Buriani Hassan Chikusa msomi mkimya

Dini itakusaidia nini katika maisha ikiwa unabagua watu
 
Hiyo Sheria ya kutokufungua mabucha ni Kwa Dar tu au Tanzania nzima? nauliza hivi kwasababu huku Arusha tuna kula kitimoto kuliko nyama yoyote na Kila mtaa ukienda utakuta mabucha Sasa inakuwaje Sheria iwe Kwa Dar peke yake
 
Walienda kuiba nyama tu
 
Hiyo Sheria ya kutokufungua mabucha ni Kwa Dar tu au Tanzania nzima? nauliza hivi kwasababu huku Arusha tuna kula kitimoto kuliko nyama yoyote na Kila mtaa ukienda utakuta mabucha Sasa inakuwaje Sheria iwe Kwa Dar peke yake
Mpuuze huyo mzee..illusion za udini zinamchanganya akili.

#MaendeleoHayanaChama
 
Huyu Mzee ni mdini sana na mwenye chuki na ukiristu
#25
--------------------------------------------------------------------
Edward A Chapa said:

Wewe ni mdini Una udini. Hapo ndio natofautiana na wewe! Na mtu kama wewe ndio kila sehemu mnaweka udini na Kupanda mbegu mbaya ya Udini katika nchi yetu. Kila kitu wewe unaleta Udini tuu. Ninyi mnarudisha nyuma maendeleo kwa ajili ya Udini.
---------------------------------------------------------------------

Bwana Edward huijui historia ya uhuru na sababu walioshika serikali wanaiogopa.

Laiti wazee wetu wangekuwa wabaguzi wa dini Nyerere asingekuwa kiongozi wa TAA, TANU na Tanganyika.

Je, unawajua waliompokea Nyerere Dar es Salaam ya miaka ya 1950 na kuishi na yeye kama ndugu yao?

Unajua nyumba aliyoishi Nyerere Dar es Salaam baada ya kuacha kazi ya ualimu Pugu?

Unaijua historia ya Abdul Sykes na mkewe Mama Daisy na Nyerere na Mama Maria?
Je na ya Ali Msham na Nyerere na Mama Maria?…

JIBU

Bwana Edward huijui historia ya uhuru na sababu walioshika serikali wanaiogopa.

Laiti wazee wetu wangekuwa wabaguzi wa dini Nyerere asingekuwa kiongozi wa TAA, TANU na Tanganyika.

Je, unawajua waliompokea Nyerere Dar es Salaam ya miaka ya 1950 na kuishi na yeye kama ndugu yao?

Unajua nyumba aliyoishi Nyerere Dar es Salaam baada ya kuacha kazi ya ualimu Pugu?

Unaijua historia ya Abdul Sykes na mkewe Mama Daisy na Nyerere na Mama Maria?
Je na ya Ali Msham na Nyerere na Mama Maria?

Je ya Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir na Nyerere?
Je historia ya Mshume Kiyate, Mwinjuma Mwinyikambi na Max Mbwana na Nyerere?

Bi. Shariffa bint Mzee na Suleiman Masoud Mnonji na Sheikh Yusuf Badi Lindi, Mtwara na Mikindani Waislam wengi wasio na hesabu Tanganyika nzima.

Wapi umesikia wametajwa?
Hawa walimbagua Nyerere kwa kuwa alikuwa Mkatoliki?

Hivi kuandika historia za mashujaa hawa waliofutwa katika historia ya uhuru wetu ndiyo imekuwa ubaguzi wa dini?

Au hujui kama historia hii ilifutwa?
Unawajua waliotishwa na historia hii na bado inawatia hofu hadi leo?

Nini sababu ya uoga huu?

Je uliridhika kuona kuwa historia hii haikuwa inafahamika na leo unachukia kuona mimi nimeiandika na watu wameanza kujua ukweli.

Unajua kuwa wenye madaraka ya kuongoza nchi si Waislam na mgao ni 20:80?

Rais Mkapa alielezwa hali tuliyonayo na akaomba ushahidi na ushahidi akapewa na Prof. Hamza Njozi kupitia kitabu cha mauaji ya Mwembechai.

Kitabu kilipigwa marufuku.
Huu ndiyo udini wenyewe.

Hili ni tatizo na linafahamika.
Wewe ungeridhika kuona Waislam wamehodhi serikali kwa 80%.

Sidhani.
Hii ndiyo mbegu mbaya uliyoitaja ati inapandwa na Waislamu.

Ukipenda naweza nikakusomesha somo hili.

Udini ulianza tu baada ya uhuru mwaka 1961 kwa kuwekwa mikakati ya kufuta historia ya Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hii ni mada ya inayojitegemea yenyewe.

Soma historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika si hii iliyoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni mwaka wa 1981.

Soma kitabu cha Abdul Sykes na mwandishi ni mie.
Kitabu kinakwenda toleo la tano toka kuchapwa mwaka wa 1998.

Kitabu kimependwa kwa kuwa kina historia ya kweli inayowavutia wasomaji wengi wao ni vijana wa kizazi ambacho hakikuwepo wakati wa kudai uhuru.

Ukweli wote umo humo ndani.

Kitabu hiki ndiyo sababu ya kuandikwa Biography of Julius Nyerere ikidhaniwa kuwa kinaweza kujibu masuala ndani ya kitabu cha Abdul Sykes.

Yapo mengi.
Ikiwa hujui kitu uliza wenye kujua ufahamishwe.

Mimi siandiki kufanya maskhara.
Naandika kuitafutia amani ya kweli nchi yangu.

Naandika ili viongozi wetu wachukue hatua kurekebisha hali hii.
Angalia picha hizo hapo chini.

Ulipatapo kuziona popote.
Ziko nyingi sana na zinajieleza wenyewe.

Je unaona ni sawa kuwa historia hii isifahamike?
Bado unaamini kuwa Waislam ni wabaguzi hata baada ya ushahidi huu?

 
Hui...
Nimewasilisha mada nzima Kenyatta University kuhusu sakata la kuvunjwa kwa mabucha ya nguruwe.

Mimi ukiniulliza kwa nini hili lilitokea nitakwambia kuwa serikali ililishughulikia vibaya tatizo hili.

Watendaji walikosa busara.
Nimesoma mada yako Mzee wangu...Mashallah ni nzuri Sana....na nimefurahishwa na harakati za Sheikh Kassimu na nimehuzunishwa na mapito aliyopitia pia...lakini alipambana kadri ya uwezo wake..Allah amstiri moja wake.
 
Binafsi nimeona viongozi wameshindwa kusimamia mamlaka Yao....ilikuwa ni ishu rahisi Sana na kutafuta ufumbuzi wake na ndio maana baada ya kuona wameboronga wakajificha ktk kivuli cha kuleta habar mpya kuwa hao wahuni walitaka kuiangusha serikali...upumbavu mtupu
 
Kongole kwako mkuu
 
Waislamu wengi hawaujui uislamu wao na wanaendeshwa na mihemko tu
Hoja zero
 
Ni maeneo gani maalum kwa ajili ya kuishi Waislamu? Sheikh Rashid alizungumzia huu mkasa wa Kuvunja mabucha ya Nguruwe. Nlikuja kuona ulikuwa ni Umaamuma, ushetani na kutokuelimika. Mtoto alitumwa makusudi akanunue nyama ya nguruwe ili akija ionekane muislamu kisha kauziwa nyama ya nguruwe. But ukitumia tu common sense.
1. Nyama ya Nguruwe bei yake ipo juu.
2. Bucha za Nyama ya Nguruwe haziuzi ya ng'ombe wala mbuzi.

Sasa muuzaji kama alimuuzia mnunuaji nyama ya nguruwe je alijuaje kuwa ni muislamu na hatumii kitimoto?

Je huyo mnunuaji kama alienda moja kwa moja bucha ya nyama ya nguruwe akasema tu nataka nyama kilo 1 muuzaji alikuwa na kosa gani?

Lakini bila chembe ya unafiq hata chembe ni waislamu wangapi wanakula kwa siri kitimoto? Ule mkakati naufahamu sana na baadhi ya wahusika walikuja kukiri baadaye kuwa lengo lilikuwa ni kuzusha chokochoko. Wakirejea na Mkutano uliofanyika Abuja Nigeria miaka hiyo. Na maazimio yake. Na ufadhili ambao ulikuja tolewa na Muamar Ghadaf...

Haya mambo tupo ambao tunayafahamu na hatuuingi mkono sababu ni upuuzi mkubwa sana. Mwinyi alitoa tamko kubwa kipindi kile. Hilo hujaliweka 😁😁😁😁 sababu ni mwenzetu. Umeangalia matamko ya wakristo peke yake.😁

Siku zinavyozidi kwenda hata sisi tunakuona umepoteza mwelekeo.tunashindwa kukutetea maana unataka nasi tuanze kuonekana mafala...no way.
 
Komeo...
Kuna mambo huandikwa hapa huwa nayakalia kimya sisemi neno kwa kuwa itakuwa ni kubishana ma ghadhabu kupanda mfano wa maneno, ''no way,'' ''mafala'' na mfano wa hayo.

Lakini yapo maneno hupenda kuyatolea kauli.
Mimi hafarajika kuleta elimu ambayo si wengi wanayo.

Mkutano wa Abuja unazungumzia ''The Two Headed Dragon'' mpango wa kueneza Uislam Afrika.

Hayo yote ni ''fake.''
Ikiwa mtu atapenda kuamini vitu kama hivyo huna la kumfanya.

Allah kakataza ndani ya Qur'an kulaziisha dini.
Hakuna Muislam anaeweza kuweka mikakati ya kuhujumu imani nyingine.

Allah kakataza kwa kuwa anajua hatari yake.

Halikadhalika kawakataza Waislam wasidhulumu na wao wasikubali kudhulumiwa.

Haya ndiyo mafunzo ya Uislam.
Kama huniamini mimi waulize masheikh watakueleza ukweli.
 
Nimecheka sana usiku huu.. wewe una utani na Mzee wetu Mzee Mohamed Said
 
Nimecheka sana usiku huu.. wewe una utani na Mzee wetu Mzee Mohamed Said
Einstein,
Hakuna aliyekimbia.

Kwangu mimi haya si mambo ya kufanya kejeli na maskhara.

Nimekujibu ili ufahamu kuwa nategemea adabu kutoka kwako.

Lakini ikiwa kama unadhani mimi ni mtu wa kuchezewa tafadhali fikiri mara mbili.

Vinginevyo nitasitisha mjadala na wewe.
Siko hapa kukejeliwa.

Mimi ni mtu na heshima yangu.

Lakini kukusaidia ungeweza kuniuliza ilikuwaje sikukamatwa na wengine wakakamatwa.

Hapa kuna stori nzuri ningependa kuieleza kama ungeuliza kwa adabu na heshima

Tafadhali tambua mimi si muhuni.
 
Mzee Mohamed Said

Sijaelewa ni kwa nini umekwazika kiasi hicho, mimi nimemnukuu EINSTEIN112 ambae kwenye post yake anasema kuwa ulikimbia, mimi nimecheka kwa sababu nimechukulia kwamba ameamua kukutania,

members wengine humu ni kama wajukuu zako tu, ni watoto wadogo, ndio maana nikamwambia kwamba ana utani na wewe.

Pamoja na kuheshimu mchango wako wa kitaaluma, mimi ninakuheshimu wewe binafsi, tunapotofautiana kimtazamo tunajadili kwa hoja, wala siwezi kukukejeli hata siku moja.

Naomba niwie radhi kama post yangu namba 264 hapo juu imeonyesha kukukosea adabu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…