Buriani Hassan Chikusa msomi mkimya

Buriani Hassan Chikusa msomi mkimya

Mzee makala yako ni ndefu lakini haujatueleza "USOMI" wa Hassani Chikusa kwamba alikuwa na elimu gani ya juu? ya dini au secular, ila maelezo yako yameegemea kwenye harakari za waislamu kuvunja mabucha na kupambana na polisi.
Mimi nimesoma kutafuta sehemu aliyoelezea usomi wake kama mada inavyosema sikuelewa. Nikahamia kwenye comments za mabucha yaliyojengwa kuwafuata wateja wa kitimoto......
 
Mimi nimesoma kutafuta sehemu aliyoelezea usomi wake kama mada inavyosema sikuelewa. Nikahamia kwenye comments za mabucha yaliyojengwa kuwafuata wateja wa kitimoto......
Huyu mzee katupanga
 
Mzee Mohamed Said

Sijaelewa ni kwa nini umekwazika kiasi hicho, mimi nimemnukuu EINSTEIN112 ambae kwenye post yake anasema kuwa ulikimbia, mimi nimecheka kwa sababu nimechukulia kwamba ameamua kukutania,

members wengine humu ni kama wajukuu zako tu, ni watoto wadogo, ndio maana nikamwambia kwamba ana utani na wewe.

Pamoja na kuheshimu mchango wako wa kitaaluma, mimi ninakuheshimu wewe binafsi, tunapotofautiana kimtazamo tunajadili kwa hoja, wala siwezi kukukejeli hata siku moja.

Naomba niwie radhi kama post yangu namba 264 hapo juu imeonyesha kukukosea adabu!
Mjuni Lwambo na mimi niombee radhi kwa mzee wangu Mohamed Said humu kuna utani sometimes kwaio aniwie radhi kama nimemkosea
 
Mimi nimesoma kutafuta sehemu aliyoelezea usomi wake kama mada inavyosema sikuelewa. Nikahamia kwenye comments za mabucha yaliyojengwa kuwafuata wateja wa kitimoto......
Inaonekana alikuwa msoni wa dini maana hata masters hajaeleza kama alikuwa nayo
 
Huyu mwanahistoria sijawahi kuona akiandika makala inayohusu chochote bila kuingiza uislam.

Imefika hatua unajua yaliyomo yanahusu uislam hata kama kichwa kiko tofauti.

Anyway endelea kupambania uislam wako maana sijawahi ona ukiandika mazuri ya wala kitimoto maana ni kama hawana jema hata moja.

Na wewe andika makala zako za uanachama wako wa Cham cha wapiga punyeto, kila mtu na kitengo chake.
 
Einstein,
Namna yangu ya uandishi ni tofauti sana.

Huenda kwenye mambo yanayoeleza hali za nyakati.

Ningeandika vinginevyo taazia hii isingechemsha watu kama unavyoona.

Nimeeleza tukio la mabucha na msimamo wa serikali na vipi Waislam walivyosimama kuikabili serikali.

Nimewaleta BBC, wahariri wa magazeti na jinsi viongozi wa nchi kuanzia Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya Ndani na Katibu wa CCM walivyolishughulia tatizo la mabucha.

Yako mengi.

Lakini nia yangu ni kukutaka wewe msomaji uhiangaishe akili yako na hivyo kuwapima hawa viongozi.

Viongozi walitupa lawama kwengine na kusema kuwa waliovunja mabucha nia yao ilikuwa kupindua serikali.

Je, huoni kuwa hapo yapo mengi ya kujifunza?
Ni wazi agenda kuu ya vurugu za kiislamu ni kuitaka SERIKALI IWE YA KIISLAMU (KUIPINDUA). Viongozi wote walikuwa sahh kwa nafasi zao.. Ila mjifunze kutafuta vitu logical vya kuanzia vurugu zenu... sio ivyo vya kitoto mnavyosimamia.

Mliosoma tumieni usomi wenu kuwaeleza wenzenu namna ya kujenga hoja zenye nguvu. Ili lengo lenu litimie
 
KII,
Mimi utaalamu wangu uko katika historia ya Uislam.
Hii ndiyo sababu kila unaposoma utawasoma.

Labda ungeniuliza kwa nini nimesoma somo hili?
Sababu ni kuwa wanahistoria wetu walipuuza historia ya Waislam kiasi yote ilifutika.

Mimi nikaamua kutafiti na kuiandika.
Ikiwa wewe unakereka na hili acha tu kusoma post zangu.
Tafakari madhara yanayoweza kutokea kwa udini wako hacha haya hakuna anayependezwa
 
Mzee Mohamed Said

Sijaelewa ni kwa nini umekwazika kiasi hicho, mimi nimemnukuu EINSTEIN112 ambae kwenye post yake anasema kuwa ulikimbia, mimi nimecheka kwa sababu nimechukulia kwamba ameamua kukutania,

members wengine humu ni kama wajukuu zako tu, ni watoto wadogo, ndio maana nikamwambia kwamba ana utani na wewe.

Pamoja na kuheshimu mchango wako wa kitaaluma, mimi ninakuheshimu wewe binafsi, tunapotofautiana kimtazamo tunajadili kwa hoja, wala siwezi kukukejeli hata siku moja.

Naomba niwie radhi kama post yangu namba 264 hapo juu imeonyesha kukukosea adabu!
Mujuni,
Mimi ndiye wa kukutaka radhi wewe.

Nilikuja kujua kuwa ni Einstein si wewe na nikasahihisha kwa kumwandikia yeye.

Soma post utaona nimeandika Mujuni.

Samahani sana kaka yangu.
Tuko sote.

Hapa siwezi kuwa na mjukuu ni umri wa wanangu.

Wajukuu zangu hakuna aliyevuka miaka saba.

Mimi nina miaka 70.
 
Tafakari madhara yanayoweza kutokea kwa udini wako hacha haya hakuna anayependezwa
Bora...
Hapa swali la udini halipo kwangu pana tatizo la dhulma.

Naona umekasirika unaandika "udini wako," lugha ya ghadhabu.

Lipo tatizo la baadhi ya watu walio madarakani kutumia imani zao kuwabagua wengine.

Hakakia hili kwetu halipendezi ndiyo unaona hapa naandika nikitumia jina langu halisi na picha zangu zipo hapa.

Hulijui tatizo hili kwa hiyo ungetafuta ukweli kwanza kabla ya kuandika.

Mimi nina ushahidi.

Ukiwa unapenda naweza nikakuwekea hapa.
 
Ni wazi agenda kuu ya vurugu za kiislamu ni kuitaka SERIKALI IWE YA KIISLAMU (KUIPINDUA). Viongozi wote walikuwa sahh kwa nafasi zao.. Ila mjifunze kutafuta vitu logical vya kuanzia vurugu zenu... sio ivyo vya kitoto mnavyosimamia.

Mliosoma tumieni usomi wenu kuwaeleza wenzenu namna ya kujenga hoja zenye nguvu. Ili lengo lenu litimie
Sky...
Soma post #280.
Lina jibu la baadhi haya uliyoeleza hapa.

Waislam hatuna ujinga wa kuwa tufanye vurugu kupindua serikali iwe ya Kiislam.

Kwanza tufanye hayo kwa mafunzo yapi?

Uislam haufunzi hivyo.

Pili Waislam ndiyo walikuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Soma kitabu cha Abdul Sykes (1998).

Unazungumza usomi.

Prof. Hamza Njozi kaandika kitabu "Mwembechai Killings..." (2002) serikali imekipigq marufuku kwa kuhofia ukweli kufahamika.

Soma rejea nilizotaja hapa zitakusaidia kulielewa tatizo.
 
Komeo...
Kuna mambo huandikwa hapa huwa nayakalia kimya sisemi neno kwa kuwa itakuwa ni kubishana ma ghadhabu kupanda mfano wa maneno, ''no way,'' ''mafala'' na mfano wa hayo.

Lakini yapo maneno hupenda kuyatolea kauli.
Mimi hafarajika kuleta elimu ambayo si wengi wanayo.

Mkutano wa Abuja unazungumzia ''The Two Headed Dragon'' mpango wa kueneza Uislam Afrika.

Hayo yote ni ''fake.''
Ikiwa mtu atapenda kuamini vitu kama hivyo huna la kumfanya.

Allah kakataza ndani ya Qur'an kulaziisha dini.
Hakuna Muislam anaeweza kuweka mikakati ya kuhujumu imani nyingine.

Allah kakataza kwa kuwa anajua hatari yake.

Halikadhalika kawakataza Waislam wasidhulumu na wao wasikubali kudhulumiwa.

Haya ndiyo mafunzo ya Uislam.
Kama huniamini mimi waulize masheikh watakueleza ukweli.
Zilongwa Mbali ,Zitendwa Mbali.
 
BURIANI HASSAN CHIKUSA MSOMI MKIMYA

Naamini si wengi wanamfahamu Hassan Chikusa na yote yaliyomsibu katika maisha yake.

Mimi nilimjua Hassan Chikusa kwa kuwa alikua jirani yangu akiishi kwa ndugu yake Masaki jirani na nyumba niliyokuwa naishi mimi na familia yangu.

Wakati ule alikuwa kijana mdogo ndiyo kwanza amemaliza masomo yake na anafanya kazi Makao Makuu National Bank of Commerce (NBC), Sokoine Drive.

Tulizoeana sana na wakati mwingine akija nyumbani kwa mazungumzo na akipenda mazungumzo yangu katika vitabu, historia na muziki kama ilivyo kawaida ya vijana.

Hassan alikuwa akiweka shajara yaani akiandika, ''diary.''

Hassan alikuwa kijana akiipenda dini yake sana kwa mapenzi makubwa.
Mwaka wa 1993 pakawa na sakata la uvunjaji mabucha ya kuuza nyama ya nguruwe Wilaya ya Kinondoni baada ya sala ya Ijumaa.

Kilichotokea ni kuwa kijana alitumwa nyama na muuza nyama pengine kwa kutokujua akamuuzia huyu kijana nyama ya nguruwe.

Palikuwa na malalamiko kuhusu haya mabucha ya kuuza nyama ya nguruwe lakini walioshika madaraka hawakujali wala kutia maanani malalamiko ya Waislam.

Mjini Dar es Salaam kulikuwa na mabucha 29 ya kuuza nyama ya nguruwe kwenye sehemu wanazoishi Waislam na hii ilikuwa kinyume cha sheria.

Tatizo hili Waislam wakalifikisha kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mustafa Nyang;anyi lakini hakuna kilichofanyika na likafikishwa pia kwa Waziri Mkuu, John Samuel Malacela.

Waswahili wanamsemo wanasema yale yalikuwa sawa na kutwanga maji katika kinu.

Hili tatizo la mabucha likashushwa chini hadi kwa Mkuu wa Wilaya, Wilson Mkama na yeye akawaita ofisini kwake maimamu wa misikiti mitano ya Wilaya ya Kinondoni kwa mazungumzo.

Serikali haikuwa tayari kufunga mabucha hayo kwa kile walichokiona ni shinikizo kutoka kwa Waislam wenye, ''siasa kali.''

Bwana Mkama akawaeleza maimam kuwa hayo mabucha yapo kihalali na wana leseni walizopewa na serikali kufanya biashara hiyo kwa ajili hii serikali ina dhima ya kuzilinda hizo bucha.

Mkutano ukamalizika na maimamu wakarejea misikitini kwao kuwaeleza Waislam kauli ya serikali kuhusu mabucha ya kuuza nyama ya nguruwe.

Waingereza wana msemo, ''The straw which broke the camel's back,'' yaani ujani uliowekwa juu ya mgongo wa ngamia ukauvunja.

Waislam walighadhibika sana kwa uamuzi wa serikali kuwapuuza.
Siku ya pili ilikuwa Ijumaa Kuu.

Baada ya sala ya Ijumaa vijana wa Kiislam walipomaliza sala waliziendea zile bucha zilizokuwa Wilaya ya Kinondoni wakazivunja zote kwa mpigo.

Dar es Salaam ilizizima.
Haya hayakupata kutokea katika kipindi chote cha uhuru.

Rais Ali Hassan Mwinyi akiwa Zanzibar akasema katika kulani kuvunjwa mabucha ya nguruwe kuwa nguvu za dola ziwaangukie wale waliovunja mabucha ya kuuza nyama ya nguruwe.

Jioni yake BBC hwakuchelewa wakafanya mahojiano na Waziri Mkuu John Samuel Malecela.

Malecela akasema kuwa waliovunja mabucha ya kuuza nyama ya nguruwe ni wahuni wanotaka kuchukua serikali kupitia dini.

Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu Augustine Mrema yeye akasema mabucha yamevunjwa kutokana na nguvu kutoka nchi ya Kiislam ili kuivuruga Tanzania.

Katibu Mkuu wa CCM Horace Kolimba yeye akahitimisha kwa kusema kuwa waliovunja mabucha si Waislam ila ni wahuni wanaotaka kupindua serikali.

Kufika asubuhi siku ya Jumamosi masheikh 40 wakawa wamekamatwa usiku wa manane kwa taadhira kubwa majumbani kwao mfano wa majambazi na kutiwa korokoroni.

Wahariri wa magazeti asubuhi yake siku ya Jumamosi wakawa katika burdani kubwa ya kuandika kuvunjwa kwa mabucha ya kuuza nguruwe na kukamatwa kwa masheikh.

Asubuhi ile ya Jumamosi kundi dogo la Waislam wakaenda Kituo Cha Kati cha Polisi kufuatilia masheikh waliokamatwa usiku na kuwekwa korokoroni hapo.
Hawa nao wakakamatwa na kuwekwa ndani.

Haukupita muda baada ya habari kuenea kuwa Waislam waliokwenda kuwauliza masheikh na wao wamekamatwa Waislam wakaja kwa wingi kituoni siku ya pili yake Jumapili iliyokuwa Easter Sunday.

Siku hiyo Waislam wakakusanyika pale kituoni ikawa kama vile kituo kimezingirwa na sala ya L'Asr ilipoingia ikapigwa adhana pale nje ya ya kituo watu wakasali barabarani.

Polisi wakataka kuwapiga mabomu ya machozi lakini pakawa na kutokubaliana baina ya askari wenyewe.

Hawakupendezewa na kitendo kile.

Askari Waislam wakawaambia wenzao hilo haliwezi kufanyika kuwapiga mabomu Waislam wanaosali kwani ni kufuru kubwa Waislam hawajafanya fujo wamekuja kituoni kufuatilia masheikh wao walioko korokoroni.

Jua lilipotua Waislam wakaondoka pale kituoni wakaamua wakutane siku ya pili Msikiti wa Mtoro washauriane.

Siku hii ya Jumapili yaani Easter Sunday mimi ndiyo niliingia Dar es Salaam nikitokea Le Havre, Ufaransa nikaja Paris kwa muda wa siku mbili kisha nikaenda London kisha Cardiff na kurejea London kupanda ndege kurudi Dar es Salaam.

Nilipofika nyumbani ndipo nilipopata taarifa ya masheikh kukamatwa na kati ya masheikh hao alikuwa mjomba wangu Sheikh Pazi wa Manzese.

Sikusubiri nikaenda kwa Hassan Chikusa wakati huo akiishi Mwananyamala kwani nilijua pamoja na kupita kwa jamaa wengine yeye ndiye ataweza kunipa taarifa ya mkasa mzima pamoja na tathmini.

Hayo niliyoandika hapo juu ni baadhi ya mambo aliyonifahamisha kuwa yametokea kuanzia siku ile ya Ijumaa yalipovunjwa mabucha hadi siku ya pii yake Jumamosi.

Hili ninalosema sasa ni jambo ambalo kwa miaka yote kila nilipokutana na Hassan moyo uliniuma sana nikiishia kumuombea dua.

Hassan siku ile nilipokwenda kwake ilikuwa Jumapili usiku na hakuwa na taarifa kuwa siku ya Jumatatu, yaani Easter Monday Waislam wameamua kufanya shura ndani ya Msikiti wa Mtoro ambao Imam Mkuu, Sheikh Kassim Juma alikuwa kakamatwa Arusha akielekea Nairobi kwenye matibabu na kurudishwa Dar es Salaam na yuko rumande.

Mimi ndiye nliyemfahamisha kuwa kesho Easter Monday kuna shura ya Waislam wote wa Dar es Salaam kujadili kwa pamoja nini kifanyike kurejesha heshima ya masheikh wetu.

Hassan aliniuliza kama mimi nitakuwepo.
Nikamwambia In Shaa Allah nitakuwapo.

Hassan Chikusa na yeye akaniambia atakuwapo pia.

Kwa ufupi siku ile ndani ya Msikti wa Sheikh Mtoro Mwinyi Mangara iliamriwa baada ya mjadala mkali sana Waislam watoke kwa maandamano hadi Kituo Cha Kati Cha Polisi kwenda kuwatoa masheikh wao korokoroni.

Katika maandamano yale Waislam walipambana na polisi na mabomu ya machozi yalipigwa.

Mapambano haya yalifanyika kati ya kituo cha polisi na Clock Tower.
Haya ndiyo yalikuwa maandamano ya kwanza ya Waislam Tanzania Bara.

Zanzibar maandamano yao yalikuwa mwaka wa 1988.
Maandamano haya yote tatizo ni Uislam.

Hassan Chikusa akakamatwa pamoja na vijana wengi wa Kiislam.
Wakawekwa rumande wakashtakiwa na kuhukumiwa vifungo jela.

Hassan Chikusa akapoteza kazi yake NBC.

Huyu ndiye Hassan Chikusa msomi mkimya ambae baada ya kutoka jela akiwa hana kazi masahibu mengi ya maisha yalimfika.

Lakini siku zote akisema yaliyomfika ni madogo sana na yote ameyakadiria Allah na na yeye bado yu hai.

Kwangu mimi maadamano yale na wale walioshiriki katika yale maandamano kile kilikuwa kipimo.

Tunamuomba Allah amsamehe makosa yake mja wake huyu na amtie Firdaws.
Amin.

View attachment 2305229
Hassan Chikusa​
Unanishangaza sana kusema "Mjini Dar es salaam kulikuwa na mabucha 29 ya kuuza nguruwe kwenye sehemu wanazoishi waislamu na hii ilikuwa kinyume na sheria"
Naomba unijibu maswali yafuatayo
1) Sheria namba ngapi ya nchi hii inakataza watu kuuza nguruwe katika maeneo wanayoishi waislamu?
2) Ilitungwa na bunge gani, mwaka gani na ilisainiwa na Rais gani ili iwe sheria?
3) Tanzania Kuna "maeneo ya waislamu na maeneo ya wakristu?
4) Baada ya vurugu zote hizo waislamu walishinda nini? Mabucha yaliindoka? Kuuza nguruwe Tanzania kulipigwa marufuku? Au ulaji wa nguruwe ulikatazwa?
5) Huyo jamaa alipata faida gani baada ya kufukuzwa kazi NBC na akarudi mtaani akaanza kukaa kwenye vibaraza?

Kitu ambacho ninasikitika kuhusu wewe ni kuwa mbaguzi, sijawahi kuona unaleta mada ya kumsifia mkristo hapa. You are living at the past. Mbaya zaidi, siku hizi waislamu ndo wanaongoza kula nguruwe. Mimi nawafahamu waislamu zaidi ya 50 wanakula nguruwe hasa. Fanya utafiti, kwanini mwezi wa ramadhan mauzo ya nguruwe yanashuka? Jibu unalo
 
Back
Top Bottom