Buriani mradi wa Liganga na Mchuchuma

Buriani mradi wa Liganga na Mchuchuma

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
ULE msemo kuwa chelewa chelewa utamkuta mwana si wako umejidhihirisha wazi kwenye suala lauwekezaji wa mradi wa Liganga na Mchuchuma wilayani Ludewa mkoani Njombe ambapo mwekezaji, Sichuan Hongda Group yuko njia panda kwa kukosa mwelekeo na kuungwa mkono.

Kampuni imesema madai yote yalikuwa na haki ya kujadiliwa kikamilifu na Serikali ambayo ilikwisha kutoa vyeti vya vibali vya madini na vishawishi vya uwekezaji.

Sichuan Hongada Group inadai mradi umekuwa ukicheleweshwa na Serikali kutofanya yanayostahili huku ikijisahau kuwa kampuni hiyo imekuwa ikibadilisha masharti yake kama vile haijui nini inatakakwenye mradi.

Wachunguzi wa mambo wanasema mradi huo kwa kila hali umepitwa na wakati kwani sheria zimebadilika na masharti yauchimbaji madini yameathiriwa kwa kiasi kikubwa na sheria mpya za Tanzania ambazo zimebadilika kudai kupata faida kwenyeutajiri wake.

Hongda Group inashauriwa nayo kubadilika ilikuzuia isijikute nje ya mradi kwani wanaohitaji mradi huowanazidi kuongezeka.

Muda mwingi umepotezwa na badilika badilika yake na dhana ya mradi ambayo sasa maudhui ya kisheria yanatoa madai mengi kutokana na Sheria ya Mali ya Taifa ya mwaka 2017 na vile vile Sheria ya Madini 2010 kwa hiyo kwa kiasi kikubwa wataalamu wa Serikali wanadai wa kulaumiwa ni kampuni yenyewe na si Serikali.

“Ieleweke wazi kuwa ukiona majadiliano yanachukua zaidi ya miaka10 ujue jambo hilo haliwezekani na hivyo kuliacha au kutafuta njia nyingine zautekelezaji kwani hakuna mradi duniani unaomalizwa mara moja ila hujadiliwa kutokana na matatizo yanayojitokezakwani hakuna mtu mwenye nia nzuri kukataa ukweli unaojitokeza kwani wakati wautekelezaji pande hizo mbili, Serikali na mwekezaji huwa ni wabia na hivyo huwezeshana ili kufanikisha malengowaliyojiwekea.

Kwa sheria mpya inawataka wawekezaji kutoa asilimia 16 ya hisa bure kwa Serikali.

Aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Dk. Chrisant Majiyatanga Mzindakaya, ameumia sana kusikia kuwa mradi huo si kipaumbele tena kwani alipigania sana kuhakikisha unakuwa hivyo. Alipotoka tu watu wameamua kuubwaga mradi bila kutoa sababu.

Wengi niliowauliza nao vile vile wananiuliza wanasema tatizo ni mradi au Wachina? Kwa sababu si vema kuachia dola bilioni 3 ambazo zingeiweka nchi kwenye ramani ya dunia na hivyo kukosa kila kitu.
Kampuni hiyo ya Sichuan Hongda Group, kampuni mzazi katika mradi ilishinda zabuni kwa mradi huo mkubwa sana wa uchimbaji madini na ujenzi tangamano wa viwanda vya chuma na makaa ya mawe na usafiri wa reli hadi bandari ya Mtwara.

Mradi ulionesha uwezo wa kuunda kazi 5,000 za moja kwa moja na nyinginezo 30,000 zisizo kuwa za moja kwa moja katika mwaka 2010.
Kampuni ya Kichina ilipewa zabuni ya kuendeleza kwa dola bilioni 3 (Sh trilioni 6.8) wa chuma lakini sasa unaonekana si kipaumbele na hivyo Hongda inaona kuwa haikutendewa haki.

Serikali kwa mazingira ya sasa inaona kuwa kampuni hiyo ni kiwingu kwa kuzuia wawekezaji wengine kuingia kwenye eneo la mradi na kufanya wanayotaka kufanya baada ya kuona hakuna maendeleo ya haja kwenye mradi huo.

Kuanguka bei ya chuma

Isitoshe wakati fulani kampuni hiyo ilisema kuzalisha chuma wakati huu hakulipi na hivyo walikuwa wanasubiri bei ipande na hivyo madai ya kukosa motisha inaonekana kuwa ni mwendelezo wa kutaka dezo.

Kimsingi katika mazingira yaliyopo si rahisi kuibana Serikali ingawa matendo ya Waziri wa Fedha, Dk. Phillip Mpango, kuutoa kwenye kipaumbele inahitaji maelezo ya kina.

Isitoshe Hongda Group inadai uzinduzi wake mradi umejaa ucheleweshaji usioeleweka na kujaa sintofahamu na sasa kukosa msukumo wa kisiasa.

Hata reli yake imepitwa na ujenzi wa reli ya SGR kwenda Mwanza na nyingine kwenda Kigoma hadi Burundi na Rwanda. Mahitaji halisi yamebadilika ndani ya miaka mitatu.
“Kama mwekezaji mkubwa na alitumia rasilimali nyingi katika maendeleo na utekelezaji wa mradi, Sichuan Hongda, bado ana nia ya kutekeleza mradi huu licha ya changamoto za mara kwa mara ndani na nje ya nchi,” inasema taarifa ya Hongda.

Mchuchuma inadaiwa kuwa na tani milioni 428 za makaa ya mawe wakati Liganga ina tani milioni 128 za chuma na kampuni ya Kichina imetoa mpango jumuishi wa madini na uzalishaji umeme MW 600.

Makampuni hayo yatatengeneza madini yote ndani ya nchi ili kutenganisha titani na vanadium kutoka kwa madini ya chuma.
Wizara ya Fedha hakupatikana kusema kwanini haijasaini utekelezaji wa mradi huo kwa kutoa motisha kwa muda mrefu licha ya ahadi ya mwaka jana ya aliyekuwa Waziri wa Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, kudai ilikuwa inasubiriwa saini ya Rais Magufuli tu.

Suala la Waziri wa Fedha, Dk. Phillip Mpango, kuunyang’anya mradi nguvu ya kisiasa, linadai maelezo ya kina kwani suala hilo limeanza kuleta joto la kisiasa nchini na wadau wa uchumi.

Chanzo: Mtanzania
 
Hahaha sisi tunajua kila kitu, sijui kwanini huwa tunatafuta wawekezaji. Yani tunawatafuta wakianza kazi tu, basi zengwe linaanza mara tunaibiwa, mara hawalipi kodi mara hatoi gawio,mara wayeyushe kila kitu humu nchini. Kwanini tusifanye wenyewe kila kitu?!
 
Sasa hapa naanza kupata picha kwanini Mh Fulani aliibuka na kudai mradi unacheleweshwa kwa makusudi na kudai Serikali imepewa Rushwa na ili kucheleweshwa! Kama Mchina mwenyewe analalamika basi nakupa siri wabunge wetu ni kama C*****m..! wako tayari kutumika!

Ninavyo mjua Mh Rais kama huyo mwekezaji angekuwa bora na hakuna kupigwa tayari uo mradi ungekuwa umeenza! hiyo kampuni yenyewe imeshinda tender kipindi cha JK.

Kinachotokea hapo sawa tu na ile Gas ya Mtwara! Rais tulienae sasa akijua huo mradi kwa nchi za wenzetu unaliingizia Taifa zaidi Trillion 10 kwa mwaka alafu wewe kwenye karatasi zako unasema utaipa Taifa Trillion 5 hapo hakubali katu..! Kulingana na masharti ya mkataba tu unakuwa siri basi hawezi kuweka wazi bila hivo angekuwa ameshalisema hilo na hakufukuzi we ukiona mambo magumu sepa naye atakuambia tupo tayari kusubiri ata miaka 20 tujilidhishe kama unafaida kwa Taifa. Hapo ujue huna chako
 
kama ni kweli basi jiwe yuko sahihi lkn kama ni kweli
 
ULE msemo kuwa chelewa chelewa utamkuta mwana si wako umejidhihirisha wazi kwenye suala la uwekezaji wa mradi wa Liganga na Mchuchuma wilayani Ludewa mkoani Njombe ambapo mwekezaji, Sichuan Hongda Group yuko njia panda kwa kukosa mwelekeo na kuungwa mkono.
Kampuni imesema madai yote yalikuwa na haki ya kujadiliwa kikamilifu na Serikali ambayo ilikwisha kutoa vyeti vya vibali vya madini na vishawishi vya uwekezaji.
Sichuan Hongda Group inadai mradi umekuwa ukicheleweshwa na serikali kutofanya yanayostahili huku ikijisahau kuwa kampuni hiyo imekuwa ikibadilisha masharti yake kama vile haijui nini inataka kwenye mradi.
Wachunguzi wa mambo wanasema mradi huo kwa kila hali umepitwa na wakati kwani sheria zimebadilika na masharti ya uchimbaji madini yameathiriwa kwa kiasi kikubwa na sheria mpya za Tanzania ambazo zimebadilika kudai kupata faida kwenye utajiri wake.
Hongda Group inashauriwa nayo kubadilika ili kuzuia isijikute nje ya mradi kwani wanaohitaji mradi huo wanazidi kuongezeka.
Muda mwingi umepotezwa na badilika badilika kwake na dhana ya mradi ambayo sasa maudhui ya kisheria yanatoa madai mengi kutokana na sheria ya Mali ya taifa ya mwaka 2017 na vile vile sheria ya Madini 2010 kwa hiyo kwa kiasi kikubwa wataalamu wa serikali wanadai wa kulaumiwa ni kampuni yenyewe na si serikali.
“Ieleweke wazi kuwa ukiona majadiliano yanachukua zaidi ya miaka10 ujue jambo hilo haliwezekani na hivyo kuliacha au kutafuta njia nyingine za utekelezaji kwani hakuna mradi duniani unaomalizwa mara moja ila hujadiliwa kutokana na matatizo yanayojitokeza kwani hakuna mtu mwenye nia nzuri kukataa ukweli unaojitokeza kwani wakati wa utekelezaji pande hizo mbili, serikali na mwekezaji huwa ni wabia na hivyo huwezeshana ili kufanikisha malengo waliyojiwekea.
Kwa sheria mpya inawataka wawekezaji kutoa asilimia 16 ya hisa bure kwa serikali.
Aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Dk. Chrisant Majiyatanga Mzindakaya, ameumia sana kusikia kuwa mradi huo si kipaumbele tena kwani alipigania sana kuhakikisha unakuwa hivyo. Alipotoka tu watu wameamua kuubwaga mradi bila kutoa sababu.
"Wengi niliowauliza nao vile vile wananiuliza wanasema tatizo ni mradi au Wachina? Kwa sababu si vema kuachia dola bilioni 3 ambazo zingeiweka nchi kwenye ramani ya dunia na hivyo kukosa kila kitu".
Kampuni hiyo ya Sichuan Hongda Group, kampuni mzazi katika mradi ilishinda zabuni kwa mradi huo mkubwa sana wa uchimbaji madini na ujenzi tangamano wa viwanda vya chuma na makaa ya mawe na usafiri wa reli hadi bandari ya Mtwara.
Mradi ulionesha uwezo wa kuunda kazi 5,000 za moja kwa moja na nyinginezo 30,000 zisizokuwa za moja kwa moja katika mwaka 2010.
Kampuni ya Kichina ilipewa zabuni ya kuendeleza kwa dola bilioni 3 (Sh trilioni 6.8) migodi huo wa chuma lakini sasa unaonekana si kipaumbele na hivyo Hongda inaona kuwa haikutendewa haki.
Serikali kwa mazingira ya sasa inaona kuwa kampuni hiyo ni kiwingu kwa kuzuia wawekezaji wengine kuingia kwenye eneo la mradi na kufanya wanayotaka kufanya baada ya kuona hakuna maendeleo ya haja kwenye mradi huo.
KUANGUKA BEI YA CHUMA
Isitoshe wakati fulani kampuni hiyo ilisema kuzalisha chuma wakati huo hakulipi na hivyo walikuwa wanasubiri bei ipande na hivyo madai ya kukosa motisha inaonekana kuwa ni mwendelezo wa kutaka dezo.
Kimsingi katika mazingira yaliyopo si rahisi kuibana Serikali ingawa matendo ya Waziri wa Fedha, Dk. Phillip Mpango, kuutoa kwenye kipaumbele inahitaji maelezo ya kina.
Isitoshe Hongda Group inadai uzinduzi wake mradi umejaa ucheleweshaji usioeleweka na kujaa sintofahamu na sasa kukosa msukumo wa kisiasa.
Hata reli yake imepitwa na ujenzi wa reli ya SGR kwenda Mwanza na nyingine kwenda Kigoma hadi Burundi na Rwanda. Mahitaji halisi yamebadilika ndani ya miaka mitatu.
“Kama mwekezaji mkubwa na alitumia rasilimali nyingi katika maendeleo na utekelezaji wa mradi, Sichuan Hongda, bado ana nia ya kutekeleza mradi huu licha ya changamoto za mara kwa mara ndani na nje ya nchi,” inasema taarifa ya Hongda.

Mchuchuma inadaiwa kuwa na tani milioni 428 za makaa ya mawe wakati Liganga ina tani milioni 128 za chuma na kampuni ya Kichina imetoa mpango jumuishi wa madini na uzalishaji umeme MW 600.
Kampuni hiyo itatengeneza madini yote ndani ya nchi ili kutenganisha titani na vanadium kutoka kwa madini ya chuma.
Wizara ya Fedha haikupatikana kusema kwanini haijasaini utekelezaji wa mradi huo kwa kutoa motisha kwa muda mrefu licha ya ahadi ya mwaka jana ya aliyekuwa Waziri wa Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, kudai ilikuwa inasubiriwa saini ya Rais Magufuli tu.
Suala la Waziri wa Fedha, Dk. Phillip Mpango, kuunyang’anya mradi nguvu ya kisiasa, linahitaji maelezo ya kina kwani suala hilo limeanza kuleta joto la kisiasa nchini na kwa wadau wa uchumi.
 
Teh teh teh 😁😁😂!!Mambo ni vululu-vululu kwa kwenda mbele.Yaani hadi marafiki wao wa Kichina wameanza kusoma namba,na kulalamika?Bwana Yule hastahili hata kumalizia miaka 2 iliyobaki.

Hao Wachina wakitaka wafanikiwe wahamishe reli yao iliyokuwa iende Ntwara sasa iende Mwanza,na hayo madini ya makaa ya mawe na chuma wayahamishe wakayachimbie Chato.Hapo Mhe.Mbinafsi ataachana na SGR na atawaunga mkono.
 
Nikiwa rais nitatengeneza 'tawi maalumu' ambalo litahakikisha yale yote tuliyokubaliana kama taifa yanatekelezwa na wale watakao kuwa madarakani muda huo na muda unaofuata. Tawi hili litapewa 'meno' ya kuwashughulikia 'wote' watao kwamisha utekelezaji wa mipango iliyokubaliwa. Ubadilishwaji wa maamuzi ya utekelezaji wa mipango lazima yakubaliwe na tawi hili katika misingi ya kiusalama na kiuchumi. Tawi litapewa uwezo wote wa kuhakikisha mipango muhimu kwa nchi inatekelezwa.
 
ULE msemo kuwa chelewa chelewa utamkuta mwana si wako umejidhihirisha wazi kwenye suala lauwekezaji wa mradi wa Liganga na Mchuchuma wilayani Ludewa mkoani Njombe ambapo mwekezaji, Sichuan Hongda Group yuko njia panda kwa kukosa mwelekeo na kuungwa mkono.

Kampuni imesema madai yote yalikuwa na haki ya kujadiliwa kikamilifu na Serikali ambayo ilikwisha kutoa vyeti vya vibali vya madini na vishawishi vya uwekezaji.

Sichuan Hongada Group inadai mradi umekuwa ukicheleweshwa na Serikali kutofanya yanayostahili huku ikijisahau kuwa kampuni hiyo imekuwa ikibadilisha masharti yake kama vile haijui nini inatakakwenye mradi.

Wachunguzi wa mambo wanasema mradi huo kwa kila hali umepitwa na wakati kwani sheria zimebadilika na masharti yauchimbaji madini yameathiriwa kwa kiasi kikubwa na sheria mpya za Tanzania ambazo zimebadilika kudai kupata faida kwenyeutajiri wake.

Hongda Group inashauriwa nayo kubadilika ilikuzuia isijikute nje ya mradi kwani wanaohitaji mradi huowanazidi kuongezeka.

Muda mwingi umepotezwa na badilika badilika yake na dhana ya mradi ambayo sasa maudhui ya kisheria yanatoa madai mengi kutokana na Sheria ya Mali ya Taifa ya mwaka 2017 na vile vile Sheria ya Madini 2010 kwa hiyo kwa kiasi kikubwa wataalamu wa Serikali wanadai wa kulaumiwa ni kampuni yenyewe na si Serikali.

“Ieleweke wazi kuwa ukiona majadiliano yanachukua zaidi ya miaka10 ujue jambo hilo haliwezekani na hivyo kuliacha au kutafuta njia nyingine zautekelezaji kwani hakuna mradi duniani unaomalizwa mara moja ila hujadiliwa kutokana na matatizo yanayojitokezakwani hakuna mtu mwenye nia nzuri kukataa ukweli unaojitokeza kwani wakati wautekelezaji pande hizo mbili, Serikali na mwekezaji huwa ni wabia na hivyo huwezeshana ili kufanikisha malengowaliyojiwekea.

Kwa sheria mpya inawataka wawekezaji kutoa asilimia 16 ya hisa bure kwa Serikali.

Aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Dk. Chrisant Majiyatanga Mzindakaya, ameumia sana kusikia kuwa mradi huo si kipaumbele tena kwani alipigania sana kuhakikisha unakuwa hivyo. Alipotoka tu watu wameamua kuubwaga mradi bila kutoa sababu.

Wengi niliowauliza nao vile vile wananiuliza wanasema tatizo ni mradi au Wachina? Kwa sababu si vema kuachia dola bilioni 3 ambazo zingeiweka nchi kwenye ramani ya dunia na hivyo kukosa kila kitu.
Kampuni hiyo ya Sichuan Hongda Group, kampuni mzazi katika mradi ilishinda zabuni kwa mradi huo mkubwa sana wa uchimbaji madini na ujenzi tangamano wa viwanda vya chuma na makaa ya mawe na usafiri wa reli hadi bandari ya Mtwara.

Mradi ulionesha uwezo wa kuunda kazi 5,000 za moja kwa moja na nyinginezo 30,000 zisizo kuwa za moja kwa moja katika mwaka 2010.
Kampuni ya Kichina ilipewa zabuni ya kuendeleza kwa dola bilioni 3 (Sh trilioni 6.8) wa chuma lakini sasa unaonekana si kipaumbele na hivyo Hongda inaona kuwa haikutendewa haki.

Serikali kwa mazingira ya sasa inaona kuwa kampuni hiyo ni kiwingu kwa kuzuia wawekezaji wengine kuingia kwenye eneo la mradi na kufanya wanayotaka kufanya baada ya kuona hakuna maendeleo ya haja kwenye mradi huo.

Kuanguka bei ya chuma

Isitoshe wakati fulani kampuni hiyo ilisema kuzalisha chuma wakati huu hakulipi na hivyo walikuwa wanasubiri bei ipande na hivyo madai ya kukosa motisha inaonekana kuwa ni mwendelezo wa kutaka dezo.

Kimsingi katika mazingira yaliyopo si rahisi kuibana Serikali ingawa matendo ya Waziri wa Fedha, Dk. Phillip Mpango, kuutoa kwenye kipaumbele inahitaji maelezo ya kina.

Isitoshe Hongda Group inadai uzinduzi wake mradi umejaa ucheleweshaji usioeleweka na kujaa sintofahamu na sasa kukosa msukumo wa kisiasa.

Hata reli yake imepitwa na ujenzi wa reli ya SGR kwenda Mwanza na nyingine kwenda Kigoma hadi Burundi na Rwanda. Mahitaji halisi yamebadilika ndani ya miaka mitatu.
“Kama mwekezaji mkubwa na alitumia rasilimali nyingi katika maendeleo na utekelezaji wa mradi, Sichuan Hongda, bado ana nia ya kutekeleza mradi huu licha ya changamoto za mara kwa mara ndani na nje ya nchi,” inasema taarifa ya Hongda.

Mchuchuma inadaiwa kuwa na tani milioni 428 za makaa ya mawe wakati Liganga ina tani milioni 128 za chuma na kampuni ya Kichina imetoa mpango jumuishi wa madini na uzalishaji umeme MW 600.

Makampuni hayo yatatengeneza madini yote ndani ya nchi ili kutenganisha titani na vanadium kutoka kwa madini ya chuma.
Wizara ya Fedha hakupatikana kusema kwanini haijasaini utekelezaji wa mradi huo kwa kutoa motisha kwa muda mrefu licha ya ahadi ya mwaka jana ya aliyekuwa Waziri wa Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, kudai ilikuwa inasubiriwa saini ya Rais Magufuli tu.

Suala la Waziri wa Fedha, Dk. Phillip Mpango, kuunyang’anya mradi nguvu ya kisiasa, linadai maelezo ya kina kwani suala hilo limeanza kuleta joto la kisiasa nchini na wadau wa uchumi.

Chanzo: Mtanzania
Je uwekezaji huo una maslahi kwa taifa?
 
Back
Top Bottom