Buriani Hassan Chikusa msomi mkimya

Hassan Chikusa akakamatwa pamoja na vijana wengi wa Kiislam.
Wakawekwa rumande wakashtakiwa na kuhukumiwa vifungo jela...
Tanzania ina Waislamu wa ajabu sana. Nakiri mimi ni Mkristu ila nimebahatika kutembea vya kutosha kwenye nchi za Kiislamu kama Malaysia, Indonesia, Dubai, Iran, Abu Dhabi, Sudan na Turkey.

Nakiri kuwa nimewahi kula nyama ya nguruwe kwenye hoteli za 5 Star nchini Dubai, Malaysia na Turkey. Ni aibu kwa Waislamu wa Tanzania kuanzisha vurugu sababu ya mboga.

Sasa huyu marehemu Hassan Chikusa pengine kwa kupoteza kazi NBC sababu ya ujinga wa kuvunja mabucha kunaweza kukawa kulimuathiri kwa kipato na akashindwa kulea familia yake vizuri including kiwapa elimu wanae.

Lesson Learnt:
Muislamu usile nyama ya nguruwe kwa vile ni haramu period, lakini usihangaike na Wala nguruwe na mali zao.
 
Haya hebu tufungue macho, ni kifungu kipi na tangu lini Manzese au Magomeni vikawa ni vitongoji vya kiislamu?
Loyol...
Maswali kama haya si lazima nijibu mimi unaweza hata wewe mwenyewe kufanya utafiti utapata majibu unayoyatafuta.

Wajomba zangu wawili Sheikh Pazi na Shomari Lupindo wakiishi Manzese kwa miaka mingi toka mimi ni mtoto na sasa nina miaka 70.

Kwa hiyo naijua Manzese vizuri sana.
Nimezaliwa Dar es Salaam.
 
Tanzania ina Waislamu wa ajabu sana. Nakiri mimi ni Mkristu ila nimebahatika kutembea vya kutosha kwenye nchi za Kiislamu kama Malaysia, Indonesia, Dubai, Iran, Abu Dhabi, Sudan na Turkey...
Hui...
Nimewasilisha mada nzima Kenyatta University kuhusu sakata la kuvunjwa kwa mabucha ya nguruwe.

Mimi ukiniulliza kwa nini hili lilitokea nitakwambia kuwa serikali ililishughulikia vibaya tatizo hili.

Watendaji walikosa busara.
 
Hui...
Nimewasilisha mada nzima Kenyatta University kuhusu sakata la kuvunjwa kwa mabucha ya nguruwe.

Mimi ukiniulliza kwa nini hili lilitokea nitakwambia kuwa serikali ililishughulikia vibaya tatizo hili.

Watendaji walikosa busara.
Tanzania ni secular state.

Ni hatari sana kuwapa uhuru usio na mipaka watu wenye itikadi kali ya upande fulani ilhali una watu wa Imani tofauti tofauti.
Watendaji walikosa busara ? Na hao waliovunja bucha walitumia busara au vurugu?

Hizi doctrination badala ya kutuunga zimetugawa, badala ya kutufanya tupendane zimetufanya tuchukiane.
Kama Mungu tunaye mhubiri ni Mungu mwenye upendo wote. ( Upendo huvumilia, Upendo haujivuni , Upendo haukosi kuwa na adabu)
Kwa nini tusimtangaze kwa upendo ? tunamtangaza kwa chaos.
 
Siku hii ya Jumapili yaani Easter Sunday mimi ndiyo niliingia Dar es Salaam nikitokea Le Havre, Ufaransa nikaja Paris kwa muda wa siku mbili kisha nikaenda London kisha Cardiff na kurejea London kupanda ndege kurudi Dar es Salaam.
Hizo sehemu zote ulizopitia nina wasi wasi nazo. Hizo ndo vichaka vya wafia dini ya kiislam.
 
Extremism kwenye dini yoyote ile siyo nzuri kabisa. Huko India wahindu wanaabudu ng'ombe. Extremist wa kihindu wanaua na kuwatesa waislamu wanaokula ng'ombe.

Huku waislamu wanavunjia watu mabucha yao. Mara kule wale hivi. Extremism hukua polepole. Watavunja mabucha, watavunja baa, viwanda vya bia, benki zinazotoza riba nk nk.
 
Kabla sijasoma maoni mzee wangu ningeomba msaada wa hicho kifungu kinacho sema "maeneo haya ni ya waislamu"

Je, ni waislamu tu ndio waliopatiwa maeneo au kumilikishwa?

Je, kama yapo ni utawala wa awamu ipi waligawa haya maeneo?

Je, dini zingine mfano kristo, hindu, dini za asili nao wanao mgao huo kama ndugu zao islamic?

Mwisho kwa mtazamo wako unaona jambo la kugawa hayo maeneo lina tija kwa taifa la sasa hususani kwenye kujenga mshikamano kitaifa?
 
Hui...
Nimewasilisha mada nzima Kenyatta University kuhusu sakata la kuvunjwa kwa mabucha ya nguruwe...
Mimi pamoja na kukubali makosa kwa Serikali katika kushughulikia tatizo hilo lakini bado nawalaumu wenzetu Waislamu wanavyo kuwa RADICALISED kwa vitu vidogo.

Unakumbuka kule Tunduma ilitokea mgogoro wa haki ya kuchinja kitoweo? Tunagombana kwa petty issues mpaka tunatia aibu
 
Ukiwa mfia dini (conservative religious extremist)
Hata usome vipi elimu yako haitakuwa na maana.
Kuna wasomi wana dini zao but when it comes to the public wanakuwa neutral.
Kwa mfano J K Nyerere alikuwa ni Mkatoliki safi lakini kwenye suala la Palestine alikuwa ni supporter kuhusu wao kuwa na nchi yao dhidi ya uvamizi wa Israel. Ndiyo maana akawapa na ruksa ya kufungua UBALOZI Tanzania
 
We jamaa,yaani nchi hii inasehemu wanayoishi "waislam"ambapo hairuhusiwi kuweka bucha ya nguruwe!!Tena unasema kisheria.Radical islamist mna mambo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…