amina amejipambanua na kuwa miongoni mwa wachangiaji mahiri bungeni, licha ya uchanga wake kisiasa.

Lakini pia alikuwa na mvuto miongoni mwa jamii, na ndiyo maana haikushangaza kuwa habari zake zilikuwa zikipewa umuhimu katika vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Hata hivyo, Mei 6, mwaka huu, vyombo vya habari vilimkariri Mpakanjia akithibitisha kutengana na mkewe huyo waliyeoana miaka sita iliyopita na kubahatika kupata mtoto mmoja wa kiume, Abdulrahman mwenye umri wa miaka mitano sasa.

Hakuna sababu zilizotolewa hadi leo kuhusu sababu za kuvunjika kwa ndoa kati ya mbunge huyo na mfanyabiashara huyo maarufu wa Dar es Salaam.

Hata hivyo, kuvunjika kwa ndoa hiyo kumehusishwa na madai ya kutembea nje ya ndoa. Lakini siku tatu baada ya taarifa hizo, baba yake Amina alikwenda Idara ya Habari (MAELEZO), na kueleza kuwa familia yake imeamua asizungumzie suala hilo kwa vyombo vya habari na kwamba CCM inao utaratibu wake wa kutatua masuala yake.

“Masuala yote yanapita katika mkondo wake. Sisi wazazi hatutaki kuharibu pensheni yetu, si mnajua kuwa siku hizi watoto ndio pensheni kwa hivyo tumeona kuwa chama kitashughulikia suala hilo,” alisema Mzee Chifupa, katika mkutano ambao ulikuwa uhutubiwe na Amina. Akiwa amefuatana na Mkurugenzi wa MAELEZO, Kassim Mpenda, alianza mazungumzo kwa kusema; “Nawaombeni radhi, lakini kwa mwitikio wenu wa kufika hapa kwa wingi, inatupa faraja sisi familia ya Chifupa…nimekuja hapa kusitisha mkutano ambao ulipangwa kufanywa na Amina…”

Aliwaeleza waandishi waliokuwa na shauku kwamba Amina amepewa talaka moja na siyo tatu kama ambavyo imeripotiwa. “Talaka moja haimwachi mke…hata kwenye bendi wameimba… gharama za kuishi kwa Amina anagharamia huyo mume wake. Lakini niwaambieni, Mpakanjia bado anampenda mke wake ndio maana ametoa talaka moja.” Wiki moja kabla ya kuthibitishwa kwa taarifa za Amina kutalikiwa, mbunge huyo anadaiwa alisambaza ujumbe wa maandishi katika simu za mkononi unaodaiwa kwenda kwa baadhi ya watu wanaoaminika kuwa karibu na Naibu Waziri mmoja aliyemtuhumu kusababisha kuvunjika kwa ndoa yake.

Ujumbe huo ulisomeka; “Alichounganisha Mwenyezi Mungu binadamu hawezi kukitenganisha. Nakuheshimu sana kama kiongozi wangu, Mwenyekiti wangu, Naibu Waziri, M-NEC, M-CCM, mkubwa wangu kiumri, mbunge na kadhalika. Nimesikitishwa sana na jitihada za kutaka kuvuruga ndoa yangu, nakutakia kila la heri, lakini usisahau malipo ni hapa hapa duniani na kila mwenye kufanyia wenzake mabaya na yeye hulipwa kwa ubaya. Nampenda sana mume wangu na ntailinda ndoa yangu kwa gharama yoyote cko tayari kumpoteza, mi ni zaidi ya mwanamke. Asante sana, kila la heri na kazi njema katika kulifanikisha hilo, wizara
yako nyeti sana, ina mambo mengi sana. Bye.”


Baadhi ya vyombo vya habari viliripoti habari za kuachika kwa Amina baada ya Naibu Waziri mmoja kudaiwa kwenda kumchongea kwa mumewe. Baada ya tukio hilo, Mbunge huyo aliahidi kumtaja Naibu Waziri huyo hadharani na sababu ya kufanya hivyo. Hata hivyo hali hiyo haikutokea.

Amina aliyegombea ubunge baada ya kujipatia umaarufu kutokana na utangazaji katika Radio Clouds FM tangu alipokuwa mwanafunzi miaka ya mwisho ya 1990, alikuwa amedai kuwa Naibu Waziri huyo alikuwa na mipango ya kumchafua katika siasa kutokana na nia aliyoitangaza ya kutaka kugombea uenyekiti wa taifa wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).
Amina alikuwa pia ameomba ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), kupitia Kundi la Vijana katika Uchaguzi Mkuu wa CCM utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
 
Wana JF kifo ni kifo jamani, tunachotakiwa sasa ni kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ili roho yake ipate pumziko la milele Amin.
Haya masuala kafa na nini na nini tusubiri uchunguzi wa maiti yake kama tutapata taarifa kama Taifa ingawa mara nyingi huwa ni suala la kifamilia zaidi kuamua kutoa hadharani taarifa ya kifo cha mwanafamilia husika.
Kuhusu Jane Mihanji yu hai ila nae aliwehuka kipindi alipokuwa anawania nafasi fulani ya uongozi katika chama hiki.
 
HAYO NAKO DODOMA WASHAJIPANGA NA KUNDI LA KUWAWAKILISHA KATIKA MAZISHI YA MBUNGE,SOMA HABARI KAMILI KUTOKA BUNGENI DODOMA

TAARIFA YA SPIKA

1. Leo shughuli za Bunge zitaahirishwa siku nzima hadi tarehe
28/06/2007.
2. Kutakuwa na ujumbe wa aina mbili kwa ajili ya uwakilishi wa
Bunge katika shughuli za msiba huu.

I. UJUMBE WA KWENDA DAR ES SALAAM

Ujumbe huu utaongozwa na Mhe. Spika ambao ni
pamoja na Wabunge wote wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Wabunge wote wa Mkoa wa Iringa, Uwakilishi kutoka
Zanzibar, Uwakilishi kutoka Kambi ya Upinzani,
Uwakilishi toka Serikalini, Uwakilishi toka Kamati ya
Maendeleo ya Jamii, Uwakilishi wa Party Caucus ya
CCM.

II. UJUMBE UTAKAOKWENDA KWENYE MAZISHI –
LUPEMBE NJOMBE

Ujumbe huu utaongozwa na Mhe. Mohamed Missanga
na orodha ya watakaowakilisha kwenye shughuli za
mazishi Njombe itatolewa Dar es Salaam.

3. Majina ya watakaoondoka saa 8:00 mchana huu ni hawa
wafuatao: -
1. Mhe. Samuel J. Sitta – Spika
2. Mhe. Dr. Batilda Burian
3. Mhe. Harith B. Mwapachu
4. Mhe. Sophia Simba
5. Mhe. Hawa Ghasia
6. Mhe. Joseph J. Mungai
7. Mhe. Prof. Peter Msolla
8. Mhe. Dr. Makongoro Mahanga
9. Mhe. Monica N. Mbega
10. Mhe. William V. Lukuvi
11. Mhe. Jenista Mhagama
12. Mhe. Anne K. Malecela
13. Mhe. Anna Lupembe
14. Mhe. Capt. John Komba
15. Mhe. Benito W. Malangalila
16. Mhe. Jackson M. Makwetta
17. Mhe. Lediana M. Mng’ong’o
18. Mhe. Dr. Binilith S. Mahenge
19. Mhe. Yono S. Kevela
20. Mhe. Stephen J. Galinoma
21. Mhe. Pindi H. Chana
22. Mhe. Hassan Rajab Khatib
23. Mhe. Hamad Rashid Mohammed
24. Mhe. Janeth Kahama
25. Mhe. Janeth Massaburi
26. Mhe. Rita Mlaki
27. Mhe. Idd Azzan
28. Mhe. Azzan Zungu
29. Mhe. Abbas Mtemvu
30. Mhe. Mwinchom Msomi
31. Mhe. Charles Keenja
32. Mhe. Halima J. Mdee
33. Mhe. Ania S. Chaurembo
34. Mhe. Fatma Maghimbi
35. Mhe. Salim Hemed
36. Bw. Damian Foka – Katibu wa Bunge

UJUMBE UTAKAOWAKILISHA BUNGE KWENYE MSIBA WA
MAREHEMU MHE. AMINA CHIFUPA MPAKANJIA
DAR ES SALAAM
__________________
1. Mhe. Samuel J. Sitta, Spika – Kiongozi wa Msafara
2. Mhe. Harith B. Mwapachu – Mwakilishi wa Serikali
3. Mhe. Hamad Rashid Mohammed
4. Bw. Abbas Kandoro – Mkuu wa Mkoa DSM
5. Mhe. Prof. Peter Msolla
6. Mhe. Dr. Maua Daftari
7. Mhe. Rita L. Mlaki
8. Mhe. Salome Joseph Mbatia
9. Mhe. Dr. Emmanuel Nchimbi
10. Mhe. Mwantumu Mahiza
11. Mhe. Jenista Mhagama
12. Mhe. Mohammed H. Missanga
13. Mhe. Anne K. Malecela
14. Mhe. Anna Lupembe
15. Mhe. Capt. John Komba
16. Mhe. Faida M. Bakar
17. Mhe. Jackson M. Makwetta
18. Mhe. Dr. Binilith S. Mahenge
19. Mhe. Lucy T. Mayenga
20. Mhe. Aziza S. Ally
21. Mhe. Martha Mlata
22. Mhe. Mohamed Rajab Soud
23. Mhe. Grace S. Kiwelu
24. Mhe. Janeth Massaburi
25. Mhe. Idd Azzan
26. Mhe. Abbas Mtemvu
27. Mhe. Mwinchom Msomi
28. Mhe. Mary Kasembe
29. Mhe. Susan A. Lyimo
30. Mhe. Halima J. Mdee
31. Mhe. Ania S. Chaurembo
32. Bw. Damian Foka – Katibu wa Bunge
33. Bw. Daniel Eliufoo – Katibu wa Spika
 


Duh..............
 
Hivi ni vipi Nchimbi amepata Umaarufu kwa kiasi hicho ndani ya CCM mpaka anakuwa Mungu Mtu?.Huyu jamaa kiumri ni mdogo mno hajafika hata 40,kielimu pia ni mtupu waulize waliosoma nae pale Forest Morogoro miaka ya mwisho wa 90,sasa inakuwaje anakuwa mtu wa kuvuruga watu kwa kiwango hicho?.Hakuna kupindwa habari kwa namna yoyote ile,Kifo cha Amina, Nchimbi anahusika kwa asilimia zisizopungua 90.
 
Sikuliona jina la Mh. Mwenyekiti wa vijana ktk orodha!.......vipi?
 
Sikuliona jina la Mh. Mwenyekiti wa vijana ktk orodha!.......vipi?

The guilty are always afraid....Hivi JK na Lowassa wako busy too busy to attend the mazishi?Where is Dr Shein?Where's Makamba?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…